Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hii inaonyesha kama ni porojo - ama mna wakati mrefu wa bure kuandika makala refu hiyo !
Kama ni kweli, je ni halali kwa mkuu huyo wa majeshi kujipa tenda kuuza hapo hapo chuoni?
kwanza yalikuwa kinyume na AZIMIO LA ARUSHA.Kakitabu alikokuwa anatembea nako mwalimi kama ka kitabu ka muongozo wa nchi.
Kwa kufuatilia majadiliano yanayoendelea kuna jambo linanitatiza. Sijui kama sheria za jeshi zimekuwa zikibadilika kwa kiasi gani, lakini kwa wale waliowahi kupitia majeshini tunafahamu kuwa kutoroka au kuondoka jeshini bila taarifa ni gross misconduct. Kama JK wakati huo alikuwa na cheo cha meja, basi ilikuwa ni kosa kubwa zaidi kwa kuzingatia nidhamu za jeshi. Sasa alipofika Dar es Salaam inaonekana alipangiwa kazi Nachingwea, sijui kama kulikuwa na usuluhishi au majadiliano kati ya Sayore, Jk na CDF!! Ikumbukwe kuwa mkufunzi wa siasa jeshini hakukumuondelea hadhi yake kama mwanajeshi!
Taarifa hii inamuonyesha kama Nyerere alikuwa kiongozi muoga wakati haikuwa tabia yake kwamba apate taarifa ya kiongozi bepari na kisha ashindwe kumshughulikia mhusika. Taarifa inaonyesha Nyerere alimtupia mpira Mkuu wa majeshi, Msuguri ili akayamalize mwenyewe.
Kama kuna sababu zilizomfanya Kikwete kuamini kwamba level za chini Jeshini haziwezi kumuwajibisha Sayore, alikuwa justified kwenda kwa Amiri Jeshi Mkuu.
Kikwete was right, and he can even argue that incidents like this proved really discouraging to his reforming zeal. Even if some Machiavellian intrigues were involved.
Kwamba Kikwete was right or not, kunategemea na kujua ukweli wa sentensi yako ya kwanza inayoanza na neno "Kama".
Ndugu,
Naomba nikujuve. Zama hizo makada wa chama walikuwepo jeshini lakini nguvu zao zilikuwa zaidi katika chama na si katika Jeshi.Vile jeshi lilikuwa linachukuliwa lama 'mkoa' wa kichama,. Watu kama Kikwete,Makamba,Chiligati,Kiwanuka n.k. hawakuwa 'career soldiers' bali ni makada wa CCM waliokuwa na kazi ya kuwatia siasa wanajeshi wetu. Sasa inawezekana huyu bwana alimalizia shughuli za kutia siasa kwa mkasa huo na kurudi katika chama makao makuu na kupelekwa Nachingwea na kwa mtazamo wangu uaskari (kama ulikuwapo) uliishia hapo.
Wewe kweli mbumbumbu....Nyerere alifanya hivyo kwa kuwa protocal haikufuatwa...JK wako alitakiwa amwandikie Msuguri au Natepe akiwa kama kamisaa mkuu wa siasa jeshini na haswa ndiye bosi wake na sio Mwalimu
Kuna wakati protocol haifuatwi kama huna imani na bosi wako aliyeko juu yako, kwa mfano Msuguri ndiye alibendekeza jina la Sayore kwa Nyerere kuwa mkuu wa chuo cha monduli hapo huwezi jua imani ya msuguri kwa Sayore. Lakini pia huwezi jua kwamba ule mradi wa Sayore pengine na Mkuu wa Jeshi alishatoa baraka zake. hapa inahitajika mtu mwenye mamlaka zaidi.
Ni kweli walikuwepo makada wa chama, hawa kwanza walikuwa ni askari waliofundishwa siasa pale kivukoni, sio watu wa nje waliovaa magwanda kwa muda fulani.
Pili kufuatana na post iliyopo, JK alikuwa meja wakati huo unaosemekana alitoroka Monduli. Kumbu kumbu zinaonyesha bila kificho kuwa JK ni kanali mstaafu. Kwa maneno mengine hata kama alirudi kwenye chama bado alikuwa mwananjeshi ndiyo maana alipanda cheo kutoka meja kwenda kanali. Ninakumbuka kuwa alikuwa kanali mwanzoni akiwa mbunge(naomba kusahihishwa).
Ni kweli walikuwepo makada wa chama, hawa kwanza walikuwa ni askari waliofundishwa siasa pale kivukoni, sio watu wa nje waliovaa magwanda kwa muda fulani.
Pili kufuatana na post iliyopo, JK alikuwa meja wakati huo unaosemekana alitoroka Monduli. Kumbu kumbu zinaonyesha bila kificho kuwa JK ni kanali mstaafu. Kwa maneno mengine hata kama alirudi kwenye chama bado alikuwa mwananjeshi ndiyo maana alipanda cheo kutoka meja kwenda kanali. Ninakumbuka kuwa alikuwa kanali mwanzoni akiwa mbunge(naomba kusahihishwa).
Hivi kwa nini JK hakushitakiwa kwa kosa la AWOL (Absent without Official Leave) kwa mujibu wa juzuu za JWTZ?