Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mchakato haramu tunda lake i.e. Katiba nayo itakuwa na u-haram. Kwa ufupi katiba iliyoko sasa haiko wazi sana ya namna ya kuibadilisha.....ila Bunge la Wananchi ndipo mahali sahihi. Kwa bahati mbaya JK alianzisha kama Rais na baadaye chama chake (CCM) kikahodhi huo mchakato na ndipo hapa tulipo sasa.Kama huu mchakato ni haramu, kwa ushauri wako ni kuendelea na katiba tuliyonayo?
Chombo halali ni kipi?
Hili ni swali ambalo jibu lake liko wazi; kuwa Rais Kikwete hakuwa na madaraka hayo. Hata hivyo, wapo wanaoamini kuwa kwa vile Rais kaamua kufanya kitu basi kitu hicho ni halali.
Mimi na baadhi yetu tumekataa kuutambua mchakato huu wa Katiba Mpya kwa sababu ni haramu; haukuanzishwa na chommbo halali na hata hivi sasa matatito tunayoyaona na yatakayotokea mbeleni (kwenye Bunge la Katiba na Kura ya Maoni) itakuwa ni mwendelezo tu wa kosa hili kubwa.
HUU NI MCHAKATO HARAMU. Sikiliza HOJA MARIDHAWA
[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=115504&stc=1&d=1381127129[/JFMP3]
Sujui wenzangu labda wamepata hoja flan kupitia huu uzi, ila binafsi huyu muheshimiwa hana hoja zaidi ya kujichekesha mwenyewe.
Mchakato wa katiba uko halali kisheria kwa7bu umepitia kwenye bunge la tanzania na sheria zote zimetoka huko.
Mkuu nakubali hoja yako, kama ni kuatafuta kasoro ili iwe sababu ya kuendelea na katiba hii tutazipta nyingi tu hata kama mchakato huu ungeanzishwa na ambaye; kwa mujibu wa Mzee Mwanakijiji, ana madaraka hayo. Jitihada zozote za kusimamisha mchakato huu zitafanya 2015 twende kwenye uchaguzi kwa katiba hii hii iliyopo.
Nina mashaka na hoja kama hizi iwapo wanaozishupalia hajabeba ajenda ya makundi ya mafisadi ambao tunasikia wasingependa katiba mpya ipite kwa vile itawakwamisha malengo yao ya 2015. Tafakari.
Kaka heshima kwako,
Nakubaliana kwa kiasi flani na hoja yako, kidogo natofautiana na wewe pengine wawezakunielewesha zaidi maana binadamu tunatofautiana kimtizamo. Kifupi nadhani mchakato wa katiba una-uhalali maana umeanzishwa kupitia bunge na sheria kutungwa kwa kutumia katiba ya sasa.
Mchakato wa Katiba hauhitaji kupata madaraka, ni wazo ambalo kwa pamoja watu hukubalina.
Nadhani alifuata ushauri wa Dr.W.Slaa, kuwa akichukuwa nchi ndani ya siku 90 atakuwa kaishaandika katiba mpya.
HUU NI MCHAKATO HARAMU. [/JFMP3]
:A S 39::A S 39::A S 39::A S 39::A S 39::A S 39:
Kama kipo hicho kifungu si ukioneshe...au hata katiba yenyewe umewahi hata kuisoma?hahaha hii akili au matope
dk 9:04 unajichekesha unacheka mwenywe
neno haramu umerudia kama mara mia
hujanukuu hata kifungu kimoja cha katiba
this is ridiculous!
Eti katiba haina sehemu ya kubadilisha katiba bali kurekebisha
khaaaaa
Nakuunga mkono, but very unfortunately, as of now, its too little too late!.
Siku ule muswada ulipoletwa bungeni, niliwauliza Chadema, kwa nini hawakuupinga kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za kupinga, Mkuu Mzee Mwanakijiji, ni miongoni mwa mlionibeza!
Nilisema kule, na ninasema hapa, "maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga!'
Rejea mjadala huu Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
Pasco.
Ni kifungu gani katika Katiba ya sasa ambacho kimeweka utaratibu wa kuandika Katiba Mpya ambao umelipa Bunge uwezo wa kutunga sheria ya kuandika Katiba Mpya?