Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Mtazamo, tumpe mara ngapi?. Yeye ndiye "The King Maker" aliyemuweka JK kwa zile fedha za Kagoda na sasa ndiye anayemweka EL mwaka 2015!. There is nothing we can do!.

Msiomkubali Lowassa, nawashauri bora mkubalini tuu vinginevyo!.

sijui CCM wenzake... Wapinzani are not bothered at all!
 
...iwavyo vyovyote vile, nadhani ikitengenezwa muvi ya hii kitu itauza sana.
 
Siasa za bongo zimekuwa kama ushirikina. Naam ni ushirikina hasa. Wachezaji wengi hawana hii kitu inaitwa "power from within" kwa viwango wa kutosha. Matokeo yake wanakaa kila wakati wanahaha huku na kule sababu hawajiamini na hawamwamini mtu. Watu wenye hii PFW huwa ni watu wanaojiamini; hata kama hana fedha huonekana kama tajiri, hata kama hana madaraka huwa power broker watu wengi wakimwogopa na kudhani anavitu anavijua ambavyo vinaweza kuwaangamiza.

Nimesema wanasiasa wengi wa bongo hawana PFW ya kutosha. PFW hutokana na hali ya ndani ya mtu kujiamini na kuridhika na kile anachokipata na alichonacho kiasi kwamba hata wale wenye vingi hujiona si kitu mbele yake. Yeye anajiamini tu na ameridhika! Watu wa hivi huwa ni watu pragmatic wanaopenda kufanya mambo hata kama wengine wanayaogopa.

Mwl. Nyerere ni kati ya watu hao waliokuwa na hii kitu PFW. Hakuwa mwoga ila alielewa limits zake na alijitahidi siku zote ku-improve. Hata pale aliposhindwa alikubali kuwa hapa mambo hayakuenda sawa. Akakiri udhaifu.

Bahati mbaya wapo wengi sana ambao hawana hii kitu kwa viwango vinavyotosheleza ila wanataka waonekane wanayo. Ni watu waoga, ila wanataka waonekane hawana woga. Ni watu wasiojiamini ila wanataka waonekane wanajiamini. Watu wa hivi hata wakiwa na madaraka wengi huishia kuwahofia wale walio chini yao na mara nyingi watakuwa wanawakandamiza sana watu. Hujawahi kuona bosi anayemuogopa "subordinate" wake? Wapo wengi sana wa hivi.

Mada kama hii hapa inayojadiliwa inatokana na watu wa namna hii! Kama nilivyosema huwa ni watu wapo wapo kama washirikina. Washirikina mtu akifa kwa ugonjwa wake tu pale mtaani akatajwa kama yeye ndo karoga, huwa hakubali wala hakatai. Anaamini katika "power of disguise" (POD). Siku zote watu wa hivi hupenda waonekane wamefanya mambo hata kama hawajafanya chochote na watu wa hivi huandaa magenge ya wapambe wa kutoa "tetesi" zinazowahusisha na kila kinachotokea. Watu hawa hata kama hawana madaraka hupenda waonekane wanayo; hata kama hawana fedha watapenda waonekane wanazo; watatumia kila aina ya hila kuudanganya umma unaowazunguka kuwa wao ndo kila kitu. Naam, wengi ndo mafisadi tunaowasema kila mara!

Binadamu wengi tunazo hizi nguvu zote mbili yaani PFW na POD kwa viwango tofauti tofauti. Viongozi wengi wazuri wanakuwa na PFW pekee na hawana hata chembe ya POD. Viongozi wengi wabaya na wa hatari sana; madikteta kama kina Hitler, Amin, Bokassa, n.k. huwa na POD peke yake na hawana hata chembe ya PFW. Watu wengi average wana nguvu hizi kwa viwango tofauti tofauti ila kadri aina moja inavyoizidi nyengine basi hata ubora wa mtu huelekea kufanana na wale wenye nguvu ya aina yake pekee ndivyo unavyozidi.

