Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)


Mwizi ni mwizi tu, hakuna mwizi mwenye afadhali. Huwezi kusema mwizi X ana afadhali kwa kuwa eti akienda kuiba hauwi victim.
 

Nakumbushia tu. Huyu si ndiye aliyetaka kutuletea dili ya mvua ya Thailand. Bahati nzuri fisadi mwezake huko Thailand akapinduliwa kabla ya kukamilisha dili lao.
 
Nakumbushia tu. Huyu si ndiye aliyetaka kutuletea dili ya mvua ya Thailand. Bahati nzuri fisadi mwezake huko Thailand akapinduliwa kabla ya kukamilisha dili lao.
Mkuu ile report ya jamaa mmoja aliyekuwa akijiita Kasori au Kisori, katibu mkuu serikali ya Nyerere aliishia wapi nakumbuka naye hakurudi kuimalizia. Kwa kukumbusha tu huyu jamaa aliandika jinsi Nyerere alivyomtoa EL ktk wagombea urais, kisha EL akamtuma nadhani Kawawa kwenda Butiama kumwambia Nyerere alisafishe jina lake ili apate kugombea Ubunge... Ile habari ilikuwa nzito sana lakini jamaa akaingia mitini...

2. Hivi wale wote waliokuwa Tume ya Mwakyembe wapo bado hai au madarakani, nakumbuika Seleli alipigwa chini wale wengine Je?..
 
Kwenye Hayo maandishi hapo juu kabla ya kusema "sitaki na kuacha" ama "nataka na kuyameza" kidogo yanahitaji ufafanuzi maana kuna contradiction ya hali ya juu,nilitoa muda jamaa arudi lakini hajafanya hivyo nimaeamua kukichambua kilichopo katika maandishi yake komoja baada ya kingine:

Tunaaminishwa kwamba marehemu Dr.Omari ali juma alikua threat kwa genge la jakaya,lowassa na rostam,sitta na wengine kwa kuwa mtandao "wake" (dr.omari)ulioongozwa na mzee mkapa ulikua "hatari" sana,mpaka hapa tunaona kwamba kuna makundi mawili "hatari" kwa jinsi alivyoonyesha mleta thread,yani kundi la kina jk,lowassa,rostam na sitta na kundi la mkapa,dr omari na apson!Lakini hapohapo jamaa anatumbie tena APSON,MKAPA,LOWASSA,ROSTAM wako kwenye kundi moja dhidi ya kikwete!hili linahitaji ufafanuzi zaidi..tujue kwanza kundi lililompoteza dr omari ni lipi kati ya hayo mawili,hii itatusaida kwenda mbele zaidi na kujua kundi hatari la mkapa lililokua na dola liliishia wapi baada ya dr omari "kupotea"

Jambo lingine ni suala la jk baada ya kupitishwa kugombea jamaa anatueleza alitaka kumuweka zakia kuwa mgombea mwenza wake lakini mtandao ukamgomea,hapa sijaelewa ni mtandao upi kati ya wa akina kikwete,lowassa na rostam ama wa mkapa,maana ni wazi mkapa hakua kwenye mtandao wa kina kikwete lowassa rostam na sitta,ndio maana hata kwenye issue ya kuteaua waziri mkuu jakaya alihitilafiana na "wazee" kina mkapa ambao hawakumtaka lowassa awe pm,hili nina (ushahidi nalo)mpaka jakaya alipopandisha mashetani ya kikwere na kuwaeleza kinaga ubaga kama hawezi tena kukubali wamchagulia waziri mkuu na yeye anataka kufanya kazi na swahiba wake lowassa,ikumbukwe hapo mwanzo "wazee" walishamchagulia watu kadhaa nyeti akiwemo mwanasheria mkuu!

otherwise tuache propaganda watz wa sasa wanakumbu kumbu nzuri ya kilichotokea nyakati za mwanzo za utawala wa kikwete na mtandao wake pamoja na wazee wa nchi!japo kutokana na ushabiki wapo baadhi watajifanya wamesahau na kukubali ulaghai wa kwamba mkapa,rostam na lowassa walikua mtandao mmoja!ingekua hivyo mkapa asingemkataa lowassa kuwa waziri mkuu mpaka jk alipopandisha mashetani ya kwao ndio wakanywea!na wala kina rostam hawakutaka shein awe mgombea mwenza,walika na mtu wao kutoka unguja na sio pemba!
 
