Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

trachomatis, join the team Lowassa awe mgombea wa CCM alete mabadiliko ya kweli, tena nilikuwa sijakuambia, kodi ya VAT ataipunguza mpaka 15% serikali itaendeshwa kwa tozo za madini na gesi asilia, yaani within the first five years, uchumi wetu utapaa kama tiger countries ambazo tulipata nazo uhuru kipindi kimoja, they had nothing and we had everything, now they have everything, we have nothing!.

Tanzania sio masikini kama tunavyoaminishwa ni mis management of our resources!, hebu tembeleeni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi halafu muangalie wazungu wanaojiita wawekezaji, wanakimbilia wapi, au wana ng'ang'ania wapi?!.

Yaani hii nchi, wee acha tuu bora Lowassa aje alete mabadiliko ya kweli!
Umenikumbusha ule msemo wa ndege yetu inapaa wakati akiahidi mvua za sayansi...
 
I am smiling at your posts...@Pasco. Anajua nini chanzo au sababu ya umasikini wetu?
trachomatis, please don't just keep smilling, just do something about it, no matter how little it may seems to be but something is better than nothing!, do something!
 
Afadhali mwizi mchapa kazi, kuliko mwizi ( au hata mwungwana) mvivu!
 
Afadhali mwizi mchapa kazi, kuliko mwizi ( au hata mwungwana) mvivu!
Duh hii kali sijawahi isikia maana jambazi linaloichapa kazi vizuri ya Ujambazi linasifika kuliko lile vivu la kuiba? Lakini kweli nakumbuka Nyau alikuwa akisifika sana TZ...
 
Afadhali mwizi mchapa kazi, kuliko mwizi ( au hata mwungwana) mvivu!

hapo nakubaliana na wewe mkuu

Lowasa ni mchapa kazi,tena hana mda wa kusubiri kukumbushwa,yeye na Magufuri hawa jamaa bwana wanafaa

watu wanamwogopa magufuri kwa kuwa yeye hakwepeshi,hapohapo anakupa kitu,lakini ndio watu wanao faa kuiongoza nchi hii

kwa upande wangu nikiwa hai nitapiga kura kama tu
1 Lowasa akiteuliwa ama
2. Magufuri akiteuliwa

waliobaki ni wale wale tu ilimradi naye aongoze.sitapiga kura
 
The Boss, kuna msemo wa Kiswahili usemao "Usiogope kugombana na nduguyu/rafikiyo katika jambo ambalo mtakuja kupatana!".

Kwa utetezi wangu kwa Lowassa bora tugombane tuu kwa sasa akishateuliwa tutapatana tuu!.

Kwa wale mnaonifahamu na kunikubali kuhusu misimamo yangu katika baadhi ya issues, natoa wito tuungane mikono tumsafishe Lowassa awe mgombea wa CCM, tumeshasema mara mia humu kama dhambi kuu ya Lowassa ni zigo la Richmond, kwenye sakata hilo Lowassa alikubali tuu kulibeba ili CCM iokoke kama Bwana Wetu Yesu Kristo alivyobeba dhambi zetu na kwa kuteswa kwake sisi tumeponywa vivyo hivyo kwa kuteswa kwa Lowassa CCM imeokoka maana laiti mngelimjua mwenye zigo lake halisi!, I can't imagine kama Lowassa angehojiwa na kuusema ukweli ingekuwaje!.

Lowassa ni mtu shupavu na jasiri sana, just imagine mpaka leo bado anaendelea kulibeba hili zigo kwa uvumilivu mkubwa na ustahimilivu wa hali ya juu!. Nani mwingine kwenye CCM angeweza kuvumilia yote hayo bila kumtaja mwenye zigo lake!.

Zawadi pekee anayostahili sasa ni kutunukiwa ugombea kwa tiketi ya CCM tena nawaombeni sana sana sana tuungane katika hili!.


