Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki


Maneno haya ungelianza kumwambia aliyeanza na tambo la kujiita yeye wakili ndio uje kunieleza mie. Legal method and jurispudence haijibu hoja ya kwanini sheria ya ndoa ya Tanzania iko monogamous wakati tanzania tuna both monogamous and polygamous marriages. Mie na Family Law nimeisoma mwaka wa kwanza na nikaja kuisoma tena kwa undani mwaka 2. Kuna mapungufu mengi katika sheria ya ndoa ambayo serikali inakosa weledi wa kuyarekebisha. Mfano nimetoa katika Sheria ya ndoa inasema waislamu wataozeshwa na kadhi. Baadae ikaja kubadilika na kuwa sheikh wa mtaani. Fahamu kuwa ndoa ni mkataba na iwapo mmoja katika wanandoa wanataka kuachana basi breach of contract. Sasa wakati wenzetu wana taasisi zao za ndoa zinazotambulika waislamu hawana. Tumeomba mahakama ya kadhi mnapiga dana dana na kujiuma. Matokeo kuna mikesi kibao imerundikana mahakamani ya waislamu kuhusu ndoa, mirathi na talaka serikali haina cha kuwajibu.

Ila serikali kuingia mkataba na taasisi za kidini na kuwalizimisha wananchi walipe taasisi ya kidini ni sahihi kwa mujibu wa fikra zenu duni. To me this is too low maana kama ilivyo Rwanda mnaona sahihi mambo yanayofanyika kupendelea kanisa wakati ni hatari kwa taasisi ya kidini kufanya shughuli za serikali ya secular. Worse enough jambo linalowasaidia waislamu na mustakabali wa maisha yao hamlitaki. Nishawahi kuwaambia na narudia tena St. Augustine (kama hamumjui ni mmoja katika wanafalsafa wa sheria) alishasema neno lake maarufu akisema an unjust law is similar to lawlessness. Hivyo sheria zenye upendeleo wa jamii fulani ni kama hakuna sheria kabisa. Mkandara na mie waropokaji ila iko siku mtayakumbuka maneno yetu. Nilikuwapo!!!
 
Hapo kwenye bold.......... HIVI SHUGHURI HIZO ZINAFANYWA NA WAKRISTO PAKEE..??
 

Sidhani kama unajua unachokiongea katika hili kwani unachanganya mambo. Unajichanganya sana. Unasema serikali inatambua ndoa za aina mbili mke na mume mmoja (monogamous) na wake wengi (polygamous). Halafu unasema inatoa kipaumbele kwa ndoa ya mke mmoja. Kipengele kipi? Ooh, "lakini ukiisoma sheria what is a priority for the government is monogamous marriage na ndio inayotambulia na serikali. Polygamous marriage inachukuliwa kipengele sawa na traditional marriages in Tanzania."
Jibu langu kwako ni kuwa ni kutokujua au kuchanganya sifa kubwa ya ndoa hizo. Ni kuwa ndoa za aina hiyo "ZAWEZA KUWA ZA WAKE WENGI." Hakuna kipengele kinachosema kuwa ndoa ya mke na mume mmoja ndiyo bora kuliko ya zile ambazo zaweza kuwa za wake wengi.
Kuhusu Bodi za Usuluhishi. Sheria inasema wazi kuwa zinaanzishwa na Waziri kwa tangazo la serikali na mara nyingi ziko chini ya watu wa Ustawi wa Jamii. Uzoefu wangu Mahakamani umeonyesha kuwa Bakwata wanafanya jukumu la usuluhishi na barua yao juu ya kufanikiwa au kutofanikiwa kwa usuluhishi hutumika kama ushahidi katika kesi za talaka. Kuhusu sheria kusema kadhi na wakati mitaani hawako hiyo ni hoja ambayo inatakiwa ifanyiwe kazi kuhakikisha kuwa mfungishaji wa ndoa za Kiislamu lazima apewe jina la kadhi. Ushauri wangu rahisi ni kuwa waweza kufungua kesi mahakamani kutaka tamko la mahakama kuwa wafungishaji za ndoa za kiislamu wawe na cheo cha kadhi kama ambavyo Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inatamka. Huo ni mchango mzuri.

Ninatofautiana na wewe unaposema kuwa sheria za ndoa za Tanzania ni za kidini (kwa maana ya ukristu) kwani kama ingekuwa hivyo tungekuwa na viongozi wa kikristu ambao wangekuwa wanahukumu kesi hizo. Sheria ya ndoa inatambua talaka Kanisa Katoliki halitambui. Licha ya upinzani huo wa Kanisa mamia kama sio maelfu ya Wakatoliki wanapata talaka Mahakamani na Serikali inatambua hilo.

Kuhusu watoto wa mitaani ni wa aina zote na siku hizi ni wa makabila na dini zote. Kwa kweli chanzo cha tatizo hilo si mirathi tu, ni mfumo wa soko, kukosekana kwa nafasi za kujikimu na kujiendeleza katika nchi yetu. Katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 40 ya vijana wake hawana kazi, unategemea nini? Ni kuparanganyika kwa mfumo wa kiuchumi na kijamii na kuwafanya wanadamu waishi maisha dhalili. Nadhani unazungumzia kitu kingine wala si dalili na chanzo cha tatizo. Ni lazima tupambane kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Kitanzania bila kujali rangi, dini, kabila, eneo, au umbo lake anathaminiwa na kuwa na nafasi ya kujiendeleza kwa kikomo cha vipaji alivyopewa na Mwenyezi Mungu.

