Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Bob,

Haiwezekani kaka! Umelikubali kundi letu la el?
Eeeeh bwana wee tatizo mimi maskini jeuri tena san,a na najijua kwamba siwezi kuwa mnafiki wala kuikarifisha nafsi yangu ktk kutenda yasiyo mema. Nashukuru Mungu na kidogo nilicho nacho lakini siwezi shika haramu kwa sababu tu ya dhiki. Nimepita sana huko mkuu wangu na sikujaliwa kama walivyojaliwa hawa inabidi sasa kuitafuta pepo...

Maana haya maswala ya kiutawala ni sawa na muuza Unga ipo siku utanasa pabaya na ktk anga za Simba wenye njaa...Tumewaona wangapi mkuu wangu. Kama mimi ningekuwa kundi hilo hizi ndizo dalili tosha za kukuonyesha Ghubu la watu na wanavyomshtakia Mola na kila siku itakuwa na malipo yake pengine hapa hapa duniani.
 
Bora ulale uamke na nguvu na hoja mpya zaidi....mi nalala

Usilale Erick tafadhali! Mbona waniacha mpweke. Hafu unajina la Rafiki yangu mpenzi mpaka nahisi ka ni yeye, lol.
 
unajua tangu nifuatilie thread hii najikuta naanza kuichukia nchi yangu mwenyewe, kumbe tunaongozwa kimafia? kweli nilikuwa gizani

Mwenyewe hamu ninayo basi? Nimepatwa Na hofu Na woga wa ajabu. People are working eheee! They are very clever. Wanaoteuliwa, nilifikiri huteuliwa kwa uchapakazi kumbe huwekwa tu kwa Kazi maalumu! Hata huyu aliyeteuliwa juzi naye ukute yupo kwa maslahi ya watu hao, from ubalozini to CS wakati kina Yambesi wapo, tena wazoefu wazuri Na utumishi. Damn them.
 
Wengi walimtegemea Yambesi au Dkt Stergomena (Katibu Mkuu wizara ya EAC), au mwanamke yeyote mwenye sifa hizo.
 
@mtoahabari, pasco et al......Nikuulize tu mambo kadhaa ya msingi......kama umeamua kufunguka ki ukweli...maana kama uko karibu na Lowasa basi utakuwa unajua yanayoendelea serikalini......ebu jibu.....hivi hawa jamaa unaowazungumzia kina Lowasa et al papoja na JK.(watawala)....pamoja na hizi siasa za makundi ktk vinyang'anyiro vya urais tz....huwa wanafikiria kuwatumikia wananchi wao maskini walio wengi??maana mnajadili hizi siasa wakati nchi ina hali mbaya sana hii kiuchumi......hawa TISS mnaowazungumzia.....je wanaliweka wapi jeshi la nchi hii tz katika hizi harakati za urais nchi hii??maana mnazungumzia TISS mnasahau kuwa jeshi likigoma hamna cha TISS wala mama zao eh???maana hapa naona siasa mnazojadili zimeingia mpaka kwenye issue za security ya nchi(TISS)....kama kuna watu kama kina Lowasa wanaweza kuwa na influence kwenye utendaji wa TISS wakati hawako madarakani na hili nyie mnaliona sawa hivi hamjiulizi kuwa nchi inakoelekea siko??????au imepotea tayari???ebu jibuni swali je hamwoni nchi ina ombwe kubwa la kiungozi? maana amini msiamini ni hivi majuzi tu nimekuwa nikiongea na wanajeshi wa ngazi za chini ambao wamechoka mbaya na maisha na mwenendo mzima wa utawala wa nchi ..........na nilipowauliza je wao wanasemaje wakajibu ......wanawasubiri wananchi walianzishe tu kinuke jumla (Egypt style).....sasa hamwoni kwamba hali hii si nzuri????.....labda tu tukumbushane......kama TISS wanainfluence madaraka nchi hii kama mlivyo jadili juu.......ikumbukwe kuwa iko siku maskini wa tz watatoka barabarani......wakishirikiana na vyama pinzani vilivyo makini na kudai kilicho chao kwa watawala na hakutakuwa na TISS wala mama zao????.........maana naona hapa mnawajadili mafisadi kama viongozi weu wa kesho......yaani imefikia tz watu ambao ni mafisadi(e.g Lowasa)wanajadiliwa positively kuchukua madaraka ya nchi?????iko wapi haki ya maskini hapa sasa???na kwanini hamna mjadala wa possibility ya opposition party kuchukua dola???au hili mnaliona haliwezekani????mnasahau yaliyotokea juzi tu Egypt,Tunisia na Libya???(nguvu ya umma)........mnajadili kama vipofu msioona mabadiliko ya kweli yanayotokea sehemu nyingine nyingine ambapo watu walichoka na tawala kama hii mnayojadili????.......wake up you guys.......only time will tell........mia

