@Mkandara, labda tukuabaliane kwanza kwamba ni kitu gani hasa kinaifanya serikali/nchi iwe ina dini, au secular? Kwa uelewa wangu ni sheria mama yaani Katiba. Katiba ndiyo inayotoa mwongozo kwamba nchi itaendeshwaje na haki za watu ni zipi etc etc.
Na ili mtu awe ametenda kosa ni lazima kwenye sheria mama kuwepo na kifungu kinachosema hivyo. Kwa mfano nchi zinazongozwa na SHARIA kama IRAN na Saudia, ndani ya sheria zao wanaruhusu watu wa dini nyingine kuabudu kivyao (with specific instructions). Pombe ni haramu na ukikamatwa unakunywa pombe hadharani hata kama wewe ni mkristo utachukuliwa hatua kwa sababu sheria za nchi hazirusuhu. Kama watakufumbia haimanishi hujavunja sheria maana sheria ipo inayokataza kufanya hivyo.
Hivyo basi, ili kuwepo na kosa, lazima katiba iwe imetamka kwamba kufanya jambo fulani ni kinyume na sheria za nchi. Sasa ni kifungu gani cha sheria kinachokataza serikali kushirikiana na taasisi za dini katika kutoa huduma za jamii?

Hapana mkuu wangu umekosea sana kwa kuchagua vile visivyofuatwa..Na wala nchi inapokuwa na dini haina maana watu wanalazimishwa kufuata ndio iwe maana ya serikali kuwa na dini. Unaweza kwenda kusali ama kutokwenda kusali hata ktk nchi yenye mfumo wa kidini..Iran wanaongozwa na serikali yao ya dini, lakini mkristu na Jews wanaendesha imani zao hawalazimishwi ya Uislaam.
Hivyo vipo vinavyowezekana ama kutowezekana, wala sii swala la kula nguruwe au kutokula ndio dini, dini ni imani ya kiroho ambayo serikali yetu haiwajibiki kufuata values zake. Na inapoweka muafaka na kanisa ndio kabisaa inaondoa hata fikra za kwamba sera (policies) hulenga kuweka sheria na fursa kwa vyombo vyote vya aina hiyo. Kazi ya serikali ni kuunda sera (policy) ambayo inawawezesha wote wenye kujihusisha na shughuli hiyo kujua haki zao sio chombo kimoja na vingine viombe vitapewa..Hii imekuwa kutafuta mapenzi au nini?
Sisi tutafuata tafsiri ya katiba yetu kulingana na hali halisi. Joint partnership baina ya serikali na kanisa haiwezi kuondoa ukweli kwamba serikali imekiuka katiba. Huwezi kuindoa serikali ndani ya mradi wa kanisa wala kanisa ktk mradi huo na maamuzi wanayafanya kamati ya kanisa wakati fedha za wananchi zinatumika kuendesha mradi huo. Wewe nambie sababu ya kukataa OIC au mahakama ya kadhi kwa kutumia mifano yako hapo juu..