Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)


Hakuna siri ndani ya TISS, kwamba RO aliwekwa na ENL na RA, chini ya usimamizi wa Abson. Chaguo lingine la mtu wa kumrithi Abson, mbali ya RO, lilikuwa ni pamoja na watu kama Job Masima, ambae kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi. Kilichomnyima Masima nafasi hiyo ni pamoja na ubinamu wake na Mzee Malecela. Vinginevyo, Masima bado ni mtu wa karibu sana kina Abson, ENL, RA.
Licha ya kustaafu mwaka 2008, Abson bado ana nguvu kubwa sana ndani ya TISS. Lakini vilevile, Hassy Kitine pia bado ana wafuasi wengi sana TISS. Suala hili lina historia ndefu kidogo. Kuna mtu anaitwa Mwambulukutu - huyu alikuwa balozi wa Tanzania Afrika Kusini kipindi fulani. Miaka ya awali ya 1970s, Mwambulukutu aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Personal and Administration, TISS, chini ya Hassy Kitine, ambae alikuwa Mkurugenzi Mkuu. Mwambulukutu na Kitine walipewa jukumu na Nyerere kuifumua idara ya usalama na kuindua upya na kuzaa TISS miaka ya mwanzo ya 70. Hatua hiyo ilitokana na Nyerere kugundua kwamba mfumo uliorithiwa baada ya ukoloni ungemletea shida baadae. Ni Mwambulukutu ndiye alim discover Bernard Membe na kumwajiri TISS na kum groom, pamoja na vijana wengine kadhaa. Na membe huwa yupo muwazi sana juu ya suala hili. Pia katika miaka ya 70 kulitokea tatizo la kiutendaji kwa upande wa Abson, hivyo kupelekea Kitine kumfukuza kazi mara moja, Abson, lakini Mwambulukutu ndiye aliemwokoa kwa kumuombea msamaha Abson kwa Kitine. Msamaha huo ndio uliomwokoa Abson mpaka kustaafu kwake 2008.

Miaka ya 2006-2007, kulikuwa na tetesi kwamba Mwambulukutu alikuwa anarudi Tanzania kuja chukua nafasi ya RO pale TISS, kwani RO hakubaliki na upande wa JK. Na kwa muda mrefu sana, RO na Mwambulukutu hawakuwa wanaiva, kwani mara kadhaa wamekuwa na migongano. Mwambulukutu ana mwanae mmoja ambae alikuwa TISS tangia kipindi cha Mkapa, lakini inasemekana kwamba tofauti zake na RO kikazi, zikapelekea RO kumsimamisha kazi kijana huyo. Vile vile kuna tetesi zilizopo kwenye corridor za TISS ni kwamba ajali iliyomkumba Mwambulukutu mwaka 2007 nchini Afrika ya Kusini, lilikuwa ni jaribio la makusudi la kuchukua maisha yake. Tetesi ni kwamba majambazi yalikodiwa kutoka msumbiji, Zimbabwe na Afrika ya kusini, na ENL, RO, RA, na maafisa wa TISS ubalozini Afrika Kusini walikuwa wana ufahamu mpango wote, hatua kwa hatua. Na hata uvamizi huo ulipotokea, uchunguzi wa kipolisi ukafutwa haraka sana kwa maombi kutoka Dar-es-salaam. Na hata Rais Mbeki kwenda kumpa pole Mwambulukutu hospitali, ilikuja baada ya Mbeki kuomba ruksa rasmi Ikulu Dar-es-salaam, kitu ambacho Kikwete alikiruhusu mara moja. Inasemekana pia kwamba Abson alitumwa rasmi na serikali kwenda Afrika ya Kusini kuweka mambo sawa.

Zipo juhudi za chini kwa chini za kumwondoa RO TISS lakini zinagonga mwamba kutokana na mkono wa kina RA na EL. RO amekuwa ni kero kwa JK, kwani uaminifu wake upo zaidi kwa ENL, RO, January, Abson na wengineo katika kundi hilo. ENL, RA pia ndio waliomweka Mwamnyange na Said Mwema kwenye nafasi zao za sasa. Safari ya ENL 2015 ina mizizi mirefu, na haitakuwa rahisi kumzuia katika nafasi hiyo. TISS imegawanyika katika makundi matatu – Kundi la waadilifu (watu wa Nyerere kama kina Kitine n.k), Kundi linalowaunga mkono RA, ENL, Abson, January, na kundi dogo linalomuunga mkono Kikwete. Kinachompa nguvu ENL pia ni kuungwa kwake mkono na Balozi na taasisi nyingi za kimataifa zilizopo Tanzania. Kwa wote hawa, chaguo lao kwa 2015 ni ENL, kutokana na uchapa kazi wake, pamoja na mtindo wake wa uongozi ambao wanasema unaendana sana na matakwa ya wawekezaji.
 
