Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

Hiki sicho ulichosema hapo juu; umenituhumu kuwa nilikubeza kana kwamba nilidharau mchango wako na kukufanya uonekane mjinga. Kumbe nilikuwa na maoni tofauti na wewe tu na yalitolewa kwa heshima yote. Maoni yako yale yalikuwa na makosa wakati ule kama ambavyo bado yameendelea kuwa na makosa. Hii si kubeza.
Nakiri makosa, kwa sisi wa Kanda Ziwa Kiswahili sanifu nacho ni kazi!, niliandika kubeza nikimaanisha kupinga, niliposema Chadema walifanya makosa wakati ule ambayo tutakuja kuyalipa, ulinipinga ukimaanisha Chadema hawakukosea. Kinachoendelea sasa ni process tuu ya malipo, malipo yenyewe kamili bado, they have a price and we'll have to pay!. Hili swali la kuhoji mamlaka ya rais kuanzisha mchakato ule, should have been asked by then na kuonyesha kwa vifungu, why not!, kuuliza hayo sasa ndio hii too little too late ninayoizungumzia mimi, kilichobaki kwa sasa ni kujindundulizia tuu hito tujisent, tukijiandaa kulipa hili deni, ili wakati wa kulipa ukiwadia, tulipe gharama ya tuliowaaminia kuzuia tusilipishwe, hawakuzuia na sasa tunalipishwa na tutaendelea kulipishwa!.

Pasco.
 
​Kwani CCM bara na visiwani hawakuliona hilo!? Tuseme JK ndiye Think tank wa CCM!?

Waliliona, lakini pengine wengi hawakutarajia solution itakuwa hii, ambayo inachanga moto kubwa zaidi. Bahati mbaya inaonekana ndani ya CCM haikupata muafaka kabla ya kuanzishwa mchakato.
 
Kweli wakati mwingine tunasikitisha; swali liko wazi kabisa lakini gumu kueleweka au ni kugumu kujibika! Kwani nimeuliza kuhusu "amepata wapi ushauri"? duh... mnaniangusha jamani...

Kwa hiyo Mzee Mwanakijiji tatizo hapa sio mchakato wa kupata katiba mpya, ila tulitakiwa tupitie, kudhibitisha na kujiridhisha kwanza kwamba wazo la kuhitaji katiba mpya ni hitaji la taifa.
 
Last edited by a moderator:
Hibi acheni kuandika pumba kama mmekosa cha kuandika soma kisha acha ...tu peni pumba na mashudu..
 
Nakiri makosa, kwa sisi wa Kanda Ziwa Kiswahili sanifu nacho ni kazi!, niliandika kubeza nikimaanisha kupinga, niliposema Chadema walifanya makosa wakati ule ambayo tutakuja kuyalipa, ulinipinga ukimaanisha Chadema hawakukosea. Kinachoendelea sasa ni process tuu ya malipo, malipo yenyewe kamili bado, they have a price and we'll have to pay!. Hili swali la kuhoji mamlaka ya rais kuanzisha mchakato ule, should have been asked by then na kuonyesha kwa vifungu, why not!, kuuliza hayo sasa ndio hii too little too late ninayoizungumzia mimi, kilichobaki kwa sasa ni kujindundulizia tuu hito tujisent, tukijiandaa kulipa hili deni, ili wakati wa kulipa ukiwadia, tulipe gharama ya tuliowaaminia kuzuia tusilipishwe, hawakuzuia na sasa tunalipishwa na tutaendelea kulipishwa!.

Pasco.

Pasco..swali hiki halijaanza leo..nalirudia yu kwa namna nyingine rejea mada zangu za nyuma kuhusu illegitimacy ya mchakato huu.
 
Simple question. Nikisema "Kimsingi katiba Mpya ni hoja ya wapinzani", nitakuwa nadanganya?
La hasha! Lakini ukisema wapinzani ndio walioanzisha mchakago huu utakuwa unadanganya. Kikwete hakuanzisha wazo la kudai Katiba Mpya..na CCM haijawahi kuwa na hoja Katiba mpya. Which bring us back to the same question:Kikwete alipotangaza kuwa serkkali yake itaanzisha mchakato wa kulipatia taifa Katiba Mpya madaraka hayo aliyatoa wapi? Sijauliza WAZO hilo alilitoa wapi?
 
Najua Kikwete anatafuta 'legacy' lakini inavyoelekea he might go down in history, not only as the worst President ever, but also as worst CCM Chairman. Amewabambikia CCM sera feki ya katiba mpya - hawajui cha kufanya - kila mmoja na lwake. Isitishe kaibambikia nchi mchakato feki wa kuandika katiba mpya. Hotuba zake zote yeye ni kung'ang'ania kuteua misururu ya watu tu! "oho Kama Nyerere aliteua kwa nini na mimi nisiteue'!!!

Umesema vizuri sana kwa wenye kuelewa watakuwa wameelewa.
 
W
By JF-MBUNGE
Mkuu kaka anashindwa kuelewa kuwa some times illegal things can be appropriate,but an issue is appropriate for what?

Simple kaka, mwizi akikufyatua risasi kukutoa maisha yako na we una silaa ukammaliza! is it legal kuua? will it not be appropriate action for ur life? I think u should learn to view in different views rather than view according 2ur view.

Mfano wako mbaya. Mtu anaruhusiwa kuua kuokoa maisha yake so yes it is legally permissible to kill in self defence.
 