Mkuu
Yaelekea unawalisha maneno hao uliowataja na kuwaaddress kwa hayo maswali na unajifanya unaamini kuwa wanatupa Habari toka ndani.
Wanajeshi wa chini Bongo wako walivyo toka enzi za Mwalimu, tena yawezekana walikuwa Hoi wakati huo kuliko sasa.Na si wao tu Waalimu, Polisi, Wauguzi na Madaktari you name it we are all in same Boat.
Sidhani kama ni Busara kutumia Lugha na mifano Chochezi.
Tulikuwa na Mfumo wa Chama Kimoja Kwa Miaka 23. Na hakuna atakaekataa kuwa ulikuwa na Matatizo na Madhila kibao. WaTz Tulikuwa wavumilivu na wenye Basara.
Hatimae Ulibadilika na hali nayo ikabadilika ya Tanzania na ya Dunia kwa jumla, moja wapo ni huu Uhuru wa kubwata bila kuhofia jirani aliyevaa Magwanda ya Mgambo.
Pamoja na kutoka mbali ndani ya miaka 50 tunakoenda ni Mbali zaidi.

Kwa hiyo: Nderingosha, Pasco,Mtoahabari,Hutaki Unaacha na sisi wengine, Tusikubali kuelekezwa nija waliopita Tunisia , Egypt, Libya na Wengineo "Just for the sake of Greediness from One among Us" Na huyo hata akiwa Baba yako, Mama yako, Ndugu yako, Rafiki yako au Mpenzi wako Usiunganne nae. Wana JF Brothers and Sisters " IF we follow that Road there will be no way Back". It is always like that, just look you and beyond. Today this is all I can say THINK!
 
Makoko UK
Usiogope Tunisia au Misri. Hawa walichoka kushuhudia limbwi la ufukara wakati wachache serikalini wakijitajirisha. Hii inatokea Tanzania yenye amani na utulivu hivi sasa. Kuna siku huo utulivu utaenda njia ya Tunisia.
 
Kikulacho ki nguoni mwako! Kama mtandao ulitumika kumpa nafasu, ataukimbiaje leo hii sababu ya threat zake? Tunavuna tuliyopanda! Vinginevyo hizi ni hadithi za kutupelekea siku na miaka. How could he survive with all these people out? Ni uongo mtupu!
 
Ni muhimu tukautofautisha uhusiano baina ya ENL na JK, ENL na RA, na JK na RA.
Uhusiano kati ya ENL na RA ulianza wakati wa mwinyi, wakati huo ENL akiwa Waziri wa ardhi. Utawala wa Mzee mwinyi ulianzisha utamaduni mpya wa kila waziri au kiongozi mkuu wa CCM au serikali kumkamata Muarabu au Mhindi wake ili mambo yake yaendelee. Kwa upande wa ENL, alimkamata RA na kumsaidia apate ubunge katika uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka 1994, mara baada ya Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Elimu, Charles Kabeho, kufariki.
Uhusiano wa JK na ENL ni wa muda mrefu zaidi, ukianzia miaka ya mwanzo ya 80, wote wakiwa UVCCM kama wabunge na wajumbe wa CCM - NEC.

