Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

Hii sasa kazi!!

Ina maana hayo mabiliono ndio yawe yamepotea bure??!!

Hivi Prof.Shivji,Tundu Lissu na wataalam wengine wa sheria hawakulijua hili!!!

Kama ni kweli basi tukabidhi nchi kwa wawekezaji waiendeshe kwani sisi imetushinda!!
 
Sujui wenzangu labda wamepata hoja flan kupitia huu uzi, ila binafsi huyu muheshimiwa hana hoja zaidi ya kujichekesha mwenyewe.

Mchakato wa katiba uko halali kisheria kwa7bu umepitia kwenye bunge la tanzania na sheria zote zimetoka huko.

Rais hakuanzisha mchakato huu, si hoja yake, ni hoja ya watanzania walio wengi, si hoja ya jana na juzi ni hoja ya miaka nadhan ukirejea nyuma historia utaona hoja nyingi sana ikiwemo ya G55.

Katiba ya Zanzibar kwa sasa imetangaza wazi kwamba Zanzibar ni Nchi! Nenda kwenye dictionary la kiswahili angalia neno "nchi" lina maana gani? Haikuishia hapo imetangaza mipaka yake na vielelezo vyenginevyo. Hili pia limezidisha haja ya katiba mpya ili Tanganyika nayo irud kwakua kisheria katiba ya zanzibar imeamuliwa na wazanzibari wenyewe.

Kuna hoja nyingi sana ila mbali ya yote mazingira nayo yanaruhusu sasa kuandika hii katiba mpya, sisi hatuigi kenya wala wapi ni muda muafaka kufanya haya hasa ikizingatiwa hii ni katiba ya muungano.

Hii si hoja ya kikwete, na maswala ya migongano ni lazima coz tunatengeneza katiba ( sheria mama) kwaiyo kutofahamiana au kuwepo na khitilafu za hapa na pale si hoja ya msingi hapa, ingekuepo hata tungefanya vipi haya ni maswala ya kisheria.

Nawasilisha.
 
Mkuu siyapingi mawazo yako pia siyaungi mkono. Kwa upande wangu napenda kusema nini haswa Watanzania wanaitaji kwa sasa. Kiukweli ukiangalia kwa jicho la tatu utaona kuwa kinachoitajika na watanzania walio wengi sio Katiba mpya bali Hawataki kuiona ccm ikiendelea kutawala na swala la katiba mpya ni njia ya mwanzo inayotumika kwa sasa kuitoa ccm madarakani, na kama katiba ikapatikana na ccm ikaendelea kutumia ubabe kutawala utaona jambo lingine linaibuka tena. Hakika nawaeleza kama ccm itaendelea kutawala baada ya katiba mpya kupatikana njia ya pili itakuwa hatari kubwa kwa taifa zima.
 
Kama huu mchakato ni haramu, kwa ushauri wako ni kuendelea na katiba tuliyonayo?

Chombo halali ni kipi?
Mchakato haramu tunda lake i.e. Katiba nayo itakuwa na u-haram. Kwa ufupi katiba iliyoko sasa haiko wazi sana ya namna ya kuibadilisha.....ila Bunge la Wananchi ndipo mahali sahihi. Kwa bahati mbaya JK alianzisha kama Rais na baadaye chama chake (CCM) kikahodhi huo mchakato na ndipo hapa tulipo sasa.
 
Tunaweza kusema Rais Kikwete hakuwa na madaraka ya kuanzisha mchakato huu kwani haukuwa kwenye ilani yao na haukuanzia kwenye ngazi za chini. Ilani ya CHADEMA ndiyo iliyokuwa inazungumzia 'kuanzisha mchakato' wa katiba mpya siku 100 baada ya mgombea wao kushinda.Lakini tunajua Kikwete ni mtu anayependa kuacha 'legacy'.Katiba mpya ndiyo iliyokuwa hoja iliyopo.Hivyo kwa kuwa Mwenyekiti wa CCM - Taifa na Rais madaraka yao ni makubwa sana, basi aliipenyeza hii hoja.Tunategemea yeye kupata upinzani toka pande zote za makundi ya kisiasa kutokana na minyukano ya kimaslahi lakini mwishoni katiba mpya itapatikana.Kama mliipitia vizuri hotuba yake, imewashtusha hata watu wake.Hawakutegemea Rais kutafuta namna ya kupata 'common ground' na vyama ya upinzani ijapokuwa kama Rais hawezi kuonyesha dhahiri.Ni kiasi cha kungoja na kuangalia.Mwisho wa siku 'the end will justify the means'..
 
