Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Watanzania,

Hivi kweli mnapenda story za udaku namna hii?.

Kila siku huwa nasema na kusisitiza anzeni kufikiri kwa kutumia ubongo wenu acheni magazeti na mitandao kuwafikiria.

Ndio maana mnalialia kila kukicha maisha magumu, hayawezi kuwa raisi kama mnaamini story ya kutunga kama hiyo hapo juu.
We kweli...udaku uko wapi???
Km udaku mbona unakuuma?? We vp.....
 
Asante sana Pasco,
Hata mimi binafsi nimemuona katika hali hiyo hiyo, lakini nasikia kuna dawa anaitumia nadhani ameletewa kutoka Malaysia, ambayo anaipaka kumsaidia kupunguza mikono kucheza cheza baada ya ile mild stroke aliyoipata miezi kadhaa iliyopita. Tatizo jingine na ENL ni kilevi - anakunywa sana Remmy Martin kavu, na ni kawaida kumaliza chupa moja kwa siku; vinginevyo ana umri mzuri tu kwa ndoto za mwaka 2015, kwani by that time atakuwa na miaka kama 61 au 62. Familia yake ingemshauri apunguze kilevi, na aendelee na mazoezi (kwani kwa kawaida anafanya sana mazoezi). Pia ni muhimu ajiangalie sana na wapambe wake maana hawa ndio wanaomletea matatizo ya kiharusi, presha etc. Wao wanamwita ENL The God Father, and in the process wanamtwisha mzigo mkubwa sana kimawazo kutokana na taarifa zao kwake kila siku za majungu n.k, kwani wao wanajipangia tayari vyeo, tender, ujaji, n.k. Vinginevyo JK sio hofu kwa ENL hata kidogo, huyo alishamkabili tangia mwaka 1995.

Pasco,
Yaelekea umehamasika sana kuwa unapata za Jikoni , lakini yaelekea si hivyo.Mtoa habari anakubali kumuona EL katika hali Dhaifu tena anongezea EL anakata Remmy Martin angalau moja kwa siku. Kisha "ANASIKIA" kuwa anatumia dawa toka Malaysia. Sasa hiki ni nini si UVUMI tu (Speculation).
Ili kujua Mtu anatumia Ulevi kiasi gani kwa siku ni lazima uwe nae karibu, pengine mnashea vikao vya ulevi na urafiki, na sioni kama Mtoa habari anasema hivyo. kwahiyo huo nao ni Uvumi si Uzushi la ni Uvumi!
Ningependekeza tuwe wachambuzi wa habari zinazomwagwa hapa Jamvini.
Mkumbuke tunasubiri sehemu ya pili...................ya Mada hii.
 
Watanzania,

Hivi kweli mnapenda story za udaku namna hii?.

Kila siku huwa nasema na kusisitiza anzeni kufikiri kwa kutumia ubongo wenu acheni magazeti na mitandao kuwafikiria.

Ndio maana mnalialia kila kukicha maisha magumu, hayawezi kuwa raisi kama mnaamini story ya kutunga kama hiyo hapo juu.

FP,
Mpaka pale Hutaki Unaacha atakapokuja na nyongeza ya Upupu na kujibu hoja zitokanazo na Mada yake, huu utaendelea kuwa UDAKU.
 
We mjinga kweli...udaku uko wapi???
Km udaku mbona unakuuma?? We vp.....

Erickb,
Hakuna haja ya Jazba hapa. Huu ni ukumbi wa Mjadala na ili uyamudu Majadiliano ni lazima uweze kukontrol Hisia zako. (Keep your cool) na kama hilo huliwezi, hapa hapakufai. (samahani huu ni ushauri usiotaka malipo).
 
