Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki

Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki

Alaa sio wewe uloniita mkimbizi? mbona mimi sijakuita jina lolote lile wala kuingilia maisha yako. haki iko kwenu tu Mlotiwa maji ya ubatizo.
Serikali haishirikiani na taasisi za dini ya Kiislam?
 
Serikali haishirikiani na taasisi za dini ya Kiislam?
Hakuna taasisi za kiislaam isipokuwa zile zilizoanzishwa na serikali na mimi nazipiga vita vile vile..Licha ya hivyo nimeshasema hizi ni NGos kama Ngos zingine za Watu na Wakristu, sio mali ya kanisa na hawapati fursa za kanisa.
 
assylum seeker, go to your motherland

unapata pressure kwa ajili tu ya kulalama lalama kama kunguru

be proud of your nationality, huna utaifa wewe, mkibizi hana taifa, ni aibu na fedheha kuishi kama allien
Huna lolote, umeishiwa hoja unataka niwe proud na kanisa? mijitu mingine bana...
 
Huna lolote, umeishiwa hoja unataka niwe proud na kanisa? mijitu mingine bana...

huna utaifa wewe

utaishia kuchinjiwa baharini kama O.B.L

you are an allien in foreign countries, halafu unajisifia unakula Genetic modified foods

my feet

tafuta uraia wako wewe mpori pori wa ukimbizini
 
wakati wengine wakipewa kwa dezo majengo ili waazishe chuo chao, wengine wanatafuta mapori na kujenga vyuo vyao, halafu siku ya siku matamko yasiyokuwa na mashiko ya mfumo kristo yanatolewa kila kukicha, duuu.
" hongera jk kwa kuleta maisha bora kwa kila wanaludewa kwa mradi mkubwa wa umeme, haya ndo maisha bora uliyoyaahidi rais wangu"
 
huna utaifa wewe

utaishia kuchinjiwa baharini kama O.B.L

you are an allien in foreign countries, halafu unajisifia unakula Genetic modified foods

my feet

tafuta uraia wako wewe mpori pori wa ukimbizini
Sawa wewe mwenye nchi na uraia. kinakuwasha nini juu yangu au?
 
Unafanya mchezo na Trilioni 1.2 wanazogaiwa na serikali kutoka katika kodi zetu na bado zile walizokuwa wanajichotea kabla. Bado tunaendelea kuchangia kanisani kwa kulipa bili wacha tuleee bomu likilipuka siku mtajua nini tunasema maana hadi yatokee ndio mtakumbuka maneno yetu.

Kumbe kuna mipango ya kuchinja watu! kama kule nigeria kwa boko haramu? basi haya makiristo yasijenge hayo matambo ya umeme wala mauniversity tuishi tuendelee kuwasha vibatari na kuuza kauzi na kahawa, tuishi kama alivyoishi moha mad kwenye karne ya 7.
 
Mkuu nimeondoka tanzania toka mwaka 1984 nikaenda Sweden nikarudi, kisha Denmark nikarudi, kisha Swiss, mwaka 1987 nimetia nanga hapa. Sina Ukimbizi wa nchi yoyote ila nimetafuta maisha isikuume sana kuchambia jiwe. Huniwezi kwa hoja sasa ingilia maisha yangu bado utabakia mtupu..

Mdini mkubwa sana wewe jamaa mbona hujawahi kwenda Pakistan, Somalia, Mauritania, Kosovo, Chechnia ukaone wenzako walivyopiga hatua unakimbilia huko kwenye makanisa tu? Nimegundua kwani nini unalilia lia sana hapa. Utakunywa sana kahawa kwa pilipili.

Hata Saudia hujafika kweli wewe mjahidina feki
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Sawa wewe mwenye nchi na uraia. kinakuwasha nini juu yangu au?

kwanini uli escape and evict your own motherland?

still you have chance to redeem and become a loyal citizen of you true country, tena wameshawachoka huko mnajaza hewa tuu

vinginevyo have a wonderful time as an illigal allien in foreign countries,
 
Hakuna taasisi za kiislaam isipokuwa zile zilizoanzishwa na serikali na mimi nazipiga vita vile vile..Licha ya hivyo nimeshasema hizi ni NGos kama Ngos zingine za Watu na Wakristu, sio mali ya kanisa na hawapati fursa za kanisa.

Inapokuja kwenye uelewa na mikakati ya kuleta maendeleo kwa jamii, wakiristo wako mbele mno kulinganisha na wale wengine, hii siyo hapa Tanzania tu bali ni duniani kote. Wale wengine wana chuki na husuda inayowapelekea kuwaza fatwa na mauaji kwa vile hawawezi ku match juhudi na taratibu za wakiristo. Lakini ukifikiria sana utaona kuwa matunda ya ukweli ni ukweli na ya uongo ni uongo. Je mtu atavuna maembe kutoka kwenye mti wa mchongoma?
 
Huna lolote, umeishiwa hoja unataka niwe proud na kanisa? mijitu mingine bana...
Mkuu nilikuwa nakuheshimu sana ...lakini huu unafiki umezidi!! Ndiyo maana FaizaFoxy na Mohamed Said walisema wewe ni Muislam fake.
Lakini mimi nadhani wengi wenu ni fake tu ndiyo maana mtaendelea kulalamika mpaka mwisho wa wakati!

quote_icon.png
By Mkandara

Swali langu lipo palepale tunazungumzia KATIBA sii navyojisikia mimi kwanza mimi siishi Tz nakula kuku kwa mrija tena basi Kanisa linafanya mengi huku kuliko Bongo na wananchi wote tunaelewa kwa sababu katiba yao imejieleza wazi -mfumokristu ndio unatawala! -The nation was found under Christian values! na naishi wala sina matatizo.. Tatizo, kwenu na katiba yenu ya uongo! ..Na nachofanya mimi ni explore reality sina ubaya na Wakristu ama kanisa hata kidogo..
 
Ndio makosa yanayofanywa kiutawala sasa iwe mfumokristu ama nini lakini swala la UMEME kuendeshwa na jumuiya za kiimani huoni kama serikali ina dini?.. mimi naomba mtu aje hapa anambie hasa maana ya kusema serikali haina dini ikiwa leo Umeme ambao serikali ina wizara yake wanashirikiana na kanisa kufungua nguvu hizo, tena akiwaagiza wananchi walipe bill za umeme huo mapema.
Nipeni maana ya neno hili -Serikali haina dini - MAANA TU, halafu tuendelee..

@Mkandara, hapo kwenye red nina hakika unajua maana yake lakini nahisi unataka kujuwa watu wengi wanatafsiri vipi!

Kwa uelewa wangu, bado serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina dini - lakini watu wake wana dini. Kinachofanya serikali iwe na dini ni pale sheria mama yaani katiba ya nchi husika inaongozwa na misingi ya dini fulani. Kwa mfano, pombe ni haram kwenye dini ya uislam na kwenye nchi zinazoongozwa na sharia (Islamic state i.e Iran, Saudi Arabia) mtu akikutwa anakunywa pombe kwenye bar etc most likely atachukiliwa hatua za kesheria. Hapa Tanzania sijawahi kusikia mtu anapelekwa mahakamani kwa sababu alikutwa anakunywa pombe! It does not matter mnywaji pombe alikuwa mkristo au muislam. Hivyo 'haram' ya kunywa pombe inabakia within the parameters za dini husika (imani) na hakuna uhusiano wowote na sheria mama! na ndio maana hapa bongo waislam wanachapa safari vilivyo maana hakuna sheria yoyote inayomkataza kufanya hivyo. Kama ni kosa la kiimani linabakiwa kuwa kati yake na mungu na sio kati yake na state (serikali).

Kwenye blue: Nahisi ulikuwa na hasira wakati unaandika maana sio ni kwa vipi kitendo cha kushirikiana na kanisa kufungua mradi wa jamii basi serikali inakuwa na dini? Huo mradi wa umeme umesaidia na watu/jumuiya mbalimbali mojawapo ni European Union. Sasa, kama mawazo yako ni sahihi basi wote waliokubali kushirikiana na European Union kwenye huu mradi watakuwa wanafuata sheria za EU? Labda nikuulize, wakati wa Mkapa kilichokuwa chuo cha mafunzo cha Tanesco kilikabidhiwa kwa jumuiya ya waisla ili kutumika kama chuo kikuu na hadi sasa tunaongea kimebakia kuwa chuo kikuu chini ya umiliki wa jumuiya ya kiislam. Je, hapo tuseme serikali ina dini kwa sababu imefanya kazi na jumuiya ya kiislam?

