Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

ni kweli katiba mpya ndo tiba, ila sidhani km hii ya sasa inakubali nchi itawaliwe na mafisadi, ama sidhani km katiba ya sasa haina miiko ya uongozi na hivyo EL kukosa sifa, tatizo ni nani anailinda katiba,

Katiba yetu ya sasa imetoa SIFA chache na rahisi sana za mgombea. Baadhi ni hizi:
-Uteuliwe na CHAMA
-Uwe na umri wa miaka 40 au zaidi ( Wakati Mwalimu alishika uongozi wa nchi kabla ya umri huo!)
-Uwe na akili timamu( hili nalo huwa hatuthibitishiwi na yeyote!)
-Elimu ya kawaida tu!
-etc., etc,
 
Utatoka mapovu bure. HuKo kwa Jesus pia tumeshaenda, tume pewa a go ahead pia. Labda uende kwenye mashetani huKo hatujaenda, kwakua tunaamini nguvu ni moja tu ni Mungu.

Lowassa chaguo la Mungu!

[h=2]God[/h]   [god]
noun1.the one Supreme Being, the creator(King Maker) and ruler of theuniverse(?Danganyika).


 
Mkuu Mtoahabari, hapo kwenye red umenikumbusha kitu fulani. kuna siku nilikuwa pale Rose Garden na nikamuona L.Masha akiwa na
vijana kama sita hivi wakipata lunch karibu sana na sehemu ambayo na mimi nilikaa kupata lunch yangu....kusema kweli kwa mbali
nilimsikia Lau Masha akimuongelea EL kwa wale vijana aliokuwa amekaanao pale,yaani ilikuwa kama kuna maagizo fulani anawapatia
kuhusiana na EL....yaani walitumia karibu nusu saa hivi kumuongelea EL,lakini Lau Masha alikuwa anaongea kwa sauti ya chini sana kwa hiyo sikuambulia kitu chochote pale zaidi ya jina la EL. Je huyu Masha nae yuko kwenye kundi la EL au yuko against EL?

Lau Masha ni mtu wa ENL mpaka kaburini.
 
Mtoahabari,

Nimekuelewa vizuri hapo unaposema wewe ni mtoa taarifa tu. Kwani taarifa si lazima iwe sahihi ama la. Ni mpaka hapo hapo itakapotokea ndio itakuwa sahihi. Kama nilivyosema huko nyuma ni jukumu letu wana JF kufanya our own independent assessment ili kabla ya kufikia kwenye final solution. "mtaohabari" katimiza wajibu wake kwa sisi watanzania tuliosoma. Nasi basi tutumie akili zetu (za kuzaliwa + darasani/vyuoni) tufikie mwisho. Na ndio hapo kila mmoja wetu ajitokeze kuplay his/her part.
Ushauri mzuri wa wahenga wetu naona upo valid kabisa katika hili "ILI KUMUUA NYOKA LAZIMA UENDE KICHWANI". Hivi sasa namkumbuka sana marehemu E. MZENA, yule kamanda alikuwa jasiri na hana uoga, kama angalikuwapo huyu EL angeshakuwa history na wafuasi wake waliobakia inakuwa rahisi kuwadhibiti. Unfortunately, operations specialists waliopo chini ya RO ni gutless and cowards! Mmebakia ma-Analyst mnaona upuuzi wote unaoendelea bila kujua la kufanya. Kuna kitu wenzetu wanaita true sons of the country they are sucrificed for the benefits of the future generations. Sijui sie kitu kama tunacho mtaohabari?

TISS haina nguvu zaidi ya umma, hakuna kilichokuwa na nguvu zaidi ya UMMA katika taifa lolote lile. Abdulla Al Senussi alikuwa Chief of Intelligence wa Ghadafi, yu wapi leo?
 
@ Mtoa Habari!

Inatisha na kukatisha tamaa. Ila pia nilikuuliza kuhusu kifo cha prof. Mwaikusa na tetesi za yeye kudaiwa kukutana na Daudi Balali (sijui ni kwa bahati mbaya au kwa kupanga) huku USA.

Je kuna ukweli wowote na nani walihusika, an ina uhusiano wowte ule na haya mambo ya kuelekea 2015?

