Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Nakiri makosa, kwa sisi wa Kanda Ziwa Kiswahili sanifu nacho ni kazi!, niliandika kubeza nikimaanisha kupinga, niliposema Chadema walifanya makosa wakati ule ambayo tutakuja kuyalipa, ulinipinga ukimaanisha Chadema hawakukosea. Kinachoendelea sasa ni process tuu ya malipo, malipo yenyewe kamili bado, they have a price and we'll have to pay!. Hili swali la kuhoji mamlaka ya rais kuanzisha mchakato ule, should have been asked by then na kuonyesha kwa vifungu, why not!, kuuliza hayo sasa ndio hii too little too late ninayoizungumzia mimi, kilichobaki kwa sasa ni kujindundulizia tuu hito tujisent, tukijiandaa kulipa hili deni, ili wakati wa kulipa ukiwadia, tulipe gharama ya tuliowaaminia kuzuia tusilipishwe, hawakuzuia na sasa tunalipishwa na tutaendelea kulipishwa!.Hiki sicho ulichosema hapo juu; umenituhumu kuwa nilikubeza kana kwamba nilidharau mchango wako na kukufanya uonekane mjinga. Kumbe nilikuwa na maoni tofauti na wewe tu na yalitolewa kwa heshima yote. Maoni yako yale yalikuwa na makosa wakati ule kama ambavyo bado yameendelea kuwa na makosa. Hii si kubeza.
Pasco.