Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki

Mkuu nilikuwa nakuheshimu sana ...lakini huu unafiki umezidi!! Ndiyo maana FaizaFoxy na Mohamed Said walisema wewe ni Muislam fake.
Lakini mimi nadhani wengi wenu ni fake tu ndiyo maana mtaendelea kulalamika mpaka mwisho wa wakati!
Nshukuru sana mkuu wangu wala huna sababu ya kuniheshimu kwa sababu ya kupigania kanisa. yes Mohammed Said na Faizafoxy wataniona hivyo kwa sababu wao na wewe hamna tofauti inapokuja maswala ya dini wewe KANISA, wao EAMWS na mimi MTANZANIA na mimi siwatetei kanisa wala EAMWS maana wote hawa ni wafanya biashara wakitumia jina la dini...Hoja hapa ni swala la Umeme, imekuwaje Mkandara awe issue kwenu? ebu jiulizeni mbona mimi sizungumziii maisha yenu lakini mara Mkandara mkimbizi na kadhalika..hakika mkiishiwa hoja mnakuja na mengi ya Udini.

Sawa niite mimi mdini, lakini haya anayoyafanya JK ambaye nyie wenyewe mnamwita Mdini sijui inabadilika vipi akiwatendea nyie na leo ndiye rais mzuri kwenu akifuata ya kanisa. CCM wataachaje kuitawala nchi milele ikiwa dawa ni kuendeleza mfumokristu!
Tatizo la Watanzania ni KANISA KATOLIKI.
 
Mdondoaji ebu fanya analysis yako . Tatizo la Tanzania nini?
  • Ni "kanisa"
  • Ni kanisa Katoliki?
  • Ni wakristu ?
  • Ni baadhi tu ya wakirstu?
  • Ni baadhi ya waislam?
  • Ni baadhi ya wakristu na baadhi waislam
  • Ni baahi ya watanzania?

BTN
kwa nini unapenda kupindua thred kuzitoa kwenye hoja ya msingi. Unamtja Nyerere mzee alishakufa wakati kwenye mada iliyopo mbele sterling ni kanisa ( RC) na Rais mrisho kikwete (Muislam) na umeme.

Tatizo la Tanzania swali moja aliuliza Mkandara Je serikali ya Tanzania HAINA DINI??? Naomba jibu tafadhali.
 
Kwa mjadala uliojitokeza hapo juu; nina imani kubwa sana kuwa Nyerere alikuwa na busara ya juu pale alipoamua kufuta huduma za jamii zinazoendana na dini. Aliwaambia viongozi wa dini kuwa wajibu wenu ni kuhubiri dini, swala la huduma za afya, elimu, umeme, barabara na nyinginzeo kama hizo ziwe ni za serikali. Inapotokea dini fulani ikatoa huduma fulani ya kijamii hata kama ni ya bure kabisa kwa wananchi bila masharti yoyote, ni wazi kuwa kuna raia wa kutoka dini nyingine watakaojiona kama vile hawana haki na huduma ile.
 
Yale yale ya Nyerere nchi yetu haifungamani na upande wowote wakati tukichukua siasa za UJAMAA na KUJITEGEMEA kupinga Ubepari.
 
Kwa mjadala uliojitokeza hapo juu; nina imani kubwa sana kuwa Nyerere alikuwa na busara ya juu pale alipoamua kufuta huduma za jamii zinazoendana na dini. Aliwaambia viongozi wa dini kuwa wajibu wenu ni kuhubiri dini, swala la huduma za afya, elimu, umeme, barabara na nyinginzeo kama hizo ziwe ni za serikali. Inapotokea dini fulani ikatoa huduma fulani ya kijamii hata kama ni ya bure kabisa kwa wananchi bila masharti yoyote, ni wazi kuwa kuna raia wa kutoka dini nyingine watakaojiona kama vile hawana haki na huduma ile.

Kichuguu you are a great thinker!!!! tungelikuwa na wengi kama wewe tungelikuwa mbali.
 
Tatizo la Tanzania swali moja aliuliza Mkandara Je serikali ya Tanzania HAINA DINI??? Naomba jibu tafadhali.

Yes sheria na katiba ya Tanzania haina si tu dini bali haina kabila na jinsia. Wewe unaonaje ? Mimi nikuulize kwa nini umeulizia dini tu

  • Thanks
Reactions: FJM
Tatizo la Tanzania swali moja aliuliza Mkandara Je serikali ya Tanzania HAINA DINI??? Naomba jibu tafadhali.