Wakati watu wenye POD wanaposaka madaraka mambo kama haya huzidi sana. Mitandao ya ukweli na feki huzidi. Tetesi nazo hutawala kila mahali.

"Political system" yetu leo hii iko "riddled with intrigues and corruption". Kwa maana kuwa POD sasa hivi inatawala na tuko more likely kuwapata watu wenye POD zaidi kwani ndo wako rafiki zaidi na mfumo wetu.

wote wameongea lakini na wasiwasi wachache wamekuelewa....
thanx a lot...
 
swali hapa ni hilik
ama huyo kingmaker ana nguvu saana
why alijiuzulu na kukubali kuitwa fisadi????????

The boss ht mimi nilijiuliza hilo swali ila nikajipa jibu kwamba rostam ni very smart pamoja na kujiweka kando lkn bd akawa na nguvu ya kupanga nani na nani wawepo kwenye kampeni, huyu jamaa ni hatari.
 
Mkuu Marehemu Nyerere (Mwenyezi Mungu amweke mahala pema Peponi) katimiza wajibu wake kwa yote aloyataka.

Alituasa kuhusu Ubepari tukampinga, leo tunalia nao, alituasa kuhusu hawa Mafisadi tukasema ana wivu sana, akatuasa kuhusu umaskini wetu na tabia ya tamaa itatuponza - The dutch disease, sisi tukaona ndio njia rahisi ya kupata Utajiri..

Matokeo yake tume fail vibaya sana hivyo yeye anacheka sana akisema - Niliwambieni hamkunisikia - Mtoto akililia wembe?.. Haya yote it's our own making!

Tena alionya waziwazi Juu ya Lowassa na Tamaa ya mali, badoooo Watu hawakusikia hatakuelewa.
 
Pasco,

..kwani EL na JK wamekosana?

..nadhani JK is doing all that he can kijinusuru yeye na hawa maswahiba zake.
JokaKuu, JK na EL hawajakosana, na wala hawajakutana barabarani hivyo ni wale wale they are one and only, tofauti yao ni sisi tunaowatazama, umdhanie ndiye, siye!, na umdhaniye siye, ndiye!. Kuna mmoja kati yao anayeonekana mchafu, kumbe ndiye msafi, ila uchafu ni kweli ameubeka ili mwenzake aonekane msafi!

Kwa wenye kumbukumbu ya 2005, JK na EL walichgukua fomu pamoja na kuzisainisha pamoja, walikodi ndege moja kwenda kuzirudisha fomu zao kwa pamoja kule Dodoma, na baada ya Mkapa kupitishwa, walifanya press conference ya pamoja na JK akalalamikia kupigwa zengwe!.

Ben baada ya kushinda, akashauriwa na sytem enzi za Abson, ambao ndio hao hao kina EL na RA, kuwa ni lazima awatumie kwenye cabinet yake, ili kuwaconsole wafuasi wao, kama walivyompa umakamo wa rais, Dr. Bilal, lengo ni kuwapooza tuu wafuasi wake kule Zanzibar ili wasipige kura ya chuki dhidi ya Shein ili kuiadhibu CCM.

Kwa vile hawa ni mafahali wawili, mara tuu baada ya kuingia cabinet, wakaamua wakiendelea kupigana, ziumiazo ni nyika, hivyo wakatengeneza mtandao wa "the winning coalition" kujiandaa kwa 2005 na kuamua iwe isiwe, lazima mmoja kati yao ateuliwe. Yeyete aliyeonekana anaweza kuwa kikwazo, alishughulikiwa ipasavyo akiwemo Magufuli, na Mwandosya, wenye kumbukumbu mtakumbuka makambora ya scandali baada ya scandali za dhidi yao zilivurumishwa.

