Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Mkuu Mkandara, there you are, now we sail the same boat!, now join the team, tumsafishe Lowassa, tumpake mafuta angare na kumeremeta, na tumpulizia manukato ya manemane anukie vizuri kila apitapo harufu ya kunukia inatangulia, hivyo kuwavuta wote wapendao vingaavyo na vinukiavyo!.

Now join the timu, sio lazima ki waziwasi kama sisi, hata kwa kunyamaza tuu na kutombomoa zaidi Lowassa, hiyo inatutosha!

Welcome on board!
Unajua siasa za Bongo hazitakiwi kufikiria kisheria ama kuna utaratibu.. Ni sawa na maisha ya wananchi wenyewe ya Kimachinga, yaani kila siku unaamka asubuhi unaenda itafuta riziki na jioni ukirudi nyumbani mkeo anakuuuliza umeshindaje?... akiwa na maana kipi kimepatikana leo?..Kimsingi Tanzania mapato ya jana sii ya leo wala ya kesho kila mtu ni machinga ktk services za kuzungusha (Udalali na ulanguzi) wakati huku majuu mfanyakazi una malipo yale yale siku hadi siku ukibamiza zaidi itakuwa imetokana na overtime ama kazi mbili - sana sana ukichomoza basi unauza Unga!.

Kufupisha ukweli huu ni kwamba Siasa za Bongo zinatisha... Na hii ndio reality ambayo inauma sana kuisikia wala kuiwazia lakini ndio ukweli..CCM wataendelea kutuburuza na wakitaka Lowassa atawale atatawala, wakitaka kumweka mtu mwingine wataweza na nadhani utabiri wa Nyerere ndio wenye uhakika zaidi kwamba Upinzani utatoka CCM kwa maana kwamba demokrasia ya vyama vingi haiwezi kuiangusha CCM aloijenga. Ikumbukwe tu Nyerere aliyasema haya akijibu hoja ambazo wanaCCM wenyewe walikuwa na mashaka na mfumo wa vyama vingi, hivyo majibu alikuwa akiwapa wao wana CCM... na sio sisi tulojiengua, that's how confi jamaa alikuwa na chama chake.

Na mimi naamini hivyo kwamba kutokea kwa makundi ndani ya CCM pekee ndiko kunaweza kuiangusha CCM ama WANANCHI wenyewe kwa ujumla wetu..Na nafasi hiyo tulikuwa nayo mwaka 2010kupitia sanduku la kura kulenga kiti cha rais tu. Na ndio maana nilipendekeza Dr.Slaa nikijua Chadema hawawezi kumshinda CCM majimbo lakini wakiweza wapata ushindi wa kitu kikubwa - Ikulu, ndio utakuwa mwisho wa CCM kama nyoka aliyekatwa kichwa..

Yet again, JK katushinda kwa mbinu ambazo zimedhihirisha kwamba CCM hata ukimshtukiza bado wamekamata sehemu zote za Dola na hivyo huwezi kumshinda kwa sanduku la kura. Na kusema kweli mimi naamini kabisa kwamba hakuna chama kinachoweza kumshinda CCM kupitia sanduku la kura - Hakuna... Hizi siasa zetu za UChadema, UCUF na kadhalika ni kujifurahisha kama ushabiki wa Mpira wengine MaU ,Arsenal, Chelsea na kadhalika ili mradi ushinda upo na maisha yanaendelea league kuu..

The only way CCM inaweza kuanguka iko sehemu mbili tu:-
1. CCM wenyewe wakivurugana na kusambaratika
2. WANANCHI wakichukua jukumu la kudai Uhuru wao wenyewe iwe kwa maandamanao ama migomo

Hakuna ushindi kupitia sanduku la kura hilo wananchi wasahau na kama CCM itamweka Lowassa basi atapita na tutaendelea kucheza ngwasuma na kiduku. Huu ndio ukweli unaouma sana lakini ndio - REALITY!
 
eeh hii ya kufungia mwaka jukwaa,hadi hiyo 2014 tunasikia mengi tuombe uzima tu..
 