Let me say it again, Serikali ya Tanzania haina dini. Ili serikali iwe ina dini ni lazima sheria za nchi ziwe kwenye misingi ya dini. Huwezi kufungua butcher nguruwe Saudi Arabia kwa sababu ni islamic state, lakini Dar sio tu kuna ma-buthcher, waislam wanakula kiti moto na huwezi kumshitaki mtu hata umemkuta anakula kwa sababu hajavunja sheria. Kanisa katoliki kwa mfano halikubaliana na vidonge vya uzazi, lakini serikali inatoa huduma hiyo tena inahamasisha watu watumie vidonge na wakoliki wengi tu wanatumia. Na huwezi kumshitaki mtu anayetumia vidonge vya uzazi kwa sababu hakuna sheria inayokataza kufanya hivyo.

Hii theory ya 'guilty by association' I believe is mis-guided. Ukipunguza jazba utaelewa tu. Pata juice ya matango - it will calm you down!
 
Kwa mjadala uliojitokeza hapo juu; nina imani kubwa sana kuwa Nyerere alikuwa na busara ya juu pale alipoamua kufuta huduma za jamii zinazoendana na dini. Aliwaambia viongozi wa dini kuwa wajibu wenu ni kuhubiri dini, swala la huduma za afya, elimu, umeme, barabara na nyinginzeo kama hizo ziwe ni za serikali. Inapotokea dini fulani ikatoa huduma fulani ya kijamii hata kama ni ya bure kabisa kwa wananchi bila masharti yoyote, ni wazi kuwa kuna raia wa kutoka dini nyingine watakaojiona kama vile hawana haki na huduma ile.
Mbali nan hivyo katika katiba tukiacha hili la serikali kutokuwa na dini kuna kipenegele kinachosema:-
J) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njiazinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njiakuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi..

Je, Kweli njia kuu za uchumi haziachwi ktk mamlaka ya watu wachache binafsi? Hii katiba inatakiwa kufutwa kabisa tunaze upya maanake mkorogo umezidi.

Yes sheria na katiba ya Tanzania haina si tu dini bali haina ukabila na jinsia

I see je matendo ya serikali yanaonyesha serikali haina dini? Kama watekelezaji wakiwa wanakiuka je tufanyaje?
 
Maandishi yale ya mwanzo niliyaita uwendawazimu, now I conclude kuwa hata wewe ni mwendawazimu.

Unajua kuwa tofauti ya genius na mwendawazimu ni 0.9999 yaani ni almost probability equal to 1 kwa maana nyengine tofauti ya genious na mwendawazimu ni ndogo sana. Wakati wewe unaconclude mie mwendawazimu mwengine ananiona genious. Kama hujavaa viatu vya waislamu na kufahamu shida zao hutaelewa kwanini wanasema hivyo.
 
Kwa mjadala uliojitokeza hapo juu; nina imani kubwa sana kuwa Nyerere alikuwa na busara ya juu pale alipoamua kufuta huduma za jamii zinazoendana na dini. Aliwaambia viongozi wa dini kuwa wajibu wenu ni kuhubiri dini, swala la huduma za afya, elimu, umeme, barabara na nyinginzeo kama hizo ziwe ni za serikali. Inapotokea dini fulani ikatoa huduma fulani ya kijamii hata kama ni ya bure kabisa kwa wananchi bila masharti yoyote, ni wazi kuwa kuna raia wa kutoka dini nyingine watakaojiona kama vile hawana haki na huduma ile.

@Kichuguu, umenikumbusha mbali sana. Wakati nasoma primary kuna bwana mmoja alikuwa anakimbia sana. Kila kukiwa na mashindano ya riadha anaacha watu mbali vibaya mno. Mwisho wa siku watu wakaanza kumchukia. they could not beat him so they decided to hate him!

Both BAKWATA na kanisa wapewe hela, mmoja anajenga vyuo, hospitali, anachimba visima vya maji, anafua umeme lakini mwingine 'anachuna' kama hajapata hata sumni.
 
Let me say it again, Serikali ya Tanzania haina dini. Ili serikali iwe ina dini ni lazima sheria za nchi ziwe kwenye misingi ya dini. Huwezi kufungua butcher nguruwe Saudi Arabia kwa sababu ni islamic state, lakini Dar sio tu kuna ma-buthcher, waislam wanakula kiti moto na huwezi kumshitaki mtu hata umemkuta anakula kwa sababu hajavunja sheria. Kanisa katoliki kwa mfano halikubaliana na vidonge vya uzazi, lakini serikali inatoa huduma hiyo tena inahamasisha watu watumie vidonge na wakoliki wengi tu wanatumia. Na huwezi kumshitaki mtu anayetumia vidonge vya uzazi kwa sababu hakuna sheria inayokataza kufanya hivyo.

