Bwana Nderingosha,
Nashukuru sana kwa swali lako. Una hoja nyingi sana na za msingi kabisa. Ila ukumbuke kwamba nilichokieleza ni ufahamu wangu juu ya hali halisi ilivyo, sio ushabiki. Na kuhusu TISS na maslahi ya nchi, ni dhahiri kwamba TISS ya sasa sio ile ya Kitine, au Maiga, kwani kwa sasa qwngi mle wapo kwa ajili ya maslahi binafsi. Hapo nyuma, baadhi yao walikuwa wanaona kama vile ENL ndiye mvurugaji, lakini baada ya ENL kumvua nguo Mkuu wa nchi Dodoma majuzi, na mkuu kukaa kimya, vijana wengi wa TISS wameanza kuhamia kwa ENL, wakidai anaonewa, lakini ni mvumilivu, na mchapa kazi, hivyo anastahili kuchukua jahazi. Lakini kama ulivyotamka mwenyewe, wenye nchi hii ni UMMA, kwani wao ndio wenye maamuzi ya mwisho, sio TISS, CCM, wala JWTZ. Pia taarifa kwamba wanajeshi ngazi za chini wamechoka, na huwa wanatoa matamshi makali sana kila mara milipuko ya mabomu inapotokea kwenye kambi. Wengi huwa wanatamka kwamba kuna umakusudi. Na kibaya zaidi ni kwamba wanajeshi wa ngazi za chini na polisi hawapo katika meli moja kuhusu masuala mengi juu ya nchi hii. Lakini ni muhimu tukumbuke pia kwamba JWTZ ni taasisi yenye nidhamu na utiifu wa hali ya juu sana, na JWTZ kama taasisi, ina ushirikiano wa karibu sana wa kikazi na TISS. Hiyo ilikuwa ni sehemu ya kazi maalum ya Kitine (Kanali Mstaafu), chini ya Nyerere.
Baada ya kusema yote haya, tunarudi kwenye ukweli kwamba, pamoja na mapungufu yake mengi na tuhuma nyingi mbali ya Richmond, ENL amejipanga vya kutosha kuwa rais wa tano wa Tanzania. Sio CCM, wala Tume ya Uchaguzi (NEC), itakayoweza kubadilisha ndoto yake, bali UMMA kwa njia ya UMMA, sio UMMA kwa njia ya KURA. Umma hautafanikiwa kumzuia ENL kupitia sanduku la KURA, bali kwa njia ya maandamano na mgomo wa UMMA kama huko Libya, Tunisia na Misri na kwingineko ulipopataja, iwapo ENL atatangazwa kuwa Rais wa Tano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) 2015. Lakini hii haina maana kwamba upinzani hauna nafasi 2015, lakini kama tetesi juu ya ENL, RA, wakisaidiwa na vijana wao Bashe na January, kukisaidia CHADEMA kwa fedha na mikakati kishinde uchaguzi mdogo wa Igunga, ni za kweli, ni vigumu kupata kuelewa ni jinsi gani wataweza upinzani utaweza kumzuia ENL na timu yake mwaka 2015.