Pamoja na umuhimu wa mjadala huu kwetu kama vijana, lakini ni dhahiri kabisa kwamba wanasiasa wote hawa miaka 15 - 20 ijayo watakuwa wastaafu wakipumzika na familia zao, huku vijana wengi humu tukiwa bado hata kufikisha miaka 50, na wengine wengi tu chini ya miaka 40. Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa hafifu sana, ni muhimu tujikite katika mjadala huu huku tukitambua hilo, na muhimu zaidi, kwa vision ya miaka 15 - 20 kutoka sasa, ambapo na sisi tutakuwa mbioni kuwaachia watoto wetu na wajukuu zetu taifa lililo imara. Ni muhimu sana kwa vijana sasahivi, kuchagua upande sahihi wa historia ya nchi hii 2011 and beyond, kuliko kuja juta na kusaga meno baadae kwa kujikuta walichagua the wrong side kwa uzembe, tamaa, ama uwoga.
Jukumu la kuamua upande upi ndio upande ndio the right side of history ni wa kijana mwenyewe, mmoja mmoja, bila ya kuingiliwa na mtu yoyote kwani huo ni uhuru na haki ya kila mtu. Zaidi ya hivyo, ni kukumbushana tu kwamba, unlike safari ya hawa wanasiasa tunaowataja taja humu ambao safari yao kisiasa itafikia ukiongoni miaka sio mingi kutoka sasa, wakiwa wastaafu HAI au HOI, safari yetu sisi kama vijana bado ni ndefu sana, na ile ya watoto na wajukuu wetu ndio ndefu zaidi, na itategemea tunafanya maamuzi gani leo i.e. between 2012 and 2015.