There you are!......na ENL alipojua hayo kupitia vijana wake alifanya nini akiwa kama kiongozi...........mbona huendelezi/humalizii?......wee unafikiri Nyerere (RIP) alikuwa zuzu?..........

usicheze na shekeli hata Yuda alimuuza Yesu, na usicheze kukaribishwa british legion, ndio maana unasikia jamaa alikwenda pale bila support ya member , akaona afadhali aishie uswazi!
sasa hivi naona kampeni za waandishi kununuliwa ahead of 2015 zinaongezeka
 

Mkandara,

Waraka wa Mzee Kasori kwenda kwa Lowassa uko hapa hapa JF, juzi juzi tena naona ulikuwa kwenye page ya juu kabisa. Sina hakika kama Hamis Kasori aliingia mitini, nadhani ujumbe wake ulikuwa umekamilika. Yeye kwa mtazamo wake alichokoza na alikuwa akisubiri tu Lowassa ajiweke kwenye kilengesho. Ila kwa kuwa Lowassa ni mjanja wa kufunika uvundo, alikaa kimya bila kujibu na hivyo ule waraka ukawa umepotezewa kiaina.

Wajumbe wa Kamati Teule ya Dr. Mwakyembe wote bado wako hai.
Dr. Mwakyembe ndio huyo ambaye anaendelea kuugua huku akiwa Naibu Waziri wa ujenzi
Eng. Stella Manyanya bado ni Mbunge wa Viti Maalum na majuzi alipewa ulaji wa Ukuu wa Mkoa wa Rukwa.
Ndugu yangu Lucas Selelii ndo huyo yuko Nzega akiuguza kupigwa chini na wapiga kura wake.
Habib Mnyaa bado ni Mbunge kupitia CUF.
Herbert Mntangi bado pia yuko Bungeni.

Kwa hiyo mjumbe pekee aliyepoteza ulaji ni Lucas Selelii.
 

Mkuu The Romantic,

Mimi nilivyomwelewa mtoa mada ni kwamba Dr. Omar A. Juma alikuwa ni threat kwa mtandao kwa sababu kubwa mbili, alikuwa ni clean [hana uchafu wa kumchafua nao] na kwa kuwa alikuwa ni Makamu wa Rais na anatokea upande wa pili wa Muungano then it was easy kujenga hoja ya kuwa mteule wa kugombea nafasi ya urais. Moja, kwa kutumia u-Zanzibari [kwamba baada ya Mkapa wa bara then angefuata wa Visiwani]. Pia hakuwa na tuhuma zozote chafu. So, the best way ya ku-deal naye ilikuwa ni kumwondoa njiani [if at all kifo chake kilitokana na hilo].

Hapo inabidi ukumbuke kwamba wana Mtandao walikuwa wana-deal na yeyote yule aliyekuwa anaonekana kwamba anaweza kuwa kizuwizi kwao. Ndio maana wale ambao walikuwa na "tuhuma" za ukweli au za majungu, tayari walishaandaliwa njia ya kuwamaliza kiaina.

JK, Lowassa, RA, Sitta, Membe na wengineo wengi tu walikuwa kundi moja la mtandao. Ingawa baada ya uchaguzi ndipo yalipozaliwa makundi mawili, mtandao original na mtandao matumaini [wale ambao hawakuambua kitu cha maana pamoja na ku-toil sana kwenye kampeni za mtandao]. Hao akina Apson walikuwa recruited along the way. Mkapa alikuja kuingizwa kwenye kundi la mtandao dakika za mwisho. Mkapa kwa kujua kwamba hilo lilikuwa ni kundi la opportunists, hakuwa na uhakika wa usalama wake wala mali zake na ndipo mtandao walipolambishwa EPA ambayo inawahenyesha mpaka leo na ndio maana akina Kikwete na Pinda wanaendelea kumtetea Mkapa mpaka leo hii kwamba mwacheni apumzike.

