Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)


Masanja,

Wala usijali jina au neno unalotumia. Mie nikisoma tu maandiko naelewa una maanisha nini.

Back to the mada. Ndugu yangu kama KWELI UNANISOMA NA KUELEWA basi usingeandika wala kufikiri kua mimi ni mnafiki. Kwanini basi?:

- Huyu EL ana nguvu kweli kama tunavyooneshwa humu au kutakiwa tuamini?, ana nguvu kupita Rais kwa hiyo hawezi kuhijiwa na Takukuru?, kweli unaamini? na kama anazo hizo nguvu ilikuaje akautema uwaziri mkuu!!!?

- Huyu EL ni mwizi kweli kiasi hicho?, maana Wildcard ameandika kila sehemu anaiba, USHAHIDI ZEROOOO!

- Kweli kama huyu jamaa angekua na nguvu kiasi hicho kwanini asihame chama?. Pesa is almost everything... kama kweli pia ana hizo hela!

Basi Masanja ukishatafakari yoote hayo wewe mwenyewe bila kutumia magazeti au JF utanielewa. Kuna watu wapo humu kumponda Lowassa, kupandikiza chuki kuonyesha kila hila mbaya nk.

Why wapo hapa, kwasababu wametumwa, Lowassa ana nguvu za utendaji na anawaumbua wazembe ambao hawampendi.

By the way WHY LOWASSA tu ndie anajadiliwa?

Hope umeelewa.
 

- Ule mradi wa Mchuchuma na Liganga pia alikwapua hela zote
- Ule mradi wa umoja wa mataifa wa kufadhili nchi masikini iliyokua chini yake alipokua waziri mkuu
- Kuna fungu la kuendeleza AICC pia alilikwapua
-Kila mkurugenzi wa manispaa kila mwezi anampelekea hela la sivyo kazi hana na ameshafukuza ishirini kwa kushindwa kupeleka hela
- Kila mkataba anaosaini lazima apewe 20% yeye hataki 10%
- Kuna hela alipewa za kusaidia jimbo lake kutoka Ujerumani alizila zote wala hakusaidia jimbo
- Ana nyumba kama nane hivi London pekee yake
- Anauza ng'ombe kama mia kila wiki anapeleka Commoro na visiwa vingine hawa ng'ombe ni wale wanaoibiwa umasaini..

ENDELEZA MENGINE MABAYA UYAJUAYO YA Lowassa!!
 
watanzania bwana wanajua kupenda bila sababu.Rost tamu haziivi,low asa na wazee wengine.wameiendesha nchi kwa muda mrefu kwa jinsi usivyoweza kufikiri.wanamiliki chama,wana muweka mgombea wanahakikisha anaipita.wanampangia jinsi ya kufanya kazi asiguse interest zao.wengine tunavaa khanga na kujidai wanachama.
 
Reactions: Ame

Kila anayetaja anamtaja Mkuu au RA. Sasa bwana EL mbona mnampakazia sana?
 

Mkandara,
Ubeti wako wa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya umeishia wapi?

Hutaki Unaacha ni kama yuko right, usimbeze.

Nawatakia kila la kheri ktk safari yenu ya kuzimu.

Fanya kazi yako ya fani achana na siasa za CCeM wanakupotosha
 
Niliyoyataja mimi hayana ubishi. Waliompelekea MAMILIONI haya wapo. Mali anazomiliki zipo ambazo nyingi zinatokana na mamilioni haya. Unadhani ni rahisi yeye mwenyewe akalikana hili?
 
Mtoa habari umesema matajiri wa nje wameaminishwa kuwa ENL ni raisi a miaka 20, 2005-2025, so u mean that he is the current president sio?huyu tulionae ni just shadow ehheeeee, fantastic!
 
Ushahidi sio ZERO. Lowasa hajawahi kuwa nje ya utumishi wa UMMA tangu alipomaliza chuo mwaka 70 na ngapi sijui. Tumefanya nae kazi katika baadhi ya sehemu alikopita. Tunamfahamu na ukusanyaji wake wa maduhuli tunaufahamu. Hivi visingizio vya kuuza maua, vocha ni vitu vidogo sana.
Mkimdanganya akachukua fomu ya URAIS tutasema sana tu. Labda mtushughulikie mapema tu kama ilivyotokea kwa Dr OA Juma ambaye kukubalika kwake, uadilifu wake tu kulimwondoa duniani.
 
Ah naona kilichoandikwa kinahitaji uchunguzi na evidence,,,,, karume na kikwete wamefanya kazi pamoja na wanaekewana kupingwa ktk siasa ni jambo la kawaida ata hao wabunge wa chama kimoja wanamitazamo tofauti,,,,,,

huyu jamaa katumwa aje kumchafua Lowassa, rostam, shein na Karume na wengn,,,, amna lolote la kuliamini, Ivi kina karume na mkapa binafsi wameshindwa kumhonga direct Maalim mpaka wamtumie Jussa.

Huyu jamaa sijui kachukua mda gani kutunga stori yake, Maalim na Karume wamekuwa marafiki ktk miaka ya ivi karibuni kuanzia awamu ya pili ya Karume, Karume ni adui wa Bilal, Salmini na Mkapa, tena vipi karume awe rfk yake Mkapa?