Pasco,

Mtandao wa ENL, RO, una nguvu kubwa sana, kifedha na kimkakati, ndani na nje ya nchi, kwani hata mwaka 1995, Kikwete alimshinda Mkapa Chimwaga chini ya mwenyekiti wa mikakati, ENL, licha ya ENL kuchafuliwa jina na Nyerere kama fisadi.
Je, Nyerere alimuonea ENL? Ni wazi kwamba ENL alikuwa na utajiri mkubwa sana na wa ghafla, na Nyerere angefanya yaleyale kwa mwana CCM yeyote ambae angekuwa na hali hiyo ya kifedha, kitu ambacho Nyerere aliona hakiendani na maadili ya uongozi. ENL alikuwa na utajiri mkubwa katika kipindi kifupi – 1989 – 1995. Ni mwaka 1989 ambao ENL aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa AICC Arusha. Kabla ya hapo, alikuwa na maisha ya hali ya chini sana akitokea Chuo Kikuu miaka ya mwisho ya 70, ambapo baada ya kipindi kifupi jeshini, aliamua kuingia kwenye siasa na kuwa Mbunge wa Taifa kupitia viti vya UVCCM mwaka 1985, na mjumbe wa NEC UVCCM (1987). Huko ndiko alipokutana na Kikwete, nae akiwa mbunge wa taifa (uvccm) na Mjumbe wa NEC UVCCM. Tofauti na sasa, miaka ya nyuma, hata wanaume walikuwa wakigombea nafasi hizi. Lakini nafasi hizi hazikuwa na maslahi yoyote kifedha zaidi ya kujijenga kisiasa.

Tangia amalize Elimu yake Chuo Kikuu DSM miaka ya katikati ya 70, ambako pia ndiko alipokutana na Mkewe Regina, na baadae kwenda Nottingham, Uingereza kwa elimu ya juu zaidi mwishoni mwa miaka ya 70, ENL hakuwahi kushika wadhifa wowote mkubwa au kiutendaji ndani ya serikali. Kabla ya mwaka 1985, ENL aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa CCM mikoa ya Shinyanga (ambako mtoto wake Fred ndiko alipozaliwa) na pia kushikilia nafasi hiyo hiyo Arusha miaka ya mwanzo ya 80.
Katika kipindi cha 1980 hadi mwaka 1988, ENL hakuwa anamiliki nyumba ya aina yoyote, na alikuwa na gari moja tu aina ya Volkswagen namba TAP 180, kwa miaka mingi sana. Nyumba ya kwanza ya ENL, mbali na ya kwa wazazi vijijini ilikuwa ni flat ya Msajili wa Majumba pale Sanawari Arusha kama mpangaji, akiwa CCM Arusha. Miaka michache baadae, alibahatika kupata nyumba nyingine ya msajili kama mpangaji, mtaa wa mahando, Masaki Dar-es-salaam. Mambo yakaanza kubadilika kuanzia Mwaka 1989 baada ya Mzee Mwinyi kumteua kuwa Mkurugenzi wa Kitu cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC). Nafasi hii aliitafuta mwenyewe. Mwaka 1990, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya Waziri Mkuu mteule (1990), John Malecela, kumuomba Mzee Mwinyi. Mawaziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mara nyingi wanapatikana baada ya Rais kushauriana na waziri mkuu.

Mwaka 1991, Mwinyi akamhamishia ENL Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, na hapo ndipo alipokutana na Haruna Masebu kama Mkurugenzi Mkuu wa NHC, na kuanza urafiki mkubwa sana wa kikazi na kimaslahi. Mwaka muhimu kukumbuka ni ule wa 1992 ulioruhusu viongozi wa CCM na Serikali kumiliki mali. Kufikia mwaka 1994, ENL akawa mmoja wa viongozi wa kizazi kipya kuwa na nyumba za kupanga, moja wapo ikiwa makazi ya Balozi wa Afrika Kusini Tanzania, kule masaki ambapo alikuwa analipwa $5,000 kama kodi ya mwezi kuanzia mwaka 1994. Mandela alipokuja Tanzania, alitembelewa na Nyerere pale kwa Balozi, na kufanya Press Conference pale pale. Ni katika hafla ile ndio Nyerere akaambiwa ile ni nyumba ya ENL, kitu kilichomsononesha sana. Ndipo Nyerere akatumia nafasi ile kufanya uchunguzi zaidi na kubaini mengi. TISS walimtengenezea Mwalumu Faili maalum juu ya hilo. Mwaka 1995, Mwalimu alikuwa anatembea katika vikao vyote vya maamuzi alipokuwa anaalikwa kutoa msimamo wake juu ya wagombea. Alipomfuta ENL, mtandao wote ulifyata, na aliebakia kumtetea ENL alikuwa ni Sitta ambae alimweleza Mwalimu waziwazi kwenye vikao kwamba sasa ni zamu ya vijana, na wamechoka kuendelea kuchaguliwa na wazee. Mwalimu alibishana sana na Sitta, na baadae Mwalimu akamwambia "Wewe ni waziri wa sheria na katiba, sasa kwa nafasi yako, nimepewa faili juu ya mtu huyu, naomba uchukue faili hili la ENL, na kwa nafasi yako kama waziri wa sheria, utusaidie kufafanua yaliyomo humo ili tubaini kama ENL anaonewa." Sitta akakaa chini na hakusimama na wala kuzungumza tena.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, ENL alitupwa nje ya baraza la mawaziri kutokana na shinikizo la Nyerere. Kikwete ilikuwa ngumu kumuacha kwenye baraza kwani alikuwa namba mbili kule chimwaga (akiwa namba moja katika matokeo ya awali). Njia pekee ya kuumaliza Kikwete ikawa ni kumpa uwaziri wa mambo ya nje ili asiwe na wizara yenye mashiko na wapiga kura (mfani kilimo n.k), lakini pia kumtoa katika mizunguko/ziara ndani ya nchi, hivyo kupunguza nguvu yake katika grassroots level. Walichokosea kina Mkapa ni kwamba kwa ENL kuwa nje ya baraza, ilimpa muda mwingi sana kuendelea na mikakati ya 2005. Lakini ENL pia aliumia sana, na aliyemrudisha kwenye Cabinet ni Abson, baada ya kumuombea sana msamaha kwa Mkapa.