Zakhia Meghji alikuwa ni mwana mtandao. So, waliomgomea hawawezi kuwa wana mtandao, bali watakuwa ni wazee wa CCM kwenye Kamati Kuu. Ubaya wa kupendekeza Mgombea Mwenza ni kwamba mgombea Urais hupendekeza jina na ndipo wazee walafi wa CCM hujadili hilo pendekezo na kukubaliana na ndipo huenda kutangazwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama. Kwa hiyo kama ni kugoma, watakuwa waligoma akina Mkapa na wengineo walio kwenye CC. Wakati huo mgombea mteule huwa hana final say na inawezekana CC inaweza kuibuka na jina tofauti kabisa na lile lililopendekezwa na mgombea mteule.

Kwenye swala la Waziri Mkuu, CC wala Rais aliyetangulia huwa hawana nafasi kwa kuwa Rais mteule anakuwa na uhuru wake wa kupanga safu ya watendaji bila kukishirikisha chama chake. Ndio maana JK alikuwa na jeuri ya kuwagomea. Ni ngumu kugoma kwenye uteuzi wa mgombea mwenza kwa kuwa kila kitu kinafanywa na chama kwa kuwatumia wale "ma-think tank" wao walio kwenye CC.
 


Hii ni sehemu ya waraka wa mzee kasori kwenda kwa Lowassa!
 
August, nakuomba uamini sio kweli watetezi wote wa Lowassa humu wamelipwa!. Just amini hivyo!.
Mimi Pasco (wa jf) ni mmoja wa watetezi wa Lowassa ateuliwe kuwa mgombea wa CCM nikiwa sina chama wala sijapewa senti tano ya mtu awaye yote!.
 
mijadala kama hii huwa inaniogopesha...imekaa kimafia mafia
Ipo siku, mtandao wa wananchi uta shinda....
 
kama mpaka Pasco ame convert....basi una haki ya kukata tamaa......
honestly huwa najiuliza hii nchi ina walakini gani?
mbona we cant finds men with balls kwenye siasa zetu?
decent men???????
The Boss, kuna msemo wa Kiswahili usemao "Usiogope kugombana na nduguyu/rafikiyo katika jambo ambalo mtakuja kupatana!".

Kwa utetezi wangu kwa Lowassa bora tugombane tuu kwa sasa akishateuliwa tutapatana tuu!.

Kwa wale mnaonifahamu na kunikubali kuhusu misimamo yangu katika baadhi ya issues, natoa wito tuungane mikono tumsafishe Lowassa awe mgombea wa CCM, tumeshasema mara mia humu kama dhambi kuu ya Lowassa ni zigo la Richmond, kwenye sakata hilo Lowassa alikubali tuu kulibeba ili CCM iokoke kama Bwana Wetu Yesu Kristo alivyobeba dhambi zetu na kwa kuteswa kwake sisi tumeponywa vivyo hivyo kwa kuteswa kwa Lowassa CCM imeokoka maana laiti mngelimjua mwenye zigo lake halisi!, I can't imagine kama Lowassa angehojiwa na kuusema ukweli ingekuwaje!.

Lowassa ni mtu shupavu na jasiri sana, just imagine mpaka leo bado anaendelea kulibeba hili zigo kwa uvumilivu mkubwa na ustahimilivu wa hali ya juu!. Nani mwingine kwenye CCM angeweza kuvumilia yote hayo bila kumtaja mwenye zigo lake!.

Zawadi pekee anayostahili sasa ni kutunukiwa ugombea kwa tiketi ya CCM tena nawaombeni sana sana sana tuungane katika hili!.
 
Lol...sasa naweza kusema kwa uhakika kabisa hata mzee wa vijisenti nae 'tulimwonea'...maana ni kweli vilikuwa 'vijisenti'! Pasco, honestly, hivi kumtetea kote huku EL ni kwa maslahi ya nchi yetu ya Tanzania? Kweli!?
SMU, tangu thread ya Vijisenti nimesimama nae, wanamuonea tuu kwani kuiukweli zile fedha alizokutwa nazo ni kweli kabisa ni 'vijisenti' tuu!.