EL na JK walijiwekea their own secret accord, (Hawakukutana barabarani), wakakubaliana JK ndie achukue fomu na EL asichukue, kwa ahadi kuwa EL atakuwa PM na baada ya zamu ya JK, EL ndie angefuatia automatically!.

CCM ilipobakiza wagombea watatu, JK , Dr. Salim na Prof. Mwandosya, zengwe lililovurumishwa kwa Dr. Salim mnalijua, mpika zengwe mnamjua na shukrani kwa wapakuaji wa hilo zengwe mnajua walivyozawadiwa!. Mtu wa ajabu kabisa kwenye CCM ni Mkapa, anajua wazi kabisa ukweli kuhusu Dr. Salim na uwezo wa JK ukimlinganisha na Mwandosya, lakini Mwenyekiti wa CCM, kama zuzu vile ( naamini teknolojia ya Mlingotini ilitumika!), alijiunga na kambi ya JK , tena sio tuu kwa mwenyekiti ku take side, bali kuwa kuwadi wa JK kwa kumpigia kampeni za wazi kuwaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM, wamchague mtu aliyetoka mbali na CCM!. Kitendo cha Prof. Mwandosya kuonekana ni mtu wa principles na Mkapa aliyajua madudu yake aliyofanya pale Ikulu, ilionekana Prof. anaweza kumtundika msalabani, bora zimwi likujualo, wakamchinjia Prof. Baharini na JK akapeta na ndio ikatoka ni mpaka magogoni!.

Kweli JK aliitimiza ahadi, EL Waziri Mkuu!.

Dili la Richmond lilivyokuja, ni dili la mzee mzima mwenyewe!, hata vile vimemo vya EL yeye alikuwa ni mjumbe tuu au tarishi wa mwenye mali! dili Richmond lilipobackfire, ndipo RA na EL wakatumia Dowans kumnusuru muzeiye! Sitta anajua, na kwa vile na yeye 2015 alijipanga kuingiza karata yake, kupitia vijana wa TISS, wakafanya utambuzi yakinifu na kupata ushahidi wa vimemo vya EL. Sitta akamtumia Mwakyembe kumtundika msalabani EL na kumsulubisha moja kwa moja bila kumuuliza chochote!.

Kwa vile l;engo lilikuwa ni kumsulubu EL, wakati wote wa uchunguzi, EL na RA hawakuwa na wasiwasi wowote, kwa vile walijiaminisha, maadam game ni la muzeiye, basi muzeiye akalipumch na kuzuia lisifumke, ndio maana kina Hosea walikuwa na viburi vya ajabu!. Kabla ripoti haijatoka, JK alishaiona, EL alishaiona na aliyeipeleka kote huko ni SS, JK alitoa go ahead EL akaangwe ili CCM inusurike, vingenevyo SS angeliomgoza bunge kwenye impeachment!. Hivyo EL akatolewa kafara, muzeiye akapona, CCM ikapona na hapo sasa ndipo vita mpya ikaanza!.

The King Maker (RA), akajiapiza, lazima atawashughulikia vimbembele wote kwenye kamati ya Mwakiembe wakianzia na SS, na kusema ukweli, faranga ilitembezwa, waliosalimika kama SS ameponea tundu la Sindano la huruma ya JK na walijiundia safe heaven ya CCJ ili watimkia kule, milango ikafungwa, SS akapiga magoti CCM ndia salama yake, hata huo uspika akapigwa chini, Selelii kilichomkuta mnakijua ilimradi ni piga ua!.

Baada ya JK kuridi 2010, akamshukuru Mwakyembe kwa kumnusuru, na asanye SS kwa kuto mu impeach, akijiaminisha EL ataendelea kunyamaza, na infact EL aliamua kunyamaza kimya kabisa!. Kilichomtibua ni vuvuzela la kile kitoto kijinga jinga ambacho kinapuliza vuvuzela la ufisadi as if hakijua nani ndio mafisadi halisi ndani ya CCM!, nawahakikishia mwisho wake ni uchaguzi wa CCM mwakani!.