ENL hakuacha kuendelea kujijengea mtandao kwa ajili ya mwaka 2005 na baadae. ENL hajijengei mtandao kwenye siasa tu bali kwenye vyombo vya usalama, taasisi za Umma, Binafsi n.k. Ana mtandao mkubwa sana kwenye sekta za Umma kama Ewura ambako alimweka ndugu yake Haruna Masebu ambae alikuwa NHC, ENL alipokuwa waziri wa ardhi. ENL pia ana mtandao mkubwa sana TRA, Tanesco, kampuni za mawakili, wamiliki wa ma-baa, taasisi mbalimbali za kidini (dini zote), polisi, TISS, taasisi za kimataifa zenye wawakilishi wake Tanzania, n.k.

Mkapa hakuwa mtu wa JK tokea mwanzo. Lakini pia Mkapa hakuwa na chaguo lolote la wazi. Je ni Kwanini? Ni kwasababu, Nyerere miaka yote amekuwa anamtaka Salim kuwa Rais. Nyerere aliposhindwa kuamsha tena jina hilo chini kwa chini mwaka 1995, Mkapa ndiye akawa "his fallback position" (yani kwa Nyerere). Kwahiyo Mkapa kumbeba mtu mwingine nje ya yule ambae Nyerere alimpenda, ingekuwa kama usaliti kwa mtandao wa Nyerere. Lakini chini kwa chini, Mkapa alimtaka Hassy Kitine kumpokea mwaka 2005. Alianza kwa kuunda nafasi mpya kabisa tangia uhuru ya Uwaziri wa nchi utawala bora (Usalaam wa taifa), na kumfanya kitine kuwa waziri wa kwanza, ili ajijengee mazingira ya 2005. Lakini kina ENL, RO, waliligundua hili mapema sana na hivyo kummaliza Kitine bungeni kwa kashfa ya kutumia dola elf 60 kwa ajili ya matibabu ya mkewe Canada. Baada ya hayo, Mkapa alibakia anaelea, asijue la kufanya. Isitoshe, hata mabalozi wa Marekani, Uingereza, na nchi nyingine kubwa walikuwa wanamuonya sana Mkapa kwamba Kikwete hafai, ataingiza nchi katika matatizo. Pia walikuwa wanalalamika sana kwamba hawapati kabisa muda na Waziri wa Mambo ya Nje, na hivyo katika kipindi cha miaka kumi (1995 – 2005), kuishia kuwa na ukaribu zaidi na manaibu mawaziri wan je, katika nyakati tofauti, Balozi Shariff na Mwambulukutu.