Pasco wa Jf.
Ngamia hana uwezo wa kutua Nundu yake. Nundu yake ni Umbile/Ameumbwa nayo.Akiitua atakufa na hata Akituliwa atakufa. Kwa bahati mbaya Lowassa hana Zigo moja yawezekana yako mazigo kumi na moja. Atayatuaje yote na yote ayatafutie wenyewe?Tabia ni umbile atatuhakikishiaje kuwa ameacha Wiziiiiiiiiiiii??
Nimesema Awali mshaurini alituwe ili tumjue muhusika Tumsakameme. nae lowassa apumue kwa nini ajitoe kibyongo? kwa zigo lisilomuhusu? Hapa utakaempata ni yule aliyeamua akijua alifanyalo, wakuburuza labda uende mitaani huko.


 
Gurti, usichanganye majina Pascal ni member mwingine wa humu humu jf na mimi namfahamu, Pasco wa jf ndio mimi.

Sijasema Mzee Mwanakijiji ame mu endorse Lowassa nimesema Mzee Mwanakijiji ni miongoni mwa wanaotaka mabadiliko ya kweli na ameishaelewa mabadiliko ya kweli yataketwa kupitia kwa Lowassa, mgombea wa CCM ambaye Mzee Mwanakijiji ame mu endorse ni Dr. Shein!. Tumemshauri Dr. Shein hatufai he is too weak kutuletea mabadiliko ya kweli, ametuelewa japo hatuungi mkono lakini ukimya wake ni uthibitisho ameridhia tuendelee kumsafisha Lowassa mpaka atakate!.
Mkuu Pasco, sasa nimeshakuelewa vizuri sana! hata mimi nimeamua kuwa upande wa EL kuelekea 2005....kwani ccm isipomsimamisha huyu mtakatifu hatuwezi kupata ukombozi wa nchi yetu! Sasa natangaza rasimi kuwa niko upande wa EL.
 
Pasco wa Jf.
Ngamia hana uwezo wa kutua Nundu yake. Nundu yake ni Umbile/Ameumbwa nayo.Akiitua atakufa na hata Akituliwa atakufa. Kwa bahati mbaya Lowassa hana Zigo moja yawezekana yako mazigo kumi na moja. Atayatuaje yote na yote ayatafutie wenyewe?Tabia ni umbile atatuhakikishiaje kuwa ameacha Wiziiiiiiiiiiii??
Nimesema Awali mshaurini alituwe ili tumjue muhusika Tumsakameme. nae lowassa apumue kwa nini ajitoe kibyongo? kwa zigo lisilomuhusu? Hapa utakaempata ni yule aliyeamua akijua alifanyalo, wakuburuza labda uende mitaani huko.
Jujuman, muda muafaka ukifika, mwenye zigo lake, atalipokea na Lowassa atapanda ghorofani, na sipotuliwa, litamwelemea na mwishowe atalibwaga na mtamjua mwenyewe!

Its only a matter of time!.
 
Jujuman, muda muafaka ukifika, mwenye zigo lake, atalipokea na Lowassa atapanda ghorofani, na sipotuliwa, litamwelemea na mwishowe atalibwaga na mtamjua mwenyewe!

Its only a matter of time!.

Lets hope that day will come and we will be a live to witness it.
 
Lets hope that day will come and we will be a live to witness it.
Mkuu wangu siku ikifika EL atayamwaga manyanga kama alivyofanya kwa Mkapa kwani tumemfanya nini swala sii kujisafisha?.. EL akisema mwenye Richmond alikuwa JK wakati kisha jiuzulu mtafanya nini zaidi ya kumpa misifa bila kujua kwamba JK hawezi kushtakiwa..