Upinzani kama inamaanisha kupinga kila jambo zuri na baya litendwalo na serikali basi Mzee Mwanakijiji umeshinda katika hili. Sikuwahi kukuona ukiunga mkono hata move +or- moja ya serikali.

si wapo wanaounga mkono moves hizo za serikali kwani lazima na mimi nifanye hivyo ili kiwe nini?
 
Last edited by a moderator:
An ox before the cart! Hata Muungano tulipaswa kutoa maoni kama tunautaka au hatuutaki. Personal hata muungano na Zenj siutaki
 
Mimi nimeisoma ibara ya 98 ya katiba yetu bado nashindwa kuona namna ilivyokiukwa katika mchakato huu.
 
La hasha! Lakini ukisema wapinzani ndio walioanzisha mchakago huu utakuwa unadanganya. Kikwete hakuanzisha wazo la kudai Katiba Mpya..na CCM haijawahi kuwa na hoja Katiba mpya. Which bring us back to the same question:Kikwete alipotangaza kuwa serkkali yake itaanzisha mchakato wa kulipatia taifa Katiba Mpya madaraka hayo aliyatoa wapi? Sijauliza WAZO hilo alilitoa wapi?

Swala ambalo ni upotoshaji ni pale unapotaka kuonyesha kwamba Kikwete amepandikiza wazo la kuwepo kwa Katiba mpya ambalo may be watanzania hawaku tayari nalo. This is not true!

Watanzania walikuwa wanataka katiba mpya. This is to say jamii ya watanzania ilikuwa na mahitaji. Rais anapogundua kuwa watu wana mahitaji anafanyaje? he has to do something about it. Rais akiona kuna mahitaji ya jambo kwenye jamii na kuliacha tu linaelea elea bado mtalalamika kama ilivyo kawaida yenu.

Wananchi wameridhia Rais wao asimamie mchakato huu wa Katiba ambao haujaelezewa kinagaubaga kwenye Katiba unapaswa kufanyika vipi. What is the problem? Utayari na ridhaa ya watu ni muhimu zaidi kuliko maandishi yoyote.

Kwani wewe unapounga mkono vurugu za kupindua serikali kupitia what you call nguvu ya umma huwa unatumia kifungu kipi cha Katiba?
 
An ox before the cart! Hata Muungano tulipaswa kutoa maoni kama tunautaka au hatuutaki. Personal hata muungano na Zenj siutaki
Hautaki wewe ni nani kwani kuna mtu amekulazimisha kuukubali.
 
Mzee mwanakijiji.

samahani, mwenye mamlaka ya kuanzisha mchakato wa katiba ni nani maana unasema katiba ya sasa haina utaratibu wa kuandika katiba mpya, kama hivyo ndivyo, JK naye kapata wapi mamlaka na madaraka ya kuanzisha mchakato wa katiba mpya?

umesema kuna utaratibu wa kuanzisha katiba mpya lakini hujasema kuwa ni utaratibu gani?. Naomba na mimi nisije nikawa nashangalia na kucheza ngoma ya wachawi.

Weka sawa role model wangu
 
Mzee Mwanakijiji,

Wazo la katiba mpya limetoka kwa wananchi wenyewe alichofanya Rais Kikwete kama rais kutimiza wajibu wake kusikia kilio cha wananchi wake ambao kimsingi ndiyo walitaka katiba mpya.

Tumeona vyama vya siasa vinavyo lalamikia hii katiba kwenye chaguzi kuwa inaupendeleo kwa chama tawala.

Tumeona Mchungaji Mtikila, pamoja na wananchi wengine wakipeleka madai yao mahakamani wakitaka katiba mpya.

Tumeona mauaji ya Pemba mwaka 2001 moja ya madai makubwa ilikuwa katiba mpya.

Tumeona maandamano ya kina Prof. Lipumba mpaka anavunjwa mkono na polisi madai yao makubwa yalikuwa katiba mpya.
 
Last edited by a moderator:
Kikwete aliona kuwa CCM hawakuwa tayari kwa mchakato wa katiba akachukua fursa hiyo kama mwenyekti wa ccm na rais. hata sasa CCM wana msimamo wa serikali mbili na Kikwete kawaambia wajiandae kiakili endapo ufumo wa serikali tatu utapitishwa. nadhani wanajiandaa. Tangu zama za zidumu fikra za ... ndani ya ccm kuna element ya ufalme hivi kwamba kitu kikisemwa na mkubwa hakuna anayethubutu kuonyesha msimamo kinzani waziwazi, hii ni kasoro kwa maendeleo ya nchi. kwangu mimi niliona vema kwa Kikwete kuanzisha mchakato, bora uwe objective na wazi kwa wote. hatari iliyokuwepo ni ile ya kumfanya awe kama kiongozi wa mageuzi Russia.
 
Mimi nimeisoma ibara ya 98 ya katiba yetu bado nashindwa kuona namna ilivyokiukwa katika mchakato huu.

Ibara ya 98 inasemaje kuhusiana na kuandika upya Katiba? siyo kufanyia marekebisho vipengele tu vya katiba ya sasa bali kuifuta ya sasa na kuleta Katiba Mpya Ibara hiyo inasemaje?
 
Mzee Mwanakijiji,

Wazo la katiba mpya limetoka kwa wananchi wenyewe alichofanya Rais Kikwete kama rais kutimiza wajibu wake kusikia kilio cha wananchi wake ambao kimsingi ndiyo walitaka katiba mpya.
Yaani akiwa "Rais" basi ana madaraka ya kufanya lolote lile hata kama linakiuka Katiba aliyoapa kuilinda, kuitetea na kuihifadhi?
 
Back
Top Bottom