Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Wagombea Urais William Ruto kutokea Umoja wa Vyama vya Kenya na Raila Odinga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa Kiongozi ya Timu ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Kenya, ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa nyakati tofauti, amekutana na kufanya mazungumzo na Wagombea Urais William Ruto kutokea Umoja wa Vyama vya Kenya Kwanza, na Raila Odinga wa Umoja wa Vyama vya Azimio la Umoja. Mgombea wa wa Azimio la Umoja Raila Odinga, aliambatana pia na Mgombea wake Mwenza Martha Karua.
 

Odinga ni mzee sana, si apumzike?
 
Odinga ni Kenyata project, akiwa Rais ni sawa sawa na muendelezo wa U Rais wa Kenyatta.
 
Hivi huyu, anaenda kuwafundisha nini Wakenya? Yeye na chama chake si ndiyo mabingwa ya kudhurumu kwenye uchaguzi!!!!?
Hao Wakenya, ndio wanaopaswa kuja kusimamia uchaguzi wetu!
anaenda kusimamia wanachotaka wakubwa wa Dunia nani awe Rais, kwasababu anauzoefu kwenye swala zima la wizi wa kura.
 
UCHAGUZI wa Tanzania Magufuli aliuvuruga Wastaafu wote walikuwa KANDO wote KIMYA
 
Mh. Kikwete kwa wakati huu, ni baba wa siasa kwa nchi za East Africa
 
Hivi huyu, anaenda kuwafundisha nini Wakenya? Yeye na chama chake si ndiyo mabingwa ya kudhurumu kwenye uchaguzi!!!!?
Hao Wakenya, ndio wanaopaswa kuja kusimamia uchaguzi wetu!
Anaenda kuwafundisha wizi wa akili bila wananchi kupigana, mpongeze kwenye hilo kwamba ccm inaiba wazi wazi na bado wananchi wanakubali na maisha mengine yanaenda. "Ona jema katika ubaya" by Amos mwijonge
 
Wanaharibu uchaguzi wa Bongo halafu wanaenda kusimamia uchaguzi wa wenzao !!!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…