Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Sina taarifa za kina juu ya hilo mbali ya kuwa na taarifa kwamba Mbowe na kina ENL, RA, wana ukaribu sana, na miaka ya nyuma walikuwa wanakunywa bia pamoja. Vilevile ENL, RA, wamefanikiwa kumteka Zitto. Homa kubwa waliyonayo ni kwa watu kama Lissu. Hata Mkuu wa nchi aliwahi sikika akitamka wakati wa kampeni za Urais mwaka jana kwamba ni mara mia kuwa na Slaa Ikulu kuliko kuwa na Lissu bungeni. Natumaini nimekuwa angalau maoni yangu kwa wewe kuyatafakari.

nilikuuliza kuhusu TISS yenye wafuasi wa Kitine/Nyerere
wamekubali EL awe Rais?
na Mwambulukutu je kasamehe??????
 
habari za mbowe kupewa bilioni tatu za maandalizi hukupata?
mwaka 2005????

Taarifa hizo zilikuwepo, lakini binafsi siwezi kuzitolea ushahidi kwani sina, na yanasemwa mengi sana. Kilichokuwa dhahiri ni kwamba, Mwaka 1995, Kikwete na ENL walitishia kuhamia Chadema kwani waliona CCM haikuwatendea haki mwaka 1995, na historia ile ilikuwa inataka kujirudia tena mwaka 2005. Na walishaanza maandalizi ya chini kwa chini ambayo taarifa zake hazina tofauti na zile za CCJ - sio taarifa zilizopo rasmi TISS, Tume ya Uchaguzi, au CCM yenyewe, bali mikononi mwa wahusika wenyewe.
 
nilikuuliza kuhusu TISS yenye wafuasi wa Kitine/Nyerere
wamekubali EL awe Rais?
na Mwambulukutu je kasamehe??????

Wafuasi wa Nyerere kilichobakia hivi sasa ni kulaumu utendaji mbovu wa serikali na ukiukwaji wa maadili wa viongozi, sana sana baada ya ENL kujiuzulu. Kina Warioba, Salim, Butiku, Kaduma, Kitine n.k. wanakerwa na mwenendo wa sasa wa nchi - kiutendaji na miiko ya maadili ya uongozi, na kama wanatofautiana na ENL, basi ni chini kwa chini, vinginevyo hakuna taarifa za wazi juu ya kumkubali au kumkataa ENL moja kwa moja.

Kuhusu Mwambulukutu kusamehe, kama nilivyoeleza awali, taarifa juu ya njama juu ya mauaji yake ni tetesi tu miongoni mwa maafisa wa TISS ambazo zimekuwa zinazagaa tangia mwanzoni mwa mwaka 2008. Vinginevyo sina taarifa zaidi kwani Mwambulukutu kwa hivi sasa ametoweka katika jamii/vijiwe, kwahiyo maoni au mtazamo wake juu ya jambo lolote ni vigumu kusikia kwa sasa. Vinginevyo, Mwambulukutu alikuwa na ukaribu sana na ENL, Kikwete, na Apson, na hakukutana nao wote hawa barabarani, bali ni mahusiano ya muda mrefu ya kifamilia.
 
@mtoahabari, pasco et al......Nikuulize tu mambo kadhaa ya msingi......kama umeamua kufunguka ki ukweli...maana kama uko karibu na Lowasa basi utakuwa unajua yanayoendelea serikalini......ebu jibu.....hivi hawa jamaa unaowazungumzia kina Lowasa et al papoja na JK.(watawala)....pamoja na hizi siasa za makundi ktk vinyang'anyiro vya urais tz....huwa wanafikiria kuwatumikia wananchi wao maskini walio wengi??maana mnajadili hizi siasa wakati nchi ina hali mbaya sana hii kiuchumi......hawa TISS mnaowazungumzia.....je wanaliweka wapi jeshi la nchi hii tz katika hizi harakati za urais nchi hii??maana mnazungumzia TISS mnasahau kuwa jeshi likigoma hamna cha TISS wala mama zao eh???maana hapa naona siasa mnazojadili zimeingia mpaka kwenye issue za security ya nchi(TISS)....kama kuna watu kama kina Lowasa wanaweza kuwa na influence kwenye utendaji wa TISS wakati hawako madarakani na hili nyie mnaliona sawa hivi hamjiulizi kuwa nchi inakoelekea siko??????au imepotea tayari???ebu jibuni swali je hamwoni nchi ina ombwe kubwa la kiungozi? maana amini msiamini ni hivi majuzi tu nimekuwa nikiongea na wanajeshi wa ngazi za chini ambao wamechoka mbaya na maisha na mwenendo mzima wa utawala wa nchi ..........na nilipowauliza je wao wanasemaje wakajibu ......wanawasubiri wananchi walianzishe tu kinuke jumla (Egypt style).....sasa hamwoni kwamba hali hii si nzuri????.....labda tu tukumbushane......kama TISS wanainfluence madaraka nchi hii kama mlivyo jadili juu.......ikumbukwe kuwa iko siku maskini wa tz watatoka barabarani......wakishirikiana na vyama pinzani vilivyo makini na kudai kilicho chao kwa watawala na hakutakuwa na TISS wala mama zao????.........maana naona hapa mnawajadili mafisadi kama viongozi weu wa kesho......yaani imefikia tz watu ambao ni mafisadi(e.g Lowasa)wanajadiliwa positively kuchukua madaraka ya nchi?????iko wapi haki ya maskini hapa sasa???na kwanini hamna mjadala wa possibility ya opposition party kuchukua dola???au hili mnaliona haliwezekani????mnasahau yaliyotokea juzi tu Egypt,Tunisia na Libya???(nguvu ya umma)........mnajadili kama vipofu msioona mabadiliko ya kweli yanayotokea sehemu nyingine nyingine ambapo watu walichoka na tawala kama hii mnayojadili????.......wake up you guys.......only time will tell........mia
 

