Elections 2010 Kikwete apendekezwa na CCM kugombea urais 2010

Elections 2010 Kikwete apendekezwa na CCM kugombea urais 2010

JK kamchagua Dr Billali kama mgombea mwenza, na anacheza muziki kwa sana. Je, anfuraahia kuwa amepata machapakazi au anaonyesha kuwa amemuogopa kutokana na vitisho alivyo toa kama hata mchagua kua mgombea urais wa zanzibar?
 
Qadhi, hawa jamaa ni ma professional kabisa bila mashaka na vyo vya journalism wamehitimu. Tatizo sio hao vijana, tatizo ni wamiliki, Dialo ni kada wa CCM, hivyo unategemea nini, "he who pays the piper may call the tune".

Hata ITV kwenye news za mmiliki, news clip ina dakika zaidi ya 6!. Standard Clip ni dakika 2 ikizidi sana 3 tuu. Professionalism hairuhusu taarifa ya habari ya lugha ya Kiswahili, kuingiza insert ya Kiingereza bila kuifasiri, haya mambo tunayaona kila siku hapo ITV.

TBC nayo siyo State Media tena, ni Public Broadcast, wameshatoa code of conduct yao kuelekea Uchaguzi Mkuu kuwa hawatapokea pesa za chama chochote kujitangaza, watatoa nafasi sawa kwa vyama vyote, hivyo hiki kinachoendelea, sijui ni kitu gani.

Nyie mlio karibu na JK, ukiwemo Mzee Invi, mshaurini, anapiga sana domo, wote wanaomzunguka wanamuogopa, hakuna wa kumweleza, watu tunataka kuona "fainali ya wedikapu!".

Mkuu,nilichokiona kwa hawa anchors:

Kiswahili ni kama lugha ngeni kwao,wana tension ya juu sana,yaani kama vile hawajui baada ya sentesi moja inakuja ipi,ile flow haijatulia na haipo ktk sequence.

Anchors ambae wanasoma ndio unaona kabsaa hawako relaxed,anadonyoa mistari kama vile kuku anadonyoa mpunga,maanake kila baada sentensi moja kaangalia karatasi.Anchors tunawaona huku anaimiliki kazi yake,na anaweza kuleta kionjo chake binafsi kulingana na mazingira bila kuharibu ujumbe wa msingi.Lakini ndugu zetu hawa wanakakamaa utafikiri wako kwenye gwaride.

Anchor anatakiwa aongee na viewer,yaani unahisi mshikaji yuko na wewe pale live.

Hawa wa Star Tv walikuwa wanajaribu kuingizia utani pale kulingana na asili na makabila ya watu,walikuwa wanaishia kutaja mikoa mi 2 tu,na kuishia kuanzisha unrelated issue kabisa.
 
Mkuu,nilichokiona kwa hawa anchors:

Kiswahili ni kama lugha ngeni kwao,wana tension ya juu sana,yaani kama vile hawajui baada ya sentesi moja inakuja ipi,ile flow haijatulia na haipo ktk sequence.

Anchors ambae wanasoma ndio unaona kabsaa hawako relaxed,anadonyoa mistari kama vile kuku anadonyoa mpunga,maanake kila baada sentensi moja kaangalia karatasi.Anchors tunawaona huku anaimiliki kazi yake,na anaweza kuleta kionjo chake binafsi kulingana na mazingira bila kuharibu ujumbe wa msingi.Lakini ndugu zetu hawa wanakakamaa utafikiri wako kwenye gwaride.

Anchor anatakiwa aongee na viewer,yaani unahisi mshikaji yuko na wewe pale live.

Hawa wa Star Tv walikuwa wanajaribu kuingizia utani pale kulingana na asili na makabila ya watu,walikuwa wanaishia kutaja mikoa mi 2 tu,na kuishia kuanzisha unrelated issue kabisa.
Bongo bado hatuna news anchors, tuna news readers. Ila kuna ma anchors wazuri kama huyu Marine Hassan wa TBC, ila hapewi news, namuona kwenye Jambo tuu. ITV, Star TV na Channel Ten, wana ma news readers tuu hawana Anchor Man.