Naomba kama una nafasi usome makala hii hapa chini toka kwa SAED KUBENEA. (Mwanahalisi - 2nd Nov 2011)

Majeraha ya udini yataangamiza taifa

KONGAMANO la kitaifa la Waislamu juu ya kile kilichoitwa, “Kupambana na mfumo Kikristo” lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee, jijini Dar es Salaam, 16 Oktoba 2011, limeibua mengi.

Kwanza, limethibitisha madai ya baadhi ya watu, kwamba shutuma, tuhuma na lawama zinazohusu mfumo wa uendeshaji serikali nchini, nyingi hazifanyiwi utafiti wa kutosha. Kwa mfano, wanazuoni wa kiislamu waliohutubia kongamano hilo la siku moja na kutoa walichoiita, “Waraka mrefu wa utafiti,” wametuhumu kitendo cha serikali kutoa misamaha mikubwa ya kodi kwa taasisi za kikristo zinazotoa huduma za jamii nchini, kuliko ilivyofanya kwa madhehebu ya kiislamu.

Aidha, wanazuoni wanasema serikali imekumbatia mfumo kikirsto; inaendeshwa kikirsto na imewageuza waislamu kuwa watu wa daraja la chini.
Pamoja na mambo mengine, wanatuhumu kuwapo wakurugenzi waislamu wawili tu, kati ya tisa katika wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi; mkaguzi mmoja kati ya wakurugenzi wakuu 11 wa kanda; maofisa elimu wa mikoa watano kati ya 21 na maofisa elimu ya msingi 23 kati ya 125.
Ukiangalia kwa haraka madai haya, unaweza kukubaliana nayo. Lakini ukijipa muda, ukapima na kutafakari kilichopo na kinachodaiwa kuwapo, utaweza kubaini kuwa kilichosemwa, ama kimepotoshwa au waliotumwa kufanya utafiti kuna mambo bado hawajaeleza.

Kwa mfano, serikali haiwezi kuwa inatoa fedha za ruzuku au misamaha ya kodi kwa taasisi zinazotoa huduma za kijamii kwa lengo la kubeba ukirsto. Inafanya hivyo kutokana na kuelemewa na mzigo wa uendeshaji serikali; mzigo unatokana na kufikia ukomo wa kufikiri katika kuhudumia wananchi.

Ukiona serikali haina uwezo wa kujenga na kuendesha hospitari zake yenyewe zinazokidhi mahitaji ya wananchi wake; haiwezi kuendesha shule, vyuo vya elimu ya juu wala vyuo vya ufundi vyenye hadhi na viwango vinavyohitajika, basi ujue hapo kuna tatizo. Matokeo yake, serikali inaamua kujisalimisha ama kwa wahisani wa nje au ndani. Baadhi yao ni madhehebu ya kidini.

Wakati taasisi za kikirsto zinamiliki msululu wa hospitali zikiwamo Bugando Medical Centre, Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na hospitari za wilaya karibu 28 nchini nzima, madhehebu ya kiislamu hayana hata hospitali moja ya rufaa, wala hospitali yenye hadhi ya kuitwa hospitali kuu ya mkoa au wilaya. Imeishia kwenye vituo vya afya na zahanati.

Kwa upande wa vyuo vikuu, madhehebu ya kikirsto yanamiliki chuo kikuu cha St. Augustine (SAUTI) cheyenye matawi ya Nyegezi, Bugando, Tabora, Iringa, Mtwara, Moshi na Bukoba. Vyuo vingine ni St. John Dodoma, Mount Meru Arusha, Kisanji Mbeya, Chuo Kikuu cha Arusha na Tumaini chenye matawi Iringa, Moshi, Makumira Arusha, Lushoto Tanga, Dar es Salaam na Mbeya. Hivi sasa, madhehebu hayo yako mbioni kufungua matawi mawili ya Karagwe na Bukoba mjini.

Taasisi za kiislamu zinamiliki chuo kikuu kimoja tu – Morogoro Islamic University (MIU), tena ambacho kiwanja na majengo yake yalitolewa na serikali. Madhehebu ya kiislamu hayamiliki hata taasisi tano zinazojihusisha na elimu ya juu. Nyingi ya taasisi za kiislamu zinaishia kumiliki shule za msingi na sekondari. Je, katika hili, serikali yaweza kulaumiwa kwa kutoa misamaha kwa madhehebu ya kidini, kwa kisingizio kwamba wanaonufaika zaidi ni madhehebu ya kikirsto?

Kilichopo ni hiki: Serikali imetoa upendeleo kwa madhehebu ya kidini kusaidia katika eneo hilo, hasa afya na elimu. Yule anayefikisha viwango vinavyotakiwa, ndiye anayepewa ruzuku, bila kujali muislamu au mkristo.

Lakini kuna hili pia. Anayetoa msamaha wa kodi kwa mujibu wa sheria ni waziri wa fedha. Kwa sasa, Mustaph Mkullo; ni muislamu. Ndani ya wizara yake, Mkullo anasaidiwa na manaibu waziri wawili – mmoja ni muislamu, Pereira Ame Silima. Yupo pia katibu mkuu, Ramadhan Khijjah; ni muislamu.

Mkullo amekuwa waziri wa fedha tangu mwaka 2008 baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda upya baraza lake la mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa aliyetuhumiwa kuingiza nchi kwenye mkataba tata wa Richmond. Alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Zakia Meghji. Ni muislamu. Sasa waislamu wanataka kusema, Mkullo anawahujumu? Kunahitajika utafiti wa ziada kuthibitisha hili.

Je, ni taasisi ngapi za kiislamu zilizopeleka maombi ya msamaha wa kodi kwake zikakataliwa? Misamaha hiyo iliyoombwa ilikuwa na thamani ya kiasi gani? Nani aliyeoomba? Ni taasisi za kiislamu au watu waliotaka kuzitumia taasisi hizo kujinufaisha binafsi? Hata kama wakurugenzi katika wizara hiyo, wengi ni kutoka madhehebu ya kikristo, hiyo haiwezi kuhalalisha madai kwamba yanayotendeka ndani ya wizara hiyo yanatokana na shinikizo la kidini; misimamo ya kidini na waislamu wameathirika kwa kiwango kikubwa na jambo hilo.

Hata hoja ya kuwapo wakristo wengi kwenye wizara ya elimu, inaweza kuonekana imetolewa bila utafiti wa kina. Ndani ya wizara ya elimu, pamoja na wakurugenzi, makamishina na watendaji wengine, yupo waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa. Huyu ni muislamu. Anasaidiwa na naibu waziri, Kassim Majaliwa. Naye ni muislamu.

Hivyo basi, kama madai haya yana ukweli, Dk. Kawambwa na Majaliwa watakuwa ndiyo wanatumika kuhujumu waislamu?
Jambo moja ni muhimu. Waislamu wasiendekeze malalamiko. Bali wajipange kama taifa kutafuta njia ya kujikwamua. Watafute mbinu elekezi zinazojenga hoja za kujadili na kuibua utambuzi, badala ya kuibua malalamiko ya “kusalitiwa kwa waislamu katika siasa za Tanzania.” Kwa mfano, Rais Kikwete hakuteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais kwa sababu yeye ni muislamu. Alichaguliwa baada ya kuonekana anaweza kushindana na wagombea wengine wa upinzani na kushinda.

Aliposhika nafasi hiyo, akateua wasaidizi kutoka madhehebu mbalimbali, kutokana na jinsi walivyojitokeza kwenye kugombea ubunge na kushinda.
Hivyo basi, kuendeleza madai ya kubaguliwa, kunaweza kuibua madai kutokana madhehebu mengine. Kwamba rais ni muislamu. Makamu wake ni muislamu. Rais wa Zanzibar na makamu wake wawili wote ni waislamu.