Matokeo yake mtampa kura zetu kumbe ujinga ni wetu wenyewe kufikiria kwamba JK mchafu na EL msafi na hawa ni maadui.. Hili mimi nitalikataa hadi naingia kaburini isipokuwa ushabiki upo ktk nani JK atamrithisha na sio swala la JK vs EL...Hizi ni siasa tu, hakuna kitu uadui bali kutofautiana kimawazo.. Hata huku majuu majuu viongozi huangushia mizigo kuchafuana maadam ni kwa faida ya chama.
 
huu ni moja ya mifano ya hali halisi ya jinsi kikundi kidogo cha watu wanaotumiwa na lowassa kumpamba aonekane ana mvuto na ushawishi kanda ya ziwa na mpaka rose garden("g 8 ")




magazeti ya mtanzania na majira mnamo januari 02,2012 yalitoka na moja ya story kurasa za ndani kwamba el alishangiliwa sana pale jina lake lilipotajwa katika shairi huko kahama sasa mwenyekiti wa mamalaka ya maji kahama ambapo ndipo sherehe husika zilifanyika na ambaye pia ni katibu mwenezi wa ccm kahama amekanusha katika taarifa ake kwa vyombo vya habari ambayo ni hii ifuaayo:..


Lowasa hajamwagiwa sifa kahama bali selikari ya awamu ya tatu na nne


taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari nchini zinazomweleza waziri mkuu mstaafu mh. Edward lowasa kuwa amemwagiwa sifa mkoani shinyanga, ni upotoshaji wa vyombo vya habari ulijaa maslahi binafsi ya baadhi ya waandishi wa habari hizo. Mimi ni mwenyekiti wa bodi ya maji safi na usafi wa mazigira mjini kahama naitwa ndugu marco mipawa ng'wanangolelwa, nalazimika kutoa maelezo juu ya kauli hiyo iliyoshamiri kwenye magazeti mbalimbali ya tarehe 02/01/2012.

Ninachofahamu mimi zilisifiwa awamu ya tatu ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania, iliyoongozwa na rais mkapa, kwa kuthubutu kuanzisha ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa victoria kuja kahama; na awamu ya nne inayoongozwa na rais kikwete, kwa kupokea kijiti na kukamilisha ujenzi huo na siyo mh. Lowasa peke yake!".ndugu ng'wanangolelwa alisema. Kama mwenyekiti ndiye nilikuwa mwenyeji kwenye sherehe za ufunguzi wa jengo la ofisi za mamlaka mjini kahama tarehe29.12.2011; ambazo zilihudhuriwa na naibu waziri wa maji mhe. Mhandisi gerson lwenge (mb) kama mgeni raism na kwamba wazo la kumtaja mh. Lowasa tu kwenye ufanikishaji wa mradi huu wa maji ni la mwandishi mwenyewe tu ambaye wala hakuwepo kwenye shughuli hiyo.

Inawezekanaje sisi kumtaja waziri tu na hali yeye siyo mkuu wa nchi na kumwacha rais?" ngwanangolelwa alihoji na kuongeza kuwa, hapa ni dhahili kuna ‘wazo binafsi tu la mwandishi wa habari' ambaye anataka kuwawekea maneno mdomoni wananchi wa kahama, shinyanga na kanda ya ziwa kwa ujumla . Watu wanatambua mchango wa mh. Lowasa kwa nafasi zake kama waziri wa maji kwenye awamu ya rais mkapa, na waziri mkuu kwa rais kikwete; lakini ilivyokuzwa kwenye magazeti hayo ni ushabiki usio na maana unaolenga kuwalaghai watu waone kama kwamba, ni mh. Lowasa peke yake tu, ndiye aliyefanikisha zoezi hili wakati ni swala la serikali nzima.

Mimi nilikuwepo kwenye sherehe hizo kama mwenyeji wa naibu waziri wa maji aliyekuwa amealikwa na mamlaka ya maji kama mgeni raimi; alikuwepo kaimu mkuu wa mkoa mama masenza, katibu tawala wa mkoa na viongozi wote wa wilaya ya kahama, wakati shairi linasomwa hatukuyasikia haya kwa picha iliyotolewa na mwandihshi huyo nina imani wote tulilisikia vizuri shairi la ndugu nkanjiwa na halikumtaja lowasa tu bali lilianza na wakuu wa nchi; baada ya hapo liliwataja mawaziri kwa ubeti mmoja tu likisema, nanukuru:- "mawaziri walo maji, hongera usimamizini, lowasa na mwandosya, mradi wanikiwani' katibu mkuu sayi,utendaji wa imani, maji safi na salama kuwasa mambo shegani. Na hii ndiyo sehemu pekee iliyomtaja mhe. Lowasa baada ya kuwa wametajwa mkapa na kikwete kwenye ubeti uliotangulia.