Mwaka 2005, mkakati wa mkapa inasemekana ulikuwa ni kuwatosa wagombea wote ambao walikuwa na nguvu kubwa kwenye jamii, ili kuepuka mfarakano iwapo kundi moja litaonekana limeonewa. Kwa mfano, Sumaye alikuwa na kundi kubwa la wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na viongozi wengi wa halmashauri za wilaya. Malecela alikuwa na kundi kubwa sana viongozi wa CCM kitaifa, lakini pia wenyeviti na makatibu wa CCM mikoa na wilaya. Kikwete alikuwa na kundi kubwa sana la viongozi wa kitaifa wa UVCCM, UWT kutokea mwaka 1995 hadi 2005, huku akidokoa dokoa wengine wengi kutoka katika makundi hayo hapo juu. Mikakati ya Mkapa ikaingia dosari pale ENL, JK, RA, walipotoa msimamo kwamba iwapo Kikwete atatoswa, watahamia Chadema. Ndipo Mkapa akaunda timu ya kutembea nchi nzima kutafiti hilo, chini ya Absom, ambae whether ni kutonana na utafiti wa kweli au uliokwisha andaliwa mapema na kina EL, RA, akamletea taarifa Mkapa kwamba Kikwete akiachwa, CCM itapasuka, na nchi itaingia katika machafuko. Huu ndio ukawa mwanzo wa Mkapa kulibeba jina la Kikwete kwa mtindo wa kura moja badala ya tatu Dodoma.

Kuhusu Kikwete kujiunga na kina Lowassa, swali la kujiuliza ni je, kama Nyerere alishindwa kuwazuia mwaka 1995, na baadae Nyerere kufanikiwa kwa mbinu za kiintelejensia, Mkapa atawezaje kuwa kambi tofauti na ENL katika mazingira ya sasa?
Suala lingine la kujiuliza hapa - nini kilibadili msimamo wa Sitta (mwaka 2007) juu ya ENL - ikifananishwa na misimamo yake huko nyuma juu ya ENL - mwaka 1995 na mwaka 2005? Msimamo wake (Sitta) Sitta ulimgharibu sana kisiasa kwani alitoweka kabisa katika nafasi ya uwaziri kwa kipindi chote cha Mkapa 1995 – 2005, huku ENL na Kikwete wakiendelea kupeta.
 
Mtoahabari, asante sana kwa taarifa hizi, natumaini ujumbe huu mzito, umeshamfikia EL, au wapambe wake waliota alaki humu jf watampelekea na kuvuta kama kweli anakata!.

Kusema ukweli, mimi binafsi ni miongoni mwa watu waliofarijika sana na ujio wako humu mtandaoni, speculations zimekuwa nyingi kuliko uhalisia hivyo uweko wako ni checks and balance muhimu sana.

Tukiachana na EL, jee huku kuugua kwa Prof.M na Dr.HM jee kuna kwa ukweli ni vijana wa kazi, au mnasingiziwa?.
wadhungu wanasema - Read between the lines..Sasa naona Ukumbi umenoga - maana sisi waswahili husema Hadithi ni documentary in process..
 
mtoa habari naomba ueleze ya Kikwete kuhamia CHADEMA na maandalizi gani waliyafanya huko
CHADEMA MWAKA 2005...hii ni muhimu
wengi hawajui hii
 
Pasco,

Mtandao wa ENL, RO, una nguvu kubwa sana, kifedha na kimkakati, ndani na nje ya nchi, kwani hata mwaka 1995, Kikwete alimshinda Mkapa Chimwaga chini ya mwenyekiti wa mikakati, ENL, licha ya ENL kuchafuliwa jina na Nyerere kama fisadi.
Je, Nyerere alimuonea ENL? Ni wazi kwamba ENL alikuwa na utajiri mkubwa sana na wa ghafla, na Nyerere angefanya yaleyale kwa mwana CCM yeyote ambae angekuwa na hali hiyo ya kifedha, kitu ambacho Nyerere aliona hakiendani na maadili ya uongozi. ENL alikuwa na utajiri mkubwa katika kipindi kifupi – 1989 – 1995. Ni mwaka 1989 ambao ENL aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa AICC Arusha. Kabla ya hapo, alikuwa na maisha ya hali ya chini sana akitokea Chuo Kikuu miaka ya mwisho ya 70, ambapo baada ya kipindi kifupi jeshini, aliamua kuingia kwenye siasa na kuwa Mbunge wa Taifa kupitia viti vya UVCCM mwaka 1985, na mjumbe wa NEC UVCCM (1987). Huko ndiko alipokutana na Kikwete, nae akiwa mbunge wa taifa (uvccm) na Mjumbe wa NEC UVCCM. Tofauti na sasa, miaka ya nyuma, hata wanaume walikuwa wakigombea nafasi hizi. Lakini nafasi hizi hazikuwa na maslahi yoyote kifedha zaidi ya kujijenga kisiasa.