eeh hii ya kufungia mwaka jukwaa,hadi hiyo 2014 tunasikia mengi tuombe uzima tu..
Shukran mkuu wangu nadhani umesema kweli nafunga Mwaka .....
Kheri ya Mwaka Mpya, ukiamka kesho jikumbushe na hayo ya Mkandara..
 
the fact kwamba huu mjadala umechukua attention yetu kubwa hivi
ni ishara moja kuwa Tanzania yetu inakwenda na maji......
things are falling apart.....so sad kwa kweli...

sisi ndo tuliokuwa kitovu cha ukombozi wa nchi zingine za Afrika....
leo tumefikia kusema nchi hii ina kingmaker tena sio raia na sio mkulima wala mfanyakazi
bali ni kabaila moja hivi janja janja......

Nyerere huko aliko anaziba uso wake kwa aibu....kina Nkurumah wakkimuuliza hii ndo Tanzania after 50 years?????
sijui anajibu nini.....
 
the fact kwamba huu mjadala umechukua attention yetu kubwa hivi
ni ishara moja kuwa Tanzania yetu inakwenda na maji......
things are falling apart.....so sad kwa kweli...

sisi ndo tuliokuwa kitovu cha ukombozi wa nchi zingine za Afrika....
leo tumefikia kusema nchi hii ina kingmaker tena sio raia na sio mkulima wala mfanyakazi
bali ni kabaila moja hivi janja janja......

Nyerere huko aliko anaziba uso wake kwa aibu....kina Nkurumah wakkimuuliza hii ndo Tanzania after 50 years?????
sijui anajibu nini.....
Mkuu Marehemu Nyerere (Mwenyezi Mungu amweke mahala pema Peponi) katimiza wajibu wake kwa yote aloyataka.

Alituasa kuhusu Ubepari tukampinga, leo tunalia nao, alituasa kuhusu hawa Mafisadi tukasema ana wivu sana, akatuasa kuhusu umaskini wetu na tabia ya tamaa itatuponza - The dutch disease, sisi tukaona ndio njia rahisi ya kupata Utajiri..

Matokeo yake tume fail vibaya sana hivyo yeye anacheka sana akisema - Niliwambieni hamkunisikia - Mtoto akililia wembe?.. Haya yote it's our own making!
 
Siasa za bongo zimekuwa kama ushirikina. Naam ni ushirikina hasa. Wachezaji wengi hawana hii kitu inaitwa "power from within" kwa viwango wa kutosha. Matokeo yake wanakaa kila wakati wanahaha huku na kule sababu hawajiamini na hawamwamini mtu. Watu wenye hii PFW huwa ni watu wanaojiamini; hata kama hana fedha huonekana kama tajiri, hata kama hana madaraka huwa power broker watu wengi wakimwogopa na kudhani anavitu anavijua ambavyo vinaweza kuwaangamiza.

Nimesema wanasiasa wengi wa bongo hawana PFW ya kutosha. PFW hutokana na hali ya ndani ya mtu kujiamini na kuridhika na kile anachokipata na alichonacho kiasi kwamba hata wale wenye vingi hujiona si kitu mbele yake. Yeye anajiamini tu na ameridhika! Watu wa hivi huwa ni watu pragmatic wanaopenda kufanya mambo hata kama wengine wanayaogopa.

Mwl. Nyerere ni kati ya watu hao waliokuwa na hii kitu PFW. Hakuwa mwoga ila alielewa limits zake na alijitahidi siku zote ku-improve. Hata pale aliposhindwa alikubali kuwa hapa mambo hayakuenda sawa. Akakiri udhaifu.

Bahati mbaya wapo wengi sana ambao hawana hii kitu kwa viwango vinavyotosheleza ila wanataka waonekane wanayo. Ni watu waoga, ila wanataka waonekane hawana woga. Ni watu wasiojiamini ila wanataka waonekane wanajiamini. Watu wa hivi hata wakiwa na madaraka wengi huishia kuwahofia wale walio chini yao na mara nyingi watakuwa wanawakandamiza sana watu. Hujawahi kuona bosi anayemuogopa "subordinate" wake? Wapo wengi sana wa hivi.