Waziri wa fedha, muislamu. Waziri wa ulinzi, naye ni muislamu. Waziri wa utumishi ni muislamu. Waziri wa afya, waziri wa mambo ya ndani na naibu wake, waziri wa uchukuzi na naibu wake, jaji mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), mkuu wa usalama wa taifa, wote ni waislamu.
Wengine wanaweza kufika mbali zaidi. Wakasema, ndani ya Benki Kuu (BoT), manaibu gavana wote watatu, ni waislamu. Bodi ya wakurugenzi yenye wajumbe 10, saba ni waislamu. Kwenye mifuko mitatu mikubwa ya hifadhi ya jamii, miwili inaongozwa na waislamu. Orodha ni ndefu.
Jambo muhimu ni iwapo walionufaika na walioshika madaraka, wamenufaika kwa sababu walikuwa na sifa, au ni kutokana na misimamo ya kimadhehebu?
Tuulizane: Ni waislamu wangapi wamenufaika kwa Kikwete kuwa rais? Kama ni wachache, ina maana amewasaliti? Kama amewasaliti, sasa wafanyeje? Mchezo huu ni mauti yetu sote!
 
Duh! Labda tukumbushane tu kwa mifano halisi, Kule Rungwe mission kuna eneo la mission na Rungwe sekondari iliyokuwa mali ya kanisa Moravian na baadaye kutaifishwa kuwa ya serikali. Huvi vilijengwa in 1891. Kuna mradi mdogo wa umeme (Hydro) na maji ambao ulikuwa ukisupply eneo lote hadi shule, nyumba za walimu, BURE mpaka 1990 ndiyo serikali ilileta umeme wa Tanesco, umeme uliokuwepo just about 20km away toka miaka ya 60. Maji sidhani kama serikali imepeleka mpaka leo.Kaniisa pamoja na kunyang'anywa shule na serikali lakini bado waliendelea kuipa umeme na maji bure.....Was there something wrong with that? Je kuna haja ya kwenda kung'oa yale mabomba ya maji katika maeneo ya kijijini karibu na misheni na kusubiri serikali ije iweke yake?

Halafu jingine ni kwamba huyu JK lazima atakuwa zezeta kwa nini anakubali kufungua miradi inayoenda kinyume na katiba??? I won't be surprised kuitwa mdini kwa kutoa mfano huu. H
ahaha ahahahahahaha!!!!!!!!!!!
 
@Mkandara, hapo kwenye red nina hakika unajua maana yake lakini nahisi unataka kujuwa watu wengi wanatafsiri vipi!

Kwa uelewa wangu, bado serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina dini - lakini watu wake wana dini. Kinachofanya serikali iwe na dini ni pale sheria mama yaani katiba ya nchi husika inaongozwa na misingi ya dini fulani. Kwa mfano, pombe ni haram kwenye dini ya uislam na kwenye nchi zinazoongozwa na sharia (Islamic state i.e Iran, Saudi Arabia) mtu akikutwa anakunywa pombe kwenye bar etc most likely atachukiliwa hatua za kesheria. Hapa Tanzania sijawahi kusikia mtu anapelekwa mahakamani kwa sababu alikutwa anakunywa pombe! It does not matter mnywaji pombe alikuwa mkristo au muislam. Hivyo 'haram' ya kunywa pombe inabakia within the parameters za dini husika (imani) na hakuna uhusiano wowote na sheria mama! na ndio maana hapa bongo waislam wanachapa safari vilivyo maana hakuna sheria yoyote inayomkataza kufanya hivyo. Kama ni kosa la kiimani linabakiwa kuwa kati yake na mungu na sio kati yake na state (serikali).

Kwenye blue: Nahisi ulikuwa na hasira wakati unaandika maana sio ni kwa vipi kitendo cha kushirikiana na kanisa kufungua mradi wa jamii basi serikali inakuwa na dini? Huo mradi wa umeme umesaidia na watu/jumuiya mbalimbali mojawapo ni European Union. Sasa, kama mawazo yako ni sahihi basi wote waliokubali kushirikiana na European Union kwenye huu mradi watakuwa wanafuata sheria za EU? Labda nikuulize, wakati wa Mkapa kilichokuwa chuo cha mafunzo cha Tanesco kilikabidhiwa kwa jumuiya ya waisla ili kutumika kama chuo kikuu na hadi sasa tunaongea kimebakia kuwa chuo kikuu chini ya umiliki wa jumuiya ya kiislam. Je, hapo tuseme serikali ina dini kwa sababu imefanya kazi na jumuiya ya kiislam?

Naomba kama una nafasi usome makala hii hapa chini toka kwa SAED KUBENEA. (Mwanahalisi - 2nd Nov 2011)

Majeraha ya udini yataangamiza taifa

KONGAMANO la kitaifa la Waislamu juu ya kile kilichoitwa, "Kupambana na mfumo Kikristo" lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee, jijini Dar es Salaam, 16 Oktoba 2011, limeibua mengi.

Kwanza, limethibitisha madai ya baadhi ya watu, kwamba shutuma, tuhuma na lawama zinazohusu mfumo wa uendeshaji serikali nchini, nyingi hazifanyiwi utafiti wa kutosha. Kwa mfano, wanazuoni wa kiislamu waliohutubia kongamano hilo la siku moja na kutoa walichoiita, "Waraka mrefu wa utafiti," wametuhumu kitendo cha serikali kutoa misamaha mikubwa ya kodi kwa taasisi za kikristo zinazotoa huduma za jamii nchini, kuliko ilivyofanya kwa madhehebu ya kiislamu.

Aidha, wanazuoni wanasema serikali imekumbatia mfumo kikirsto; inaendeshwa kikirsto na imewageuza waislamu kuwa watu wa daraja la chini.
Pamoja na mambo mengine, wanatuhumu kuwapo wakurugenzi waislamu wawili tu, kati ya tisa katika wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi; mkaguzi mmoja kati ya wakurugenzi wakuu 11 wa kanda; maofisa elimu wa mikoa watano kati ya 21 na maofisa elimu ya msingi 23 kati ya 125.
Ukiangalia kwa haraka madai haya, unaweza kukubaliana nayo. Lakini ukijipa muda, ukapima na kutafakari kilichopo na kinachodaiwa kuwapo, utaweza kubaini kuwa kilichosemwa, ama kimepotoshwa au waliotumwa kufanya utafiti kuna mambo bado hawajaeleza.

Kwa mfano, serikali haiwezi kuwa inatoa fedha za ruzuku au misamaha ya kodi kwa taasisi zinazotoa huduma za kijamii kwa lengo la kubeba ukirsto. Inafanya hivyo kutokana na kuelemewa na mzigo wa uendeshaji serikali; mzigo unatokana na kufikia ukomo wa kufikiri katika kuhudumia wananchi.

Ukiona serikali haina uwezo wa kujenga na kuendesha hospitari zake yenyewe zinazokidhi mahitaji ya wananchi wake; haiwezi kuendesha shule, vyuo vya elimu ya juu wala vyuo vya ufundi vyenye hadhi na viwango vinavyohitajika, basi ujue hapo kuna tatizo. Matokeo yake, serikali inaamua kujisalimisha ama kwa wahisani wa nje au ndani. Baadhi yao ni madhehebu ya kidini.

Wakati taasisi za kikirsto zinamiliki msululu wa hospitali zikiwamo Bugando Medical Centre, Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na hospitari za wilaya karibu 28 nchini nzima, madhehebu ya kiislamu hayana hata hospitali moja ya rufaa, wala hospitali yenye hadhi ya kuitwa hospitali kuu ya mkoa au wilaya. Imeishia kwenye vituo vya afya na zahanati.

Kwa upande wa vyuo vikuu, madhehebu ya kikirsto yanamiliki chuo kikuu cha St. Augustine (SAUTI) cheyenye matawi ya Nyegezi, Bugando, Tabora, Iringa, Mtwara, Moshi na Bukoba. Vyuo vingine ni St. John Dodoma, Mount Meru Arusha, Kisanji Mbeya, Chuo Kikuu cha Arusha na Tumaini chenye matawi Iringa, Moshi, Makumira Arusha, Lushoto Tanga, Dar es Salaam na Mbeya. Hivi sasa, madhehebu hayo yako mbioni kufungua matawi mawili ya Karagwe na Bukoba mjini.