Bwana Nderingosha,
Nashukuru sana kwa swali lako. Una hoja nyingi sana na za msingi kabisa. Ila ukumbuke kwamba nilichokieleza ni ufahamu wangu juu ya hali halisi ilivyo, sio ushabiki. Na kuhusu TISS na maslahi ya nchi, ni dhahiri kwamba TISS ya sasa sio ile ya Kitine, au Maiga, kwani kwa sasa qwngi mle wapo kwa ajili ya maslahi binafsi. Hapo nyuma, baadhi yao walikuwa wanaona kama vile ENL ndiye mvurugaji, lakini baada ya ENL kumvua nguo Mkuu wa nchi Dodoma majuzi, na mkuu kukaa kimya, vijana wengi wa TISS wameanza kuhamia kwa ENL, wakidai anaonewa, lakini ni mvumilivu, na mchapa kazi, hivyo anastahili kuchukua jahazi. Lakini kama ulivyotamka mwenyewe, wenye nchi hii ni UMMA, kwani wao ndio wenye maamuzi ya mwisho, sio TISS, CCM, wala JWTZ. Pia taarifa kwamba wanajeshi ngazi za chini wamechoka, na huwa wanatoa matamshi makali sana kila mara milipuko ya mabomu inapotokea kwenye kambi. Wengi huwa wanatamka kwamba kuna umakusudi. Na kibaya zaidi ni kwamba wanajeshi wa ngazi za chini na polisi hawapo katika meli moja kuhusu masuala mengi juu ya nchi hii. Lakini ni muhimu tukumbuke pia kwamba JWTZ ni taasisi yenye nidhamu na utiifu wa hali ya juu sana, na JWTZ kama taasisi, ina ushirikiano wa karibu sana wa kikazi na TISS. Hiyo ilikuwa ni sehemu ya kazi maalum ya Kitine (Kanali Mstaafu), chini ya Nyerere.

Baada ya kusema yote haya, tunarudi kwenye ukweli kwamba, pamoja na mapungufu yake mengi na tuhuma nyingi mbali ya Richmond, ENL amejipanga vya kutosha kuwa rais wa tano wa Tanzania. Sio CCM, wala Tume ya Uchaguzi (NEC), itakayoweza kubadilisha ndoto yake, bali UMMA kwa njia ya UMMA, sio UMMA kwa njia ya KURA. Umma hautafanikiwa kumzuia ENL kupitia sanduku la KURA, bali kwa njia ya maandamano na mgomo wa UMMA kama huko Libya, Tunisia na Misri na kwingineko ulipopataja, iwapo ENL atatangazwa kuwa Rais wa Tano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) 2015. Lakini hii haina maana kwamba upinzani hauna nafasi 2015, lakini kama tetesi juu ya ENL, RA, wakisaidiwa na vijana wao Bashe na January, kukisaidia CHADEMA kwa fedha na mikakati kishinde uchaguzi mdogo wa Igunga, ni za kweli, ni vigumu kupata kuelewa ni jinsi gani wataweza upinzani utaweza kumzuia ENL na timu yake mwaka 2015.
 
Bwana Nderingosha,
Umma hautafanikiwa kumzuia ENL kupitia sanduku la KURA, bali kwa njia ya maandamano na mgomo wa UMMA kama huko Libya, Tunisia na Misri na kwingineko ulipopataja.
Mhn! mtoahabari you're kind of Arrogant lol

BTW i am more interested on that..
 
Ama kweli wahenga walinena usilolijua ni sawa na usiku wa kiza!
 
Natumaini lakini pia kwamba umeelewa mtiririko mzima wa majibu yangu kwa Nderingosha, kwani ulichokinukuu hapo juu ni sehemu ndogo tu ya majibu yangu kwake.
Mkuu kwani sehemu hiyo ndogo haina maana hiyo iliyoko kwenye sehemu hiyo?

Mbona ni kama a sentence "that carries pararagraphs"?

Mtiririko nimeupata, lakini the fact kwamba kura hazitupatii viongozi really is disturbing.
 