Wewe unahisi hapa kuna nini?. Haya ya lowassa peke yake yametoka wapi?. Mimi binafsi nina shahada ya kwanza ya uandishi wa habari kutoka chuo kikuu cha st augustin cha mwanza na nadiriki kusema hashangazwi na jambo hili la kunyambulisha habari ,kwa sabababu anafahamu siku hizi kuna waandishi wa habari za watu na za umma .

Ninachowaomba tu wana habari wenzangu tujaribu kujitahidi kutumikia umma hata kama tuna shida kupita kiasi labda niwakumbushe sababu ya kutoa ufafanuzi huu,baadhi ya magazeti ya hapa nchini yalitamka kwamba wananchi mkoani shinyanga wamesifia lowassa kwa kuwapelekea maji na kunukuriwa kwa shairi la ndugu marco nkanjiwa lililoimbwa kwenye sherehe za ufunguzi wa ofisi ya mamlaka ya maji mwishoni mwa mwaka jana mjini kahama mkoani shinyanga
 
Nadhani ni muhimu sasa tuanze kumjadili Lowassa kwa hoja na vigezo vya sifa za kiongozi, badala ya ushabiki. Zoezi hili ni muhimu sana lianze sasa ili kuwe na muda wa kutosha kabla ya mwaka 2015. Ni zoezi muhimu sana kwa pande zote mbili – ule unaotaka kumjenga na ule unaotaka kumboboa. Ikumbukwe kwamba vizazi vya baadae vitarudia mijadala hii na kubaini wazazi wepi walifanya chaguo sahihi, na wepi walifanya chaguo lisilo sahihi. Na Jamiiforum ni mahala pazuri kwa hilo kwani, tofauti na kina Absolom Kibanda na wenzake ambao walishanunuliwa na Lowassa mwaka 2009 na ndio wanayoyalipa sasa mahakamani, wanachama wa JF hawawezi nunulika kirahisi, vinginevyo Lowassa awanunue MODs. Mimi, binafsi ningependa historia ininukuu kwamba, "Sikumkubali Lowassa kwa sababu hana sifa wala vigezo vya kuliongoza taifa hili maskini. Sasa kama historia itanihukumu, au kama Lowassa atagundua mimi ni nani, hivyo kunimaliza kwa sumu, hilo ni suala jingine. Sasa ebu tutazame sifa Lowassa na ningependa kina Pasco na wafuasi wengine wa kiongozi Lowassa tusaidiane katika hili.

Moja - Uzoefu wa uongozi ndani ya Chama – Hili halina ubishi, kwani Lowassa ana uzoefu mkubwa kichama, pengine kuliko wengine wote wanaotajawa kuwania Urais 2015. Key issue hapa ni "miongoni tu mwa wale wanaotajwa tajwa hadi sasa".

Mbili - Uzoefu wa kutosha katika serikali – Hii sifa anayo kutokana na Uwaziri wa miaka 12 (1990 – 1995 PLUS 1998 – 2005, na Uwaziri Mkuu wa miaka miwili – 2006 – 2008. Lakini ifahamike kwamba pia wapo wengine wengi wenye sifa serikalini kama Lowassa, na pengine kumpita both, uongozi wa muda mrefu kama waziri na utendaji mzuri mawizarani, ni kwamba tu hawajajitokeza bado kutanganza nia ya 2015.

Tatu - Umri – Lowassa an umri mzuri kugombea Urais mwaka 2015, kama ilivyo wengine kadhaa.

