Ni muhimu tukautofautisha uhusiano baina ya ENL na JK, ENL na RA, na JK na RA.
Uhusiano kati ya ENL na RA ulianza wakati wa mwinyi, wakati huo ENL akiwa Waziri wa ardhi. Utawala wa Mzee mwinyi ulianzisha utamaduni mpya wa kila waziri au kiongozi mkuu wa CCM au serikali kumkamata Muarabu au Mhindi wake ili mambo yake yaendelee. Kwa upande wa ENL, alimkamata RA na kumsaidia apate ubunge katika uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka 1994, mara baada ya Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Elimu, Charles Kabeho, kufariki.
Uhusiano wa JK na ENL ni wa muda mrefu zaidi, ukianzia miaka ya mwanzo ya 80, wote wakiwa UVCCM kama wabunge na wajumbe wa CCM - NEC.
Uhusiano wa JK na RA ni wa kutambulishwa na ENL miaka ya mwanzo ya 90. Baada ya utambulisho huo, Ra alikuwa na uhuru wake na JK, na hakuwa na haja ya kumshirikisha ENL katika kila jambo lake na JK. Cha msingi hapa ni kwamba, RA alipewa ahadi kwamba akifanikisha zoezi la 2005, Uchumi wa Nchi utakuwa ni yeye kuuchezea anavyotaka. Kwa mfano, katika safari nyingi sana za JK nje ya nchi, ilikuwa jadi kutomwona RA akipanda ndege na JK pale JKIA, lakini kumkuta akichomoza New York, Capetown, Dubai, London n.k, na kujiunga na JK kwenda kuweka biashara zake sawa. Lakini haikuwa mazoea sana kwa RA kumfuata ENL nje wakati alipokuwa safarini kikazi kama Waziri Mkuu.
Mifano michache ipo ya kutusaidia kutenganisha mahusiano haya. Kwanza, mwaka 2006, RA na Alex Stewart na Mramba, waliandaa chakula maalum cha usiku (Dinner), jijini Cape Town kwa ajili ya JK, huku akikubali mwaliko ule na kutoa hotuba nzuri ya pongezi kwa Alex Stewart kwa kazi nzuri kwenye sekta ya madini, huku akiahidi kuwapa ushirikiano mkubwa zaidi baadae. ENL hakuwa katika mpangi huu. Lakini baade hiyo ikageuka na kumkuta Mramba akiwa na kesi ya kujibu. Mfano wa pili, mwaka 2007 akiwa Waziri Mkuu, ENL aliungana na rafiki yake Bwana Karamagi, jijini London ili kufanikisha mkataba wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi. Sio RA wala JK waliohusishwa na mradi huo. Mfano wa tatu, mmiliki wa Dowans alipoletwa Tanzania na RA kama njia ya RA kujinasua baada ya JK kusema hamjui mmiliki, vijana maalum walimwona Al Adawi jijini, akizunguka nyakati za usiku kwa ajili ya Dinner n.k na mtoto wa JK, sio mtoto au mwanafamilia yeyote wa ENL. Na mtoto wa JK alimhakikishia Al Adawi kwamba Dowans watalipwa na watapewa miradi mingine mingi, na muda mfupi baadae Simbion ikaja, huku Mama Clinton, akibariki ujio huo.
Mfano wa nne, muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005, CCM ilipatiwa fedha kutoka mfuko wa EPA kwa ajili ya kumsaidia JK uchaguzi mkuu. Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha watu watano - RA, Apson, Balali, Mkapa na Peter Noni. ENL hakuitwa katika kikao hicho. Mfano wa Tano, Vodacom Pty Limited iliingia Tanzania kwa mgongo wa Joseph Mungai, lakini kosa alilofanya ni kumwamini RA na kumkabidhi ujumbe wa wawekezaji hao ili awasaidie kumalizia mchakato wa kupata leeni ya GSM, huku Mungai akitegemea atahusishwa na kumegewa hisa, only to realize baadae RA kamzunguka, na badala yake, kumshirikisha Peter Noni, kwani, RA alishapanga kwamba Noni ndiye atakuwa Gavana wa BOT baada ya Balali kustaafu. ENL hakushirikishwa moja kwa moja, lakini kila inapobidi, ENL huwa anadai mkato wake, na hakukubali mradi wa Vodacom Pty Limited uingie Tanzania bila ya yeye kupata kitu. Baada ya mvutano kidogo, RA na Noni wakajichukulia hissa Vodacom, na kumpa ENL biashara ya kuuza vocha kupitia kampuni ya Alphatel. Mfano wa Sita, Benki ya T.I.B - ni taasisi iliyoteuliwa na JK kwa kushauriana na RA, ili kupokea marejesho ya fedha za EPA, na Mkurugenzi Mkuu akateuliwa Peter Noni, mmoja wa watuhumiwa wakuu wa EPA. Hii ilikuwa ni kazi ya Rostam, sio ya ENL.
