Hii story authenticity yake haijajulikana vizuri, so let's say all with a grain of salt. Lakini nilishawahi kusikia kwamba Kikwete aliondoka Monduli kwa political intrigue na alikuwa hapatani na "real soldiers". So I am not very surprised to hear these details.
1. Probably hapo kulikuwa na political intrigue and ladder climbing kama motive kwa Kikwete.
2. Hata kama 1. ni kweli, Kikwete alichofanya kilikuwa sawa (as much as I don't like him, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni). Huwezi kuwa na Mkuu wa Chuo anayeuzia Chuo chakula kutoka shamba lake, conflict of interest.
3. Inawezekana kabisa Kikwete karuka escalation points kibao katika food chain. Lakini vipi kama aliona katika mfumo wa jeshi kuna kulindana kwingi na hatua hazitachukuliwa? Vipi kama aliona mtu pekee mwenye uwezo wa kumaliza haya ni Nyerere?
4. Nyerere kwa kusema "nendeni kayamalizeni huko huko" bila hata kutoa msimamo wakati anajua jeshi linaenda kwa kulindana na kumpata whistleblower kama Kikwete ni adimu ali abdicate majukumu kama kiongozi.
5. Nyerere kwa kumsaliti whistleblower Kikwete alikiuka maadili, ni kama alikuwa anataka kulindana kuendelee jeshini halafu Kikwete apatwe na mabaya. Kiongozi gani anafuga migogoro na kuacha jeshi ligubikwe na kulindana? Kwa kusema "Nendeni kayamalizeni huko huko" ina maana alikuwa hajali outcome itakuwaje.
Kama hii story ingekuwa imeandikwa kwa nia ya kumpamba Kikwete ningekuwa na mashaka nayo zaidi, lakini kwa sababu imelenga kumpaka matope Kikwete kama "mnafiki" wakati kwa ukweli ukiangalia utaona ali act kama whistleblower aliyekuwa betrayed, kwangu mimi ni moja ya stories chache sana za Kikwete zinazonionyesha Kikwete katika a positive light.
Labda Kikwete ni kiongozi mbovu sasa kwa sababu alivyokuwa kijana zaidi katika siasa alijaribu kuja na moto wa kupinga ufisadi akaona disappointment tu. Mtu unaenda kuripoti ufisadi kwa rais, rais anakusaliti. Akaona ha, kumbe style yenyewe ndiyo hii, ngoja na mimi niwe fisadi tu kieleweke, maana unaweza kujidai unapinga ufisadi ukauawa bure.
I am just saying.