Tangia amalize Elimu yake Chuo Kikuu DSM miaka ya katikati ya 70, ambako pia ndiko alipokutana na Mkewe Regina, na baadae kwenda Nottingham, Uingereza kwa elimu ya juu zaidi mwishoni mwa miaka ya 70, ENL hakuwahi kushika wadhifa wowote mkubwa au kiutendaji ndani ya serikali. Kabla ya mwaka 1985, ENL aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa CCM mikoa ya Shinyanga (ambako mtoto wake Fred ndiko alipozaliwa) na pia kushikilia nafasi hiyo hiyo Arusha miaka ya mwanzo ya 80.
Katika kipindi cha 1980 hadi mwaka 1988, ENL hakuwa anamiliki nyumba ya aina yoyote, na alikuwa na gari moja tu aina ya Volkswagen namba TAP 180, kwa miaka mingi sana. Nyumba ya kwanza ya ENL, mbali na ya kwa wazazi vijijini ilikuwa ni flat ya Msajili wa Majumba pale Sanawari Arusha kama mpangaji, akiwa CCM Arusha. Miaka michache baadae, alibahatika kupata nyumba nyingine ya msajili kama mpangaji, mtaa wa mahando, Masaki Dar-es-salaam. Mambo yakaanza kubadilika kuanzia Mwaka 1989 baada ya Mzee Mwinyi kumteua kuwa Mkurugenzi wa Kitu cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC). Nafasi hii aliitafuta mwenyewe. Mwaka 1990, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya Waziri Mkuu mteule (1990), John Malecela, kumuomba Mzee Mwinyi. Mawaziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mara nyingi wanapatikana baada ya Rais kushauriana na waziri mkuu.

Mwaka 1991, Mwinyi akamhamishia ENL Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, na hapo ndipo alipokutana na Haruna Masebu kama Mkurugenzi Mkuu wa NHC, na kuanza urafiki mkubwa sana wa kikazi na kimaslahi. Mwaka muhimu kukumbuka ni ule wa 1992 ulioruhusu viongozi wa CCM na Serikali kumiliki mali. Kufikia mwaka 1994, ENL akawa mmoja wa viongozi wa kizazi kipya kuwa na nyumba za kupanga, moja wapo ikiwa makazi ya Balozi wa Afrika Kusini Tanzania, kule masaki ambapo alikuwa analipwa $5,000 kama kodi ya mwezi kuanzia mwaka 1994. Mandela alipokuja Tanzania, alitembelewa na Nyerere pale kwa Balozi, na kufanya Press Conference pale pale. Ni katika hafla ile ndio Nyerere akaambiwa ile ni nyumba ya ENL, kitu kilichomsononesha sana. Ndipo Nyerere akatumia nafasi ile kufanya uchunguzi zaidi na kubaini mengi. TISS walimtengenezea Mwalumu Faili maalum juu ya hilo. Mwaka 1995, Mwalimu alikuwa anatembea katika vikao vyote vya maamuzi alipokuwa anaalikwa kutoa msimamo wake juu ya wagombea. Alipomfuta ENL, mtandao wote ulifyata, na aliebakia kumtetea ENL alikuwa ni Sitta ambae alimweleza Mwalimu waziwazi kwenye vikao kwamba sasa ni zamu ya vijana, na wamechoka kuendelea kuchaguliwa na wazee. Mwalimu alibishana sana na Sitta, na baadae Mwalimu akamwambia “Wewe ni waziri wa sheria na katiba, sasa kwa nafasi yako, nimepewa faili juu ya mtu huyu, naomba uchukue faili hili la ENL, na kwa nafasi yako kama waziri wa sheria, utusaidie kufafanua yaliyomo humo ili tubaini kama ENL anaonewa.” Sitta akakaa chini na hakusimama na wala kuzungumza tena.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, ENL alitupwa nje ya baraza la mawaziri kutokana na shinikizo la Nyerere. Kikwete ilikuwa ngumu kumuacha kwenye baraza kwani alikuwa namba mbili kule chimwaga (akiwa namba moja katika matokeo ya awali). Njia pekee ya kuumaliza Kikwete ikawa ni kumpa uwaziri wa mambo ya nje ili asiwe na wizara yenye mashiko na wapiga kura (mfani kilimo n.k), lakini pia kumtoa katika mizunguko/ziara ndani ya nchi, hivyo kupunguza nguvu yake katika grassroots level. Walichokosea kina Mkapa ni kwamba kwa ENL kuwa nje ya baraza, ilimpa muda mwingi sana kuendelea na mikakati ya 2005. Lakini ENL pia aliumia sana, na aliyemrudisha kwenye Cabinet ni Abson, baada ya kumuombea sana msamaha kwa Mkapa.