Sasa kinachoendelea, nadhani RO ni implant ya RA pale TISS hivyo they are not sure EL atanyamaza mpaka lini!, hivyo the only way ni au wamshughulikie au wampe anachotaka ambacho ni urais 2015!. JK ni powerless with nothing to do maana EL ndio kashika mpini mtake msitake, mkubali msikubali
El in this game, "this (EL) is the name of the game!.
 
By The Boss swali hapa ni hilik
ama huyo kingmaker ana nguvu saana
why alijiuzulu na kukubali kuitwa fisadi????????




The boss ht mimi nilijiuliza hilo swali ila nikajipa jibu kwamba rostam ni very smart pamoja na kujiweka kando lkn bd akawa na nguvu ya kupanga nani na nani wawepo kwenye kampeni, huyu jamaa ni hatari.

Jamaa ana nguvu kuliko maelezo mmesahau mwaka jana kwenye uchaguzi yeye ndiye aliyesimamia uaandaaji wa karatasi za kura huko kwa madiba? na siku moja kabla hazijaingia tz yeye ndio akaingia? mnajua kwenye karatasi za kura za wabunge na rais zilifanyiwa mafyoso? unajua dr slaa kura zake zilitangazwa kwa kukadiriwa badala ya kusabiwa? mnajua yeye ndio alioimaliza cdm na slaa? ilifahamika karatasi za uraisi mwaka 2010 ziliweza kubatilishwa au kufutwa kwa tone la maji kwenye jina la mgombea slaa na kujaza jk?

sikulazimishi kuamini wala sitaki maswali ni uchunguzi wangu binafsi kushirikiana na wataalamu wengine.
 
Upuuzi! Very simple brain washed! Aaaaaaagh!!!

EL For CCM Chairman 2012 and Eventualy CCM Presidential Candidate for 2015, We believe there is only one in CCM for 2015 and that is Laig'wanani Lowasa
 
Theories on politics are allowed.. however do not be fooled...

By the way poilitcs means -poli-TRICKS

Atakayeshinda ni mwenye tricks nzuri; na EL hana tricks na tricks zake zote zina leak..so easily

Aliyekuwa anawasaidia kwenye ule mtandao ni JK kiasi kwamba aliweza kuwa lead (provide leadership qualities) hata trikcs hazileak na kuwa successfully with all odds and resistance from the within the party..

Mtandao wa EL hauna tena mtu makini ..wala mtandao wa sitta hauna watu makini..tricks zao zina leak easily (no leadership kama iliyokuwepo wakati wa JK)

Nani atachaguliwa hawezi kuwa EL wala SS; you will be surprised..
 
Theories on politics are allowed.. however do not be fooled...

By the way poilitcs means -poli-TRICKS

Atakayeshinda ni mwenye tricks nzuri; na EL hana tricks na tricks zake zote zina leak..so easily

Aliyekuwa anawasaidia kwenye ule mtandao ni JK kiasi kwamba aliweza kuwa lead (provide leadership qualities) hata trikcs hazileak na kuwa successfully with all odds and resistance from the within the party..

Mtandao wa EL hauna tena mtu makini ..wala mtandao wa sitta hauna watu makini..tricks zao zina leak easily (no leadership kama iliyokuwepo wakati wa JK)

Nani atachaguliwa hawezi kuwa EL wala SS; you will be surprised..

Acha kujihadaa Mkuu

By the way Heri ya Mwaka Mpya
 
By swali hapa ni hilik
ama huyo kingmaker ana nguvu saana
why alijiuzulu na kukubali kuitwa fisadi????????.
Alijiuzulu kupisha kero la CCM na sasa ndio ataonyesha yeye ni nani,
Yeye ndiye alimuweka JK pale alipo, akamuweka SS, akamtoa SS akamuweka Anna, 2015 anamuweka EL!
Davis Mwamunyange ni mtu wake!, Rashid Othman ni mtu wake!, Said Mwema ni mtu wake!, Othman Chande ni mtu wake!, Mama Spika ndio usiseme, ndani ya NEC na CC yake ni njaa tupu, nenda kashuhudie foleni pale kwake jinsi ombaomba hawa wanavyojipanga kusubiria chochote!, what does JK has?, nothing!, just nothing at all!.
 