http://udadisi.blogspot.com/2011/11/kikwete-has-point-but-here-is.html

FRIDAY, NOVEMBER 18, 2011


KIKWETE HAS A POINT BUT HERE IS A COUNTERPOINT


"We don't need JK's Commission! It will disturb the process by being malicious to the process in favour of the ruling party....we need first of all to amend the current Constitution especially article 98. The amendment that shall allow formation of an independent commitee not emanating from JK or any president thereto. This commission shoul include representatives from all walks of life ranging from ordinary citizens, religious leaders, CSOs, politicians and political parties, legal experts etc in our country that will collect the views of the people...it is not possible to suspend a constitution in any society if there is no revolution by mass or military coup de tat. In peaceful mood as in Tanzania we cannot suspend the current constitution...mind you to suspend a current constitution in absence of military coup de tat or mass revolution like the ones in Egypt, Tunisia or elsewhere amount to treason which is one of the capital offences in our law. Even JK HAS NO POWER legally to suspend a constitution because he was sworn in to defend it no matter how bad it is...." - A Young Tanzanian Lawyer in a Constitutional Debate, March 2011

Cf. Kikwete's speech:Hotuba ya "mazungumzo" ya Rais Kikwete na "Wazee wa Dar es Salaam" siku ya Ijumaa 18 Novemba 2011 - wavuti.com
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hili ni swali ambalo jibu lake liko wazi; kuwa Rais Kikwete hakuwa na madaraka hayo. Hata hivyo, wapo wanaoamini kuwa kwa vile Rais kaamua kufanya kitu basi kitu hicho ni halali.

Mimi na baadhi yetu tumekataa kuutambua mchakato huu wa Katiba Mpya kwa sababu ni haramu; haukuanzishwa na chommbo halali na hata hivi sasa matatito tunayoyaona na yatakayotokea mbeleni (kwenye Bunge la Katiba na Kura ya Maoni) itakuwa ni mwendelezo tu wa kosa hili kubwa.

HUU NI MCHAKATO HARAMU. Sikiliza HOJA MARIDHAWA

[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=115504&stc=1&d=1381127129[/JFMP3]

Mkuu nakubali hoja yako, kama ni kuatafuta kasoro ili iwe sababu ya kuendelea na katiba hii tutazipta nyingi tu hata kama mchakato huu ungeanzishwa na ambaye; kwa mujibu wa Mzee Mwanakijiji, ana madaraka hayo. Jitihada zozote za kusimamisha mchakato huu zitafanya 2015 twende kwenye uchaguzi kwa katiba hii hii iliyopo.

Nina mashaka na hoja kama hizi iwapo wanaozishupalia hajabeba ajenda ya makundi ya mafisadi ambao tunasikia wasingependa katiba mpya ipite kwa vile itawakwamisha malengo yao ya 2015. Tafakari.
 
Last edited by a moderator:
Heri tupate hiyo ya mchakato haramu,kwani tunaweza kusubiri hiyo ya mchakato halali wala tusiipate
kabisa chini ya ccm,na uwezekano wa kupata serikali nyingine yenye dhamira ya dhati ya kuleta katiba
halali,chini ya katiba hii haupo.So mimi namuunga mkono JK tuendelee tu,tutafika somewhere japo si pale tunapotaka'
 
Sujui wenzangu labda wamepata hoja flan kupitia huu uzi, ila binafsi huyu muheshimiwa hana hoja zaidi ya kujichekesha mwenyewe.

Mchakato wa katiba uko halali kisheria kwa7bu umepitia kwenye bunge la tanzania na sheria zote zimetoka huko.

Jifunze kusoma swali kabla hujajibu; usijibu kitu kisichoulizwa.
 
Mkuu nakubali hoja yako, kama ni kuatafuta kasoro ili iwe sababu ya kuendelea na katiba hii tutazipta nyingi tu hata kama mchakato huu ungeanzishwa na ambaye; kwa mujibu wa Mzee Mwanakijiji, ana madaraka hayo. Jitihada zozote za kusimamisha mchakato huu zitafanya 2015 twende kwenye uchaguzi kwa katiba hii hii iliyopo.