Taasisi za kiislamu zinamiliki chuo kikuu kimoja tu – Morogoro Islamic University (MIU), tena ambacho kiwanja na majengo yake yalitolewa na serikali. Madhehebu ya kiislamu hayamiliki hata taasisi tano zinazojihusisha na elimu ya juu. Nyingi ya taasisi za kiislamu zinaishia kumiliki shule za msingi na sekondari. Je, katika hili, serikali yaweza kulaumiwa kwa kutoa misamaha kwa madhehebu ya kidini, kwa kisingizio kwamba wanaonufaika zaidi ni madhehebu ya kikirsto?

Kilichopo ni hiki: Serikali imetoa upendeleo kwa madhehebu ya kidini kusaidia katika eneo hilo, hasa afya na elimu. Yule anayefikisha viwango vinavyotakiwa, ndiye anayepewa ruzuku, bila kujali muislamu au mkristo.

Lakini kuna hili pia. Anayetoa msamaha wa kodi kwa mujibu wa sheria ni waziri wa fedha. Kwa sasa, Mustaph Mkullo; ni muislamu. Ndani ya wizara yake, Mkullo anasaidiwa na manaibu waziri wawili – mmoja ni muislamu, Pereira Ame Silima. Yupo pia katibu mkuu, Ramadhan Khijjah; ni muislamu.

Mkullo amekuwa waziri wa fedha tangu mwaka 2008 baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda upya baraza lake la mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa aliyetuhumiwa kuingiza nchi kwenye mkataba tata wa Richmond. Alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Zakia Meghji. Ni muislamu. Sasa waislamu wanataka kusema, Mkullo anawahujumu? Kunahitajika utafiti wa ziada kuthibitisha hili.

Je, ni taasisi ngapi za kiislamu zilizopeleka maombi ya msamaha wa kodi kwake zikakataliwa? Misamaha hiyo iliyoombwa ilikuwa na thamani ya kiasi gani? Nani aliyeoomba? Ni taasisi za kiislamu au watu waliotaka kuzitumia taasisi hizo kujinufaisha binafsi? Hata kama wakurugenzi katika wizara hiyo, wengi ni kutoka madhehebu ya kikristo, hiyo haiwezi kuhalalisha madai kwamba yanayotendeka ndani ya wizara hiyo yanatokana na shinikizo la kidini; misimamo ya kidini na waislamu wameathirika kwa kiwango kikubwa na jambo hilo.

Hata hoja ya kuwapo wakristo wengi kwenye wizara ya elimu, inaweza kuonekana imetolewa bila utafiti wa kina. Ndani ya wizara ya elimu, pamoja na wakurugenzi, makamishina na watendaji wengine, yupo waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa. Huyu ni muislamu. Anasaidiwa na naibu waziri, Kassim Majaliwa. Naye ni muislamu.

Hivyo basi, kama madai haya yana ukweli, Dk. Kawambwa na Majaliwa watakuwa ndiyo wanatumika kuhujumu waislamu?
Jambo moja ni muhimu. Waislamu wasiendekeze malalamiko. Bali wajipange kama taifa kutafuta njia ya kujikwamua. Watafute mbinu elekezi zinazojenga hoja za kujadili na kuibua utambuzi, badala ya kuibua malalamiko ya "kusalitiwa kwa waislamu katika siasa za Tanzania." Kwa mfano, Rais Kikwete hakuteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais kwa sababu yeye ni muislamu. Alichaguliwa baada ya kuonekana anaweza kushindana na wagombea wengine wa upinzani na kushinda.

Aliposhika nafasi hiyo, akateua wasaidizi kutoka madhehebu mbalimbali, kutokana na jinsi walivyojitokeza kwenye kugombea ubunge na kushinda.
Hivyo basi, kuendeleza madai ya kubaguliwa, kunaweza kuibua madai kutokana madhehebu mengine. Kwamba rais ni muislamu. Makamu wake ni muislamu. Rais wa Zanzibar na makamu wake wawili wote ni waislamu.

Waziri wa fedha, muislamu. Waziri wa ulinzi, naye ni muislamu. Waziri wa utumishi ni muislamu. Waziri wa afya, waziri wa mambo ya ndani na naibu wake, waziri wa uchukuzi na naibu wake, jaji mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), mkuu wa usalama wa taifa, wote ni waislamu.
Wengine wanaweza kufika mbali zaidi. Wakasema, ndani ya Benki Kuu (BoT), manaibu gavana wote watatu, ni waislamu. Bodi ya wakurugenzi yenye wajumbe 10, saba ni waislamu. Kwenye mifuko mitatu mikubwa ya hifadhi ya jamii, miwili inaongozwa na waislamu. Orodha ni ndefu.
Jambo muhimu ni iwapo walionufaika na walioshika madaraka, wamenufaika kwa sababu walikuwa na sifa, au ni kutokana na misimamo ya kimadhehebu?
Tuulizane: Ni waislamu wangapi wamenufaika kwa Kikwete kuwa rais? Kama ni wachache, ina maana amewasaliti? Kama amewasaliti, sasa wafanyeje? Mchezo huu ni mauti yetu sote!

Tatizo moja nyie baadhi ya ndugu zetu wakristo pamoja na Saed Kubenea mnakuwa wanafiki kwani hamsemi makanisa hasa kanisa katoliki limekuwa likifanya ufisadi tangu kipindi cha Nyerere (Kamsome Mohamed Said, John Sivalon na John Illife). Vile vile kanisa lilifanya kila njia kuua nguvu za waislamu kwa kuwabandikia taasisi ya Bakwata ambayo haina mbele wala nyuma iliyoundwa kwa malengo ya kuwasambaratisha waislamu. Vile vile mkiulizwa kuhusu Trillioni 1.2 mnakauka na kukosa la kujibu kwasababu ni ufisadi na hamna justification zaidi ya kuporomosha matusi tu. Vile vile mnafanya subbotage kwa rais mwislamu ili aonekane vizuri kama hafai kama huyu mdau anavyowaumbua waziwazi

Yataka moyo lakini inapolazimika hakuna budi ila kupasua ukweli. Ni kanisa
ndilo ambalo linahusika na utendaji mbovu wa serikali ya muheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete.
Yawezekana ana mapungufu yake katika utendaji
lakini kuna watu wamekaa katika ofisi za serikali kwa manufaa ya kanisa hivyo
wako tayari kuvuruga mambo ili utendaji wa Kikwete uonekane mbovu na si
Kikwete tu hili ni kwa mtawala yeyote ambaye ataonekana kuwa na angalau
kaharufu ka - uislamu.

Kwa maslahi ya kanisa hilohilo hata waandishi wa habari nao wamekuwa mstari
wa mbele kumchafua Kikwete. Na hii ndiyo maana pamoja na utendaji mbovu
kabisa wa B.W Mkapa bado mapungufu yake hayaonekani na amekuwa akibeba
sifa kubwa sana za kukuza uchumi huku ufisani uliofanyika kipindi chake ukifumbiwa
macho. Ni kanisa hilo hilo ambalo limehusika na kushusha hadhi ya
Rais wa awamu ya pili ndugu A.H. Mwinyi.

SULUHISHO.Kanisa liache kufanya mambo nyuma ya pazia!

Mwambieni Saeed Kubenea amjibu basi Mohamed Said kwa data na facts kama alivyofanya Mohamed Said ndio utajua jinsi gani mlivyo wanafiki nyie
 
Kama ina dini...ni dini gani? Sidhani kama serikali ya Tanzania inaamini kuwa Yesu Kristo mwenye umungu mmoja na baba ndiye Bwana na mkombozi wetu! Kwa hiyo mnataka kutuambia hii serikali inayoongozwa na Dr JK akisaidiana na Dr Bilali na kule visiwani Dr Shein na mweziwe Maalim Seif (Dr?) nayo ni ya kikristo/kikatoliki?