Uhusiano wa JK na RA ni wa kutambulishwa na ENL miaka ya mwanzo ya 90. Baada ya utambulisho huo, Ra alikuwa na uhuru wake na JK, na hakuwa na haja ya kumshirikisha ENL katika kila jambo lake na JK. Cha msingi hapa ni kwamba, RA alipewa ahadi kwamba akifanikisha zoezi la 2005, Uchumi wa Nchi utakuwa ni yeye kuuchezea anavyotaka. Kwa mfano, katika safari nyingi sana za JK nje ya nchi, ilikuwa jadi kutomwona RA akipanda ndege na JK pale JKIA, lakini kumkuta akichomoza New York, Capetown, Dubai, London n.k, na kujiunga na JK kwenda kuweka biashara zake sawa. Lakini haikuwa mazoea sana kwa RA kumfuata ENL nje wakati alipokuwa safarini kikazi kama Waziri Mkuu.

Mifano michache ipo ya kutusaidia kutenganisha mahusiano haya. Kwanza, mwaka 2006, RA na Alex Stewart na Mramba, waliandaa chakula maalum cha usiku (Dinner), jijini Cape Town kwa ajili ya JK, huku akikubali mwaliko ule na kutoa hotuba nzuri ya pongezi kwa Alex Stewart kwa kazi nzuri kwenye sekta ya madini, huku akiahidi kuwapa ushirikiano mkubwa zaidi baadae. ENL hakuwa katika mpangi huu. Lakini baade hiyo ikageuka na kumkuta Mramba akiwa na kesi ya kujibu. Mfano wa pili, mwaka 2007 akiwa Waziri Mkuu, ENL aliungana na rafiki yake Bwana Karamagi, jijini London ili kufanikisha mkataba wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi. Sio RA wala JK waliohusishwa na mradi huo. Mfano wa tatu, mmiliki wa Dowans alipoletwa Tanzania na RA kama njia ya RA kujinasua baada ya JK kusema hamjui mmiliki, vijana maalum walimwona Al Adawi jijini, akizunguka nyakati za usiku kwa ajili ya Dinner n.k na mtoto wa JK, sio mtoto au mwanafamilia yeyote wa ENL. Na mtoto wa JK alimhakikishia Al Adawi kwamba Dowans watalipwa na watapewa miradi mingine mingi, na muda mfupi baadae Simbion ikaja, huku Mama Clinton, akibariki ujio huo.

Mfano wa nne, muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005, CCM ilipatiwa fedha kutoka mfuko wa EPA kwa ajili ya kumsaidia JK uchaguzi mkuu. Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha watu watano - RA, Apson, Balali, Mkapa na Peter Noni. ENL hakuitwa katika kikao hicho. Mfano wa Tano, Vodacom Pty Limited iliingia Tanzania kwa mgongo wa Joseph Mungai, lakini kosa alilofanya ni kumwamini RA na kumkabidhi ujumbe wa wawekezaji hao ili awasaidie kumalizia mchakato wa kupata leeni ya GSM, huku Mungai akitegemea atahusishwa na kumegewa hisa, only to realize baadae RA kamzunguka, na badala yake, kumshirikisha Peter Noni, kwani, RA alishapanga kwamba Noni ndiye atakuwa Gavana wa BOT baada ya Balali kustaafu. ENL hakushirikishwa moja kwa moja, lakini kila inapobidi, ENL huwa anadai mkato wake, na hakukubali mradi wa Vodacom Pty Limited uingie Tanzania bila ya yeye kupata kitu. Baada ya mvutano kidogo, RA na Noni wakajichukulia hissa Vodacom, na kumpa ENL biashara ya kuuza vocha kupitia kampuni ya Alphatel. Mfano wa Sita, Benki ya T.I.B - ni taasisi iliyoteuliwa na JK kwa kushauriana na RA, ili kupokea marejesho ya fedha za EPA, na Mkurugenzi Mkuu akateuliwa Peter Noni, mmoja wa watuhumiwa wakuu wa EPA. Hii ilikuwa ni kazi ya Rostam, sio ya ENL.

Mifano ni mingi sana, lakini suala la msingi hapa ni kwamba haina maana kwamba ENL ni msafi, kwani na yeye ana madudu mengi sana kama vile mradi wa kifisadi wa UVCCM ambao ulipelekea ugomvi mkubwa baina yake na Nape, ukwapuaji uliopitiliza wa Ardhi, ubadhirifu mkubwa wa fedha za walipa kodi katika ziara zake ndani na nje ya nchi akiwa Waziri Mkuu, kujinyakulia viwanja na majengo kupitia kampuni ya Real Estate, anayomiliki na mkewe, n.k.