Mada kama hii hapa inayojadiliwa inatokana na watu wa namna hii! Kama nilivyosema huwa ni watu wapo wapo kama washirikina. Washirikina mtu akifa kwa ugonjwa wake tu pale mtaani akatajwa kama yeye ndo karoga, huwa hakubali wala hakatai. Anaamini katika "power of disguise" (POD). Siku zote watu wa hivi hupenda waonekane wamefanya mambo hata kama hawajafanya chochote na watu wa hivi huandaa magenge ya wapambe wa kutoa "tetesi" zinazowahusisha na kila kinachotokea. Watu hawa hata kama hawana madaraka hupenda waonekane wanayo; hata kama hawana fedha watapenda waonekane wanazo; watatumia kila aina ya hila kuudanganya umma unaowazunguka kuwa wao ndo kila kitu. Naam, wengi ndo mafisadi tunaowasema kila mara!

Binadamu wengi tunazo hizi nguvu zote mbili yaani PFW na POD kwa viwango tofauti tofauti. Viongozi wengi wazuri wanakuwa na PFW pekee na hawana hata chembe ya POD. Viongozi wengi wabaya na wa hatari sana; madikteta kama kina Hitler, Amin, Bokassa, n.k. huwa na POD peke yake na hawana hata chembe ya PFW. Watu wengi average wana nguvu hizi kwa viwango tofauti tofauti ila kadri aina moja inavyoizidi nyengine basi hata ubora wa mtu huelekea kufanana na wale wenye nguvu ya aina yake pekee ndivyo unavyozidi.

Wakati watu wenye POD wanaposaka madaraka mambo kama haya huzidi sana. Mitandao ya ukweli na feki huzidi. Tetesi nazo hutawala kila mahali.

"Political system" yetu leo hii iko "riddled with intrigues and corruption". Kwa maana kuwa POD sasa hivi inatawala na tuko more likely kuwapata watu wenye POD zaidi kwani ndo wako rafiki zaidi na mfumo wetu.
 
Karibuni mkandara na wengineo katika kubariki Lowassa apite!
Naapa Hamjui msemalo! Kimbinu hata mimi nimewakubali! Something will happen to make this country safe.kuna wazalendo wa kweli na wameamua kufanya lolote! Potezeni pesa na muda!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Pasco Unataka kusema bomu la kumlazimisha JK asujudie kumsimamisha EL kuwa Rais ni lipi ilo ambalo Watanzania wa Chini wasilojua mchezo wa Richmond ilikuwa ni BLACKMAIL.
Tafuta hoja nyingine kuwahalalishia wanajamii forum nguvu za EL, wabongo mpaka wa mitaani kwenye vijiwe wanajua mmoja ALiBRACKMAIL mwenzie.Ndio maana limekuwa ni kaa linalochoma kila siku.sema jingine tusilojua.
Ndugu yangu DSN, sio bomu, bali huu ni mchezo wa chess ambapo JK amesukumwa kwenye imposible angle na kuachiwa one and only move, nje ya hapo ni checkmate!.

Suala la uteuzi wa mgombea wa CCM kwa 2015, EL ndio ameshika kwenye mpini na JK ndio anapewa kwenye makali aamue kushika akatwe au kukubali EL ndie mgombea. Kumbuka Makinda ni kazi ya EL hivyo iwapo CCM haitamsafisha EL kwenye uchaguzi wao mwakani na sio tuu kumrudisha EL kwenye CC, bali kumpangua Nape, Mukama na Chiligati ili kusafisha njia ya EL kwenye uteuzi.

Mpini alioushika EL ni ukweli kuhusu richmond ni ya nani haswa, JK akikubali kumtosa EL, basi EL atamwaga mboga bungeni na impeachment process kuanza, hivyo Makinda atamwaga ugali na itakuwa end of the road for the game, unless vijana wa TISS wamshughulikie EL kabla!.
 
Nataka copy ya hii novel nitainunua kwa gharama yeyote ikitoka, maana jamaa anaandaa manuscript anacheki soko kama linalipa
 
mwandishi wa story hii anaonekana na yeye ni mtu ndabi ya system ya magogoni. Tafadhali lete haraka part II.
 
mwandishi wa story hii anaonekana na yeye ni mtu ndani ya system ya magogoni. Tafadhali lete haraka part II maana hii ni NYETI sana.
 
