Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Hata hii inaweza kuwa club,Wako wapi kina Es na mwanakijiji,mbona pamepooza hapa club..ni sawa sawa club siku asipokuwepo jenerali na balozi ami au chenge inavokua doro ati,kuna watu wameumbwa hivyo uwepo wao unakua ni a million dollar!
 
Uyo mbunge Ps ndio nani jamani?ata kwa kuniPM.
 
Huuh! Toka saa 2 ucku ndo nimemaliza nw, duh mambo mazito. Ngoja nipumzike kwa kucheki live scores man cty vs liva.. Jf ni noma. Mzuka wakucheki epl leo umekata
 
Hata hii inaweza kuwa club,Wako wapi kina Es na mwanakijiji,mbona pamepooza hapa club..ni sawa sawa club siku asipokuwepo jenerali na balozi ami au chenge inavokua doro ati,kuna watu wameumbwa hivyo uwepo wao unakua ni a million dollar!

Kuna vi-clons vyao hapa.......kwa hiyo mambo mswano tu........!
 

Mtoahabari.
Nimepigwa na Butwaa!! "Nambie unafurahisha Baraza" Yani yote haya mada ni hii ya Mtandao Hatari??
Kijana anatuletea za Balasconi! Mwambieni hapa sio Utaliani, Kisha amwangalie Nzi atapata somo "Kama yeye ajua wa mbele, wenzie wajua wa nyuma." Tena kazi mbaya si mchezo mwema.....................
 

Mkuu T R,
Mimi nilikuwa na hisia kuwa Mtoa Mada ( Hutaki Unaacha) na Mtoa habari ni Mtu na Kivuli chake!! Nadhani unanielewa? Angalia huu mjadala ulivyopoteza Afya. Isipokuwa siamini kuwa unahusiana na uchaguzi wa CCM mwakani.
 
uliwezaje kununua kinywaji wakati pale bill inatakiwa kwenda kwa member aliye kuleta? au siku hizi wamelegeza masharti? kwamba yeyote tu anaweza kwenda? si patajaa kama swazi na kuharibu usalama wa nji!
 

Aliwahi sikika mara kadhaa miaka ya nyumba kabla tu ya kuwa waziri mkuu, baada ya Remmy Martini zake kadhaa, kwamba IDOL wake ni Berlusconi. Na hivi sasa ameingia kwenye biashara na umiliki wa Magazeti, kituo cha Televisheni, na Radio.
 
Mkuu.
Tetesi tafsiri yake si Lisemwalo lipo?

Tetesi ni umbea ambao unaweza kupuuzwa kwani ni mchanganyiko wa ukweli na uwongo, unaosafirishwa kwa njia ya mdomo au maandishi. Umbea huu unapokufikia, ni jukumu lako kuuthibitisha, kisha kuufanyia kazi.
 
For the kingdom, the power and the glory are yours God, for ever, Amen
 


Z train.
Ndio hivyo Mkuu Wanasema ukistajabu ya Musa utaona ya Farao/Firauni.
 
Mkuu T R,
Mimi nilikuwa na hisia kuwa Mtoa Mada ( Hutaki Unaacha) na Mtoa habari ni Mtu na Kivuli chake!! Nadhani unanielewa? Angalia huu mjadala ulivyopoteza Afya. Isipokuwa siamini kuwa unahusiana na uchaguzi wa CCM mwakani.

Jamaa yuko maandishi yake yako very technical,ukiingia kichwa kichwa utacheza ngoma ya lowassa bila kujielewa,si unasikia kuna watu wanakwambia kesho maofisini na kwenye barza za kahawa wataipata?hapo lengo la "mleta mada" hutaki unaacha litakua limetimia au halijatimia kwa watz wa kawaida ambao wanapenda sana kuhadithiwa ili wakahadithie kama walikuwepo mahali husika?si unajua wabongo wanavyopenda kuonekana ni watu wa usalama wa taifa kwa kuhadithia story za "hatari" huko uswahilini kwetu?tuwe makini.

Leo utaambiwa Rashid othman kwa kuwa ana undugu wa damu na jaji wetu mkuu na ro inasemekana alichaguliwa na Lowassa na rostam nae pia kawekwa na hao japo hawakuwako madarakani jaji mkuu akichaguliwa,lakini wabongo kwa kupenda stori wanakubali bila kuchallenge,leo utaambiwa lowassa na rostam wana miguvu mpaka ya kutishia watu wasizungumze kwenye vijiwe lakini ukiuliza jamani eeeh hawa watu wakubwa kuliko chama na serikali walioshika kila sehemu nyeti si waliapa jimbo la igunga litaenda upinzani sasa imekuwaje bila msaada plus hujuma zao ccm imeshinda igunga?hawakujibu utaambiwa aidha hutaki unaacha au tulikua tunatoa taarifa tu,basi ili mradi sarakasi za maneno zisizoisha lakini wabongo wa wengi wa humu bado wako usingizini,hawahoji hoja za wazi kama hizi zinazohitaji ufafanuzi zaidi,wanataka stori zaidi za kwenda kutishia watu mitaani!
 

