Elections 2010 Kikwete apendekezwa na CCM kugombea urais 2010

Elections 2010 Kikwete apendekezwa na CCM kugombea urais 2010

Nadhani wanatafuta mzanzibari mkristu ili kubalance...... sasa nani yuko kule eeeee, ahaaa Mwakanjuki au Issac Sepetu!!!!!
 
Hivi hawa watangazaji wa Star Tv ni professional anchors/presenters/journalists kweli.???????...maana wanajing'atang'ata tu hapa.
Safari ndeeefu sana tunayo.
Qadhi, hawa jamaa ni ma professional kabisa bila mashaka na vyo vya journalism wamehitimu. Tatizo sio hao vijana, tatizo ni wamiliki, Dialo ni kada wa CCM, hivyo unategemea nini, "he who pays the piper may call the tune".

Hata ITV kwenye news za mmiliki, news clip ina dakika zaidi ya 6!. Standard Clip ni dakika 2 ikizidi sana 3 tuu. Professionalism hairuhusu taarifa ya habari ya lugha ya Kiswahili, kuingiza insert ya Kiingereza bila kuifasiri, haya mambo tunayaona kila siku hapo ITV.

TBC nayo siyo State Media tena, ni Public Broadcast, wameshatoa code of conduct yao kuelekea Uchaguzi Mkuu kuwa hawatapokea pesa za chama chochote kujitangaza, watatoa nafasi sawa kwa vyama vyote, hivyo hiki kinachoendelea, sijui ni kitu gani.

Nyie mlio karibu na JK, ukiwemo Mzee Invi, mshaurini, anapiga sana domo, wote wanaomzunguka wanamuogopa, hakuna wa kumweleza, watu tunataka kuona "fainali ya wedikapu!".
 
Kikwete na bilali lazima washindwe tu hawa nyie subirini
 
Ah.. si alisema haya maelezo mareeefuuu atayachapisha???? Tutajie huyo jamaa basi.. wedikap karibia inaanza!!
 
Naona Shamra shamra za Wedi Kapu zianendelea tutaendelea kuwapasha kupitia Jukwaa hili hili
 
Timu zinakaguliwa hapa,namuona Zuma, sep blatter, Hayatou ( Rais wa CAF) wanakagua timu tayari kuanza mtanange! Nyinyi endeleeni na li CCM lenu
 
Timu zinasalimiana hapa, naona JK bado anapiga porojo wakati wananchi wanataka kuangalia Mtanange
 
ni BILALI ndio mwenza....may be itapunguza tension za Wazenj au Makundi CCM ZNZ.
 
Back
Top Bottom