Huwa sipendi kuchangia mada za kidini au ambazo zinachochea udini kwani nadhani wengi huwa hawataki kuelimishana au kuelimishwa bali kusambaza chuki ambazo zinaegemezwa na mifano isiyotokana na ukweli au viinimacho ambavyo husemwa sana na baadae wengi wetu wasio na uwezo wa kuchambua mambo au kufanya utafiti huanza kuyaamini na kuzungumza mambo hayo kama ukweli. Mwisho wa siku watu wengi huanza kuamini. Karl Marx alisema, na ninaomba mniwie radhi kwa kuinukuu kauli hii yenye ukakasi "Wengi ni Wapumbavu." Kwani ni rahisi sana kuwadanganya watu kwa maneno ya rejareja au yale yanayoamsha miemuko ili kufunika ukweli. Leo naomba nichangie.

Mimi ninaamii kuwa Mtanzania lazima atangulize Utanzania na uafrika wake kwanza kabla ya vitu vingine vyote ikiwa ni pamoja na dini,madhehebu, kabila, jimbo nikitaja tu mambo machache. Nchi yetu ni masikini sana na watu wake wanaishi katika maisha ya dhiki sana. Wachache wetu--manyapara wa Wanyonyaji na Wachukuaji na vibaraka wao--ndio wenye hali nzuri. Wanyapara hawa hawana uhalali au ukubalikaji kutoka kwa watu wao. Hili kuendelea kunyapara na kuwatumikia mabwana na mabibi zao, Wanyapara hawa hutafuta njia ya mkato ya kuweza kujiondoa katika matatizo. Njia hiyo ni kuleta mgawanyiko katika wananchi---"wagawanye ili uwatawale." Wanyapara hawa wataanza kutafuta visingizio vya matatizo ya Wananchi kuwa yanaletwa na watu fulani na kuwa watu hao wamekula njama ya kuwakandamiza wenzao. Wanyapara hao watafuta wachumia tumbo na waganga njaa ambao ni wazuri katika kusema kwa mifano ya rejareja ili kujenga chuki katika mioyo ya Watawaliwa na wadhulumiwa. Wataanza kusema kabila fulani ni wakabila.

Mimi ni Mhaya na nimeshuhudia dai hili la kipuuzi tu likisemwa sana na watu wenye kauli za rejareja. Wamerudia maneno hayo hadi Watanzania wengi wakaelekea kulikubali. Ukabila wao nini? Wanapenda kuzungumza kilugha, wanajidai wamesoma, wanajipendelea sana, na wanadharau. Je, watu wa makabila mengine hawana dharau, je hawajipendelei? Je, hawakuajiri pale walipokuwa na madaraka na nyadhifa katika mashirika yetu ya mbaga(umma) watu wengi wa kutoka kwao? Je, Shirika kama la Bima, BET siku hizo hayakujaa watu wa kutoka Mbeya na Tanga, na si juzi tu Idara ya Wanyamapori imetuhumiwa kujaza watu wa kutoka Wilaya Moja ya Njombe? Je, Jeshi letu halikutuhumiwa kujaza watu wa kutoka Mkoa wa Mara hadi likaitwa "Jeshi la Wakurya Tangu Zamani? (Wakurya hawatakiwi kusema lolote katika hili kwani Mimi Babu yao ninazungumza!(Utani huo). Jibu lao ni jepesi "Hapana Bwana lakini Wahaya wamezidi."

Tulipopata uhuru Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya kwanza kwa Bunge la Jamhuri ya Tanganyika alisema kuwa serikali yake haitasita kuwaaajiri watu waliosoma na wenye ujuzi kufanya kazi kwa kuogopa kuwa inapendelea watu wa makabila fulani. Alisema kuwa wakati huo watu kutoka makabila matatu ya Wahaya, Wachaga na Wanyakyusa (wala ndizi)-- ndio walikuwa wamesoma. Serikali haikuwa na chaguo jingine kwa wakati ule bali kuwaajiri kufanya kazi mbalimbali serikalini na ndivyo walivyofanya na hivyo watu wa makabila haya kuajiriwa katika nafasi mbalimbali serikalini na mashirika ya umma. Lakini serikali ilifanya njia za makusudi za kuinua watu wa makabila mengine kwa kusambaza elimu ya sekondari sehemu mbalimbali na kupandisha alama za kufaulu kwa wanafunzi wa wanaomaliza darasa la saba kuingia shule za sekondari kutoka mikoa ya Ziwa Magharibi (Kagera) Kilimanjaro na Mbeya huku ikishusha kiwango hicho kwa mikoa mingine. Kwa mfano, wakati mwanafunzi wa darasa la saba kutoka mikoa hiyo mitatu alitakiwa apate alama zaidi ya 80-90 katika somo moja yule wa mikoa ya Pwani, Kusini, Kati na Magharibi alitakiwa apate kati ya 40-50.

Kana kwamba hiyo haitoshi, mnamo mwaka 1968 serikali itaifisha shule zote zinazomilikiwa na madhehebu ya dini-ukiondoa seminari. Madhehebu ya kikristu yalikuwa na shule nyingi na nzuri. Raisi mwenyewe alikuwa mkristu tena mkatoliki. Alichukua uamuzi huo mzito ambao kwa wale ambao leo hii wanazungumza kwa kauli za rejareja wanaona kama hiyo ilikuwa danganya toto. Shule ya Sekondari kama Rugambwa kanisa lake ninambiwa liligeuzwa kuwa darasa au bweni. Shule hizo zikawa mali ya serikali na watoto wa makabila yote na dini zote nchini mwetu wakawa na haki ya kusoma huko na walisoma huko. Serikali hiyo ikaanzisha mfumo wa kusambaza watoto hao kutoka upande mmoja wa nchi kwenda kusoma upande mwingine wa nchi. Watoto wa Wakitanzania wakachangamana na kuelewana na kujenga utahi(urafiki), hatimaye wakaenda JKT na huko wakasota na kuhemea pamoja. Wakajifunza mambo mengi juu ya makabila yao na vilevile kuondokana na dhana potofu juu ya makabila na dini fulani wakaweza kuoana. Kabila na dini ya mtu vikawa si vitu vinavyomfahamisha mtu bali matendo yake. Hivi sasa idadi ya Watanzania wenye wazazi wa makabila tofauti inazidi kukua sana na ndugu zangu Wasukuma wanaongoza kwa kuoa na "kuwasukumisha" watu wa makabila mengi nchi mwetu.

Serikali ya Mwalimu vilevile ilifanya maamuzi mengine makubwa. Wakati wa ukoloni Sikukuu ya Iddi haikuwa siku ya mapumziko. Serikali ya Mwalimu ilifanya kuwa Sikukuu ya kitaifa na kufanya uwiano wa sikukuu za kitaifa kuwa karibu sawa kwa Waumini wa madhehebu ya Kiislamu na Kikristu --Iddi-el-Fitr (siku 2), Idd-el-Hajj (1) na Maulid(1) na Ijumaa Kuu (1) na Jumatatu ya Pasaka(1), Krismas (1). (Sikukuu ya Boxing Day(Desemba (26) ilfanywa sikukuu na Raisi Mkapa baada ya Watanzania kukataa ufidiaji wa sikukuu zinazoangukia siku za mwisho wa wiki). Na kwa faida ya wasomaji Sikukuu ya Mwaka Mpya ilifanywa Sikukuu na Raisi Mwinyi mnamo tarehe 1 Januari 1986. Mwalimu Nyerere alikuwa ameifuta kuwa sikukuu kwani alisema ni siku ambayo watu wanatakiwa kufanya kazi na si kupumzika. Na ukumbuke kuwa wakati wa utawala wa Mwalimu Jumamosi ilikuwa siku ya kazi (nusu siku) na ni Raisi Mwinyi ambaye kabla ya kumaliza kipindi chake cha Uraisi ndiye aliyeifanya kuwa siku ya mapumziko.