Kinachowakera viongozi wenzake ndani ya CCM ni mambo makuu matatu. Kwanza, sio kwamba wanakerwa na hulka ya ufisadi ya ENL, ambayo hata wenzake karibia wote wanayao, bali ni tabia ya ENL ya kutoridhika na pesa, na kugeuza kila kitu kuwa mradi, badala ya kuachia vingine viwe kwa manufaa ya umma. Tabia yake ni kama vile amegundua umuhimu wa pesa, jana. Suala la pili linalowakera wenzake ndani ya CCM ni tabia yake kuufanya Urais wa Tanzania kuwa ni mali, haki au halali yake pekee, na kama watakuja wengine, basi ni baada ya yeye kuwa Rais wa Tanzania. Na mwisho ni dharau zake na familia yake kwa JK, tangia akiwa waziri mkuu kwamba JK sio kitu bali boya, na kwamba yeye ENL ndiye anaemshika JK masikio.

Nimalizie kwa kuzungumzia kidogo utajiri wa ENL. Huyu bwana alianza kujijengea uwezo wa kifedha alipoteuliwa kuwa waziri wa Ardhi mwaka 1991. Kupitia nafasi hiyo, alijilimbikizia viwanja vingi katika prime areas za DSM na Arusha, ambapo alitumia nafasi yake kikamilifu kujenga nyumba na flats za kupanga DSM na Arusha, property yake ya kwanza ikiwa ni ile aliyokuwa makazi ya muda mrefu ya Balozi wa kwanza wa Afrika Kusini Tanzania, kule Masaki ambapo kwa kuanzia mwaka 1994, alikuwa anapokea dollar 5,000 kwa mwezi – tax free, kama kodi. Hizi zilikuwa ni pesa nyingi sana miaka ile. Vilevile ENL aliweza kutumia nafasi yake akiwa wizara ya ardhi na nyumba, kwa kumpendekeza Haruna Masebu, kuwa Mkurugenzi wa NHC wakati ule, na kuwa na mahusiano nae ya karibu ya kibiashara. Lakini Bwana Masebu alipoteza nafasi ile, na kurudishwa wizara ya ardhi, mara baada ya ENL kutoswa na Mkapa kwenye baraza la mawaziri mwaka 1995. Lakini aliporudi kwenye cabinet tena, miaka minne baadae, baada ya juhudu kubwa ya Apson, ENL akiwa waziri wa maji, ndiye alieunda EWURA, na kumweka Haruna Masebu kama Mkurugenzi Mkuu wa kwanza.

Lakini kasi ya utajiri wa ENL ilitokana na ujio wa Vodacom, Tanzania, kupitia kampuni ya Alphatel anayoimiliki 50/50 na Mkewe Regina, huku mwanae wa kwanza, Fred, akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji. Mbali ya Alphatel, ENL na mkewe pia wanamiliki kampuni ya kufua nguo – Alpha laundry ambayo imekamata asilimia kubwa sana ya biashara hiyo Tanzania. Vile vile anamiliki gazeti, kituo cha redio kilichopo Arusha kinachosimamiwa na mwane wa pili wa kiume, na yupo mbioni kuanzisha Kituo Kikubwa cha Televisheni kitachorusha matangazo nchi nzima. ENL pia amezidi kujikita katika biashara ya Real Estate (Flats na Nyumba za Kupanga) DSM na Arusha, pamoja na biashara za hoteli Arusha, kupitia kampuni ya real estate, anayomiliki 50/50 na mkewe. Lakini fedha za haraka haraka zisizo na jasho ni zile za kuuza vocha, kwa mfano, kwa mwaka jana pekee, biashara yake ya kuuza vocha za Vodacom ilimuingizia zaidi ya USD 2 Million (Gross Revenue). Ukiachilia na biashara hizi mbali mbali, ENL pia ni hodari sana wa kujitafutia pesa rahisi rahisi kutoka kwa matajiri mbali mbali wa ndani na nje, wakiaminishwa kwamba yeye ndiye Rais wa Tanzania kwa miaka 20 yani, 2005 – 2025.

Huyo ndiyo ENL. Sina uhakika ule usemi wa wahenga wetu kwamba “Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpe, unamtosha vipi ENL.
 