Nne - Mvuto – Lowassa ana sura nzuri, ni mweupe, mrefu, jasiri (ingawa ujasiri wake zaidi unatokanana zaidi na asili yake ya jamii ya wafugaji, ujasiri ambao tunauona pia kwa kina Dr. Slaa, Patrick Koro, Edward Sokoine, Mateo Qaresi, Daniel Ole Njoolay, Tundu Lissu, n.k). Mama mzazi wa Lowassa ni mmasai wa Monduli, kijiji cha Ngarash, Baba yake mzazi ni Mmeru karibia na Tengeru, lakini kule Milimani, anatokea ukoo wa Ndossi, ingawa leo hii Lowassa, hapendi hilo lijulikane sana. Ukifanya utafiti leo hii, utagundua haraka tu kwamba UMASAINI HAKUNA UKOO UNAOITWA LOWASSA, ZAIDI YA ULE AMBAO UTATOKANA NA LOWASSA WA SASA NA WANAE WATATU WA KIUME. Baba yake Lowassa (yani mzee Ndossi) alikuwa mtumishi serikali ya kikoloni, alihamishiwa monduli kikazi akitokea maeneo ya Arumeru. Ukizitazama picha za Mzee Ndossi, mzee huyu alikuwa mtanashati na msafi sana wa kimwili na mavazi. Katika ujana wake, kwa sasa angeitwa "Sharobaro", alikuwa anavaa kaptura zake safi, mashati masafi, viatu vinavyowaka, na soksi nyeupe hadi magotini. Mzee Ndossi alikuwa ni mtu wa madaha sana, kwa mwendo na vitendo. Umasaini, mtu wa namna hiyo huitwa "LAWASA", na hivyo ndivyo mzee yule alivyopata jina lake la utani wakati ule wa ukoloni kutoka kwa wamasai. Mzee yule baadae akaoa mama wa kimasai, akazaa nae watoto, na baadae akaamua kuwaandikisha shuleni watoto wao kwa majina ya Edward Lowassa badala ya Edward Ndossi n.k, nia ikiwa kuwageuza wawe wamasai. Tuendelee na sifa ya tano ya uongozi.

Tano – uadilifu na uaminifu – Lowassa sifa hii hana, na hata wafuasi wake wengi wanakubali ukweli huo. Hoja yao ni kwamba, hakuna msafi CCM, bila ya kujua kwamba hoja hiyo ni mbovu kuliko zote, kumtetea Lowassa kama kiongozi mahiri au bora. Uadilifu na Uaminifu ni sifa ni moja ya sifa muhimu sana kwa kiongozi, mbali na ile ya vision/dira/upeo au mwono wa mbali. Ni dhahiri kwamba, wafuasi wa Lowassa kaam vile Pasco na wengineo, hawajui Vision ya Lowassa kwa taifa hili ni nini. Ebu watueleze, je: Ni ile ya kutoa tahadhari kwa taifa kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana Tanzania ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote? Kama ni hiyo, kwanini leo? Kwanini katika ziara yake akiwa waziri mkuu kule kanda ya ziwa, mwaka 2007, mtoto mmoja wa shule ya msingi alipomuuliza "Mheshimwa Waziri Mkuu, kwanini vijana hawana ajira, huku unakuta wanasiasa wana vyeo zaidi ya kimoja kama vile ubunge na ukuu wa Mkoa", kwanini Lowassa hakuwa na jibu, na badala yake akawaacha wana TISS wamshughulikie mtoto wa watu na kusema ametumwa? Nani kamtuma Lowassa aje na kauli inayofanana na mtoto yule, miaka minne baadae?

Wafuasi wa Lowassa, jengeni hoja kumwokoa kiongozi wenu kwamba yeye ndiye chaguo pekee lililobakia, msisukumwe na ushabiki. Pia tuelezeeni mna maana gani mnaposema Lowassa ni Chaguo la Mungu. Mungu yupi? Wakati tunasubiri jibu hilo kutoka kwa wafuasi wa kiongozi Lowassa, ebu tuone kwa juu juu watalamu katika masuala ya uongozi wanasemanini juu ya sifa za mtu kuwa kiongozi. Ni muhimu tukaacha tabia ya ku copy and paste sifa za uongozi kutoka kwenye google bila ya kutambua kwamba, yote hayo, asili yake ni pamoja na maandiko ya mwanafalsafa aliyeitwa PLATO ambae alitamka kwamba ‘Being a leader isn't about a person's self interest". Je Lowassa anatosha vipi katika hili?

