Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

hii inaonyesha kama ni porojo - ama mna wakati mrefu wa bure kuandika makala refu hiyo !
 
nyie watot wa miaka ya 1996 huwezi kujua lolote......baba yangu alikuwepo monduli nyakati hizo na hili lililosemwa hapa n kweli mtupu

umekaa kifitna fitna kama kikwete
 
Kama ni kweli, je ni halali kwa mkuu huyo wa majeshi kujipa tenda kuuza hapo hapo chuoni?

Ni halali katika zama zake, hakukuwa na sheria iliyokataza hilo.

kwanza yalikuwa kinyume na AZIMIO LA ARUSHA.Kakitabu alikokuwa anatembea nako mwalimi kama ka kitabu ka muongozo wa nchi.

ni wazi hujalisoma Azimio la Arusha, hakuna mahali ambapo azimio lilikataza hilo.

`
 
Kwa kufuatilia majadiliano yanayoendelea kuna jambo linanitatiza. Sijui kama sheria za jeshi zimekuwa zikibadilika kwa kiasi gani, lakini kwa wale waliowahi kupitia majeshini tunafahamu kuwa kutoroka au kuondoka jeshini bila taarifa ni gross misconduct. Kama JK wakati huo alikuwa na cheo cha meja, basi ilikuwa ni kosa kubwa zaidi kwa kuzingatia nidhamu za jeshi. Sasa alipofika Dar es Salaam inaonekana alipangiwa kazi Nachingwea, sijui kama kulikuwa na usuluhishi au majadiliano kati ya Sayore, Jk na CDF!! Ikumbukwe kuwa mkufunzi wa siasa jeshini hakukumuondelea hadhi yake kama mwanajeshi!
 
Sayore alipewa kibali na nani kuuza hivyo vitu?
Bila shaka mkuu wa majeshi alihusu hapo na ndio maana alipopewa ile barua na yeye alimpa sayore moja kwa moja na hakuwa na maamuzi mengine.
 
Duh kumbe ndio maana!! Nyerere aliwakataa kabisa waziwazi kina EL lakini jamaa yetu kawapiga kumbatio la kufa mtu. Visasi tu ,ila asiyesekia la mkuu huvunjika guu..atimae EL kwa kashfa nzito ya ufisadi akajiuzulu.
 
Kwa kufuatilia majadiliano yanayoendelea kuna jambo linanitatiza. Sijui kama sheria za jeshi zimekuwa zikibadilika kwa kiasi gani, lakini kwa wale waliowahi kupitia majeshini tunafahamu kuwa kutoroka au kuondoka jeshini bila taarifa ni gross misconduct. Kama JK wakati huo alikuwa na cheo cha meja, basi ilikuwa ni kosa kubwa zaidi kwa kuzingatia nidhamu za jeshi. Sasa alipofika Dar es Salaam inaonekana alipangiwa kazi Nachingwea, sijui kama kulikuwa na usuluhishi au majadiliano kati ya Sayore, Jk na CDF!! Ikumbukwe kuwa mkufunzi wa siasa jeshini hakukumuondelea hadhi yake kama mwanajeshi!

Ndugu,

Naomba nikujuve. Zama hizo makada wa chama walikuwepo jeshini lakini nguvu zao zilikuwa zaidi katika chama na si katika Jeshi.Vile jeshi lilikuwa linachukuliwa lama 'mkoa' wa kichama,. Watu kama Kikwete,Makamba,Chiligati,Kiwanuka n.k. hawakuwa 'career soldiers' bali ni makada wa CCM waliokuwa na kazi ya kuwatia siasa wanajeshi wetu. Sasa inawezekana huyu bwana alimalizia shughuli za kutia siasa kwa mkasa huo na kurudi katika chama makao makuu na kupelekwa Nachingwea na kwa mtazamo wangu uaskari (kama ulikuwapo) uliishia hapo.
 
jamni si mgoogle kujua mashine za kutolea copyzimegunduliwa lini?
kwan zamani kulikuwa na zile za kuzungusha kwa mkono kama zakumenya kahawa,
 
Taarifa hii inamuonyesha kama Nyerere alikuwa kiongozi muoga wakati haikuwa tabia yake kwamba apate taarifa ya kiongozi bepari na kisha ashindwe kumshughulikia mhusika. Taarifa inaonyesha Nyerere alimtupia mpira Mkuu wa majeshi, Msuguri ili akayamalize mwenyewe.
 