Hutaki Utaacha:
Toka mafichoni ujibu hoja za Wadau.
Mjada unafrezzzzzzzz unakusuburi mtoa mada.
Mtoa habari amesaidia, lakini wewe ndie Mweye Chungu jikoni.
Wanaodai kuwa umeleta Udaku watapandisha Bendera ya Ushindi.
Je upo??
 
Mtoa habari,

Ukichunguza kwa umakini utajiri wa EL ameuongeza sana kwa UHALALI kuliko tunavyoambiwa. Na pia hajashiriki deals kubwa kubwa kama magazeti na wengi tunavyoamini. Miradi yake halali inatosha kumfanya awe tajiri.

Vipi biashara ya mauwa kupeleka nje ya nchi?

Vipi hujataja biashara ya ng'ombe kupeleka nje ambayo kwa sasa imesitishwa (sijui kama imefufuka)?
Kwahiyo utaona mengi ni majungu. He is a self made millionaire!
 
Unakosea sana FP.............mbona ingekuwa rahisi kwa watu wengi tu CCM kuwa millionaires.............ENL hana tofauti na money launderer.......FYI............unaposikia wanamuita "The Godfather".......usifikiri wanatania tu.........

kama nilivyoeleza huko nyuma kwenye mada tofauti........ENL ana dharau na kiburi sana..........

Kuna dili za mafuta pia na nishati....wee acha tu!

usisahau....shughuli ya EPA ilianza kama hivi.........
 
Mkuu Ogah,

Mie la dharau sijui maana ni perception. Unajua mtu ukiwa maarufu ni taabu kidogo.

Ninachomaanisha ni kua EL alitumia nafasi zilizopo kuweka biashara halali.

Money laundering ina apply kwenye biashara kubwa kubwa ambazo ni capital intensive, biashara za airtime voucher au laundry hazihitaji capital kubwa. Labda real estate business.

Lakini si tuna takukuru? Mbona tuhuma nyingi lakini hamna uthbitisho? Isije ikawa ya HIZBU ya SAS!
 
Bob,

Wala usidhani tunajipendekeza. Tunatoa maoni yetu kadri tuonavyo!
 
Mtoa habari,

Ukichunguza kwa umakini utajiri wa EL ameuongeza sana kwa UHALALI kuliko tunavyoambiwa. Na pia hajashiriki deals kubwa kubwa kama magazeti na wengi tunavyoamini. Miradi yake halali inatosha kumfanya awe tajiri.

Vipi biashara ya mauwa kupeleka nje ya nchi?

Vipi hujataja biashara ya ng'ombe kupeleka nje ambayo kwa sasa imesitishwa (sijui kama imefufuka)?
Kwahiyo utaona mengi ni majungu. He is a self made millionaire!
Miradi gani halali hiyo unayozungumzia? Hata wauza madawa ya kulevya wanaweza kujenga nyumba na kuzipangisha na kusema ni biashara halali. Chochote kile ambacho chanzo chake ni ufisadi na udhulumu wa public trust huwezi kuita ni biashara halali. Biashara zote za Lowassa chanzo chake ni "abuse of public trust." Hakuna cha uhalali hapo.
 
Kuongezea tu major recruitments ni kutokea jeshini. Vijana waliofudhu trainings zao Uchina/Cuba wenye maximum ranks za Captain.
Colonel Kitine
"Captain" Cornel Apson
Captain Ndossi -- Marehemu.
Lupembe mtoto sina uhakika kama naye ni former JWTZ soldier
Capt J. Zoka
 
Mkuu Ogah,

Mie la dharau sijui maana ni perception. Unajua mtu ukiwa maarufu ni taabu kidogo.

Ninachomaanisha ni kua EL alitumia nafasi zilizopo kuweka biashara halali.

Money laundering ina apply kwenye biashara kubwa kubwa ambazo ni capital intensive, biashara za airtime voucher au laundry hazihitaji capital kubwa. Labda real estate business.

Lakini si tuna takukuru? Mbona tuhuma nyingi lakini hamna uthbitisho? Isije ikawa ya HIZBU ya SAS!

hahahahaha.............TAKUKURU!...............hahaha..........
 
Back
Top Bottom