Mr President,
Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).
Hapa huyu Hutaki Unaacha, amejitambulisha vizuri, kuwa ameandika haya, sio ili kumtisha jk, bali kumpa warning na pia kujitanabaisha, yeye hamtegemei jk kuishi, hivyo huyu ni mtu wa TISS! aliyekereka na mambo yalivyokwenda na yanavyo kwenda! nawashauri japo tusimwaminie 100% kwa 100%, but sio wa kupuuzwa hata kidogo!. Mimi naendelea kuisoma makala yake mara mbili mbili na kila nikisoma, napata vitu vipya!
Ninachozungumzia hapa ni kundi kubwa na hatari linaloaminika kuongozwa na Edward, Rostam, Othman, Apson, Karume na Shein na Mkapa. Ninakufahamu vizuri sana na ungekuwa uwezo wako, hawa wote ungeweza kufanya uwezalo ili kumweka madarakani mtu unayemtaka kwa maana ya Asha au Nahodha. Huu ni mtandao unaofanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana. Ukitaka kuamini, jiulize swali la kipuuzi sana kuwa kwanini kila plans unazofanya (zisizo na faida) kwa kundi hili zote zimefail?
Kumbe JK anamtaka Nahodha na Asha?. Hapa jamaa amechapia!, JK anamtaka Shein, Asha ndie makamo wake! Naodha anarudi Zanzibar kuwa rais, Makamo wake ni Dr. Mwinyi!. Kitu ambacho CCM hawajui ni kuwa 2015 Zanzibar ni zamu ya CUF! na wakikashinda watavunja muafaka ..mtaniambia!
Nataka nikukumbushe ''issue'' ya Omar Juma. Huyu alikuwa threat kubwa kwa kundi lenu kwa ajili ya 2005. Mtandao wake ukibebwa na Mkapa ulikuwa ni hatari sana. The only way ilikuwa ni ''kumwondoa'' na hilo liliwezekana. Siku nikiwa na muda nitaeleza mchezo wote ulivyofanyika. Wakati jina limeletwa tukiwa hotel moja maarufu hapa Dar, nakumbuka hukuweza kumfahamu Shein wala kulitamka jina lake vizuri. Ulikosea mara tatu kulitamka. Tukacheka wote. Hatimaye Shein akawa makamu wa rais.
Kumbe Dr. Omar, aliondolewa!, japo binafsi siamini!, nikiamini kifo chake ilikuwa ni kazi ya Mwenyeenzi Mungu, ila hii hoja jina lilitetwa wakiwa hoteli moja na eti jina la Shein lilikosewa mara tatu mpaka watu wakacheka!, hili jina la Shein lina ugumu gani mpaka likosewe mara tatu?. Hii ni fix!
Baada ya wenzako kukuweka madarakani (mgombea ndani ya CCM), kosa ambalo Shein hataweza kukusamehe katika maisha yake (Mimi sio Mungu, kwani anaweza kukusamehe vilevile) ni pale ulipo-attempt kumfanya Zakhia kuwa makamu wa rais. Asingekuwa Edward, Rostam, Mkapa na Karume, leo hii Shein angekuwa mwenyekiti wa TPDC au TANAPA!. Kitendo cha Shein kuletwa na kundi hili, kutetewa na kundi hili achilia mbali kushawishiwa na kundi hili agombee urais wa Zanzibar ili kummaliza nguvu Nahodha chaguo lako kinamfanya awe mtiifu kwao kuliko hata kwa Mwanamwema!. Unafahamu vizuri Shein alivyoshinda urais Zanzibar, rafiki zako walikuchezea akili wakikuambia kuwa wamemleta Shein ili kupunguza kura za Bilal na ulipomkubali Shein wao wakaenda kumpigia Bilal kampeni wakijua kazi ya kumweka Shein imekamilika. Baada ya hapo uliendelea kumng'ang'ania Zakhia kuwa makamu. Mkapa akishirikiana na Rostam (ambaye alikuwa akim-install Bilal kuwa makamu huku yeye akiwa South Africa kuangalia World Cup) walimweka Bilal hapo alipo.