PLATO anazidi kutamka kwamba: Leadership requires a person to sacrifice his/her immediate self interest…In a city of good men, if it came into being, the citizens would fight in order not to rule . . . There it would be clear that anyone who is really a true ruler doesn't by nature seek his own advantage but that of his subjects. And everyone, knowing this, would rather be benefited by others than take the trouble to benefit them. Ni mtazamo huu wa PLATO ambao unafanya jamii nyingi duniani kubaini kwamba, kiongozi mzuri sio yule anaetafuta madaraka na uongozi kwa udi na uvumba, bali yule anayeo yaogopa madaraka kama ukoma. Katika jamii zilizoendelea, watu huwaogopa sana wale wote wanaoyatafuta madaraka kwa nguvu, hila na vitisho. Kuna mtaalam mmoja wa siasa aliwahi kusema (kutokana na tafsiri yake ya PLATO) kwamba: If you see a person who is too eager to lead, its either, he/she wants the power or position for self interes, or he/she doesn't fully understand the enormous responsibility and burden of leadership.

Inawezekana Lowassa ana sifa kadhaa za kuwa kiongozi wan chi, lakini anakosa vigezo muhimu vya uongozi ambavyo ni Vision, honesty, na integrity. Kwa wale wanaosema Lowassa ni chaguo la Mungu, hakuna sehemu kwenye biblia ambayo inatoa mfano wa mtu anayefanana na Lowassa katika hayo matatu, na kama yupo, tuelezeni ili tuyajadili.
 
mengi yanaongewa kuhusu Lowassa lakni niseme mimi siku niliyomdharau Lowassa ni siku ile ya
bajeti ya kwanza ya serikli ya Kikwete bungeni
alipokuwa anasoma bajeti ya ofisi ya waziri mkuu nafikiri na aka introduce 'mabilioni ya Kikwete'

alikuwa anazungumza kwa kujisifu na kusema kuna wafanyabiashara maarufu wa hapa TZ
wamempigia simu kumsifia juu ya hiyo idea ya kukopesha wajasiriamali utasema ndo 'blue print'
ya kumalza umasikini wa Watanzania......it was very sad.......nilimuona mweupe mno kwenye
suala zima la kupambana na umasikini.......
 
Mimi alinifurahisha cku ya kwanza pale aliposema atajenga hoteli za kutosha kwenye mbuga zetu sana sana serengeti. Niliona ni jambo la maana sana kutengeneza ajira nyingi na kuongeza pato la taifa kuliko kukalia uchumi tukiwapa wakenya watuchezee wanavyotaka
 
Mkuu Mkandara,

Hayo maneno ya ndege inayopaa huwa yananikumbusha mbali sana na kila nikiyakumbuka ninakumbuka Makala ya Ndege ya Lowassa inayopaa [sikumbuki kama ilikuwa ni Makala ya Mzee Mwanakijiji or someone else]. Ili kunogesha stori, makala hiyo iliambatana na katuni ya ndege inapaa huku ikiwa imewaacha walalahoi wanashangaa airport. Kile kikatuni kilikuwa na ujumbe mzito sana. Makala hiyo na Katuni vilimkera sana Lowassa na ninadhani alituma watu wake waijibu.

Baada ya makala hiyo na katuni, wakaja wapambe wake [sijui wamesomea wapi uchumi wao, sorry sijawahi kubeza elimu ya mtu ila ninabeza pale theories zinapotumika vibaya ku-justify kauli za wana siasa] na Theory ya Five Stages za Growth ya uchumi ambayo iliandikwa na W. W. Rostow, nilisoma makala hiyo ya utetezi wala haikuwa ina-make sense.