And this is 2012 hahah ahahaha ahahahah!!!!!!!!!!!!! Naona bora tukapige mbege tu!
 
mtoahabari, kwanza karibu sana jf, wewe ni mtu muhimu sana hapa kutupa hizo za corridors za TISS.

Kusema ukweli, mimi nimezungumza na EL Desemba mwanzoni, nimemnote kama afya yake ni dhoofu!, kama yuu dhoofu sasa, 2012, jee 2015 atakuwaje?.
 
mtoahabari, kwanza karibu sana jf, wewe ni mtu muhimu sana hapa kutupa hizo za corridors za TISS.

Kusema ukweli, mimi nimezungumza na EL Desemba mwanzoni, nimemnote kama afya yake ni dhoofu!, kama yuu dhoofu sasa, 2012, jee 2015 atakuwaje?.

Asante sana Pasco,
Hata mimi binafsi nimemuona katika hali hiyo hiyo, lakini nasikia kuna dawa anaitumia nadhani ameletewa kutoka Malaysia, ambayo anaipaka kumsaidia kupunguza mikono kucheza cheza baada ya ile mild stroke aliyoipata miezi kadhaa iliyopita. Tatizo jingine na ENL ni kilevi - anakunywa sana Remmy Martin kavu, na ni kawaida kumaliza chupa moja kwa siku; vinginevyo ana umri mzuri tu kwa ndoto za mwaka 2015, kwani by that time atakuwa na miaka kama 61 au 62. Familia yake ingemshauri apunguze kilevi, na aendelee na mazoezi (kwani kwa kawaida anafanya sana mazoezi). Pia ni muhimu ajiangalie sana na wapambe wake maana hawa ndio wanaomletea matatizo ya kiharusi, presha etc. Wao wanamwita ENL The God Father, and in the process wanamtwisha mzigo mkubwa sana kimawazo kutokana na taarifa zao kwake kila siku za majungu n.k, kwani wao wanajipangia tayari vyeo, tender, ujaji, n.k. Vinginevyo JK sio hofu kwa ENL hata kidogo, huyo alishamkabili tangia mwaka 1995.
 
Wacha wa-kolimbane kwani si wote Mafisadi?
 
Mtoahabari, asante sana kwa taarifa hizi, natumaini ujumbe huu mzito, umeshamfikia EL, au wapambe wake waliota alaki humu jf watampelekea na kuvuta kama kweli anakata!.

Kusema ukweli, mimi binafsi ni miongoni mwa watu waliofarijika sana na ujio wako humu mtandaoni, speculations zimekuwa nyingi kuliko uhalisia hivyo uweko wako ni checks and balance muhimu sana.

Tukiachana na EL, jee huku kuugua kwa Prof.M na Dr.HM jee kuna kwa ukweli ni vijana wa kazi, au mnasingiziwa?.
 
Pasco! Mimi nakuona Kama mtu yeyote wa Kitanzania wenye tabia za kufanana, wenye umaskini mwingi, wenye tabia ya kujipendekeza Na wenye uchu wa madaraka tena kuupata kwake tunategemea fadhila, wote tumeoza hakuna aliyepona katika hili, lol natania tu. Lakini pili, umesema una MAPENZI Na nchi yako, hivi ni EL tu ndo bora kuliko wote in this country? Tumeomba basi tupeni mazuri ya EL tuyaone mtuaminishe nasi tumpigie chapuo. Mimi naona hata Kama suala la Richmond halikuwa lake Kama Kiongozi safi alitakiwa kuwa upande wa nchi yake si upande wa ubinafsi wake eti ape we fadhila za uraisi, je ni Viongozi tuwatakao? Niaminishe Pasco.
 

Umepoteza ushawishi.kaogee.
 

... hope u meant to say 'welcome aboard' ..
 
mtoahabari, kwanza karibu sana jf, wewe ni mtu muhimu sana hapa kutupa hizo za corridors za TISS.

Kusema ukweli, mimi nimezungumza na EL Desemba mwanzoni, nimemnote kama afya yake ni dhoofu!, kama yuu dhoofu sasa, 2012, jee 2015 atakuwaje?.


kwa hiyo hiyo TISS ya kundi la Kitine na Nyerere wamekubali EL ndo awe next
President pia??????
 