Uwingi au uchache ni relative na terns of comparison. Kwa mfano mishahara ya juu nchini Tanzania ni Milioni mbili!. Hiyo ndio mishahara ya wakurugenzi, makatibu wakuu, wakuu wa wilaya, mikoa, majaji na wabunge. Kwenye benki ya ADB, hizo milioni 2 ndio kima cha chini, watu wanalipwa mpaka zaidi ya milioni 30 pm!.

Pesa alizokutwa nazo Mzee wa Vijisenti ni peanut ukilinganisha na migawo wenzake waliopata!. Kosa lake ni kutuhifadhi tule tujisenti twake ile benki ya kule Virgin Island hatimaye tukaonekana!. Wenzake wamehifadhi fedha kweli kule Credit Sussie hivyo hazijaonekana!.

Hivyo Chenge was right kuviita vijisenti maana kwenye ule mgao yeye ndie amemegewa fungu dogo!. Jee laiti mngelijua waliovuta fungu nene ni kina nani?. Mngeshindwa hata kushangaa mgebaki midomo wazi!. Mnajua ni kwa nini licha ya ushahidi huo hajashitakiwa?!. Amini nawaambieni hahashitakiwa kwa sababu ni heri aachwe ajikalie kimya asije kushitakiwa na kuwataja washirika wake ambao kwa kwa macho ya kawaida ni 'Watakatifu'!.

SMU nakuhakikishia asilimia 100% kwa 100% utetezi wangu kwa EL ni kwa maslahi ya taifa!. Sina maslahi binafsi yoyote na sijapokea hata senti tano ya yeyote!
 
Pasco,
Anaekamatwa amebeba, si ndie Mwizi?

Jujuman ni kweli anaekutwa na ngozi ndie aliyeiba ng'ombe!. Lakini wakitokea watu waliomshuhudia mwizi halisi wa ng'ombe na kumshuhudia akimchinja na kumchuna ngozi aliyoibwaga hapo chini na yeye kusepa na nyama huku nyuma masikini wa watu kajionea ngozi iliyotupwa na kujiokotea ili ikamfae ndie sasa ahukumiwe kwa wizi wa ng'onbe!. Jee hii ni haki?!. Jee hii ni halali?.
Kwenye sakata la Richmond, Lowassa amekutwa tuu na ngozi siye aliyeiba ng'ombe!.
 
August, nakuomba uamini sio kweli watetezi wote wa Lowassa humu wamelipwa!. Just amini hivyo!.
Mimi Pasco (wa jf) ni mmoja wa watetezi wa Lowassa ateuliwe kuwa mgombea wa CCM nikiwa sina chama wala sijapewa senti tano ya mtu awaye yote!.
Mkuu Pasco hebu jifikirishe kidogo.tunaambiwa juzi Lowasa amemvua nguo mkuu wa Kaya kwa kuonesha lile zigo si lake lakini kwa alivyonukuliwa akizungumza alisema alimpigia mkuu akiwa nje ya nchi akitaka kuifuta Richmond! Hivi Pasco kweli lowasa anajua kampuni ya mkuu wa kaya alafu ampigie kumwambia naifuta!toka awali hii Richmond ilibebwa na Lowasa bila kujua zigo la nani? Tunaaminishwa Lowasa alishirikishwa mwishoni kuokoa jahazi,mwisho gani? Pale akina mwakyembe walipoanza uchunguzi? Au kuwajibika kwakwe haraka ndio kumuokoa Mkuu wa Kaya? Tunaambiwa mkuu alisoma ripoti ya Richmond kabla haijaenda bungeni alafu akaruhusu isomwe! Dili lake alafu ajiumbue vile! Hiyo kampuni toka inaingia Tz inaitwa Richmond na hilo jina ENL analitumia hata sasa kwenye biashara zake ni coincidence tu? Wakuu nisaidieni kunitoa kwenye hili lindi la maswali lisilo na majibu! Kweli Richmond isiwe zigo la ENL liwe la Mkuu wa Kaya? Inafikirisha sana!
 
Keil,

Mkuu wangu sijui nianzie wapi. Maana umesema sana na upo sahihi kabisa. Bado namtetea Lowassa, naamini vyama vya upinzani havijakomaa na sio instutionalized kama CCM.
CUF = Maalim
CDM = Mtei, Ndesa, Mbowe, Makani
NCCR = Mbatia

Kwahiyo mgombea urais wa CCM ndio atashinda na CCM ndo chama huru ANGALAU.

