Mkuu kuhusu msimamo wa mmkijiji nina wasiwasi,
thread imejadiliwa sana kuliko thread iwayo yote wiki hii
Hata hivyo, yeye ameamua kutochangia hoja hiyo inayohusu kama Lowasa anafaa au La. Kilichonishtua ni wapambe wa Lowasa akiwepo Pascal kujenga hoja kwamba baada ya Mzee Mwanakijiji kuona kwamba Lowasa lazima atakuwa Rais, yeye ameona heri amuunge mkono Lowasa. Hata hivyo kinachonishangaza zaidi ni Mzee Mwanakijiji kukaa kimya na kuacha kutoa msimamo wake hata baada ya maeleozo hayo.
Nikaanza kuwaza mwenyewe kuwa;
Kusema kwamba M M Mwanakijiji hajasoma thread hiyo ni jambo lisiloingia akilini mwangu kwa kuwa ni thread ambayo mpaka sasa imechangiwa na watu karibu 1000 na na kusomwa na watu kuelekea 24,000 mpaka leo.
Jambo jingine, kichwa cha habari kilivyowekwa lazima mtu yo yote aliyeko ndani ataisoma, kwa hiyo sikubaliani kwamba hajaisoma.
Ukienda mbele zaidi, ni kuwa thread hiyo imekaa karibu wiki ktk ukurasa wa Mbele bila kuondolewa na Mods.
Kali zaidi, Mzee MM anawekewa maneno mdomoni ili kumprovoke na yeye ameamua kukaa kimya. Kwanini ? Ndo kusema tayari na yeye ameingia EL airline? Au ni kweli hajasoma hiyo thread? Au amesoma thread hajasoma comment za akina Pasco zinazosema kuwa amepanda EL airline? Najiuliza tu. Point of doubt to me.
What do you think?