Unajua siasa za Bongo hazitakiwi kufikiria kisheria ama kuna utaratibu.. Ni sawa na maisha ya wananchi wenyewe ya Kimachinga, yaani kila siku unaamka asubuhi unaenda itafuta riziki na jioni ukirudi nyumbani mkeo anakuuuliza umeshindaje?... akiwa na maana kipi kimepatikana leo?..Kimsingi Tanzania mapato ya jana sii ya leo wala ya kesho kila mtu ni machinga ktk services za kuzungusha (Udalali na ulanguzi) wakati huku majuu mfanyakazi una malipo yale yale siku hadi siku ukibamiza zaidi itakuwa imetokana na overtime ama kazi mbili - sana sana ukichomoza basi unauza Unga!.Mkuu Mkandara, there you are, now we sail the same boat!, now join the team, tumsafishe Lowassa, tumpake mafuta angare na kumeremeta, na tumpulizia manukato ya manemane anukie vizuri kila apitapo harufu ya kunukia inatangulia, hivyo kuwavuta wote wapendao vingaavyo na vinukiavyo!.
Now join the timu, sio lazima ki waziwasi kama sisi, hata kwa kunyamaza tuu na kutombomoa zaidi Lowassa, hiyo inatutosha!
Welcome on board!
Kufupisha ukweli huu ni kwamba Siasa za Bongo zinatisha... Na hii ndio reality ambayo inauma sana kuisikia wala kuiwazia lakini ndio ukweli..CCM wataendelea kutuburuza na wakitaka Lowassa atawale atatawala, wakitaka kumweka mtu mwingine wataweza na nadhani utabiri wa Nyerere ndio wenye uhakika zaidi kwamba Upinzani utatoka CCM kwa maana kwamba demokrasia ya vyama vingi haiwezi kuiangusha CCM aloijenga. Ikumbukwe tu Nyerere aliyasema haya akijibu hoja ambazo wanaCCM wenyewe walikuwa na mashaka na mfumo wa vyama vingi, hivyo majibu alikuwa akiwapa wao wana CCM... na sio sisi tulojiengua, that's how confi jamaa alikuwa na chama chake.
Na mimi naamini hivyo kwamba kutokea kwa makundi ndani ya CCM pekee ndiko kunaweza kuiangusha CCM ama WANANCHI wenyewe kwa ujumla wetu..Na nafasi hiyo tulikuwa nayo mwaka 2010kupitia sanduku la kura kulenga kiti cha rais tu. Na ndio maana nilipendekeza Dr.Slaa nikijua Chadema hawawezi kumshinda CCM majimbo lakini wakiweza wapata ushindi wa kitu kikubwa - Ikulu, ndio utakuwa mwisho wa CCM kama nyoka aliyekatwa kichwa..
Yet again, JK katushinda kwa mbinu ambazo zimedhihirisha kwamba CCM hata ukimshtukiza bado wamekamata sehemu zote za Dola na hivyo huwezi kumshinda kwa sanduku la kura. Na kusema kweli mimi naamini kabisa kwamba hakuna chama kinachoweza kumshinda CCM kupitia sanduku la kura - Hakuna... Hizi siasa zetu za UChadema, UCUF na kadhalika ni kujifurahisha kama ushabiki wa Mpira wengine MaU ,Arsenal, Chelsea na kadhalika ili mradi ushinda upo na maisha yanaendelea league kuu..
The only way CCM inaweza kuanguka iko sehemu mbili tu:-
1. CCM wenyewe wakivurugana na kusambaratika
2. WANANCHI wakichukua jukumu la kudai Uhuru wao wenyewe iwe kwa maandamanao ama migomo
Hakuna ushindi kupitia sanduku la kura hilo wananchi wasahau na kama CCM itamweka Lowassa basi atapita na tutaendelea kucheza ngwasuma na kiduku. Huu ndio ukweli unaouma sana lakini ndio - REALITY!