The logic behind kuweka msoma habari zaidi ya mmoja ni ili ku anchor news, ile style ya kuilift news prom the paper into the reality, inaitwa 'presence', msoma habari has to own it, mtazamaji anamsikia kama ni expert anayeijua hiyo habari na kutueleza tusiojua, lakini wasomaji wetu, wanaonesha wanasoma, tena wengine sio tuu unajua wameandikiwa, bali hawana hata uhakika wanasoma nini.
 
alimohammedshein.jpg
DK Shein

Na Ramadhan Semtawa

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohamed Shein jana aliweka bayana kuwa atafanya kampeni zake kistaarabu na kwamba iwapo atashinda kwenye uchaguzi hatakuwa tayari kufanya kazi na mtu ambaye hapendi maridhiano.

Dk Shein pia ameeleza kuwa iwapo atachaguliwa atahakikisha anaendeleza anasimamia amani na utulivu kwa nguvu zake zote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Zanzibar katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

Dk Shein aliibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha kugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM baada ya kupata kura 117, akifuatiwa na mtu aliyekuwa akipewa nafasi kubwa kushinda, Dk Mohamed Ghalib Bilal, aliyepata kuta 54 na ambaye jana alitangazwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Jakaya Kikwete na hivyo kuwa na uhakika wa kushika nafasi ya makamu mwenyekiti.

Akizungumza baada ya kuopewa nafasi ya kuwashukuru wanachama kwa kubebeshwa mzigo wa kuiongoza Zanzibar ambayo bado inahaha kuondoa taswira ya chuki na uhasama iliyotawala siasa za visiwa hivyo kwa muda mrefu, Dk Shein alisema kuwa kampeni zake zitakuwa za kuzungumzia mambo ya msingi.

"Tegemeeni uchaguzi na kampeni za kistaarabu... hatutamgusa mtu wala kumsengenya wala kumsema, tutazungumza masuala ya msingi yanayohusu taifa letu," alisema Dk Shein kwenye mkutano mkuu wa CCM uliofanyika kwenye ukumbi wa Kizota.

Aliongeza kwamba kampeni zake zitajikita katika kueleza mambo ya msingi ambayo yamo kwenye Ilani ya chama hicho kwa kuyafafanua vema kwa wananchi na kuongeza kwamba, hatafanya kampeni chafu.

"Tutahakikisha tunaendeleza na kudumisha mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 , kuhakikisha tunatunza na kuendeleza Muungano wa taifa letu kwa kujitahidi kuondoa kero za Muungano kwa kuwa tunazifahamu," alisema msomi huyo wa masuala afya ya binadamu.

Hotuba ya Dk Shein haikujaa shamrashamra kama zilivyo za viongozi wengine wa chama hicho, na badala yake ukumbi ulitulia kumsikiliza makamu huyo wa rais akielezea jinsi alivyojiandaa kuipeleka Zanzibar kwenye hatua nyingine baada ya kuwashinda wanachama wenzake 10 waliokuwa wanawania urais wa Zanzibar.

Historia ya visiwa hivyo imekuwa ikisababisha siasa ziwe za chuki na uhasama na mara nyingi kampeni hutawaliwa na kejeli, wakati mwingine matusi na tuhuma, lakini Dk Shein aliweka bayana kuwa atajitenga na vitu hivyo vilivyoumiza baadhi ya wananchi wa Zanzibar.

"Zanzibar imepitia kwenye misuguano ya kisiasa wakati fulani... sasa tunataka tuendeleze maridhiano. Mtu yeyote ambaye hatakuwa tayari kwa maridhiano, sitakuwa naye," alisema Dk Shein, akirejea mazungumzo baina ya Rais Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad ambayo yalimalizika kwa kukubaliana kuwepo kwa serikali ya mseto.

Kura ya maoni ya kupitisha suala hilo itafanyika Julai 31 kupitisha mfumo huo wa utawala visiwani Zanzibar ambako mshindi hutofautiana kwa kura chache na mshindi wa pili.