 

Adui mkubwa wa mtandao original (2005), alikuwa ni Mwandosya. Salim ilijulikana wazi hatapita, ingawa ilihitaji nguvu ya ziada dakika za mwisho kummaliza 2005. Vinginevyo Nyerere alijaribu 1985 na 1995 kumbeba Salim bila mafanikio. Mwandosya na ENL walikuwa maswahiba wakubwa sana miaka ya nyuma, kiasi cha kufikia hata mtoto mkubwa wa ENL bwana Fred kufanya kituo cha utafiti cha Mwandosya kama sehemu yake ya kujipatia uzoefu na pia vijisenti wakati wa likizo zake alipokuwa anarudi kutoka chuo kikuu cha Birmingham, akisome degree ya engineering. Hata binti mkubwa wa Mwandosya alikuwa chuo hicho hicho, idara hiyo hiyo, na alikuwa mpenzi wa muda mrefu wa fred. Ni siasa zilikuja kuwavuruga baadae, haswa lile tendo la ENL kujiunga upande wa Kikwete, ambae tayari alikuwa haivi na Mwandosya tokea walipokuwa wizara ya nishati - huko walikuwa na vita vya wazi wazi na hadharani, kutokana na tofauti za kiutendaji - siasa versus utaalam. Lakini pia inasemekana ugomvi ule ulichangiwa na yale mambo yetu huko maofisini.

Kina Sitta na Mwakyembe ni vipenzi vya Mwandosya, na Nape nae kaingia humo baada ya kusoma mchezo kwamba hao ndio wanaweza kumkabili adui yake namba moja, ENL. Walichokuwa wanafanya hawa wote kabla ya kuugua kwao ni kumtengenezea Mwandosya mazingira mwaka 2015, vinginevyo Sitta hatafuti urais, sana sana ni uwaziri mkuu, huku kina mwakyembe, Nape n.k wakitegemea kupata vyeo vingine nyeti chini ya Serikali ya Mwandosya. Lakini ndoto hiyo inafifia kwani nyota za wapiganaji wao zinaanza kuzimika polepople kwa sababu ya maradhi yao lakini vilevile mikakati na kasi kubwa ya ENL na timu yake kujinasua na Richmond, kazi ambayo imeanza kuonyesha mafanikio.

Kuugua kwa Mwakyembe, Mwandosya, hakuna taarifa rasmi juu ya hilo, lakini tetesi ni kwamba hao wanaotajwa ndio wanahusika. Shughuli kama hizo huwa hazifanwyi ki-idara ambapo information ina circulate au trickle down.
 

mmhhh,you smell like JASON BOURNE
 
Maneno mazito sana haya Pasco........

Hauoni kama yanaweza kumharibia EL?,maana nayaona kama yamekaa kiuchonganishi vile.......Sidhani kama ulikuwa na haja ya kuyaandika haya(kama kweli una nia ya dhati kabisa ya Lowassa for 2015).....

Ni mtazamo tu....

Bala.
 
Ubarikiwe mkuu kwa kuendelea kutufumbua macho,binafsi naamini maadui wa lowasa hawajui uchafu wake mwingi tena wa kumharibia,wanakomaa na Richmond ambayo inaonesha ni nyepesi kujivua gamba.kama si unafiki wanapaswa kuanika mengi zaidi ya hayo ili kuwakatisha tamaa! Mtoa Habari uwe unatutembelea japo mara 1 kwa wiki kutuelimisha mwenendo wa mambo nyuma ya pazia!
 
Inawezekana wakawa wanaujua uchafu mwingi ila muda muafaka wa kuutoa ukawa haujafika.....Kumbuka SAS alichafuliwa ndani ya miezi tu(ya mwaka 2005).......Ukute ni suala la muda tu..

Binafsi nawashauri wapambe wa EL(Pasco & Co) watulie,wanaongea sana kiasi kwamba 'wanavuka mipaka' na kumuharibia EL.....Kuna mengine wanayawahisha mno,hayapaswi kuongewa sasa hasa kwa siasa za kuviziana za ndani ya CCM na Tanzania kwa ujumla....

Bala.
 

Mkuu Pasco,
Una uhakika gani kuwa Mtoahabari sio Speculeta kama Walivyo/Tulivyo wengine hapa Jamvini? Mengi katika makala yake yamo mitaani.
Kama kusema kuwa ENL na RA ndio wanaoweka watu katika nafasi za juu inamainisha kuwa JK ni picha/Robbot linaloendeshwa tu, fanya hivi, mweke Juma/Joni Pale. Mnataka tuamini hivyooo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…