Mifano ni mingi sana, lakini suala la msingi hapa ni kwamba haina maana kwamba ENL ni msafi, kwani na yeye ana madudu mengi sana kama vile mradi wa kifisadi wa UVCCM ambao ulipelekea ugomvi mkubwa baina yake na Nape, ukwapuaji uliopitiliza wa Ardhi, ubadhirifu mkubwa wa fedha za walipa kodi katika ziara zake ndani na nje ya nchi akiwa Waziri Mkuu, kujinyakulia viwanja na majengo kupitia kampuni ya Real Estate, anayomiliki na mkewe, n.k.
Kinachowakera viongozi wenzake ndani ya CCM ni mambo makuu matatu. Kwanza, sio kwamba wanakerwa na hulka ya ufisadi ya ENL, ambayo hata wenzake karibia wote wanayao, bali ni tabia ya ENL ya kutoridhika na pesa, na kugeuza kila kitu kuwa mradi, badala ya kuachia vingine viwe kwa manufaa ya umma. Tabia yake ni kama vile amegundua umuhimu wa pesa, jana. Suala la pili linalowakera wenzake ndani ya CCM ni tabia yake kuufanya Urais wa Tanzania kuwa ni mali, haki au halali yake pekee, na kama watakuja wengine, basi ni baada ya yeye kuwa Rais wa Tanzania. Na mwisho ni dharau zake na familia yake kwa JK, tangia akiwa waziri mkuu kwamba JK sio kitu bali boya, na kwamba yeye ENL ndiye anaemshika JK masikio.
Nimalizie kwa kuzungumzia kidogo utajiri wa ENL. Huyu bwana alianza kujijengea uwezo wa kifedha alipoteuliwa kuwa waziri wa Ardhi mwaka 1991. Kupitia nafasi hiyo, alijilimbikizia viwanja vingi katika prime areas za DSM na Arusha, ambapo alitumia nafasi yake kikamilifu kujenga nyumba na flats za kupanga DSM na Arusha, property yake ya kwanza ikiwa ni ile aliyokuwa makazi ya muda mrefu ya Balozi wa kwanza wa Afrika Kusini Tanzania, kule Masaki ambapo kwa kuanzia mwaka 1994, alikuwa anapokea dollar 5,000 kwa mwezi tax free, kama kodi. Hizi zilikuwa ni pesa nyingi sana miaka ile. Vilevile ENL aliweza kutumia nafasi yake akiwa wizara ya ardhi na nyumba, kwa kumpendekeza Haruna Masebu, kuwa Mkurugenzi wa NHC wakati ule, na kuwa na mahusiano nae ya karibu ya kibiashara. Lakini Bwana Masebu alipoteza nafasi ile, na kurudishwa wizara ya ardhi, mara baada ya ENL kutoswa na Mkapa kwenye baraza la mawaziri mwaka 1995. Lakini aliporudi kwenye cabinet tena, miaka minne baadae, baada ya juhudu kubwa ya Apson, ENL akiwa waziri wa maji, ndiye alieunda EWURA, na kumweka Haruna Masebu kama Mkurugenzi Mkuu wa kwanza.
Lakini kasi ya utajiri wa ENL ilitokana na ujio wa Vodacom, Tanzania, kupitia kampuni ya Alphatel anayoimiliki 50/50 na Mkewe Regina, huku mwanae wa kwanza, Fred, akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji. Mbali ya Alphatel, ENL na mkewe pia wanamiliki kampuni ya kufua nguo Alpha laundry ambayo imekamata asilimia kubwa sana ya biashara hiyo Tanzania. Vile vile anamiliki gazeti, kituo cha redio kilichopo Arusha kinachosimamiwa na mwane wa pili wa kiume, na yupo mbioni kuanzisha Kituo Kikubwa cha Televisheni kitachorusha matangazo nchi nzima. ENL pia amezidi kujikita katika biashara ya Real Estate (Flats na Nyumba za Kupanga) DSM na Arusha, pamoja na biashara za hoteli Arusha, kupitia kampuni ya real estate, anayomiliki 50/50 na mkewe. Lakini fedha za haraka haraka zisizo na jasho ni zile za kuuza vocha, kwa mfano, kwa mwaka jana pekee, biashara yake ya kuuza vocha za Vodacom ilimuingizia zaidi ya USD 2 Million (Gross Revenue). Ukiachilia na biashara hizi mbali mbali, ENL pia ni hodari sana wa kujitafutia pesa rahisi rahisi kutoka kwa matajiri mbali mbali wa ndani na nje, wakiaminishwa kwamba yeye ndiye Rais wa Tanzania kwa miaka 20 yani, 2005 2025.
Huyo ndiyo ENL. Sina uhakika ule usemi wa wahenga wetu kwamba Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpe, unamtosha vipi ENL.