Dk Shein ambaye alikuwa akifafanua mambo mbalimbali ya msingi ambayo ameyaweka kuwa kipaumbele cha serikali yake iwapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar, akiweka bayana kuwa suala la kwanza litakuwa ni kulinda mapinduzi ya visiwa hivyo.

Dk Shein pia alisema katika kampeni zake atahakikisha anashirikiana na wana-CCM wengine 10 ambao aliwashinda kwenye mbio za kuwania urais kwa tiketi ya CCM ili kuhakikisha chama hicho kikongwe barani Afrika kinashinda uchaguzi huo wa Oktoba.

Alisema zipo kazi nyingi za kufanya hivyo ni vema wanachama hao waliokuwa kwenye mbio hizo, wakaunganisha nguvu zao pamoja ili kuwezesha chama kufanikisha programu mbalimbali za ushindi.

"Kwa wale wanachama wenzangu 10 ambao sote tulikuwa katika kutafuta nafasi hii ya kuchaguliwa na chama, huu ni wakati wa kuunganisha nguvu pamoja. Tutaangalia tunapanga vipi ili sote tushiriki katika kampeni hizi," alisema Dk Shein.

Alisema atatoa kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani Zanzibar huku akisisitiza, atachukua yote mema yatakachoachwa na serikali ya Rais Karume.

"Katika kupeleka mbele gurudumu la maendeleo ya Zanzibar, nitachukua yote mema yatakayoachwa na serikali ya Rais Karume, kwa sababu tulimchagua alete maendeleo Zanzibar na Tanzania, kwa hiyo mema aliyofanya tutapaswa kuyaendeleza kwa kuwa hayakuwa yake binafsi," alifafanua.

Awali baada ya kushinda kwenye kura za maoni, baadhi ya wanachama wa CCM waliosafiri kutoka Zanzibar hadi Dodoma, walidai kuwa kushindwa kwa Bilal ni njama na hivyo hawatakuwa tayari kumpigia kura Dk Shein kwenye uchaguzi mkuu.

Lakini baada ya Rais Kikwete kumtangaza Dk Bilal kuwa mgombea mwenza, wafuasi wake sasa watakuwa wametuliza mioyo na kuangalia mbele kwenye kampeni za urais visiwani Zanzibar, ambako CUF imekuwa ikitoa upinzani mkali.

Chanzo Dk Shein: Nitafanya kampeni za kistaarabu

Dk Shein ataweza kupambana na Maalim Seif Sharriif Hamad?
 
Na lazima afanye za kistaarabu ,kwani akijidai tu basi wapemba wenziwe wataanza kutembea na mikasi !!! 😛ound:
 
Na lazima afanye za kistaarabu ,kwani akijidai tu basi wapemba wenziwe wataanza kutembea na mikasi !!! 😛ound:
Lakini hata yeye mwenyewe kwa hulka yake ni mtu mstaarabu. Sitegemei awe tofauti.
 
Ewe mwananchi... ewe Mtanzania mwenzangu. Kabla hujapiga kura yako ya kuchagua ni nani awe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania 2010-2015 jiulize mara mbili mbili? Wagombea wote wa urais NI WAZIMA KIAFYA?

Case 1 - Kikwete (mgombea wa urais):
Nyie ni mashuhuda wazuri. Huyu mgombea ni 'mzoefu' wa kuzirai majukwaani. Japo wasaidizi wake wamekuwa wanakana hana matatizo lakini mhh... kwa nini azimike zimike kama kifaulongo? Hili swali bado hawajaweza kulipatia jibu!

Case 2 - Bilal (mgombea mwenza wa Kikwete)
Kutoka gazeti la Tanzania Daima tunaarifuwa...

ZIKIWA zimesalia takriban wiki sita kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu, afya ya mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mohamed Gharib Bilal, imezua mjadala ndani na nje ya chama hicho, Tanzania Daima Jumatano imebaini.