Ni kwa nini mkishaona post inamgusa EL mnaanza kukoroma sana,hivi huu si ni utahila?mnataka kutuambia ya kwamba mnamuandaa fisadi aje aongoze nchi?mnaota kweli mimi sitaki wala sifikrii kumuunga mkono,post iwe ni ya kutunga au ni ya kweli cha mno kuna cha kuchukua kutoka kwenye hii post
 
Naona wana Jf mmeanza kutapeliwa na huyu jamaa, hebu mnamkumbuka wa 16? Akili zenu wana Jf ni lazima zifikiri zaidi ya hii thread, sasa huyu usalama wa taifa anataka kutuamisha nini? There is some thing hiden inside of this post, wait.
 
Ndugu yangu DSN, sio bomu, bali huu ni mchezo wa chess ambapo JK amesukumwa kwenye imposible angle na kuachiwa one and only move, nje ya hapo ni checkmate!.

Suala la uteuzi wa mgombea wa CCM kwa 2015, EL ndio ameshika kwenye mpini na JK ndio anapewa kwenye makali aamue kushika akatwe au kukubali EL ndie mgombea. Kumbuka Makinda ni kazi ya EL hivyo iwapo CCM haitamsafisha EL kwenye uchaguzi wao mwakani na sio tuu kumrudisha EL kwenye CC, bali kumpangua Nape, Mukama na Chiligati ili kusafisha njia ya EL kwenye uteuzi.

Mpini alioushika EL ni ukweli kuhusu richmond ni ya nani haswa, JK akikubali kumtosa EL, basi EL atamwaga mboga bungeni na impeachment process kuanza, hivyo Makinda atamwaga ugali na itakuwa end of the road for the game, unless vijana wa TISS wamshughulikie EL kabla!.
Mkuu hapa hakuna wa Kumbeba mtu kwa game hili kikwetu tunasema ACHA VIUMANE,sana sana aliyeshika kisu ni JK,na ukweli anaujua kuwa EL hauziki sema wamesha msoma rafiki yake huyo wa zamani HAMBILIKI na HASIKIII NI KINGANGANIZI,HATA PASIPO WEZEKANA YEYE KWA KUWA NI POD HAELEWI.Japo pale anaponusishwa jikoni na anajua jikoni kukoje basi ufilkilia kuwa yeye ndie kinala wa mchezo kumbe anachezeshwa na yeye anaona anahusika kupanga watu wake huko ila ajui Bongo ni noma amuulize mwenzie aliekosa tiketi ya ndege huku akiwa madarakani.Watakachofanya ni kumvutia muda uku wakitafuta kikosi chake timilifu,kufumba na kufungua atajikuta anaamlishwa kusimama mbele kutangaza sifa za Rais mtarajiwa yeye mwenyewe.

Hapa ndipo Watanzania huwa wanakosea na kusema Serikali imekolimba mtu kumbe wajuzi wa elimu ya tabia na mienendo ya binadamu wanachofanya ni wanatriger sehemu ambayo mlengwa hategemei wala hawazii kisha kutahamaki pressure na kiharusi juu.

Hiyo ndiyo Bongo ya Nyerere watu wamefundwa wakafundikwa wanaweza wakakupa shavu la kusikika Bongo, Mungu wangu ukajiona wewe ndio Mungu Mtu,dakika za Mwisho wanakunyanganya kata ya maji ndani ya bonge la kiu.Kuna Mkuu alipandikiza watu wake Serikali nzima wa kumpa support ya urais 2005, Mungu kufumba na kufumbua anataharuki kusikia zinasomwa sifa KUMI NA TATU ZA RAIS KIJANA, Mtu chali akaona vipi MBONA BONGO HIVI nikaongeze maujuzi japo kujua hivi bongo inaendeshwaje.