Hii theory ya 'guilty by association' I believe is mis-guided. Ukipunguza jazba utaelewa tu. Pata juice ya matango - it will calm you down!
Hapana mkuu wangu umekosea sana kwa kuchagua vile visivyofuatwa..Na wala nchi inapokuwa na dini haina maana watu wanalazimishwa kufuata ndio iwe maana ya serikali kuwa na dini. Unaweza kwenda kusali ama kutokwenda kusali hata ktk nchi yenye mfumo wa kidini..Iran wanaongozwa na serikali yao ya dini, lakini mkristu na Jews wanaendesha imani zao hawalazimishwi ya Uislaam.

Hivyo vipo vinavyowezekana ama kutowezekana, wala sii swala la kula nguruwe au kutokula ndio dini, dini ni imani ya kiroho ambayo serikali yetu haiwajibiki kufuata values zake. Na inapoweka muafaka na kanisa ndio kabisaa inaondoa hata fikra za kwamba sera (policies) hulenga kuweka sheria na fursa kwa vyombo vyote vya aina hiyo. Kazi ya serikali ni kuunda sera (policy) ambayo inawawezesha wote wenye kujihusisha na shughuli hiyo kujua haki zao sio chombo kimoja na vingine viombe vitapewa..Hii imekuwa kutafuta mapenzi au nini?

Sisi tutafuata tafsiri ya katiba yetu kulingana na hali halisi. Joint partnership baina ya serikali na kanisa haiwezi kuondoa ukweli kwamba serikali imekiuka katiba. Huwezi kuindoa serikali ndani ya mradi wa kanisa wala kanisa ktk mradi huo na maamuzi wanayafanya kamati ya kanisa wakati fedha za wananchi zinatumika kuendesha mradi huo. Wewe nambie sababu ya kukataa OIC au mahakama ya kadhi kwa kutumia mifano yako hapo juu..
 
@Kichuguu, umenikumbusha mbali sana. Wakati nasoma primary kuna bwana mmoja alikuwa anakimbia sana. Kila kukiwa na mashindano ya riadha anaacha watu mbali vibaya mno. Mwisho wa siku watu wakaanza kumchukia. they could not beat him so they decided to hate him!

Both BAKWATA na kanisa wapewe hela, mmoja anajenga vyuo, hospitali, anachimba visima vya maji, anafua umeme lakini mwingine 'anachuna' kama hajapata hata sumni.

Hembu tuambie Bakwata ni taasisi gani? Pili wanapewa hela gani tukuelewe maana tunajua makanisa yanapewa Billioni 91 kutoka katika kodi zetu je Bakwata wanapewa nini?
 
I see je matendo ya serikali yanaonyesha serikali haina dini? Kama watekelezaji wakiwa wanakiuka je tufanyaje?

Nimejibu swali lako lakini kabla ya kuuliza lingine ingelikuwa vema kwnza ujibu na langu . Kwa nini i umeuliza kuhusu dini na sio kuhusu jinsia au kabila au umri? Yaani napenda kujua kwa nini demographic analysis yako mswali yake yanaishia kwenye scope ya hoja za dini tu.

Lakini kabl sijajibu hoja yako japo mimi si msemaji wala mtetezi wa serikali. Mwenyewe nataka nione reform mbali mbali
  • ebu fafanua Wanaiuka kifungu gani cha katiba? kwa kufanya vitendo gani? ebu toa mifano specific vitu vichache labda tunawez kujua tunatkiwa tuchukue hatua gani
 
Hembu tuambie Bakwata ni taasisi gani? Pili wanapewa hela gani tukuelewe maana tunajua makanisa yanapewa Billioni 91 kutoka katika kodi zetu je Bakwata wanapewa nini?

Nilikuuliza hapo awali lakini ukakaa kimya. Na msingi wa swali langu ni kwamba kama una uwezo wa kutambua kanisa wanapata 1.2 trillion then tumia mbinu hizo hizo kutuambia BAKWATA wanapata kiasi gani. Au unataka kusema BAKWATA hawapati chochote? Mkandara anaweza kutoa mchango kwenye hili, I know he can!
 