Pamoja na umuhimu wa mjadala huu kwetu kama vijana, lakini ni dhahiri kabisa kwamba wanasiasa wote hawa miaka 15 - 20 ijayo watakuwa wastaafu wakipumzika na familia zao, huku vijana wengi humu tukiwa bado hata kufikisha miaka 50, na wengine wengi tu chini ya miaka 40. Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa hafifu sana, ni muhimu tujikite katika mjadala huu huku tukitambua hilo, na muhimu zaidi, kwa vision ya miaka 15 - 20 kutoka sasa, ambapo na sisi tutakuwa mbioni kuwaachia watoto wetu na wajukuu zetu taifa lililo imara. Ni muhimu sana kwa vijana sasahivi, kuchagua upande sahihi wa historia ya nchi hii 2011 and beyond, kuliko kuja juta na kusaga meno baadae kwa kujikuta walichagua the wrong side kwa uzembe, tamaa, ama uwoga.

Jukumu la kuamua upande upi ndio upande ndio the right side of history ni wa kijana mwenyewe, mmoja mmoja, bila ya kuingiliwa na mtu yoyote kwani huo ni uhuru na haki ya kila mtu. Zaidi ya hivyo, ni kukumbushana tu kwamba, unlike safari ya hawa wanasiasa tunaowataja taja humu ambao safari yao kisiasa itafikia ukiongoni miaka sio mingi kutoka sasa, wakiwa wastaafu HAI au HOI, safari yetu sisi kama vijana bado ni ndefu sana, na ile ya watoto na wajukuu wetu ndio ndefu zaidi, na itategemea tunafanya maamuzi gani leo i.e. between 2012 and 2015.


 
mtoboasiri, nasikitika kuona kwamba umesign out all over a sudden.
 
jmushi1 ni lini kura zimeleta viongozi tanzania? ni lini?........hakuna hata siku moja......halafu wiki ijayo tunaweza kupita na dada huko kwako...
 
Hutaki Unaacha sijui kasahau password ya kuingilia JF? Maana part 2 tunaisubiri kwa hamu...
 
Pamoja na umuhimu wa mjadala huu kwetu kama vijana, lakini ni dhahiri kabisa kwamba wanasiasa wote hawa miaka 15 - 20 ijayo watakuwa wastaafu wakipumzika na familia zao, huku vijana wengi humu tukiwa bado hata kufikisha miaka 50, na wengine wengi tu chini ya miaka 40. Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa hafifu sana, ni muhimu tujikite katika mjadala huu huku tukitambua hilo, na muhimu zaidi, kwa vision ya miaka 15 - 20 kutoka sasa, ambapo na sisi tutakuwa mbioni kuwaachia watoto wetu na wajukuu zetu taifa lililo imara. Ni muhimu sana kwa vijana sasahivi, kuchagua upande sahihi wa historia ya nchi hii 2011 and beyond, kuliko kuja juta na kusaga meno baadae kwa kujikuta walichagua the wrong side kwa uzembe, tamaa, ama uwoga.

Jukumu la kuamua upande upi ndio upande ndio the right side of history ni wa kijana mwenyewe, mmoja mmoja, bila ya kuingiliwa na mtu yoyote kwani huo ni uhuru na haki ya kila mtu. Zaidi ya hivyo, ni kukumbushana tu kwamba, unlike safari ya hawa wanasiasa tunaowataja taja humu ambao safari yao kisiasa itafikia ukiongoni miaka sio mingi kutoka sasa, wakiwa wastaafu HAI au HOI, safari yetu sisi kama vijana bado ni ndefu sana, na ile ya watoto na wajukuu wetu ndio ndefu zaidi, na itategemea tunafanya maamuzi gani leo i.e. between 2012 and 2015.


Mkuu nimekuelewa sana! Lakini kwa complication hizi,nguvu zimeisha! Sijui tutoke vipi!
 
Niliwahi kusema upinzani bongo utachukua nchi miaka 15 ijayo nikaonekana kituko!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hizi hadithi za sungura na fisi zitaendelea huku mkitafuta vyanzo na vyanzo mtakapo jikuta kila mmoja akimhisi vibaya mwenzake ndo mtajua kuwa ilikuwa hivyo kwa kuta za Jerico kudondoka. Hakuna kati yenu ninyi atakaye kanyaga Ikulu sikieni tena kwa sauti kubwa HAKUNA mtengeneze mitando mtando utandao it does not make any difference.....Not again in my country dead or alive hakuna tena!
 
inavoonekana hapa Mtoa habari na Hutaki Unaacha ni kama watoto mapacha walio sare. Nina wasiwasi kuwa huenda ni mtu yuleyule. Tuendelee na mjadala wetu.
 
nchi hii sijui tunakoelekea! Natamani bomu lilipuke na kuwafukia wote wanaotajwa ili tuanze upya... maana naona sie watoto wa wanyonge tuishia kuwa vibarua no chances for prospering in any how akitoka huyu anampendekeza shoga ake, shost, swahiba n.khuu ni uhuni na si kitu cha kushangilia either side la sivyo yatatukuta! Yangu macho nione mwisho wa movie hii
 
Back
Top Bottom