@Mkandara, labda tukuabaliane kwanza kwamba ni kitu gani hasa kinaifanya serikali/nchi iwe ina dini, au secular? Kwa uelewa wangu ni sheria mama yaani Katiba. Katiba ndiyo inayotoa mwongozo kwamba nchi itaendeshwaje na haki za watu ni zipi etc etc.
Na ili mtu awe ametenda kosa ni lazima kwenye sheria mama kuwepo na kifungu kinachosema hivyo. Kwa mfano nchi zinazongozwa na SHARIA kama IRAN na Saudia, ndani ya sheria zao wanaruhusu watu wa dini nyingine kuabudu kivyao (with specific instructions). Pombe ni haramu na ukikamatwa unakunywa pombe hadharani hata kama wewe ni mkristo utachukuliwa hatua kwa sababu sheria za nchi hazirusuhu. Kama watakufumbia haimanishi hujavunja sheria maana sheria ipo inayokataza kufanya hivyo.
Hivyo basi, ili kuwepo na kosa, lazima katiba iwe imetamka kwamba kufanya jambo fulani ni kinyume na sheria za nchi. Sasa ni kifungu gani cha sheria kinachokataza serikali kushirikiana na taasisi za dini katika kutoa huduma za jamii?