Hivi hawa watangazaji wa Star Tv ni professional anchors/presenters/journalists kweli.???????...maana wanajing'atang'ata tu hapa.
Safari ndeeefu sana tunayo.
Qadhi, hawa jamaa ni ma professional kabisa bila mashaka na vyo vya journalism wamehitimu. Tatizo sio hao vijana, tatizo ni wamiliki, Dialo ni kada wa CCM, hivyo unategemea nini, "he who pays the piper may call the tune".
Hata ITV kwenye news za mmiliki, news clip ina dakika zaidi ya 6!. Standard Clip ni dakika 2 ikizidi sana 3 tuu. Professionalism hairuhusu taarifa ya habari ya lugha ya Kiswahili, kuingiza insert ya Kiingereza bila kuifasiri, haya mambo tunayaona kila siku hapo ITV.
TBC nayo siyo State Media tena, ni Public Broadcast, wameshatoa code of conduct yao kuelekea Uchaguzi Mkuu kuwa hawatapokea pesa za chama chochote kujitangaza, watatoa nafasi sawa kwa vyama vyote, hivyo hiki kinachoendelea, sijui ni kitu gani.
Nyie mlio karibu na JK, ukiwemo Mzee Invi, mshaurini, anapiga sana domo, wote wanaomzunguka wanamuogopa, hakuna wa kumweleza, watu tunataka kuona "fainali ya wedikapu!".