Kuhusu Profesa ni tetesi kwamba alikutana na Marehemu aliyehai kwenye shopping Mall katika nchi moja, alipoenda kwenye semina, na haikuwa Marekani. Profesa akapiga simu nyumbani kuelezea tukio hilo, na yakatokea yaliyotokea. Hizi ni tetesi lakini, hazina uthibitisho.
 
loooh! mkuu km hii habari ni ya kweli napata mashaka na DR.Slaa jembe nilililoliamini,
hata hivyo siwezi kukuamini sana, maana km batilda arusha ni mtu wa EL na bado wakahenyeshwa na G.Lema wa CDM wakati huo huo unasema miundo mbinu yote ya CDM kaitengeneza EL, ngoja nifikirishe kichwa changu zaidi kabla yakukubali maneno yako yaote.

Ukumbuke kwamba ENL na Chadema walikuwa hawana tofauti zozote mpaka lilipoibuka suala la Richmond. Pia, Karatu na Monduli ni majimbo yanayopakana kama Segerea na Ilala, na wahusika huko wanaheshimiana vizuri sana. Baada ya yaliyotokea Dodoma na kuvuana nguo kwenye Halmashauri Kuu, msimamo cha Chadema kwa ENL upo vipi? Ni suala la mjadala.
 
Duh! shekhe yahya kafufuka? au mrithi wake anatafuta attention ndio aanze kazi
 
hujajibu swali la magogoko

je huko TISS hakuna true sons of this generation wa kuamua to end all this rubbish??????

Nilishamjibu ila sio moja kwa moja. Narudia tena, TISS haina nguvu zaidi ya UMMA. Chifu wa intelligence wa Ghadafi, Abdulla Al Senussi, yu wapi leo?
 
Nashindwa ku-guess wewe ni nani.Kwa vyovyote vile si kambi ya Kikwete.Most likely wewe ni kambi ya EL,unachofanya ni ku-expose ujinga wa Kikwete.Kwa vile wengi tuko fedup with him, tumefurahi.It's good information.ambayo inanisaidia to more correctly guess on the future,that for example Lowasa will be our next president.Too bad indeed,ingwa it now seems most likely.
Mr President,

Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).

Mtandao

Ninachozungumzia hapa ni kundi kubwa na hatari linaloaminika kuongozwa na Edward, Rostam, Othman, Apson, Karume na Shein na Mkapa. Ninakufahamu vizuri sana na ungekuwa uwezo wako, hawa wote ungeweza kufanya uwezalo ili kumweka madarakani mtu unayemtaka kwa maana ya Asha au Nahodha. Huu ni mtandao unaofanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana. Ukitaka kuamini, jiulize swali la kipuuzi sana kuwa kwanini kila plans unazofanya (zisizo na faida) kwa kundi hili zote zimefail?

1. Shein ni nani?

Nataka nikukumbushe ''issue'' ya Omar Juma. Huyu alikuwa threat kubwa kwa kundi lenu kwa ajili ya 2005. Mtandao wake ukibebwa na Mkapa ulikuwa ni hatari sana. The only way ilikuwa ni ''kumwondoa'' na hilo liliwezekana. Siku nikiwa na muda nitaeleza mchezo wote ulivyofanyika. Wakati jina limeletwa tukiwa hotel moja maarufu hapa Dar, nakumbuka hukuweza kumfahamu Shein wala kulitamka jina lake vizuri. Ulikosea mara tatu kulitamka. Tukacheka wote. Hatimaye Shein akawa makamu wa rais.

Baada ya wenzako kukuweka madarakani (mgombea ndani ya CCM), kosa ambalo Shein hataweza kukusamehe katika maisha yake (Mimi sio Mungu, kwani anaweza kukusamehe vilevile) ni pale ulipo-attempt kumfanya Zakhia kuwa makamu wa rais. Asingekuwa Edward, Rostam, Mkapa na Karume, leo hii Shein angekuwa mwenyekiti wa TPDC au TANAPA!. Kitendo cha Shein kuletwa na kundi hili, kutetewa na kundi hili achilia mbali kushawishiwa na kundi hili agombee urais wa Zanzibar ili kummaliza nguvu Nahodha chaguo lako kinamfanya awe mtiifu kwao kuliko hata kwa Mwanamwema!. Unafahamu vizuri Shein alivyoshinda urais Zanzibar, rafiki zako walikuchezea akili wakikuambia kuwa wamemleta Shein ili kupunguza kura za Bilal na ulipomkubali Shein wao wakaenda kumpigia Bilal kampeni wakijua kazi ya kumweka Shein imekamilika. Baada ya hapo uliendelea kumng'ang'ania Zakhia kuwa makamu. Mkapa akishirikiana na Rostam (ambaye alikuwa akim-install Bilal kuwa makamu huku yeye akiwa South Africa kuangalia World Cup) walimweka Bilal hapo alipo.

