mtoahabari
Member
- Dec 27, 2011
- 76
- 223
Na usikute ni wao waliomuweke Othman Chande pale alipo!, then wao ndio the most powerful persons in Tanzania!, usikute hata ni hao hao ndio waliyemuweka Rashid Othman pale alipo!, usikute ndie waliyemuweka Said Mwema pake alipo!, usikute ndio waliyemuweka Davis Mwamunyange pale alipo!, usikute ndo waliomuweka Hosea pale alipo!, and the list goes on...then if that is true, hii inamaanisha 100% sure 2015 ni Lowassa!. Hii inamaanisha JK na serikali yake yote si chochote, si lolote kwa watu hawa! This is not a joke!.
Hakuna siri ndani ya TISS, kwamba RO aliwekwa na ENL na RA, chini ya usimamizi wa Abson. Chaguo lingine la mtu wa kumrithi Abson, mbali ya RO, lilikuwa ni pamoja na watu kama Job Masima, ambae kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi. Kilichomnyima Masima nafasi hiyo ni pamoja na ubinamu wake na Mzee Malecela. Vinginevyo, Masima bado ni mtu wa karibu sana kina Abson, ENL, RA.
Licha ya kustaafu mwaka 2008, Abson bado ana nguvu kubwa sana ndani ya TISS. Lakini vilevile, Hassy Kitine pia bado ana wafuasi wengi sana TISS. Suala hili lina historia ndefu kidogo. Kuna mtu anaitwa Mwambulukutu - huyu alikuwa balozi wa Tanzania Afrika Kusini kipindi fulani. Miaka ya awali ya 1970s, Mwambulukutu aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Personal and Administration, TISS, chini ya Hassy Kitine, ambae alikuwa Mkurugenzi Mkuu. Mwambulukutu na Kitine walipewa jukumu na Nyerere kuifumua idara ya usalama na kuindua upya na kuzaa TISS miaka ya mwanzo ya 70. Hatua hiyo ilitokana na Nyerere kugundua kwamba mfumo uliorithiwa baada ya ukoloni ungemletea shida baadae. Ni Mwambulukutu ndiye alim discover Bernard Membe na kumwajiri TISS na kum groom, pamoja na vijana wengine kadhaa. Na membe huwa yupo muwazi sana juu ya suala hili. Pia katika miaka ya 70 kulitokea tatizo la kiutendaji kwa upande wa Abson, hivyo kupelekea Kitine kumfukuza kazi mara moja, Abson, lakini Mwambulukutu ndiye aliemwokoa kwa kumuombea msamaha Abson kwa Kitine. Msamaha huo ndio uliomwokoa Abson mpaka kustaafu kwake 2008.
Miaka ya 2006-2007, kulikuwa na tetesi kwamba Mwambulukutu alikuwa anarudi Tanzania kuja chukua nafasi ya RO pale TISS, kwani RO hakubaliki na upande wa JK. Na kwa muda mrefu sana, RO na Mwambulukutu hawakuwa wanaiva, kwani mara kadhaa wamekuwa na migongano. Mwambulukutu ana mwanae mmoja ambae alikuwa TISS tangia kipindi cha Mkapa, lakini inasemekana kwamba tofauti zake na RO kikazi, zikapelekea RO kumsimamisha kazi kijana huyo. Vile vile kuna tetesi zilizopo kwenye corridor za TISS ni kwamba ajali iliyomkumba Mwambulukutu mwaka 2007 nchini Afrika ya Kusini, lilikuwa ni jaribio la makusudi la kuchukua maisha yake. Tetesi ni kwamba majambazi yalikodiwa kutoka msumbiji, Zimbabwe na Afrika ya kusini, na ENL, RO, RA, na maafisa wa TISS ubalozini Afrika Kusini walikuwa wana ufahamu mpango wote, hatua kwa hatua. Na hata uvamizi huo ulipotokea, uchunguzi wa kipolisi ukafutwa haraka sana kwa maombi kutoka Dar-es-salaam. Na hata Rais Mbeki kwenda kumpa pole Mwambulukutu hospitali, ilikuja baada ya Mbeki kuomba ruksa rasmi Ikulu Dar-es-salaam, kitu ambacho Kikwete alikiruhusu mara moja. Inasemekana pia kwamba Abson alitumwa rasmi na serikali kwenda Afrika ya Kusini kuweka mambo sawa.
Zipo juhudi za chini kwa chini za kumwondoa RO TISS lakini zinagonga mwamba kutokana na mkono wa kina RA na EL. RO amekuwa ni kero kwa JK, kwani uaminifu wake upo zaidi kwa ENL, RO, January, Abson na wengineo katika kundi hilo. ENL, RA pia ndio waliomweka Mwamnyange na Said Mwema kwenye nafasi zao za sasa. Safari ya ENL 2015 ina mizizi mirefu, na haitakuwa rahisi kumzuia katika nafasi hiyo. TISS imegawanyika katika makundi matatu Kundi la waadilifu (watu wa Nyerere kama kina Kitine n.k), Kundi linalowaunga mkono RA, ENL, Abson, January, na kundi dogo linalomuunga mkono Kikwete. Kinachompa nguvu ENL pia ni kuungwa kwake mkono na Balozi na taasisi nyingi za kimataifa zilizopo Tanzania. Kwa wote hawa, chaguo lao kwa 2015 ni ENL, kutokana na uchapa kazi wake, pamoja na mtindo wake wa uongozi ambao wanasema unaendana sana na matakwa ya wawekezaji.