Wewe kweli mbumbumbu....Nyerere alifanya hivyo kwa kuwa protocal haikufuatwa...JK wako alitakiwa amwandikie Msuguri au Natepe akiwa kama kamisaa mkuu wa siasa jeshini na haswa ndiye bosi wake na sio Mwalimu
 
Kama kuna sababu zilizomfanya Kikwete kuamini kwamba level za chini Jeshini haziwezi kumuwajibisha Sayore, alikuwa justified kwenda kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Kikwete was right, and he can even argue that incidents like this proved really discouraging to his reforming zeal. Even if some Machiavellian intrigues were involved.

Kwamba Kikwete was right or not, kunategemea na kujua ukweli wa sentensi yako ya kwanza inayoanza na neno "Kama".
 
Kwani yeye JK alijaribu kulima huo mchicha na kuiuzia kambi na akazuiwa? Au ndio uvivu wenyewe wa kikwere,jembe halishikiki?
 
Ndugu,
Naomba nikujuve. Zama hizo makada wa chama walikuwepo jeshini lakini nguvu zao zilikuwa zaidi katika chama na si katika Jeshi.Vile jeshi lilikuwa linachukuliwa lama 'mkoa' wa kichama,. Watu kama Kikwete,Makamba,Chiligati,Kiwanuka n.k. hawakuwa 'career soldiers' bali ni makada wa CCM waliokuwa na kazi ya kuwatia siasa wanajeshi wetu. Sasa inawezekana huyu bwana alimalizia shughuli za kutia siasa kwa mkasa huo na kurudi katika chama makao makuu na kupelekwa Nachingwea na kwa mtazamo wangu uaskari (kama ulikuwapo) uliishia hapo.

Ni kweli walikuwepo makada wa chama, hawa kwanza walikuwa ni askari waliofundishwa siasa pale kivukoni, sio watu wa nje waliovaa magwanda kwa muda fulani.
Pili kufuatana na post iliyopo, JK alikuwa meja wakati huo unaosemekana alitoroka Monduli. Kumbu kumbu zinaonyesha bila kificho kuwa JK ni kanali mstaafu. Kwa maneno mengine hata kama alirudi kwenye chama bado alikuwa mwananjeshi ndiyo maana alipanda cheo kutoka meja kwenda kanali. Ninakumbuka kuwa alikuwa kanali mwanzoni akiwa mbunge(naomba kusahihishwa).
 
Wewe kweli mbumbumbu....Nyerere alifanya hivyo kwa kuwa protocal haikufuatwa...JK wako alitakiwa amwandikie Msuguri au Natepe akiwa kama kamisaa mkuu wa siasa jeshini na haswa ndiye bosi wake na sio Mwalimu

Kuna wakati protocol haifuatwi kama huna imani na bosi wako aliyeko juu yako, kwa mfano Msuguri ndiye alibendekeza jina la Sayore kwa Nyerere kuwa mkuu wa chuo cha monduli hapo huwezi jua imani ya msuguri kwa Sayore na Natepe. Lakini pia huwezi jua kwamba ule mradi wa Sayore pengine na Mkuu wa Jeshi alishatoa baraka zake. hapa inahitajika mtu mwenye mamlaka zaidi.
 