Kuingia kwa mfumo wa uchumi huria kuanzia mwaka 1986 baada ya nchi yetu kuwa katika msukosuko mkubwa sana wa uchumi kulibua kundi la watu ambao waliona kuwa njia pekee ya wao kujipatia chochote na kujikomba na viongozi wa nchi ni kuanza kuzungumza maneno ya udini. "Sasa huu ni wakati wetu sisi Waislamu kula kwani wakati ule ulikuwa ni wakati wa Wakristu kula." Maneno haya ya wachumia tumbo hawa ambao wakati ule walikuwa wakipata misaada midogo midogo kutoka nje kwa misingi ya "kusambaza uislamu" ikapanda kasi. Mnamo Januari 1987, nikiwa mwanafunzi wa kidato cha tano, nilipanda treni kutoka Mwanza kuja Dar es Salaam (safari iliyotuchukua siku nne badala ya mbili kutokana na reli kujaa maji) (tiketi ile ilikuwa ni ya waranti ya serikali). Kikundi cha watu wanaojiita ni Waislamu wakawa wanazungumza kukosoa dini ya Kikristu kwa kukosoa vipengele mbalimbali vya Biblia. Kama Mkristu na mtu nisiyekubali kuona upotoshaji nilijitosa katika mabishano nao. Je, tulielewana? Hapana. Imani ya dini ni ukuta wa fikira au kufikiri. Watu hao walikuwa wamepata misaada yao kutoka Irani na kwa wale wanaokumbuka wakati ule magazeti-jarida kutoka Irani yaliyokuwa yakisifia Jamhuri hiyo ya Kiislamu na hivyo walikuwa wakiganga njaa zao. Vikundi hivyo vilisambazwa katika pande mbalimbali za nchi "kumwaga sumu." Viongozi wa vikundi hivyo ambao waliona njia ya kumwaga sumu ndio salama yao.

Kwa Wakristu muda si mfupi kukaanza kuibuka makanisa na Wachungaji, Maaskofu, Mitume, Manabii wa kila namna wakiomba misaada huku hadi kule na kuanza kueneza "neno la Mungu." Mabishano ya kidini yakaanza kuenea Wakristu wa madhehebu mapya wakiyashambulia yale makongwe, Wakatoliki (adui namba moja), Waluteri na Waanglikana. Vilevile mabishano na Waislamu katika mihadhara ya "Biblia ni Jibu" na mingineyo mingi.

Serikali ya Mwinyi mnamo mwaka 1990 ilitikiswa na migomo ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Mlimani) (sasa Kampasi ya Mwalimu Nyerere). Ufukuzaji huu ulitokea baada ya kuanza kuparaganyika kwa mfumo wa Kikomunisti mwaka 1989 na hatimaye kuparaganyika kwa nchi ya Kisoviet ya Urusi. Raisi Mwinyi alifukuza wanafunzi wote wa Chuo Kikuu hicho kwa kushindwa kutatua matatizo yao ya msingi kabisa ikiwa ni pamoja na fedha za vitabu (dola 20). Mgomo wa Wanafunzi hao ulionyesha uzalendo na mafanikio ya uchangamano wa Watanzania. Viongozi wa Wanafunzi wakati huo walikuwa ni Dr. Cyril Chami(sasa Waziri) na Matiku Matare. Mmoja wa wazungumzaji na wajenga hoja wakubwa walikuwa ni Ally Salehe (Alberto) sasa mtangazaji wa BBC Zanzibari. Serikali ya Mwinyi ilishindwa kujibu hoja za Wanafunzi na kufikia uamuzi ovyo wa kuwatimua wanafunzi wote chuoni kwa kipindi cha mwaka mzima eti kwa "kumtukana matusi ya nguoni" licha ya kuwa madai yao kuwa ni ya msingi. Kana kwamba hiyo haitoshi, ikawakataza kufanya kazi. Kwa wale wanafunzi ambao walikuwa ni watu wazima matatizo waliyoyapata ni makubwa. Mwisho wa siku wanafunzi 11 walifariki kwa kukosa namna ya kujitibu na kujikimu. Uchunguzi wa Jaji Mrosso wa chanzo cha mgomo na mapicha ya kingono ngono juu ya Raisi Mwinyi na Mkewe Siti Mwinyi ulionyesha kuwa picha hizo zilichorwa na watu wa Usalama wa Taifa. Aibu mbona aibu!

Wanafunzi waliporudishwa hawakuacha kudai haki zao na ndio walipopigania nchi yetu kubadili mfumo wa chama kimoja na kuwa vyama vingi. Mwaka 1992 wakaitisha mgomo mwingine wa kupinga uchangiaji wa gharama za elimu. Kinara wa sera hii alikuwa Dk. William Shija. Wanafunzi wakagoma kwa nguvu zote na mgomo wao uliambatana na mgomo wa Madaktari wa Muhimbili. Kitwana Kondo ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo aliamuru madaktari hao (111) waswekwe ndani Ukonga. Kiongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu Haruni Kimaro (sasa mtangulizi (Marehemu) aliwaomba wanafunzi kufanya maandamano kudai kuachiliwa madaktari hao. Wanafunzi waliandamana hadi Ikulu na kuilazimisha serikali kuwachia madaktari hao. Dai la pili la Wanafunzi la kufukuzwa kwa Kitwana Kondo lilikutana na ghadhabu ya Raisi Mwinyi, ambaye hakuwa nchini (alikuwa Zambia) wakati wa mgomo na maandamano, ya kuamuru Wanafunzi hao ambao pia walikuwa wamempa Siku Saba afute mfumo wa uchangiaji wa elimu, kufukuzwa kwa muda wanafunzi wa mwaka wa 2 na 3 wa Kitivo cha uhandisi, 'kufukuzwa maisha" kwa wanafunzi kumi na mmoja ikiwemo James Mbatia, Haruni Kimaro, Jasson Kaishozi (mtangulizi), Omari (mtangulizi). Nami na wengine tisa akiwemo Kaiza Bubelwa, Abdi Kagomba, tukasimamishwa masomo kwa vipindi vya wiki sita hadi mwaka mzima.

Udhaifu wa serikali ya Raisi Mwinyi ukaanza kuonekana na licha ya kusutwa, kukejeliwa, na kusimangwa na viongozi wa serikali Wanafunzi wakawa wameanza kuwafumbua midomo na macho na kuwazibua masikio Watanzania. Kipindi hiki cha mabadiliko akaibuka Mchungaji Christopher Mtikila na mbiu yake "Saa ya Ukombozi ni Sasa." Yeye akawa ameiga mbinu ya Alyatollah Khomeini ya kurekodi ujumbe wake katika kanda za kaseti. Kanda zake zikaanza kusambazwa nchi nzima. Hoja yake mbali ya kumshambulia Mwalimu Nyerere akadai kuvunjwa kwa Muungano wa nchi yetu na kusema Wazanzibari warudi kwao na Watanganyika nao warudi kwao kwani nchi zao zina mpaka uliowekwa na Mungu (maji ya bahari). Hofu ikatanda. Na sumu ya Mtikila dhidi ya muungano wetu ilikuwa kubwa kwani Raisi alikuwa Mzanzibari (au Mzanzibara kama wenzetu wa visiwani wanavyomuita). Udhaifu wake ukawa mkubwa zaidi pale Kundi la Wabunge 55 (G-55) likiongozwa na Njelu Kasaka na kukolezwa na Jenerali Ulimwengu lilipowezesha kupitishwa kwa hoja ya kuundwa serikali ya Tanganyika. Hoja hii ilitokana na kitendo cha Serikali ya Zanzibari chini ya Komandoo wa mezani, Salmini Amour, kuingiza Zanzibar katika Jumuia ya Nchi za Kiislamu (OIC) wakati Zanzibar ikiwa haina mamlaka ya kufanya makubaliano kama hayo kwani mambo yote ya nje ni masuala ya Serikali ya Muungano. Vilevile kitendo cha Zanzibar kilikuwa ni ukiukaji wa wazi wa Ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inayoikataza serikali kuwa na dini yoyote.