Nina mashaka na hoja kama hizi iwapo wanaozishupalia hajabeba ajenda ya makundi ya mafisadi ambao tunasikia wasingependa katiba mpya ipite kwa vile itawakwamisha malengo yao ya 2015. Tafakari.

Huwezi kuwa na katiba mpya haramu ambayo baadaye italalamikiwa tena kama hii ya sasa inavyolalamikiwa. Kutaka tu katiba mpya bila kujali inapatikana vipi ni recipe ya migogoro na tayari tumeshaona dalili zake.
 
Kaka heshima kwako,

Nakubaliana kwa kiasi flani na hoja yako, kidogo natofautiana na wewe pengine wawezakunielewesha zaidi maana binadamu tunatofautiana kimtizamo. Kifupi nadhani mchakato wa katiba una-uhalali maana umeanzishwa kupitia bunge na sheria kutungwa kwa kutumia katiba ya sasa.

Ni kifungu gani katika Katiba ya sasa ambacho kimeweka utaratibu wa kuandika Katiba Mpya ambao umelipa Bunge uwezo wa kutunga sheria ya kuandika Katiba Mpya?
 
Nadhani alifuata ushauri wa Dr.W.Slaa, kuwa akichukuwa nchi ndani ya siku 90 atakuwa kaishaandika katiba mpya.

Kweli wakati mwingine tunasikitisha; swali liko wazi kabisa lakini gumu kueleweka au ni kugumu kujibika! Kwani nimeuliza kuhusu "amepata wapi ushauri"? duh... mnaniangusha jamani...
 
HUU NI MCHAKATO HARAMU. [/JFMP3]

Nakuunga mkono, but very unfortunately, as of now, its too little too late!.

Siku ule muswada ulipoletwa bungeni, niliwauliza Chadema, kwa nini hawakuupinga kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za kupinga, Mkuu Mzee Mwanakijiji, ni miongoni mwa mlionibeza!. Hiki kinachoendelea ni matokeo tuu!, watu tunadeal na matokeo huku tunasahau chanzo!. Laiti Chadema wange "do the right thing, at the right time, and doing it right!", tusingalifika hapa tulipofika!.

Nilisema kule, na ninasema hapa, "maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga!'

Rejea mjadala huu Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Pasco.
 
:A S 39::A S 39::A S 39::A S 39::A S 39::A S 39:

IMG_1966.JPG

Muugwana, Safari_ni_Safari;
Hili ni baraza la kutunga sheria la yule mshirika wa Muungano au ni kikao cha kujadili sikukuu ya Eid Al Hadji wiki ijayo!!!

Nijuze Muugwana mwenzangu...
 
hahaha hii akili au matope

dk 9:04 unajichekesha unacheka mwenywe

neno haramu umerudia kama mara mia

hujanukuu hata kifungu kimoja cha katiba

this is ridiculous!

Eti katiba haina sehemu ya kubadilisha katiba bali kurekebisha

khaaaaa
Kama kipo hicho kifungu si ukioneshe...au hata katiba yenyewe umewahi hata kuisoma?
 
Nakuunga mkono, but very unfortunately, as of now, its too little too late!.

Siku ule muswada ulipoletwa bungeni, niliwauliza Chadema, kwa nini hawakuupinga kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za kupinga, Mkuu Mzee Mwanakijiji, ni miongoni mwa mlionibeza!

Nilisema kule, na ninasema hapa, "maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga!'

Rejea mjadala huu Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Pasco.

Pasco naomba urejee nada yako hiyo na unioneshe nilipokubeza kwani ukosoaji wangu wa mchakato huu haujaanza baada ya mswada kuletwa bungeni bali ulianza pale Kikwete alipotangaza tu nia ya kutaka kuanzisha mchakato huu. So nioneshe nilipokubeza ili nikuuombe radhi.
 
Ni kifungu gani katika Katiba ya sasa ambacho kimeweka utaratibu wa kuandika Katiba Mpya ambao umelipa Bunge uwezo wa kutunga sheria ya kuandika Katiba Mpya?