Kuna wakati protocol haifuatwi kama huna imani na bosi wako aliyeko juu yako, kwa mfano Msuguri ndiye alibendekeza jina la Sayore kwa Nyerere kuwa mkuu wa chuo cha monduli hapo huwezi jua imani ya msuguri kwa Sayore. Lakini pia huwezi jua kwamba ule mradi wa Sayore pengine na Mkuu wa Jeshi alishatoa baraka zake. hapa inahitajika mtu mwenye mamlaka zaidi.

Kwa nini hakumjulisha bosi wake Meja Jenerali Natepe? Kwa madai yako kuwa Msuguri pia alihusika mbona hakumshitaki naye kwa Nyerere?
 
Ni kweli walikuwepo makada wa chama, hawa kwanza walikuwa ni askari waliofundishwa siasa pale kivukoni, sio watu wa nje waliovaa magwanda kwa muda fulani.
Pili kufuatana na post iliyopo, JK alikuwa meja wakati huo unaosemekana alitoroka Monduli. Kumbu kumbu zinaonyesha bila kificho kuwa JK ni kanali mstaafu. Kwa maneno mengine hata kama alirudi kwenye chama bado alikuwa mwananjeshi ndiyo maana alipanda cheo kutoka meja kwenda kanali. Ninakumbuka kuwa alikuwa kanali mwanzoni akiwa mbunge(naomba kusahihishwa).

Alikuwa Luteni Kanali alipotoka Monduli na hakupanda tena mpaka leo ni Luteni Kanali...cheo above next kwa Meja
 
Ni kweli walikuwepo makada wa chama, hawa kwanza walikuwa ni askari waliofundishwa siasa pale kivukoni, sio watu wa nje waliovaa magwanda kwa muda fulani.
Pili kufuatana na post iliyopo, JK alikuwa meja wakati huo unaosemekana alitoroka Monduli. Kumbu kumbu zinaonyesha bila kificho kuwa JK ni kanali mstaafu. Kwa maneno mengine hata kama alirudi kwenye chama bado alikuwa mwananjeshi ndiyo maana alipanda cheo kutoka meja kwenda kanali. Ninakumbuka kuwa alikuwa kanali mwanzoni akiwa mbunge(naomba kusahihishwa).

Hivi kwa nini JK hakushitakiwa kwa kosa la AWOL (Absent without Official Leave) kwa mujibu wa juzuu za JWTZ?
 
Mwalimu aliweza kumshughulikia mpambe wake wa harusi (best man) na waziri wake wa nchi za nje, Oscar Kambona hadi akakimbia nchi kwa sababu ya tuhuma za ubepari. Nadhani suala la Sayore lilikuwa dogo sana kwake.
 
Kweli kwenye jamii forum kuna watoto, wafitini, mabinafsi na mabeberu ya kisasa. Yaani mtu alikua anapinga utumwa nyie mnasema mfitini? kama mnachuki binafsi msilete humu, siasa haina urafuki wala undugu kwa sasa mnaweka chuki against JK but kumbuka atakuja Mbowe au Slaa vizuri tu siku akimess up wote mtamchukia binafsi and this is what is happening in Libya.

Tuwe makini sana na tunapotoa comments zetu na tusilete story za vijiweni humu JF. Nikukumbushe tu kuwa JK alimaliza mafunzo yake vyema kabisa (alihitimu). Pia kumbuka kwa kipindi kile shimbo hakuwa Monduli fuatilia vizuri historia ya shimbo, na unapomuita Pimbi maana yake unajiita mwenyewe pimbi mdogo. Kimbuka wakati ule ilikua ukitoka nnje ya kambi ukiacha walinzi wa kambi kulikua na wanyama wakali kama simba na chui katika pori linalozunguka kambi hiyo hata leo kuna ushahidi wa kutosha kuhusu hilo.

Ndugu zangu lets be firm on useful issues and not on gossip na majungu na fitna zisizokuwa na maana kwetu.
 
Back
Top Bottom