Unajua kuwa tofauti ya genius na mwendawazimu ni 0.9999 yaani ni almost probability equal to 1 kwa maana nyengine tofauti ya genious na mwendawazimu ni ndogo sana. Wakati wewe unaconclude mie mwendawazimu mwengine ananiona genious. Kama hujavaa viatu vya waislamu na kufahamu shida zao hutaelewa kwanini wanasema hivyo.

Ofcourse wanakuona wewe ni genious hahaha ahahaha ahahah!!!!!!!!! Mkuu nadhani na wewe hutaelewa kuhusu personal struggles nilizozifanya na zinazofanywa na watu wengine bila kujali dini zao ndani ya Tanzania ili kuondokana na umasikini na ujinga. I for one from a very tender age I had to stand some real tall orders kuweza kuiondoa familia na ukoo wangu katika lindi la umasikini. Ndiyo maana naudhika sana watu kama wewe mnavyoleta hiyo blanket of deception kuhusu upendeleo. It's sick, disgusting and completely innacurate kudhania kwamba kila aliyefanikiwa basi kuna namna ya upendeleo imefanyika. Anywayz ni nje ya mada lakini kama kuna ulazima sisi kama watanzania tupeane mbinu za mafanikio na si kubebeshana huo mblanketi wa deception.
 
Nimejibu swali lako lakini kabla ya kuuliza lingine ingelikuwa vema kwnza ujibu na langu . Kwa nini i umeuliza kuhusu dini a sio kuhusu jinsia au kabila au umri? Yaani napenda kujua kwa nini demographics analysis yako mswali yake yanaishi a kwenye scope hoja za dini tu.

Lakini kabl sijajibu hoja yako japo mimi si msemaji wala mtetezi wa serikali. Mwenyewe nataka nione reform mbali mbali
  • ebu fafanua Wanaiuka kifungu gani cha katiba? kwa kufanya vitendo gani? ebu toa mifano specific vitu vichache labda tunawez kujua tunatkiwa tuchukue hatua gani

Kujibu swali ndio serikali ina dini na dini yake ni Ukristo dhehebu la katoliki.

Sababu yake nenda katika thread ya OIC na Mahakama ya Kadhi na thread ya MoU ya serikali na makanisa niliposema serikali inapinga hivyo vitu lakini yenyewe iko katika kupendelea ukristo na nimetoa vifungo mfano kifungu cha sheria ya ndoa ya mwaka 1970s kinasema mke anayetambuliwa kisheria ni mke mmoja (waislamu wameachwa pembeni). Pia kuna kifungu katika katiba section 11 kimebadilishwa hasa haki ya elimu kutoka kuwa jukumu la serikali kuwa serikali itasaidia upatikanaji wa elimu. Vile vile sheria ya Education Act No 25 ya 1975 imebadilishwa hasa section 30 imeondolewa katika Education Cap (353)na Education Act ya 1995 kwani sheria ile inapingana na MoU ya Kanisa na Serikali.

Sasa nakuuliza je watendaji wa sheria wakiwa wanavunja katiba (misingi yake) je bado suala la serikali haina dini litakuwapo????
 
Mbali nan hivyo katika katiba tukiacha hili la serikali kutokuwa na dini kuna kipenegele kinachosema:-
J) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njiazinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njiakuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi..

@Mkandara
Shughuli kuu za uchumi na njia zake ni zipi kwa Tanzania?

Nilikuuliza hapo awali lakini ukakaa kimya. Na msingi wa swali langu ni kwamba kama una uwezo wa kutambua kanisa wanapata 1.2 trillion then tumia mbinu hizo hizo kutuambia BAKWATA wanapata kiasi gani. Au unataka kusema BAKWATA hawapati chochote? Mkandara anaweza kutoa mchango kwenye hili, I know he can!

Kwanini mimi na Mkandara tuchangie wakati tunachangia katika hela mnayoiba kutoka kwenye kodi zetu. Kila mwezi 0.01 ya kodi yangu inaenda katika MoU ya kanisa je Bakwata wanapata ngapi???? Pia ni akina nani Bakwata na imeanzishwaje na je inawawakilisha akina nani?
 
@Mkandara
Shughuli kuu za uchumi na njia zake ni zipi kwa Tanzania?
/QUOTE]Unauliza huleiwi au! Kama huelewi ulikuwa unabisha kitu gani.. na sijui kama umenisoma vizuri naona kama umerukia treni kwa mbele vile!​
 
Back
Top Bottom