EL na RA kuikosa igunga katika uchaguzi mkuu mdogo, na badala yake JK na watu wake kuibuka kidedea...,JK na watu wake kushindwa kwenye uchaguzi wa wabunge wa viti maalum UVCCM, na badala yake EL na RA kubeba viti vyote, yote ni sehemu ya mapambano. Kuelezwa jinsi gani EL anafanya kazi mitaani sio kutishwa, bali kupewa tahadhari. Mtu anaye threat ni yule anaye inspire fear or dread kwa wenzake kuhusu jambo fulani, lengo likiwa kuwafanya wafuate maelekezo yake ili wasipate madhara. Mtu anaye toa tahadhari, ni yule anaye elezea mwenzake/wenzake juu ya hatari fulani iliyopo, ili wenzake hao waifahamu na hivyo kuikwepa. Ninachofanya sio kuwaeleza wenzangu wafuate maelekezo yangu na waache matendo yao kulipigania taifa lao, bali kuwaeleza wenzangu juu ya hatari iliyopo katika mapambano yanayoendelea kulikomboa taifa lao, ili waifahamu hatari hiyo, na hivyo waikwepe, na kujizatiti zaidi, bila ya kuacha mapambano. Vinginevyo mpaka baina na threat na caution ni mwembamba sana mithili ya uzi wa kushonea, hivyo kupelekea taarifa zangu kuonekana kama vile zinaangukia pande zote. Vinginevyo wa kuelewa wataelewa, na wakuhisi vinginevyo, watahisi vinginevyo.
 
uliwezaje kununua kinywaji wakati pale bill inatakiwa kwenda kwa member aliye kuleta? au siku hizi wamelegeza masharti? kwamba yeyote tu anaweza kwenda? si patajaa kama swazi na kuharibu usalama wa nji!

hivi kweli unaweza kuingia club bila kuwa member ama kualikwa na mwenyeji?ckub sio bar jamani,ni sawasawa uende pale cosmo au pan enzi zile au simba na yanga bila kuwa member useme utajiingilia tu na kukaa kwenye benchi ukaanza kusikiliza yanayoongelewa mle na wanachama,ingekua ni hivyo basi habari za club na watu wanachama wake zingekuwa hadharani kwa kila mtu kujua jana wendo na chande walitukanana au juzi Bade na mfuruki walicheza sana muziki,ama jenerali alimtukana sana vijisenti,nawamegea haya kwa kuwa yanatokea sana na yanaishia pale,kama mtakumbuka issue ya pekee ambayo iliwahi ku leak pale angalau ni ya jenerari na Lau masha nayo ilivujishwa na mtoto wa kike aliyekuja pale kama mualikwa bahati mbaya badala ya kukaa private akajichanganya pale kwenye matusi,napenda sana ku share but nahofia kujulikana nikapigwa "global" ban,kule kuna ban pia bandugu!ila mtu asiwadanganye eti anaweza kuleta pua yake pale bila kuwa member na akaingia,na membership iko wazi tu wala mtu asikutishe..hao vijana wengi wanaotajwa tajwa hapa wameingia juzi juzi tu na wengine hata hawana majina na kuna wenye majina na misifa wamepigwa chini kwenye hatua ya applications,mfano huyu jamaa wa kampuni ya sign boords mwenye ofisi pale shauri moyo ilala..
 
Huyu mtoa mada kama kasahau boxer guest bhana sa ni nini hii aisee...ninachoamini hii ni story iliyotungwa kwa mpangilio ili kushika mabrain wash wake hapa whaai..tupa kule inachosha ubongo tu.....speed ile ile CCM kimewawakia na mtaisoma 2015....
 
The Romantic,
Kumbe na wewe ni memba pale British Legion? Nisalimie Wendo.
 

Natamani uniruhusu nianze kukunukuu andishi moja hadi lingine katika yale yanayoleta shaka ya vitisho zaidi na yanayomjenga jamaa na kuonyesha kujaribu kuonyesha kwamba kuchagua kupambana nae ama kumdhibiti kama nguvu ya umma ni kuchagua kifo na kwamba hakuna njia ya kumzuia?japo sipendi sana tuiteke ionekana ni mpambano wa mimi na wewe bali kila mwenye lake aliweke
 

Mkuu
Uhanga kwa Mbongo? Pamoja na shida zake jioni hupata wasaa wa moja moto moja baridi................! Lisilo budi hutendwa, labda tupeleke kijitimu huko Afgani au hatajirani mitaa ya Mogadishu wakirudi tunawaita G 12, kwa hiyo g8 atakuwa cha Mtoto.
 

Hatuna haja ya kufika huko kwani wapo wenye akili timamu humu wenye ufahamu fika kwamba Lowassa ni mchafu na hafai kuliongoza taifa hili. Wanaomwona anafaa wanafuata haiba (personality) ya Lowassa ambayo itaondoka nae akienda kaburini hata kesho, hawafuati dira au itikadi ambayo itasimama hata pale atakapotoweka duniani, kwani haipo. Ushabiki wa Lowassa ni wa mchezaji kama David Beckham, wanahama nae, iwe china, Marekani, Hispania, n.k. Sio timu pamoja na historia na utamaduni wa timu husika. Mimi ni shabiki wa timu, wachezaji wanakuja baadae, sishabiki golikipa Juma Pondamali ambae alikuwa Pan African na Baadae kuhamia Yanga, nashabikia Yanga, hata ikimsajili Issa Michuzi kama beki namba tatu. Vinginevyo, mwenye mashaka na maandiko yangu ni wewe tu, ambae hata kauli zako juu ya hiyo club ni haiba/personality za mtu mmoja mmoja, sio utashi wao kwa pamoja katika jamii. Na hicho ndio kiini cha wewe kutilia mashaka utoaji wangu wa taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…