Hakuna Cha King Maker wala cha nani wote hao ndani ya Mafisadi nia aina ya POWER OF DISGUISE [POD] wanachezeshwa bila kujua, kuna mdau hapo Juu KIPIMA PEMBE kaeleza vipi vizuri sana aina ya vichwa vilivyoko bongo vilivyofundwa kama POWER FROM WITHIN [PFW]. Mafisadi ambao ni POD wataendelea kuchezeshwa sindimba hiyo mpaka wanaingia kaburini kwa kuwa kwa UTASHI WAO WALICHAGUA AINA HIYO YA MAISHA YAO,tukija kwenye ubinadamu swali ni moja wanataka kuachive nini?kwa faida ya nani?.

Hakuna tatizo kwa binadamu yoyote yule kuwa tajiri chini ya uso wa dunia,lakini Intellectuals wanasema njia zitakazo tumika kukupa utajiri huo ndio itamua haki au haramu ya utajiri wako.

Utajili wa MAFISADI ambao umepita mikononi mwa baadhi ya watu aina ya POWER FROM WITHIN [PFW] Wanaujua A-Z ,Lakini POWER OF DISGUISE [POD] ambao ni Mafisadi pasipokujua ambalo sio kosa lao bali kosa lao ni uelewa wao,ambao kwa PFW bado UWA NI SHULE kwao ni kuongeza makarabrasha ya kuendeleza kizazi na kizazi kupitia evelution mbalimbali zinazokuja na zitakazokuja kwa PFW watakaozaliwa kuja kuwachezesha uzao wa mpya wa POD utakaozaliwa upya na kada nyingine baada ya iliyopo kuonekana uozo wake na kutoa shule ambayo watanzania wameiona na kuinua kiwango cha ufahamu wa Watanzania kupitia Dowans na Richmond.Leo hii hata mtoto wa dalasa la pili anajua Dowans na Richmond.



 
Wakuu, Hili la nani kampendekeza Fulani, na fulani hakumtaka nani sioni Msingi wake hapa, kwani hao jamaa ni wao kwa wao huo ni Mduara wao kwa hiyo mkuu Pasco, Mkandara na wengine msitegemee kuvutwa huko si wanaimba Kuna wenyewe?
Hayo wote tunayahisi ndivyo yanavyokwenda kama hatuyajui kwa uhakika.

Hoja kwa mtoa Mada:
1.Uelewa wangu kutokana na Somo hili ni Kuwa Wewe ni "Mtoto wa Jikoni"ie ulikuwapo in Person kiasi ukashiriki kucheka jina la Shein lilipokosewa kwa mara tatu. Unataka tuamini hivyo??
2.Kwa vile unamfahamu vizuri JK kama unavyodai hapa, kwa nini usimpelekee ushauri wako Ana kwa Ana kwa uelewa ninaopata mimi, weew huwezi kuwa Mgeni kwake.
3.Huoni Kigugumizi chako kinaweza kusababisha Madhara ? Zile Vurugu na Fujo Usizozitaka hujui na sisi hatuzitaki pia!!
4.Tupe mifano Miwili ya Plani za JK alizopanga Zikafeli/kufelishwa na Jamaa hao.
5.Wakati Jussa anapokezwa Kitita kikao hicho ulikihudhuria? Au ulihudhuria cha Jussa kumkabidhi Maalim Seif ?

What am traying to Establish is A Sense of Reality and Realstic.

Tafadhali Muda usiwe kisingizio Tuletee sehemu ya pili Ukizingatia Hoja hapo juu.
Nawasilisha.

Wakuu wenzangu nianze kwa kuwatakia "Heri za Mwaka mpya 2012".
Baada ya Masiku mengi natumai wengi wenu mu wema wa Afya na bado mko Jamvini.
jujuman, niruhusu niongeze hoja kwa mtoa mada.

Hili la Anna kupewa Nishani Na Kura ya kutokuwa na Imani vina mahusiano gani? Anna ana nguvu gani Kikatiba kuweza kuzuia hilo lisitokee? Majuzi tu, Tuliambiwa Idara inayoongozwa na Othman ina Njama za Kumuua Lowassa, Leo hutaki Unaacha anatwambia Mtandao unaongozwa na Lowassa na Othman ni Mwanachama, Hivi Inangia Akilini? Au ndio (dabo Ajent inafanya kazi!)

Harakisha hiyo sehemu ya pili: Hadithi njo Utam kolea Uongo Sogea...........................!
 
Back
Top Bottom