Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Mkuu nimekuelewa sana! Lakini kwa complication hizi,nguvu zimeisha! Sijui tutoke vipi!

Kwa hali ya sasa, wa kufanya maamuzi magumu sio viongozi bali vijana, na hapa sina maana ya UVCCM bali vijana wa Tanzania, haswa wale wenye bahati ya elimu na upeo, kuwaongoza wenzao waliokosa bahati hiyo, katika uelewa wa mambo; Ni bahati mbaya sana kauli mbiu muhimu kama hizi za 'maamuzi magumu', 'ukosefu wa ajira kwa vijana ni timing bomb', n.k. huwa tunaletewa na viongozi badala ya chimbuko lake kuwa ni vijana wenyewe, ikiwa sehemu ya msimamo na dira ya vijana; Badala yake, vijana tumekuwa tunashirikiana kwa kauli tu, huku tukielekeza nguvu na akili zetu zote kwenye ushabiki na ufuasi wa pande mbili au tatu zilizopo badala ya vijana wenyewe kutengeneza upande wa nne, kwa manufaa yetu wenyewe.
 

Mtoahabari,
Hii tafsiri kuwa Jk alivuliwa nguo/kufadhaishwa na Hoja za EL mbona ni Potofu na mnaiendeleza? Hizo hoja zimo ndani ya Threand moja hapa JF (zisomeni kwa kituo kisha mtafakari, labda ziwe zimenukuliw vinginevyo, ingekuwa vema ipatikane Audi/vidio yake) sababu kubwa ya madai hayo ni kuwa Jk alitikisa kichwa kukubali alichohoji EL na halafu hakujibu. Hiyo imesababisha mumtie hatiani Jk bila kurudi katika historia ya jambo lenyewe, Mkameza aliyosema EL bila kuzingatia Busara za Jk za Kukaa Kimnya.
 
MN
Na hasa katika mchakato wa kuandika Katiba Vijana mtahitajika sana kwani nyie ndio mnaoelekea katika miaka 50 ijayo.
 


Naona karibu tutaivisha Karamu ya (Mh. EL) kuingia Magogoni. Tumeanza maandalizi mapema na bila shaka mialiko imeshatolewa. Kuna Mstahiki mmoja naona amesahauliwa kabisa, sijui nafasi ya Muungano na Wateule wao tumeiweka wapi. Its all EL hapa na bla.........bla.....blaaa..............!
 
Kwa kuhitimisha ndio kusema ili kumshinda EL..
1. Upinzani utatoka CCM..
2. Nguvu ya UMMA.
Lakini kwa UNAFIKI wa mwafirka kweli haya yawezekana?..
 
Kama kawaida tunaanza kuwajadili mtoa habari na hutaki unaacha badala ya contents@Royals.
 
ENL na Haruna ni ndugu?
 
Erickb,
Hakuna haja ya Jazba hapa. Huu ni ukumbi wa Mjadala na ili uyamudu Majadiliano ni lazima uweze kukontrol Hisia zako. (Keep your cool) na kama hilo huliwezi, hapa hapakufai. (samahani huu ni ushauri usiotaka malipo).
Unajua mtu anapokuja na jazba na kuanza kutulaumu watanzania kwa maneno ya kashfa haifai hata kidogo,kila mtu ana mitizamo yake so asituone watanzania wajinga wakati kila siku tunahangaikia haki zetu ila wenye mamlaka wametuzidi nguvu.Kama ana hoja aseme kistaarabu ila mtoa mada HAJAMTETEA EL wala JK ye katoa aliyonao then sisi tuyatafakari.Over...!
 
Hakika nimejifunza mengi, hata Yale ambayo sikuwahi kuota Na kuwaza, JF idumu milele tuendelee kujua mengi, watu Kazini wanatapika tu. Nahisi hii ndio thread bora ya kuanza mwaka.
 
Nina usingizi lakini nimeamua kuweka Miguu kwenye maji ili niendelee kusoma mastori. Bora Kama tutakesha wote, usinitose.
Bora ulale uamke na nguvu na hoja mpya zaidi....mi nalala
 
You are the one on medication. Popote unapotokea,huna unalolijua kuhusu hao uliwaandika kwamba hawajasoma,especially........,,tatizo mnadharau vyombo vya ulinzi,mnadhana kule hakuna phd
 
kazi aliyotumwa ameikamilisha.
kazi hiyo ni kupanda mbegu miongoni mwa jamii
kwamba enl na mtandao wake hawashikiki katika mbio
za 2015.

kwa kiasi kikubwa amefanikiwa na sasa watu wanasheherekea 2012
kwa rèmy martin.

nami nawatakia mwaka 2012 mwema
 

Kwa hiyo Mtoahabari Unazomwaga Hapa hazitoki ndani kama wengi wanavyoelekea kuamini. Ni za Vijiweni kama unavyithibitisha kupotea kwa Mwambulukutu Vijiweni Kumekupunguzia Vyanzo vya kujaza kurasa
. Je maoni hayo ni sahihi??
 
 
Nina usingizi lakini nimeamua kuweka Miguu kwenye maji ili niendelee kusoma mastori. Bora Kama tutakesha wote, usinitose.

unajua tangu nifuatilie thread hii najikuta naanza kuichukia nchi yangu mwenyewe, kumbe tunaongozwa kimafia? kweli nilikuwa gizani
 
Asante Bala, kwa vile EL kachafuliwa sio mikono tuu useme atanawa na kuisha, amechafuliwa mpaka nguo za ndani, hivyo njia sahihi ya kumsafisha ni kumvua nguo zote ili uchafu wake wote uonekane, na atakapotakata, usafi wake ujidhihirishe, tatizo kubwa la EL ni hilo zigo la uchafu wa Richmond, anatakiwa alibwage hilo zigo, watu wamjue mwenye zigo lake, ndipo atakapotakata!.

Tatizo langu ni kusema ukweli daima, japo umesha nicost sana, ila mwisho wa siku ni ukweli utasisimama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…