Alijiuzulu kupisha kero la CCM na sasa ndio ataonyesha yeye ni nani,
Yeye ndiye alimuweka JK pale alipo, akamuweka SS, akamtoa SS akamuweka Anna, 2015 anamuweka EL!
Davis Mwamunyange ni mtu wake!, Rashid Othman ni mtu wake!, Said Mwema ni mtu wake!, Othman Chande ni mtu wake!, Mama Spika ndio usiseme, ndani ya NEC na CC yake ni njaa tupu, nenda kashuhudie foleni pale kwake jinsi ombaomba hawa wanavyojipanga kusubiria chochote!, what does JK has?, nothing!, just nothing at all!.

Off Topic Mkuu Pasco

Unaweza kuanzisha Thread ya Kumhusu Mtu aliyekuwa anaitwa James Mapalala? Yuko wapi sasa hivi na Ilikuwaje Hasikiki CUF pamoja na kwamba alikuwa mmoja wa waanzilishi wa CUF

Beki To Ze Point

EL for CCM 2015
 
Theories on politics are allowed.. however do not be fooled...

By the way poilitcs means -poli-TRICKS

Atakayeshinda ni mwenye tricks nzuri; na EL hana tricks na tricks zake zote zina leak..so easily

Aliyekuwa anawasaidia kwenye ule mtandao ni JK kiasi kwamba aliweza kuwa lead (provide leadership qualities) hata trikcs hazileak na kuwa successfully with all odds and resistance from the within the party..

Mtandao wa EL hauna tena mtu makini ..wala mtandao wa sitta hauna watu makini..tricks zao zina leak easily (no leadership kama iliyokuwepo wakati wa JK)

Nani atachaguliwa hawezi kuwa EL wala SS; you will be surprised..
SS is history!, ila nimegundua wewe ni mtu wa timu ya joka la mdimu, yule mzee wa kimbelembele, kujikomba komba komba na kujipendekeza!, ndugu yangu, lili ni boya tuu, sio tuu linaelea, bali halina hata kamba, hivyo litaperushwa hata na upepo!.

Joka la mdimu, kama ni mti, basi ni mpapai dume, haufai kwa kivuli, kwa kuni tena wala hauzai matunda!, sasa unataka kuulinganisha na kisiki cha mpingo!.

Welcome on board!.
 
"Sasa kinachoendelea, nadhani RO ni implant ya RA pale TISS hivyo they are not sure EL atanyamaza mpaka lini!, hivyo the only way ni au wamshughulikie au wampe anachotaka ambacho ni urais 2015!. JK ni powerless with nothing to do maana EL ndio kashika mpini mtake msitake, mkubali msikubali
El in this game, "this (EL) is the name of the game!."

Mkuu Pasco,
Uchambuzi mzuri umetupa katika kutukumbusha yale ambayo tunayajuaa. Na yale ambayo hatuyajui ni dhana kama hitimisho lako,"Unadhani Rostam" ndio kainfluensi kuwapo kwa Othmai TISS.
Je si Dhana hiyo hiyo kwamba Rostam alitumia Pesa kuwasambaratisha waliomsulubisha Lowassa? (kwanza Lowassa kasulubiwa au Kajisulubisha?).
Je Unweza kutupa Dhana ni Vipi huyu Mtengeza Wafalme (Rostam) anavyofanya kazi zake mpaka anafanikisha Malengo yake?(Anaopareti vipi?).
 
Back
Top Bottom