Gumzo la chini chini juu ya afya ya Dk. Bilal liliibuka ghafla kwa mara ya kwanza kutoka kwa baadhi ya wana CCM wenyewe wakiwamo wabunge na vigogo wa chama hicho, alipojitosa kutafuta tiketi ya kuwania urais wa Zanzibar mwaka huu.

Hata baada ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, udadisi wa kutilia shaka afya ya Dk. Bilal umeendelea kushika kasi miongoni mwa wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini.

Baadhi ya wana CCM waliodai kumjua vizuri Dk. Bilal, kwa nyakati tofauti hawakusita kuelezea hofu yao juu ya afya ya kigogo huyo pindi walipoombwa kutoa tathmini zao juu ya wagombea wa chama hicho waliokuwa wamejitokeza kutafuta tiketi ya kuwania urais wa Zanzibar.

Bila kumng’unya maneno, mbunge mmoja wa CCM kutoka upande wa Zanzibar alisema Dk. Bilal wa sasa si yule wa miaka michache iliyopita, kwani anaonekana amepoteza nuru, amekonda na kunyong’onyea sana kiafya na kusisitiza kuwa ni dhahiri mwanasiasa huyo yupo kwenye msukosuko mkubwa wa kiafya.

Aidha, siku chache kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma, uliowashindanisha wagombea hao na Dk. Shein kuibuka mshindi, mwandishi wetu alifanya mahojiano na kigogo mmoja katika ofisi ndogo ya makao makuu ya chama hicho Lumumba, jijini Dar es Salaam, ambaye naye alitoa maoni yaliyotilia shaka afya ya Dk. Bilal.

“Unajua kuna mambo mawili ya kutazama hapa, kuna suala la nani atawafaa zaidi Wazanzibari kimaendeleo na suala la yupi ataweza kushinda huo urais kwa urahisi zaidi. Kwa vigezo vyote hivyo, Shein sioni kama atafaa…maana kwa nafasi kubwa ya umakamu hakuwafanyia lolote la maana Wazanzibari, yeye na mwenzake Nahodha hakuna mwenye jipya kwa Wazanzibari na Wazanzibari wanalielewa hilo. Lakini pia Shein si mwanasiasa, ni mpole sana na hana umaarufu wa kutosha katika siasa za Zanzibar.

“Pale mtu ambaye angewafaa Wazanzibari ni Dk. Bilal, lakini afya yake inatia wasiwasi, amechuja mno miaka ya hivi karibuni, we chukua picha yake ya mwaka 2005 alipotaka urais na hizi za sasa, utaona kuwa amekongoroka sana, sasa uongozi pia unataka afya,” alisema kigogo huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake.

“Kikwete asipoangalia safari hii ataangushwa na huyu mwenzie, huyu mzee anaonekana kabisa afya yake ni mgogoro, hakuwa hivi huyu, hivi huko CCM ukishakuwa mtu wa juu, basi ni kupeana vyeo tu hata kama watu wako hoi namna hii?” alihoji kijana mmoja aliyekuwa akitazama habari moja gazetini, iliyotoka na picha ya Dk Bilal kwenye meza moja ya kuuzia magazeti kituo kidogo cha mabasi Ubungo.

Hata hivyo, gazeti hili lilifanikiwa kufanya mahojiano maalumu kwa njia ya simu na Dk. Bilal juzi, ambapo alielezea kushangazwa kwake na kuenea kwa mijadala hiyo ya chini chini kuhusu kutetereka kwa afya yake.

“Kumbe hili suala la kuwa mgombea mwenza limekuwa zito eeh…...(kicheko),” alisema Dk. Bilal.
Alisema kabla hata ya kuamua kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar, alikwenda kupima afya yake na majibu aliyopata yarimridhisha kabisa kuwa hana matatizo kiafya.

“Kabla sijagombea nilikwenda for a medical check up na sina matatizo kiafya, niliridhika kabisa,” alisema Dk. Bilal.

Kwa upande mwingine, alipoulizwa ni mambo gani alikusudia kuwafanyia Wazanzibari iwapo angepitishwa na CCM na hatimaye kushinda uchaguzi na kuwa rais wa visiwa hivyo, alitoa jibu moja tu:
“Yote niliyotaka kuyafanya Zanzibar nitamwambia mgombea wetu Dk. Shein, atayafanya na mtaona.”