Shein hakushinda uchaguzi Zanzibar. Kilichofanyika ni Mkapa, Rostam, Karume kumhonga pesa za kutosha sana Maalim kupitia kwa kijana wao hatari sana Jussa (kumbuka huyu aliletwa na Rosatm ili umteue awe mbunge). Today, umeshindwa kumweka mtu wako Zanzibar na makamu wa rais Muungano. Walichoweza kufanikisha ni kuiteka Zanzibar yote (Bilal na Shein). Nakukumbusha ya kwamba, ili uwe mgombea kupitia CCM, unahitaji Zanzibar na 'Lake Zone'. Kule 'Lake Zone' wamekushinda. Hilo unalifahamu vizuri. Hii ndiyo maana Wanzanzibar wamekutesa sana ndani ya CC iliyopita. Ili kukuonyesha kwamba hufai, Shein kampa udaktari wa heshima ''Baba yake'' mdogo Karume. Ninafahamu jinsi unavyojikosha kwa Anne kwa kumpa nishani ili kusiwe na vote of no confidence mwakani hasa kwa sakata la Richmond na Twiga. Napenda kumhakikishia Anne ya kwamba that's a strategy anayoitumia Mugabe ya kuwamaliza watu. JK ameiiga huko. Naomba Anne uwe makini sana. Waweza kufa kwa ''presha'' usipoangalia.

2. Karume ni nani?

Huyu alipigiwa kampeni kubwa sana na Edward na Rostam mwaka 2000 licha ya CCM Zanzibar kumkata jina lake. Kwa hili Karume hawezi kuwasahau hawa jamaa mpaka anakufa. Karume alikupinga Butiama. Yeye, Edward na Rostam wakaenda ku-design ''mwafaka'' wao wanaoujua ambao leo hii unafanya kazi Zanzibar. Nataka nikukumbushe mara ya pili kuwa Jussa aliletwa kwako na Rostam ili umpe ubunge. Think twice! Karume ndiye rais aliyeleta maendeleo makubwa Zanzibar. Shein will do more than what Karume did. Usishangae ukisikia Karume kuwa makamu wa Lowassa 2015!. Karume ana msimamo. Hayumbi na bahati mbaya sana hakuogopi.


NITAENDELA SIKU NYINGINE WAPENDWA WANA JF
 
Ukumbuke kwamba ENL na Chadema walikuwa hawana tofauti zozote mpaka lilipoibuka suala la Richmond. Pia, Karatu na Monduli ni majimbo yanayopakana kama Segerea na Ilala, na wahusika huko wanaheshimiana vizuri sana. Baada ya yaliyotokea Dodoma na kuvuana nguo kwenye Halmashauri Kuu, msimamo cha Chadema kwa ENL upo vipi? Ni suala la mjadala.
dah! tena la mjadala mzito, na ile kauli ya Dr.Slaa kuwa nusu ya TISS wanaripoti kwake ni kwasababu ya lowasa au?
 
Ukumbuke kwamba ENL na Chadema walikuwa hawana tofauti zozote mpaka lilipoibuka suala la Richmond. Pia, Karatu na Monduli ni majimbo yanayopakana kama Segerea na Ilala, na wahusika huko wanaheshimiana vizuri sana. Baada ya yaliyotokea Dodoma na kuvuana nguo kwenye Halmashauri Kuu, msimamo cha Chadema kwa ENL upo vipi? Ni suala la mjadala.
Ahsante sana mkuu!....na je watu wa TISS wako upande wa chama gani? CDM au CCM? Dr Slaa au EL?
 
Ingawa unaijua kweli SIASA. Tena kwa nguvu ya hoja na msimamo usioyumba hasa juu ya Lowasa!

Sababu mmeshindwa kunishawishi vinginevyo. Mmebakia na kumsakama Lowassa bila kuja na rais mmbadala.
 
Back
Top Bottom