Kaka too direct kutaka kifungu maalumu kinacho lipa bunge mamlaka ya kutunga sheria ya katiba mpya.Anyway, ninavyoelewa mie katiba ni mwongozo, nakubaliana na wewe kuwa hakuna specific kifungu katika katiba kinalipa bunge uwezo wa kutunga katiba mpya..Lkn bunge ni chombo cha kisheria kinachotunga sheria za nchi yetu nahakuna chombo kingine kinachofanya kazi hiyo.

Hivyo, kutungwa sheria ya mchakato wa katiba bungeni ndio hoja yangu inalalia hapo kuwa ni chombo cha kisheria kilichotunga sheria ya mchakato wakatiba hivyo mchakato ni halali.

Pia nivizuri kuwekana sawa tusiwe wajuzi wa kusema si halali tuu, je ili uwe halali we unadhani mchakato ungekuwaje? na je uhalali ungetoka wapi kama katiba haina kifungo hicho chauhalali unachokitaka mkuu?

Ndio maana mie nashawishika kujua malengo ya kubadili katiba kabla ya kujadili machakato maana katika hoja yako na hilo umeligusia indirect pale umesema kuna vifungu katika katiba ya sasa vinaruhusu kubadili mapungufu ktk katibalknsio kubadili...sasa tukijua main objective ya kuunda katiba mpya uhalali unaoutaka utapatikana hapo hayo ni maoni yangu twende kwa hoja mtanzania mwenzangu
 
Mliomba Mchakato wa Katiba Mpya mkidhan mtaumiliki, sasa mnapigwa za Mbavu mnaanza kuhoji Mamlaka, ushamkabidhi Kinyozi kichwa subirini kushuhudia Kiduku!
 
MM
Kwakweli nimecheka sana, swali ni rahisi lakini lina majibu tofauti kabisa. Watu wanafeli mitihani si kwa kutojua bali kwa kutoelewa swali.

Swali ni hivi, ili katiba ibadilishwe kwa kutumia sheria na utaratibu wa bunge unaosemwa ni lazima kuwepo na chanzo cha kufanya hivyo. Sasa hivi tunajua chanzo ni JK kwasababu hakuna mahali CCM au Serikali yake imejadili kuhusu kuandikwa kwa katiba.

Kwa mantiki hiyo hili ni wazo la JK. Swali wazo hili limepataje uhalali hadi liandikiwe katiba?
Kupitia taratibu za bunge ni matokeo ya wazo hilo, uhalali wa wazo umepatikana wapi?

Yupo aliyesema wazo limepitia njia halali, well hata wenye pesa chafu za damu wakiziingiza katika mzunguko zinakuwa na uhalali lakini je chanzo cha pesa hizo ni halali?

Maana ya swali hili ni kuwa kama tutaruhusu mtu aamke asubuhi na kubadili mambo mazito kama haya basi rais X ajaye naye anaweza kuamka asubuhi na kuamua iandikwe katiba nyingine. Kila baada ya maiaka 5 tutaandika tu kwasababu kuna mtu ana wazo hilo.

Wazo lililopoletw tulihoji kama ilikuwa ipo katika ilani ya uchaguzi au ni sera au kuna kikao chochote kilichofikia maamuzi japo kwa uchahce. Jibu ni hakuna.
Tunajua ilikuwa hoja ya wananchi kupitia wapinzani.Hata hivyo kama taifa hatujawahi kukaa na kupanga tunataka taifa la namna gani na tuliandae vipi.

Tukasema mchakato wa katiba wa kutumia wazo la JK si sawa na kuanzisha chuo cha UDOM.
Hili ni suala zito linaloweza kuivuruga nchi sana. Tulihitaji mjadala wa kitaifa na siyo 'suprise suprise ya hotuba za mwezi' tena ikipigiwa vigelegele na viongozi wa upinzani!!!
Tukaambiwa ni fataani sasa nadhani ukweli unaonekana.

Huu ni mwanzo tu ninachokiona ni nchi kuingia katika machafuko. Hilo ninaliona kwa mbali.
Tunaingia huko kutokana na ukiukwaji wa misingi ya kuandika katiba ya wananchi. Sasa hivi katiba ya CCM inaandikwa halafu itaitwa ya Tanzania. Nchi inachafuka wenye macho wanaona! wabishi wasubiri utaratibu wa sheria halali.
 
Back
Top Bottom