Kuhusu kusoma napenda nikuhakikishie kuwa kama msomi kwako ni mtu mwenye digrii tatu au zaidi nami nimo katika kundi hilo. Sasa kama unataka kusema inategemea kuwa umesomea wapi? Nitakujibu lakini ukifanya google search utapata jibu kwani Rugemeleza ni jina langu la kwanza na huwa sifichi utambulisho wangu. Ninajiamini na simuogopi kiumbe yeyote aliyeumbwa na Mungu wetu isipokuwa yeye Mungu ambaye pia ninamuabudu na kumtukuza, hivyo sina sababu ya kuficha utambulisho wangu au kuogopa kuwakera watu fulani na hivyo kukitia mchanga kitumbua changu.
 
wakristo bana watatetea kila kitu kinachofaidisha kanisa hata kama ni hela za kuiba, kunyang'anya etc..

No wonder ni kichaka cha wanasiasa mafisadi kama EL wanaitumia sana

hongerani kwa kutetea uwizi as long it benefits church..iko siku miradi inayotumia kodo za waislamu zitawatokea puani..
 

Kinachonifanya nikuambie hivyo ni kuona kuwa uelewa wako wa Sheria sio wa mtu aliyesoma sheria na namna ya kuisoma na kuitafsiri. Uchambuzi wangu wa sheria ni jinsi sheria yetu inavyosema sasa. Ndoa zote ziwe za Kikristu, Kiislamu au za Kitamaduni ni sawa mbele ya sheria. Mahakama zetu ndizo zenye haki ya kutoa talaka. Talaka inaruhusiwa kwa dini ya Kiislamu, na kitu kigumu kwa Wakristu, lakini Serikali iliamua kuwa talaka ni haki na inatolewa. Hiki ni kikwazo kwa Wakristu lakini hawana ujanja kwani serikali inasema haifungamani na dini na huo ndio uamuzi wake kwani kimila na kiislamu talaka inatolewa kwa utaratibu wake. Udhaifu wa sheria hiyo ni vizuri kuusema, lakini sikubaliani na kauli kuwa Sheria hiyo inapendelea ndoa za mke mmoja au ndoa za wakristu na kuonea za Waislamu.

Nimeendesha kesi za mirathi ikiwepo ya Mama mmoja wa Kikristu aliyeghushi hati ya cheti cha ndoa akidai kuwa mwanamume mkristu na yeye, walifunga ndoa ya wake wengi. Wakati ndoa ya kwanza ilikuwa ni ya mke mmoja Mwanamume Mkristu na Mwanamke Mwislamu. Mwanamke Mwislamu hakutoa idhini ya kubadilishwa ndoa hiyo kuwa ya wake wengi. Mwanaume (Marehemu) aliacha fedha benki mwaka 1994 shilingi bilioni moja na milioni mia tatu (1.3bn). Huyo Mama Shangingi la Kikristu alishindwa Mahakamani kwani hati ile ilionekana ni ya uongo na hapakuwepo na uthibitisho wa kugeuzwa kwa ndoa hiyo kuwa ya wake wengi. Hiyo haimaanishi kuwa ndoa ya mke mmoja inapendelewa bali chaguo la wanandoa la ndoa ya mke mmoja lazima liliheshimiwa.
 
Ndugu,kwanza tutofautishe serekali na watendaje wa serekali;
Serekali bila watendaji; huu ni mfumo wa utawala wa nchi utakaotumiwa watendaji watakapopatikana kufuatana na utaratibu uliomo kwenye mfumo huu.
watendaji wa serekali; hawa ni watu wanao tawala/kuongoza kufuatana na miogozo ya kiutendaji iliyomo kwenye mfumo waserekali husika.ikumbukwe kwamba watendaji wanauhuru wa asilimia mia ya kujiunga na dini na kutumikia dini yeyote wapendavyo bila ya kuvunja (a) sheria ya nchi (b) kanuni za uongozi/utawala ikiwa wamo serekalini.

sasa naamini utaelewa maana hii:serekali kutokuwa na dini maana yake ni kutofungamana/kuipendelea dini yeyote dhidi ya nyingine zozote.

Pia ukumbuke kuwa serekali ina wajibu wa kushirikiana na taasisi yoyote ya kidini au la, katika shughuli yoyote ya kimaendeleo.kwa haya basi msimhukumu Jk kwa ajili ya wakatoliki.
hawajamaa wanastahili hayo kwa maana unachokionaleo walikiona siku nyingi sana.Wanashirika zima kazi yake ni miradi ya maendeleo duniani na linaangalia nchi nzima in details(Country resource analyisis), ukikaa nao (watu washirika hilo) wanaweza kukwambia resource iloyoko mahali ambapo hata wizara husika sio tu haina kumbukumbu bali haijui. tujifunze kwao japo imani yao ni tofauti na zetu.
nawasilisha
 
Mbona upande wa afya hauoji? Ni hospitali ngapi zimejengwa na madhehebu ya dini,na nyingi zaidi na bora ni zile zilizojengwa na kuendeshwa na madhehebu ya kikristu:yawn:
 
wakati waslam wanaandamana kudai kudhulumiwa na wakristo....wakristo wapobize kuwapatia umeme ili waondokane na giza...so funny huh...
 
wakati waslam wanaandamana kudai kudhulumiwa na wakristo....wakristo wapobize kuwapatia umeme ili waondokane na giza...so funny huh...

Umeongea zaidi mimi sina cha kuongeza vinginevyo nisije haribu falsafa nzuri uliyoandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…