Tukubaliane kutokubaliana mpaka nitakapomshawishi Mkandara akija bongo naye anisaidie namna ya kuelezea kuhusu Lowassa.

Ila bado naamini ELairline ndo airline pekee inayostahili kuwa NATIONAL carrier wa kuanzia 2015.
 
MTAZAMO, naomba tusiendelee kuandikia mate ilhali wino upo!. Vuta subira kidogo tuu and time will tell!.
 

nimesoma maandishi yako naona hayana chembe ya shaka na ndicho ninachokijua mimi,kama umesoma sawasawa nilichoandika nilikua namchallenge mtoa tetesi ama mleta thread,kwamba katuchanganya aliposema kwamba DR. alikua tishio kwa mtandao wa kina lowassa na rostam(kikwete,sitta etc)kutokana na kuwemo kwenye mtandao aliouita "hatari" wa mkapa na apson ambapo kama umemuelewa ilibidi aondolewe duniani,hapa ni wazi kama mtandao wa lowassa ndio ulihusika kumuondoa mtu wa mtandao "hatari" wa mkapa na apson kulitokea kutoelewana kwa mitandao hii miwili,sasa ilikuwaje tena mtandao wa kina lowassa uungano na mtandao wa mkapa kumshinikiza mtu wa mtandao wao amchukukue mtu wa mtandao wa mkapa?nakataa kusema mkapa alikua mtandao mmoja na kina lowassa wakati wa kumtafuta mgombea mwenza wa kikwete,ingekuwa hivyo angekua anaujua mkakati mzima wa kumuweka lowassa kuwa waziri mkuu na wala asingemtoa jasho kikwete na kulia kwamba wamemchagulia mgombea mwenza,wamemchagulia mwanasheria mkuu na sasa wanataka kumchagulia waziri mkuu ambae alikua huyu pinda na hiyo hawezi kukubali tena!Lengo langu ni kueleza aliyembeba lowassa mbele ya wazee wa nchi ambao walikua hawamtaki ni kikwete japo pengine baadae alikuja kujuta au bado anajuta...

unajua jk asingeleta ubishi kwa kina mkapa pale mwanzo haya matatizo yatokanayo na lowassa yasingekuwepo,na pia kumtosa mangula kwenye sekretariet licha ya tofauti zao kwenye mchakato(mangula hakumtaka jk wala genge lao) na kumuandama kuhakikisha haingii nec kupitia uenyekiti wa mkoa ccm iringa lilikua kosa pia
 
Nakumbushia tu. Huyu si ndiye aliyetaka kutuletea dili ya mvua ya Thailand. Bahati nzuri fisadi mwezake huko Thailand akapinduliwa kabla ya kukamilisha dili lao.

.......alikuwa ANATHUBUTU!.........
 
Usicheze na kitu inaitwa love of shekeli.....The root of all evils!

"Extreme Ukosefu" wa Shekel ndio root ya all evil. Tatizo la ulafi wa EL lazima tukumbuke alipoanzia ni ile decade (1979/80-1989) alikuwa na njaa ya ajabu. Si ajabu aliwahi kukosa pesa ya matibabu ya watoto! na huo ndio kuwa mwanzo wa kuapa kuhakikisha akipata mwanya basi aendelee kuchoto. Alipofikia hivi sasa ni kama depression/addiction au kama si hivyo ni pathological related issues ambazo zinahitaji matibabu. Ni very rare kuona mtu asiyeridhika kwa kiwango chake.

Ndugu yangu Pasco unanitisha kwa jinsi ulivyo "up the ante" kumtetea "ELAirline"...Mkandara tafadhali mkumbushe rafiki yako kwenye mazungumzo yenu awe makini asitake kukutana naye huyo "mgombea wake" kwani (kwa mujibu wa mabandiko yaliyopita) mwenzie inasemekana kafudhu techniques za ku-unlock wanaume wenzie. Sio vizuri kuanzisha ugomvi kati yako na "PS" wa EL kisha tukaishia kukufungulia thread humu kwani JF ni kiboko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…