Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge

Msijaribu kupotosha umma, huo ni uongo na ufisadi. Hivi mnapata raha gani mnaposema uongo?? Kwanini tunashindwa kujadidi issue na ukweli wenyewe. Tuwache udini na chiku zisizokua na msingi!!


Kwa hiyo tuogope kusema kama tunaona kuna chembe za rasilimali za taifa kutumika kunufaisha watu kifamilia zaidi? Kwani unafikiri ni siri kwamba Mama Meghji ni mkwe?

Hebu niambia kama kweli meghji na mwanamke mchapakazi kwani nini kwa zaidi ya miaka 35 haendi jimboni kugombea? Kwa nini asubiri kutunukiwa ubunge?

Mbona Halima Mdee kaenda jimboni? Mbona wana Kawe wamemtosa mgombea wa CCM na NCCR na kumpa mwanadada Halima Mdee? Tena jimbo la Kawe lenye changamoto nyingi?

Kwanini Meghji asiende kugombea jimboni? Kweli miaka 35 ya kuwa mbunge wa kutunukiwa hajapata ujasiri wa kwenda kugombea?

Au kuna kingine ambacho watanzania hatukijui na hatukioni ambacho Mkuu wa Kaya anakiona? Na vipi kuhusu uhusiano wake na kigogo mmoja mkubwa? Je uteuzi wake umefuata merits? Hicho ndo tunachokijadili hapa!!
 


Kwa mara ya kwanza mkuu umeongea pointi. Thx.
 
Hiki kipindi ni cha lala salama, hiyo ya maam'kwe ni cha mtoto subiri all stars watangazwe:deadhorse:
 
huyo mwingine ni mpya katokea wapi? Prof Makame mnyaa Mbarawa, nani ana cv yake?

Makame Mnyaa Mbarawa
mechanical engineer, researcher

Location: Pretoria
Country: South Africa
Makame Mnyaa Mbarawa is recognized in Marquis Who's Who.:tape:
 

Wewe na wenzako ndio mliosema kuwa zakia ni mama mkwe, sasa unaruka ruka nini?? Wewe ulichojadili ni kuleta uongo kuwa Zakia ni mkwe, sijaona wapi umejadili kingine. Ingekua jambo la hekima kama ungeweza kusema ukweli uliodanganya, au kuthibitisha madai yako. It is that simple!
 
Makame Mnyaa Mbarawa
mechanical engineer, researcher

Location: Pretoria
Country: South Africa
Makame Mnyaa Mbarawa is recognized in Marquis Who's Who.:tape:

Kwenye uchaguzi wa mwaka huu;wapiga kura wamemnyang'anya Rais JK na CCM yake majimbo zaidi ya 20 ya Uchaguzi waliyokuwa wanayashikilia;na sababu moja wapo kubwa ni hii ya ukubwa wa serikali yake lkn BADO HAJASIKIA NA ANAENDELEA KUITANUA SERIKALI!

Kuteua hata Mbunge mmoja tu ni kuiongezea serikali gharama kubwa za uendeshaji ZISIZO NA ULAZIMU WOWOTE lkn yeye hadi sasa kateua watatu na likely atazidi kuteua zaidi;Mwaka 2015 huu ni ushahidi mwingine kama CCM bado hawajifunza kwa kichapo cha mwaka huu!
 

Inawezekana siyo kweli kwa mila zetu huwezi kumpa mkweo bega...au hapa alikuwa hajaoa maana huyo jamaa kushoto sasa hivi mvi kuliko EL

 

ivi hii directorate sijui takataka gani ya ikulu, hii kuchanganya kiswahili na kiingereza ndo nn?? juu kiingereza chini kiswahili kwani hawawezi weka kiswahili koote??au ndo sheria??ovyoooo!!!!
 
ivi hii directorate sijui takataka gani ya ikulu, hii kuchanganya kiswahili na kiingereza ndo nn?? juu kiingereza chini kiswahili kwani hawawezi weka kiswahili koote??au ndo sheria??ovyoooo!!!!

Halafu barua ilikuwa ina mwadress nani? Umma au ofisi ya RAIS?Hata kuandika barua tumeshasahau jamani?
 
Inawezekana siyo kweli kwa mila zetu huwezi kumpa mkweo bega...au hapa alikuwa hajaoa maana huyo jamaa kushoto sasa hivi mvi kuliko EL


Safari, najua kwa mila zetu mtu mzima kukubali makosa inakua kazi kidogo. Tuachie hapo!! Ahsante kwa picha
 
:A S cry: so, tumtarajie kuwa waziri wa sayansi teknolojia na elimu ya juu??
 
umesahau wengine

Dkt JK
Dkt Mkapa
Nk
 

William, nimekusoma. Lakini naomba uwe mkweli katika mjadala. Sio kweli Zakia aliondoka kwa kashfa, kama ulivyoweka hapo juu. Jaribu kuwa mkweli....wewe ni CCM kama sikosei. Wewe uko kundi gani??? Kwanini chama chenu kinakosa nguvu sasa ? Je ni uchu wa madaraka sababu moja wapo? Ni uongozi mmbovu wa katibu na mwenyekiti wake?
 
:nono: Kwani kuna siri, nani hajui? kamwulize Mama Meghji au JK atakueleza. Is is such a shame
 
Hongera zao....mambo mengine mjengoni huko mkafanye kazi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…