ENL hakuacha kuendelea kujijengea mtandao kwa ajili ya mwaka 2005 na baadae. ENL hajijengei mtandao kwenye siasa tu bali kwenye vyombo vya usalama, taasisi za Umma, Binafsi n.k. Ana mtandao mkubwa sana kwenye sekta za Umma kama Ewura ambako alimweka ndugu yake Haruna Masebu ambae alikuwa NHC, ENL alipokuwa waziri wa ardhi. ENL pia ana mtandao mkubwa sana TRA, Tanesco, kampuni za mawakili, wamiliki wa ma-baa, taasisi mbalimbali za kidini (dini zote), polisi, TISS, taasisi za kimataifa zenye wawakilishi wake Tanzania, n.k.

Mkapa hakuwa mtu wa JK tokea mwanzo. Lakini pia Mkapa hakuwa na chaguo lolote la wazi. Je ni Kwanini? Ni kwasababu, Nyerere miaka yote amekuwa anamtaka Salim kuwa Rais. Nyerere aliposhindwa kuamsha tena jina hilo chini kwa chini mwaka 1995, Mkapa ndiye akawa “his fallback position” (yani kwa Nyerere). Kwahiyo Mkapa kumbeba mtu mwingine nje ya yule ambae Nyerere alimpenda, ingekuwa kama usaliti kwa mtandao wa Nyerere. Lakini chini kwa chini, Mkapa alimtaka Hassy Kitine kumpokea mwaka 2005. Alianza kwa kuunda nafasi mpya kabisa tangia uhuru ya Uwaziri wa nchi utawala bora (Usalaam wa taifa), na kumfanya kitine kuwa waziri wa kwanza, ili ajijengee mazingira ya 2005. Lakini kina ENL, RO, waliligundua hili mapema sana na hivyo kummaliza Kitine bungeni kwa kashfa ya kutumia dola elf 60 kwa ajili ya matibabu ya mkewe Canada. Baada ya hayo, Mkapa alibakia anaelea, asijue la kufanya. Isitoshe, hata mabalozi wa Marekani, Uingereza, na nchi nyingine kubwa walikuwa wanamuonya sana Mkapa kwamba Kikwete hafai, ataingiza nchi katika matatizo. Pia walikuwa wanalalamika sana kwamba hawapati kabisa muda na Waziri wa Mambo ya Nje, na hivyo katika kipindi cha miaka kumi (1995 – 2005), kuishia kuwa na ukaribu zaidi na manaibu mawaziri wan je, katika nyakati tofauti, Balozi Shariff na Mwambulukutu.

Mwaka 2005, mkakati wa mkapa inasemekana ulikuwa ni kuwatosa wagombea wote ambao walikuwa na nguvu kubwa kwenye jamii, ili kuepuka mfarakano iwapo kundi moja litaonekana limeonewa. Kwa mfano, Sumaye alikuwa na kundi kubwa la wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na viongozi wengi wa halmashauri za wilaya. Malecela alikuwa na kundi kubwa sana viongozi wa CCM kitaifa, lakini pia wenyeviti na makatibu wa CCM mikoa na wilaya. Kikwete alikuwa na kundi kubwa sana la viongozi wa kitaifa wa UVCCM, UWT kutokea mwaka 1995 hadi 2005, huku akidokoa dokoa wengine wengi kutoka katika makundi hayo hapo juu. Mikakati ya Mkapa ikaingia dosari pale ENL, JK, RA, walipotoa msimamo kwamba iwapo Kikwete atatoswa, watahamia Chadema. Ndipo Mkapa akaunda timu ya kutembea nchi nzima kutafiti hilo, chini ya Absom, ambae whether ni kutonana na utafiti wa kweli au uliokwisha andaliwa mapema na kina EL, RA, akamletea taarifa Mkapa kwamba Kikwete akiachwa, CCM itapasuka, na nchi itaingia katika machafuko. Huu ndio ukawa mwanzo wa Mkapa kulibeba jina la Kikwete kwa mtindo wa kura moja badala ya tatu Dodoma.

