Nakubaliana na wewe rev. kwamba ccm imeoza toka zamani ,huoni watu ni wa fitini sana kumsifia Nyerere kumbe ndo aliozesha mambo yote, hii ni kwa staili mleta maada.
Rev, sio ccm iliyooza ni watanzania karibu wote wenye umri fulani (sitautaja) wamefubaha (bakubhaga) regardless ya chama walichomo.
No! No! MkamaP,
Usifanye makosa kirahisi Mkuu. Tupo ambao tunamsifu Nyerere kuwa ni Baba wa Taifa ambaye kipindi chake cha kuanza kulikomboa na kiliongoza Taifa hili alipata changa moto kali sana kwa kuwa mfumo wa dunia wakati ule ulikuwa mgumu sana. Halafu nchi haikuwa na wasomi wa kuweza kuendesha nchi. Wakati mwingine wale ambao tunaelewa mambo yalivyokuwa hata kipindi cha miaka ya sabini tu wala si nyuma sana, mambo yalikuwa ovyo sana.
Halafu viongozi waliofuata baada ya Mwalimu ndiyo walitakiwa waendeleze kuliimarisha Taifa. Sasa badala yake wako katika juhudi za kuuza nchi. Kwa kifupi tunawiwa kumwonea huruma baba wa Taifa kuwa alitawala kipindi kilichokuwa kigumu sana, kuangalia wenzetu Afrika wakiteswa na kuuwawa, kubaguiliwa, na kudharauliwa kama wanyama.
Nakuhakikishia hilo lilitosha kumsamehe kabisa Nyerere. Wale waliosaidiwa na wanaofahamu maana ya uhuru leo hii watakuambia kuwa hawatamsahau Nyerere. Sisi hatukupitia kipindi kigumu kupigania uhuru wala hatukumwaga damu na kama ilitokea ni kidogo sana ukilinganisha na majirani zetu.
Viongozi waliofuata ndiyo wanaotakiwa kulaumiwa, maana walipoteza dira ya Taifa letu. Wamechafua muungano na umoja wa Kitaifa ambao Nyerere alijitahidi sana kuuunda. Baadhi yetu huwa bado wanabakia kulaumu sana, wapo wanaosema kuwa hakuwatendea waisalamu haki nk.
Wengine watakumbuka kuwa alituweka katika uhusiano mbaya na baadhi ya nchi kama Nigeria alipounga mkono uasi wa Biafra, wapo watakaomlaumu sana kwa kumpa support Savimbi, uhusiano wetu na Angola utaendelea kuwa mbaya kaisi kwa muda.
Lakini nataka tu uelewe kuwa Baba wa taifa aliliongoza Taifa letu kipindi kigumu sana cha siasa duniani. Kipindi cha vita baridi. Kiliendelea mpaka maraisi walioona kuwa hakuna manufaa kwa upande wowote wakaunda shirikisho la nchi zisizofungamana na upande wowote, lakini hata hilo halikusaidia sana.
Kwani nchi za magharibi zilikuwa na nguvu za kiuchumi na kisayansi waliendelea kutawala tena kwa nguvu na uhakika sana. Nchi moja baada ya nyingine zikawa zinaanguka na kuelekea upande wao. Kuanguka kwa Shirikisho la mataifa ya Kirusi kulihitimisha vita hiyo baridi duniani.
Baada ya jambo hili kila nchi duniani ilichukua mwelekeo wake, including China, ambayo mpaka leo hawajaweza kusema kama ni mfumo wa kibepari au la! Lakini nataka tu nifupishe maneno kuwa Nyerere hakustahili tena kubeba lawama za baada yake maana waliofuata walikuwa na wajibu wa kutafuta kwa haraka na umakini na kugundua wapi taifa lielekee. Utafiti huo ulitakiwa uwe wa kisayansi zaidi. Badala yake ukawa wa kichawi au kishirikina zaidi. Ndiyo maana tuko hapa tulipo.
Ndiyo maana unaanza kuona watu wanasema eti "hata yeye alishindwa". Sasa kama yeye alishindwa ndiyo ina maana na wewe ushindwe? Kwanini sasa uligombea uraisi? Maana anayegombea Uraisi wa nchi anatakiwa awe na lengo jema analotaka kulifanyia Taifa. Siyo tu kwenda pale Ikulu kufanya bishara binafsi kama alivyofanya Mwinyi, Mkapa na wanaoendeleza ufisadi.
Kipindi cha Nyerere mtanzania pamoja na umaskini watu tulikuwa tunajiskia vizuri. Kumbuka lile bango moja kwenye yale mazishi ya watu waliouwawa kwenye maandamano ya Arusha kuwa "Ni Bora kufa shujaa kuliko kuishi kwa aibu" Haya ni maneno mazito sana. Sijui kama viongozi wameyachukilia vipi maneno haya.
Kipindi chake Nyerere kilikuwa na mambo mengi sana yaliyolikumba Taifa, lakini hakukaa kimya mpaka kupelekea wananchi kuchanganyikiwa kwa kutopata majibu. Alikuwa na taratibu za kuhutubia Taifa kila jambo linapotokea na kutoa ufumbuzi na jambo jema sana kwake ni kwamba pale alipokosea alikiri tena wazi wazi au hadharani.
Tukizungumzia maswala ya uchumi, Nyerere was a complete failure. Hilo halina ubishi wala mjadala kabisa. Lakini pamoja na hilo ninakumbuka alipokataa kuanza kuchimba madini aina mbali mbali nchini kwa kuhofia wananchi kutopata faida ya madini ya nchi au ardhi yao. Hili mpaka leo tunaliona.
Viongozi wamefikiri kuwa wanatawala wakati muafaka kuchimba madini yaliyoko kwenye ardhi yetu lakini matokeo yake wawekezaji wanachukua zile almasi na dhahabu sisi wanatuonyesha vipande vya chupa na mabati kuwa ndivyo walivyopata tunabakia kuchekelea kama mazuzu! Hii ni pamoja na mikataba feki iliyokithiri serikalini. Si Mwinyi, si Mkapa na si Kiwete wataweza kukana hilo maana taifa limeendelea kudidimia kiuchumi baada ya kuanza kumilikisha wageni machimbo ya vito mbali mbali nchini.
MSAMEHENI NYERERE KUNA ALIYOKOSEA LAKINI ALILIPENDA TAIFA LAKE KWA MOYO WAKE WOTE NA AMELIFIA TAIFA. MPENI HESHIMA YAKE. HASWA BAADA YA KUONA WALIOMPOKEA WANAVYOBORONGA.
RIP MWALIMU.