Kauli za Mtikila dhidi ya Muungano na Wazanzibari zikawafanya baadhi ya Wazanzibari watahamaki na kutafuta namna ya kuziminya. Wakapindisha maneno kuwa Mtikila hawachukii Wazanzibari kama Wazanzibari bali Uislamu wao. Wakaanza kampeni ya kupambana na Mtikila kwa kupandikiza chuki hiyo katika mawazo ya Waislamu wa Bara. Kuwa adui wa Mtikila ni Waislamu na kuwa Zanzibari ni gheresha kwani baada ya kuvunja muungano atawageuka Waislamu wa Bara. Hoja hizi za rejareja zikapata nguvu pale Chuo Kikuu vijana wazalendo wa Kislamu ghafla wakiongozwa na Umoja wao wa wa Kiislamu[SIZE=-0](Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam)(MSAUD) wakaanza kutoa kauli z[/SIZE][SIZE=-0]a sisi Waislamu tunaonewa hivi mara vile na kuwa Mtikila ni adui wa Uislamu na kuwa Kanisa Katoliki lina fungate na Serikali ya nchi yetu.[/SIZE]Vijana hawa wakalitumia kikamilifu gazeti la AN-NUUR na kuanza kujibu mashambulizi ya Mtikila na kuonyesha jinsi Waislamu "wanavyoonewa" wakati wao ndio waliomkaribisha Mwalimu mtu wa Bara Dar es Salaam na kuwezesha kupatikana kwa Uhuru wa nchi yetu. Kana kwamba Watanganyika au Watanzania Bara wengine hawakupigania Uhuru huo-walipewa tu! Mambo yakawa yameanza na hata baada ya Mtikila kupoteza mvuto na ufuasi kidonda cha udini kikawa kimekua.

Azimio la Bunge lilimchefua sana Mwalimu Nyerere ambaye aliona linataka kuvunja Muungano aliouasisi. Akamtaka Raisi Mwinyi amtimue kazi Samwel Malecela (Waziri Mkuu) na Horace Kolimba ambao alidai walimshauri vibaya Raisi. Na kwamba Serikali ya Zanzibari ijitoe OIC. Yote yakafanywa na Bunge likatengua azimo lake la kuunda serikali ya Tanganyika. Lakini mbegu za udini na kuoneana zikawa zimemea. "Waislamu tunaonewa kwa nini Tanzania ina uhusiano wa Kibalozi na Vaticani" ikawa ni miongoni mwa kauli zinazosemwa katika baadhi ya misikiti na mihadhara. Nyingine "Kwamba kwanini tusiingie OIC tutapata misaada mingi na sisi Waislamu tutaweza kuendelea?" Kabla ya hapo mnamo mwaka 1992 Raisi Mwinyi katika Baraza la Iddi akasema kuwa serikali haikatazi watoto wa kike wa Kiislamu kuvaa hijabu katika shule za serikali. Leo hii licha ya kwamba vyombo na taasisi za kiserikali zinatakiwa kutokuwa na taswira za kidini wanafunzi na wafanyakazi wake wanavaa mavazi hayo. Msingi wa kutokuwa na dini ukawa umemomonyoka na unaendelea.

Serikali ya Mwinyi ikawa katika hali ya udhaifu mkubwa na isiyoweza kutoa kauli imara na makini huku ikishindwa kukusanya kodi. Chuki dhidi ya Wazanzibari zikawa ni nyingi na ndiyo sababu iliyomfanya Dr. Salim Ahmed Salim akataa maombi ya Mwalimu Nyerere kuja kugombe Uraisi tena. Ikumbukwe kuwa mwaka 1985 yeye ndiye alikuwa chaguo la Mwalimu lakini Mwalimu na Kawawa walizidiwa kete na Sheikh Thabiti Kombo na Getrude Mongela ambao walifanikiwa kuwashawishi wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kumteua Mwinyi. Kauli yake ya kukubali uteuzi ilikuwa "Zawadi haikataliwi."

Tokea hapo madai ya udini na kashfa za kidini zimeshika kasi mnamo tarehe 13 Februari 1998 Jeshi la Polisi likafanya mauaji pale Mwembechai. Hussein Njozi katika kitabu chake[SIZE=-1] "MWEMBECHAI KILLINGS[/SIZE][SIZE=-2]AND THE POLITICAL FUTURE OF TANZANIA[/SIZE]" anasema serikali ilifanya hivyo kutokana na kuchagizwa na Kasisi wa Kanisa Katoliki Mburahati. Damu ya udini ikawa imemwaga. Hakuna uchunguzi huru juu ya mauaji hayo. Yakafatia yale ya Pemba Januari 26 2001. Hakuna uchunguzi. Lakini mihadhara ya pande zote mbili ikawa imepanda kasi.

Serikali ya Mkapa na hata ya Kikwete zimeshindwa kupambana na hoja za wadini na wachumia tumbo tu na sasa katika mawazo ya Watanzania uteuzi wowote ule serikalini unaangaliwa kwa misingi ya udini na hata ukabila na kwa kweli hata ushemeji na ukwe. Je, namna gani serikali inaweza kujihami na kukwepesha mashambulizi dhidi ya utendaji wake mbovu? Ni kupata watu ambao wanaweza kusambaza mbegu za udini na ukabila na kutafuta chanzo-kivuli cha matatizo ya Watanzania. Chanzo hicho kivuli ni kile kinachoitwa "mfumo Kristu."

Uthibitisho huo ni kitabu cha Kasisi Mmoja wa Kikatoliki, John Sivalon, kuwa serikali ya Mwalimu ilikuwa na mahusiano mazuri na Kanisa Katoliki. Sasa kama alikuwa na mahusiano mazuri kwa nini alitaifisha shule na hospitali zao na kuzifanya zitumiwe na watu wa madhehebu na dini, rangi na makabila yote? Je, mtu msomi hawezi kuandika kitabu kingine na kuonyesha kuwa Mwalimu alikuwa adui mkubwa wa Ukristo kwa sababu hizo kama ambavyo Waislamu wanamtuhumu Mtangulizi Rashid Kawawa kuwa alishiriki katika kuvunjwa kwa chama huru cha Waislamu East African Muslim Welfare Society mnamo mwaka 1968? Ni wazi kuwa wachumia tumbo na waganga njaa hawa wako kazini kupata misaada kutoka kwa wale wanaowaambia kuwa wanaeneza Uislamu kumbe wanaeneza chuki. Uislamu maana yake amani, upendo na maelewano. Kama ambavyo ulivyo Ukristu. Bahati mbaya watu hawa wa pande zote mbili hawaelewi historia sahihi ya dini hizi na vita vilivyopiganwa kati ya Wakristu na Waislamu vya Crusade na Jihad. Je, ni Waislamu na Wakristu wangapi wanaelewa kuwa Waislamu waliitawala Hispania kwa zaidi ya miaka 800. Na kwamba licha ya kuwa pale Wakristu waliamuka na kupigana nao na kuwaondoa pale na kufuta Uislamu pale? Je, ni Wakristu na Waislamu wangapi wanaofahamu kuwa Waislamu na Wakristu walipigania Mji wa Jerusalem, na Wakristu wakashinda kwa muda na baadae Waislamu kuwashinda?

Hivyo ndugu Watanzania ni lazima tuelewe mustakabali wetu ni mmoja licha ya tofauti za dini na makabila yetu. Ni lazima tusimame kidete kupambana na ujinga huu wa udini na ukabila. Ni lazima tuwakemee watu wote ambao badala ya kudai uwajibikaji wa kweli serikalini, wanawalinda viongozi wazembe kwa kauli hizi za rejareja. Wachumia njaa hawa ukiwabana wamepokea mamilioni ya pesa kutoka nje kwa kigezo cha kusambaza "Uislamu" au "Ukristu" pesa nyingi zimeishia katika matumbo yao. Ni misikiti na makanisa mangapi yamebakia magofu licha ya Wafadhili wa ndani na nje kutoa mamilioni kama si mabilioni ya shilingi kuyajenga? Je, kwa nini shule ya Sekondari kama ya Al-Haramaani isiwe tajiri kushinda zote hapa nchini kwani imekaa katika eneo zuri za uwekezaji? Badala yake wajanja wachache kwa kigezo cha "Muislamu mwenzetu" wameikodisha na Muislamu huyo mwenzao atachuma kwa zaidi ya miaka 50 huku wanafunzi hao Waislamu wakipata elimu ya Kanumba. Kama Mwalimu alivyosema Mwaka 1962 "TUJISAHIHISHE."

"Mungu Ibariki Tanzania na watu wake"
 
Yataka moyo lakini inapolazimika hakuna budi ila kupasua ukweli. Ni kanisa
ndilo ambalo linahusika na utendaji mbovu wa serikali ya muheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete.
Yawezekana ana mapungufu yake katika utendaji
lakini kuna watu wamekaa katika ofisi za serikali kwa manufaa ya kanisa hivyo
wako tayari kuvuruga mambo ili utendaji wa Kikwete uonekane mbovu na si
Kikwete tu hili ni kwa mtawala yeyote ambaye ataonekana kuwa na angalau
kaharufu ka - uislamu.