Kuhusu Kikwete kujiunga na kina Lowassa, swali la kujiuliza ni je, kama Nyerere alishindwa kuwazuia mwaka 1995, na baadae Nyerere kufanikiwa kwa mbinu za kiintelejensia, Mkapa atawezaje kuwa kambi tofauti na ENL katika mazingira ya sasa?
Suala lingine la kujiuliza hapa - nini kilibadili msimamo wa Sitta (mwaka 2007) juu ya ENL - ikifananishwa na misimamo yake huko nyuma juu ya ENL - mwaka 1995 na mwaka 2005? Msimamo wake (Sitta) Sitta ulimgharibu sana kisiasa kwani alitoweka kabisa katika nafasi ya uwaziri kwa kipindi chote cha Mkapa 1995 – 2005, huku ENL na Kikwete wakiendelea kupeta.
Asante Mtoa habari, kweli wewe ni mtoa habari za ukweli toka jikoni!.

Hilo jina la Ex Chief ni Abson au Apson?.
 
halafu Mtoahabari jibu basi maswali tunakuuliza
so far nimekuuliza mara mbili hujanijibu
 
Kweli mtoa habari yaonesha unafaili la cv ya mmasai, sasa kwanini umeasi UWT? kwani kile kiapo umetengua.....!
 
halafu Mtoahabari jibu basi maswali tunakuuliza
so far nimekuuliza mara mbili hujanijibu

Sina taarifa za kina juu ya hilo mbali ya kuwa na taarifa kwamba Mbowe na kina ENL, RA, wana ukaribu sana, na miaka ya nyuma walikuwa wanakunywa bia pamoja. Vilevile ENL, RA, wamefanikiwa kumteka Zitto. Homa kubwa waliyonayo ni kwa watu kama Lissu. Hata Mkuu wa nchi aliwahi sikika akitamka wakati wa kampeni za Urais mwaka jana kwamba ni mara mia kuwa na Slaa Ikulu kuliko kuwa na Lissu bungeni. Natumaini nimekuwa angalau maoni yangu kwa wewe kuyatafakari.
 
Acha hizo kaka ,just wait the guy iz real so b cool and wait 4 another topic
 
mtoa habari naomba ueleze ya Kikwete kuhamia CHADEMA na maandalizi gani waliyafanya huko
CHADEMA MWAKA 2005...hii ni muhimu
wengi hawajui hii

Kumbe chadema ni kimbilio la wengi humo ccm? sasa mbona jk juzi kule nec dodoma kahamaki kusikia vijana wake
watahamia chadema? ...alianza yeye kutishia...wanafwata nyayo...!
 
Sina taarifa za kina juu ya hilo mbali ya kuwa na taarifa kwamba Mbowe na kina ENL, RA, wana ukaribu sana, na miaka ya nyuma walikuwa wanakunywa bia pamoja. Vilevile ENL, RA, wamefanikiwa kumteka Zitto. Homa kubwa waliyonayo ni kwa watu kama Lissu. Hata Mkuu wa nchi aliwahi sikika akitamka wakati wa kampeni za Urais mwaka jana kwamba ni mara mia kuwa na Slaa Ikulu kuliko kuwa na Lissu bungeni. Natumaini nimekuwa angalau maoni yangu kwa wewe kuyatafakari.

habari za mbowe kupewa bilioni tatu za maandalizi hukupata?
mwaka 2005????
 
Sie wa kambi ya Lowassa tunapiga mluzi taratiibu.

Lowassa hoyeeee

Bob Mkandara umeanza kutuelewa mie na Pasco sasa??
 
Back
Top Bottom