Baada ya kuskia Znz kunataka kuwepo Mseto kilimuuma sana Mkapa coz alijua wapunzani wanaanza kuingia Madarakani, na hayo yamefanikishwa na Karume na Mkapa hakulipenda,,,,,

Dondoo nlizozipata ni kuwa Mkapa alikutana na mamake Karume na kumlalamikia about anachotaka kufanya Karume, mama akajibu muueni km mlivyomuua babake!

Karume ni kiongozi aloleta maendeleo mengi visiwani kuliko hata Shein, shein yy ataebdeleza tu lkn mwanzilishi ni Karume.

Na aliewaamsha waznz ni Karume na amewapa nafasi ya kujitetea, hilo halijamfurahisha mkapa kbs, tena vipi useme Karume na Mkapa wamo kwenye mtandao 1? Bora ungesema Karume, Kikwete, shein na maalim ni timu 1, afu umuweke Bilal na Mkapa timu nyengine!!
 

Waambie wewe , nikisema mie naonekana namtetea Lowassa. Vitu vingi sana havi ADD up!

Wildcard,

Achana na habari ya kwenye mitandao, hakuna anayeshughulikia mtu. Kila mtu na arobaini zake tu kama alivyopangiwa na Mungu.
 

Naona kama nimekupata kidogo. Nnachokiona dunia inaelekea mahali ambapo Policing itaanza kufanywa from the central point (katika level ya dunia) kuwainvestigate ikiwezekana hata viongozi wa nchi na kuwafungulia mashtaka. Hii njia hatuwezi kuiepuka na hasa ukitilia maanani kuwa uchumi wa dunia upo pabaya sana.

Mataifa makubwa yamekamua wananchi wao ili kusaidia masikini wa third world lakini misaada hiyo inaishia kwa wajanja wachache and the rest wanabaki masikini wa kutupwa. There will be a strategy to deal with this Mafia kwa nguvu zote, huko ndio tunakokwenda sasa.

Lets wait and see, ila this trend will come to an end, i do not know when though.
 
pale magogoni kuna rubber stamp tu
 
Waambie wewe , nikisema mie naonekana namtetea Lowassa. Vitu vingi sana havi ADD up!

Wildcard,

Achana na habari ya kwenye mitandao, hakuna anayeshughulikia mtu. Kila mtu na arobaini zake tu kama alivyopangiwa na Mungu.
FP,
Umenikumbusha kauli ya Mh Spika Sitta juu ya taarifa za Dr Slaa kuhusu ufisadi wa EPA nadhani. Alimtaka aachane na taarifa za mitandao. Kilichokuja kuthibitika baadae ni suala jingine sasa. Kama Lowasa anautaka Urais kwa udi na uvumba kiasi hiki na sio WANANCHI wanaomtaka awe Rais, atang'oa kila kisiki atakachokumbana nacho kwa namna yoyote ile kama walivyofanya kuanzia 1995-2005.
Hofu yangu ni kwamba huenda hata kifo cha Mwalimu hakikuwa cha kawaida? Kiliharakishwa?
 

Gogomoka,

I understand your point, lakini​ukweli bado unasimama kwamba Mtoa Habari is playing a very dangerous game, these are gruesome accusations, ambazo for sure leaves many of our jaws dropped; If he has evidence (it looks like ni mtu wa ndani), Jamiiforums sio mahala pake, kwani there are institutions that are specially designed to handle such.

Vinginevyo ni muhimu sana sisi kama Vijana tuka focus katika mijadala yenye ukweli na uhakika, and whenever taarifa kama hizi zikiwa zina pop up every now and then, busara ya kawaida kabisa, in my humble opinion, ni kuchukua tu notes.

Otherwise, personally, my unshakable belief is that, kutumia muda mwingi katika mijadala dominated na taarifa zisizo na ukweli au uhakika, doesn't provide us with a better future kama vijana. Discussions zenye traffic kubwa namna hii, laiti zingekuwa zinalenga kwenye mada on youth development e.g. employment generation, elimu, leadership, our new constitution, etc,

sio tu kwamba ingetujengea msingi imara for a better future, but also even our sons, daughters, grandsons and granddaughters, wangefaidika sana kwa kurudia and review our archives in JF, and in the process determine challenges za waliowatangulia zilikuwa ni zipi, hence put them in a better position kuzikabili changamoto zao.
 
Mkuu tunakushukuru endelea kutujuza,MUNGU akupe uhai ili tujue mengi
 
kesha sema kama HUTAKI UNAACHA

Siachi!
JF hatuzibani midomo, huwezi kuleta topic ikabaki bila challenge.
Read between the lines
Kuna mada nyingine ya namna hiyo hiyo aliileta mwaka jana, ipo katika kiungo hiki, soma jue mtoa mada katoka wapi na mada za namna hiyo. Usilale mwanangu.
 
Let me watch and learn..
:juggle:
 
Lowasa will never be the president of Tanzania...never...na hawa walipanda ELairline daraja la economy na business nawashauri wasiendelee na safari maana hawatafika.....

kuhusu kifo cha mwl ..hili tuliongea kwa kirefu snaa jukwaa la inteligence tafuta thread inayosema ''did mwali die a natural death?''
 

YES sir! alikufa kawaida. NI PM nikuongezee kidogo. Ila hakukua na mkono wa mtu alie HAI kwenye kifo cha Mwalimu.

Usiogope hakuna atakaye kutafuta wewe WildCard.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…