Alipoulizwa zaidi ni kipi atawafanyia Wazanzibari ikiwa watashinda na yeye kuwa makamu wa rais, alisema: “Katiba ya nchi imeainisha kazi zote za makamu wa rais, lakini kama mnataka kujua zaidi kile nitakachowafanyia Wazanzibari na hata wa Bara, basi hayo yamo kwenye ilani yetu ya uchaguzi tutakayoanza kuinadi kampeni zitakapoanza rasmi.”

TAFAKARI... CHUKUA HATUA KABLA HUJACHELEWA!!!!
 
mhhhhh-hapa pagumu saaana,mi nasubiria kampeni maana cwezi kuhukumu,kwani hata mungu anasema usihukumu hautaukumiwa
 
Sio swala la kuhukumu yakhe..... ila ni kuchukuwa tahadhari...... kwani dalili za mvua ni....
Unajua katika nchi zetu za dunia ya tatu, kuongelea afya ya mtu/kiongozi imekuwa kama 'taboo'. Lakini ukweli ni kwamba afya/kifo cha binadamu yeyote sio 'by product' ya maneno wanayozungumza watu...
 
Ewe mwananchi... ewe Mtanzania mwenzangu. Kabla hujapiga kura yako ya kuchagua ni nani awe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania 2010-2015 jiulize mara mbili mbili? Wagombea wote wa urais NI WAZIMA KIAFYA?

Case 1 - Kikwete (mgombea wa urais):
Nyie ni mashuhuda wazuri. Huyu mgombea ni 'mzoefu' wa kuzirai majukwaani.
Madaktari walituhakikishia kuwa ni mzima, HANA UKIMWI isipokuwa ni mgonjwa wa AKILI
 
Dr. Bilal alicheck na afya ya akili yake? Je, afya ya akili ya JK iko safi pia? Maanake mwili uendeshwa na ubongo, kama kuna shida upstairs matokeo yake ni kubisha hata vitu vya maana na msingi na kutoa maneno yasiyo na kichwa wala miguu kama eti foleni DSM ni moja ya dalili za maisha bora kwa kila mtanzania na kukua kwa uchumi!!
 
Mimi nataka kuona wakifanya mdahalo wa pamoja, tuone wakitetea hoja zao. Tumsikilize na Mh. Kikwete akijibu maswali kutoka kwa wananchi na wasomi juu ya uongozi wake na matarajio na mikakati yake katika miaka mitano ijayo akipata huo urais. Jiunge nasi katika kupigania kufanyika kwa huo mdahalo; Campaign for Presidential Debate in Tanzania 2010 | Facebook

Saa sijui hii debate unataka iwe kwa msaada wa watu wa Marekani? Nenda toa pledge na kuwa tayari kuchangia huu mdahalo. Vitu vizuri huwa haviji kiraisi namna hiyo
 
nimesoma habari yote sijaona mahali maradhi yanayomsumbua dr. bilali yametajwa ama jamabo lolote la kitabibu limezungumzwa. nilichoona ni hisia kuwa katika miaka aliyokuwa nje ya siasa uzee umeongezeka.!!!

sasa hapo napata shida sana na uandishi wa habari wa tanzania. ina maana mlitegemea binadamu abaki kuwa vilevile katika kipindi cha miaka zaidi ya 10? asizeeke? kwani anampiikia Mungu chai? kuzeeka si maradhi na wala dhambi ni jambo la asili na hutokea bila msukumo wowowte na hakuna njia ya kuzuia... tusilemazwe na chuki dhidi ya ccm hadi tukakaribia kukufuru.

tz daima si gazeti la kusoma kila kinachoandikwa humo. habari yenyewe inaonekana ya kutunga tu, tena na mtu aliyejifungia chumbani!! aibu tupu kwa uandishi wa aina hii!!
 
mmmh..! hapo pagumu kucoment,mana hatuna taarifa rasmi za madaktari.
 
Back
Top Bottom