Kumbe JK alimtaka Mama Mkwe Zakia?. Kumbe Shein aliibukia Zanzibar kummaliza Nahodha?, kumbe king maker anaweza kufanya kazi kwa remote?, kumbe JK alimng'ang'ania Zakia akashindwa na wenye nguvu zaidi yake?. Kumbe hao rafiki zake, walimchezea akili? hapa wajameni hata mimi niko gizani!.
Shein hakushinda uchaguzi Zanzibar. Kilichofanyika ni Mkapa, Rostam, Karume kumhonga pesa za kutosha sana Maalim kupitia kwa kijana wao hatari sana Jussa (kumbuka huyu aliletwa na Rosatm ili umteue awe mbunge). Today, umeshindwa kumweka mtu wako Zanzibar na makamu wa rais Muungano. Walichoweza kufanikisha ni kuiteka Zanzibar yote (Bilal na Shein). Nakukumbusha ya kwamba, ili uwe mgombea kupitia CCM, unahitaji Zanzibar na 'Lake Zone'. Kule 'Lake Zone' wamekushinda. Hilo unalifahamu vizuri. Hii ndiyo maana Wanzanzibar wamekutesa sana ndani ya CC iliyopita. Ili kukuonyesha kwamba hufai, Shein kampa udaktari wa heshima ''Baba yake'' mdogo Karume. Ninafahamu jinsi unavyojikosha kwa Anne kwa kumpa nishani ili kusiwe na vote of no confidence mwakani hasa kwa sakata la Richmond na Twiga. Napenda kumhakikishia Anne ya kwamba that's a strategy anayoitumia Mugabe ya kuwamaliza watu. JK ameiiga huko. Naomba Anne uwe makini sana. Waweza kufa kwa ''presha'' usipoangalia.
Kumbe CCM haikushinda Zanzibar?!. Kumbe Maalim Seif kahongwa kukubali matokeo?!. Kumbe ule ubunge wa Jussa kipindi cha lala salama ndiko ulikotokea?!,Kumbe ile nishani ya Anne ni kuzuia impeachment ?!- Hapa kuna kama vijiukweli ndani yake!
Huyu alipigiwa kampeni kubwa sana na Edward na Rostam mwaka 2000 licha ya CCM Zanzibar kumkata jina lake. Kwa hili Karume hawezi kuwasahau hawa jamaa mpaka anakufa. Karume alikupinga Butiama. Yeye, Edward na Rostam wakaenda ku-design ''mwafaka'' wao wanaoujua ambao leo hii unafanya kazi Zanzibar. Nataka nikukumbushe mara ya pili kuwa Jussa aliletwa kwako na Rostam ili umpe ubunge. Think twice! Karume ndiye rais aliyeleta maendeleo makubwa Zanzibar. Shein will do more than what Karume did. Usishangae ukisikia Karume kuwa makamu wa Lowassa 2015!. Karume ana msimamo. Hayumbi na bahati mbaya sana hakuogopi.
NITAENDELA SIKU NYINGINE WAPENDWA WANA JF
Kumbe hata muafaka ulidesginiwa na RA na EL?!, then kama ni kweli, ni RA na El ndio waliomuweka JK madarakani, na wao ndio wakamleta Bilal, ninauhakika wa asilimia 100% chini ya 100% ndio waliomuweka Anne Makinda pale alipo!, na usikute ni wao waliomuweke Othman Chande pale alipo!, then wao ndio the most powerful persons in Tanzania!, usikute hata ni hao hao ndio waliyemuweka Rashid Othman pale alipo!, usikute ndie waliyemuweka Said Mwema pake alipo!, usikute ndio waliyemuweka Davis Mwamunyange pale alipo!, usikute ndo waliomuweka Hosea pale alipo!, and the list goes on...then if that is true, hii inamaanisha 100% sure 2015 ni Lowassa!. Hii inamaanisha JK na serikali yake yote si chochote, si lolote kwa watu hawa!
This is not a joke!.