Mdondoaji kilichoandikwa hapo juu ni uwendawazimu, hakuna jina lingine. Yaani Kikwete huyu tunayeambiwa humu kila siku kafanya mambo makubwa na wewe mwenyewe umeshatuletea stats mbalimbali kuthibitisha kukua kwa uchumi chini ya Kikwete halafu leo unamgeuka? Yaani leo kupyaya kwa uongozi/ uraisi wa Kikwete ni sababu ya kanisa? Where are u guys going to stop at? Yaani kuna watu serikalini wamekaa kwa manufaa ya kanisa na wako tayari kuvuruga mambo ili Kikwete aoonekane mbaya? Really? Halafu Kikwete huyo huyo bingwa wa kudhibiti mafisadi anawashindwa hao watu???? C'moon guyz this is the lowest ever to be discussed humu JF.
 
Tatizo moja nyie baadhi ya ndugu zetu wakristo pamoja na Saed Kubenea mnakuwa wanafiki kwani hamsemi makanisa hasa kanisa katoliki limekuwa likifanya ufisadi tangu kipindi cha Nyerere (Kamsome Mohamed Said, John Sivalon na John Illife). Vile vile kanisa lilifanya kila njia kuua nguvu za waislamu kwa kuwabandikia taasisi ya Bakwata ambayo haina mbele wala nyuma iliyoundwa kwa malengo ya kuwasambaratisha waislamu. Vile vile mkiulizwa kuhusu Trillioni 1.2 mnakauka na kukosa la kujibu kwasababu ni ufisadi na hamna justification zaidi ya kuporomosha matusi tu.

Mwambieni Saeed Kubenea amjibu basi Mohamed Said kwa data na facts kama alivyofanya Mohamed Said ndio utajua jinsi gani mlivyo wanafiki nyie

@Mdondoaji, Jambo tunalozungumzia hapa ni je serikali ya Tanzania ina dini au la? Na kama umesoma vizuri my argument serikali haina dini kwa sababu sheria zake haziko based kwenye principles za dini fulani. Na mfano nimetoa waislam kunywa pombe (haram) lakini hawezi kuchukuliwa sheria (labda sheikh aongee naye). Haya madai ya kuwa kanisa limeibandikia waislam BAKWATA ni total nonsense as far I am concerned na fikra za kipuuzi kama hizi ndio zinaharibu sifa ya Islam. Hivi ni mahakama ipi uliwahi kwenda ukakuta hukumu inatolewa kwa kutumia vifungu vya Quaran au Biblia?

Ukikazania kum-treat mtu kama victim iko siku ataamini kweli yeye ni victim hata kama tatizo lenyewe liko ndani ya uwezo wake. Kuna wajanja ndani wa dini ya kiislam wameamua kuimba wimbo u-victims ili waislam wasihoji mapato badala yake wajikite kwenye kilio cha kuonewa!

Miaka kama 2 hivi iliyopita KKKT walikuwa wanafanya uchaguzi mkuu (kiongozi wa KKKT -TZ) na kukawa na habari kuwa mafisadi walitaka kuchomekeza mtu wao. Lakini baadhi ya viongozi wa KKKT waliweza kupambana na kuhakikisha wanampata kiongozi ambaye 'sio wa kubandikwa'. Waislam wanashindwa nini hasa kuivunja hiyo BAKWATA kama wanaona haiwafai? Mnaweza nini kama mnashindwa kurekebisha taasisi ya dini yenu? Kikwete ni rais wa pili mwislam baada ya Mwinyi aliyekaa miaka 10. Nao wameshiriki kuwashindilia BAKWATA? Mlitaka nani awabandulie? Why cant you put your house in order?

Kuhusu Trillion 1.2 hili mbona liko wazi ndugu yangu. Soma list ya miradi kwenye hiyo article ya Kubenea; universities chini ya kanisa, kuna Hospitali ngapi za kanisa tena za rufaa? Do you know the real cost za kuendesha hospitali kama Bungado? au KCMC? Au ni mpaka Mohamed Said, John Sivalon na John Illife wawandikie kitabu kingine tena? Action speaks louder, wakisto wanajibu hoja kwa kufungua miradi kama huu wa umeme! Feasibility study ya huu mradi wa umeme ni more than Tsh 8billion. hiyo ni study tu.

Na kwa nini huulizi BAKWATA wanapata kiasi gani. Inakuwaje mko busy kuchunguza kanisa linapata kiasi gani lakini mnakaa kimya kwenye jumuiya/taasisi za kiislam? Hata kama hamuipendi BAKWATA lakini hamko curious kujuwa hawa watu wanapata kiasi gani kwa mgongo wa waislam? na wanazifanyia nini? Ni lini jumuiya au taasisi ya kiislam ilianzisha mradi wa kufua umeme serikali ikajitenga (ikakataa kuwasaidia).
 
Mdondoaji said:
Tatizo moja nyie baadhi ya ndugu zetu wakristo pamoja na Saed Kubenea mnakuwa wanafiki kwani hamsemi makanisa hasa kanisa katoliki limekuwa likifanya ufisadi tangu kipindi cha Nyerere (Kamsome Mohamed Said, John Sivalon na John Illife). Vile vile kanisa lilifanya kila njia kuua nguvu za waislamu kwa kuwabandikia taasisi ya Bakwata ambayo haina mbele wala nyuma iliyoundwa kwa malengo ya kuwasambaratisha waislamu. Vile vile mkiulizwa kuhusu Trillioni 1.2 mnakauka na kukosa la kujibu kwasababu ni ufisadi na hamna justification zaidi ya kuporomosha matusi tu. Vile vile mnafanya subbotage kwa rais mwislamu ili aonekane vizuri kama hafai kama huyu mdau anavyowaumbua waziwazi

Mdondoaji ebu fanya analysis yako . Tatizo la Tanzania nini?
  • Ni "kanisa"
  • Ni kanisa Katoliki?
  • Ni wakristu ?
  • Ni baadhi tu ya wakirstu?
  • Ni baadhi ya waislam?
  • Ni baadhi ya wakristu na baadhi waislam
  • Ni baahi ya watanzania?

BTN
kwa nini unapenda kupindua thred kuzitoa kwenye hoja ya msingi. Unamtja Nyerere mzee alishakufa wakati kwenye mada iliyopo mbele sterling ni kanisa ( RC) na Rais Mrisho kikwete (Muislam) na umeme.
Ushaiga style za Mohamed said za kupindisha hoja
 
Mdondoaji kilichoandikwa hapo juu ni uwendawazimu, hakuna jina lingine. Yaani Kikwete huyu tunayeambiwa humu kila siku kafanya mambo makubwa na wewe mwenyewe umeshatuletea stats mbalimbali kuthibitisha kukua kwa uchumi chini ya Kikwete halafu leo unamgeuka? Yaani leo kupyaya kwa uongozi/ uraisi wa Kikwete ni sababu ya kanisa? Where are u guys going to stop at? Yaani kuna watu serikalini wamekaa kwa manufaa ya kanisa na wako tayari kuvuruga mambo ili Kikwete aoonekane mbaya? Really? Halafu Kikwete huyo huyo bingwa wa kudhibiti mafisadi anawashindwa hao watu???? C'moon guyz this is the lowest ever to be discussed humu JF.

Uchumi wa JK unakuwa kweli na economic facts zinajisema but vile vile ufisadi unaongezeka na kuzorota kwa huduma mbali mbali . Wanaorudisha maendeleo wanafahamika vizuri vp nimekugusa kwenyewe nini? Waislamu wa karne mkuu ni wengine wanawafahamu vizuri njama zenu. Ni kweli kuna baadhi ya watu serikali wako kwa ajili ya manufaa ya kanisa na hilo wala si uongo (ndio sababu Mohamed Said aliwahi kusema hadi Rais Mwinyi alikuwa anaogopa kuongea ofisini kwake na Professa Malima akihofia the office may be bugged).
 
Back
Top Bottom