Hahaha ahahaha! Yaani hoja ya umeme vijijini sasa tunatambiana kusoma ndani ya the top 50 universities in the world? Mkuu huo ni ulimbukeni na uthibitisho kwamba elimu yako ni ya mashaka na ya kuunga unga. Kwa nini hujiamini kiasi hicho ndugu yangu???. Sasa naelewa kwa nini umekubuhu kushusha pumba kila kukicha. Humu tunajadili hoja na si nani kasoma nini na wapi. Hayo ni mambo ya vijiweni na si JF.
That is too low mkuu, humu tunasomana maandishi wala hakuna haja ya kufahamiana wewe ni nani na umesoma nini. Ni wajinga wajinga tu wanaweza kutishwa na eti fulani kasoma wapi!!
Alichosema Rugemeleza ni hiki hapa chini:
Sasa ghafla mkuu badala ya kujibu hoja unakimbilia kwenye premise ya kusoma degree zaidi ya tatu kwenye top 50 universities in the world. Poor you. Kutokufahamu usichofahamu si kosa na wala si kukosa hadhi. Hakuna anayefahanu au aliyesomea kila kitu. Sasa mkuu nadhani kwa sababu ya kupenda ligi na kulazimisha kuaminiwa unaingiza mambo tofauti kabisa. Kweli Tanzania zaidi ya uijuavyo.
Maneno haya ungelianza kumwambia aliyeanza na tambo la kujiita yeye wakili ndio uje kunieleza mie. Legal method and jurispudence haijibu hoja ya kwanini sheria ya ndoa ya Tanzania iko monogamous wakati tanzania tuna both monogamous and polygamous marriages. Mie na Family Law nimeisoma mwaka wa kwanza na nikaja kuisoma tena kwa undani mwaka 2. Kuna mapungufu mengi katika sheria ya ndoa ambayo serikali inakosa weledi wa kuyarekebisha. Mfano nimetoa katika Sheria ya ndoa inasema waislamu wataozeshwa na kadhi. Baadae ikaja kubadilika na kuwa sheikh wa mtaani. Fahamu kuwa ndoa ni mkataba na iwapo mmoja katika wanandoa wanataka kuachana basi breach of contract. Sasa wakati wenzetu wana taasisi zao za ndoa zinazotambulika waislamu hawana. Tumeomba mahakama ya kadhi mnapiga dana dana na kujiuma. Matokeo kuna mikesi kibao imerundikana mahakamani ya waislamu kuhusu ndoa, mirathi na talaka serikali haina cha kuwajibu.
Ila serikali kuingia mkataba na taasisi za kidini na kuwalizimisha wananchi walipe taasisi ya kidini ni sahihi kwa mujibu wa fikra zenu duni. To me this is too low maana kama ilivyo Rwanda mnaona sahihi mambo yanayofanyika kupendelea kanisa wakati ni hatari kwa taasisi ya kidini kufanya shughuli za serikali ya secular. Worse enough jambo linalowasaidia waislamu na mustakabali wa maisha yao hamlitaki. Nishawahi kuwaambia na narudia tena St. Augustine (kama hamumjui ni mmoja katika wanafalsafa wa sheria) alishasema neno lake maarufu akisema an unjust law is similar to lawlessness. Hivyo sheria zenye upendeleo wa jamii fulani ni kama hakuna sheria kabisa. Mkandara na mie waropokaji ila iko siku mtayakumbuka maneno yetu. Nilikuwapo!!!