Kama kweli uchumi wa Tanzania ulikuwa unapaa, basi leo hii tusingekuwa tunalia lia kwamba hali ya uchumi ni mbaya huku watu wako gizani. Ni takribani miaka 4 tu iliyopita Lowassa alipotamka maneno hayo, lakini hali tuliyonayo leo wapo wanaoweza kusema heri ya zama za Ukapa wa Mkapa.
 
Mkuu Mkandara, we are facing two choices only! hawa jamaa waendelee kutawala milele, au tuamke tufanye mabadiliko ya kweli!
Mkiamua waendelee kututawala milele, tuleteeni Dr. Shein, na wale sportless wao kama Nahodha au Dr. Mwinyi. Lakini kama tunataka mabadiliko ya kweli, we have one and only choice, Lowassa ateuliwe mgombea wa CCM!. Kwa uzoefu wangu wa siasa za bongo, CCM itamteua mtu anaeuzika kirahisi, Lowassa atafishwa na atateuliwa ili kutuletea ukombozi wa kweli! Mtu anayeuzika kwa wananchi kwa urahisi ni Lowassa tuu maana track record yake ipo, alitaka kutengeneza hadi mvua!

Mkuu Pasco,

Nimekuuliza ukombozi unaouongelea ni upi, lakini kwa bahati mbaya sijapata jibu.

Lowassa ndo anauzika kirahisi? Unatumia kigezo gani kupima mtu anavyouzika kirahisi?

Ulishasoma report ya Mukama iliyochunguza kwamba kwanini CCM ilifanya vibaya kwenye uchaguzi wa 2010? Unafikiri ni kwanini Kamati Kuu iliamua kujiuzulu? Kwanini JK alikuja na kauli mbiu ya CCM kujivua gamba? Kwanini Mukama aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu? Kwanini Phillip Mangula alienda kupiga kampeni Igunga? Baada ya hizo Kampeni ulishamsikia tena kwenye medani za siasa?

Ni mapema sana kusema kwamba Lowassa atateuliwa na CCM. Tukae tusubiri uchaguzi wa ndani wa chama na haswa wenyeviti wa Jumuiya za Chama ambao automatically wanaingia kwenye CC. Pia tusubiri maamuzi ya Mkutano Mkuu wa chama wa kubariki mapendekezo ya kuwaengua wastaafu kwenye ujumbe wa kudumu ndani ya Kamati Kuu.

Kuna madudu mengi sana ambayo yanaendelea chini chini, so ni ngumu kuweza kujua nini kitatokea na hasa baada ya kubadilisha mfumo wa uchaguzi wa wajumbe wa NEC.

Kama ulisoma Makala ya Mzee Jenerali Twaha Ulimwengu siku ya jana, kitakachokuwa kinaendelea ndani ya CCM mwaka huu ni uhuni kwa kwenda mbele ikiwa ni pamoja na kuchezeana mchezo mchafu. Ndio maana magazeti ya Mtanzania yamekuwa yanachapa nyeti za ndani ili kuvurugana na ku-frustrate moves zote ambazo zinaweza ku-work against kundi "lao".
 
Mkuu Mkandara,

Hayo maneno ya ndege inayopaa huwa yananikumbusha mbali sana na kila nikiyakumbuka ninakumbuka Makala ya Ndege ya Lowassa inayopaa [sikumbuki kama ilikuwa ni Makala ya Mzee Mwanakijiji or someone else]. Ili kunogesha stori, makala hiyo iliambatana na katuni ya ndege inapaa huku ikiwa imewaacha walalahoi wanashangaa airport. Kile kikatuni kilikuwa na ujumbe mzito sana. Makala hiyo na Katuni vilimkera sana Lowassa na ninadhani alituma watu wake waijibu.

Baada ya makala hiyo na katuni, wakaja wapambe wake [sijui wamesomea wapi uchumi wao, sorry sijawahi kubeza elimu ya mtu ila ninabeza pale theories zinapotumika vibaya ku-justify kauli za wana siasa] na Theory ya Five Stages za Growth ya uchumi ambayo iliandikwa na W. W. Rostow, nilisoma makala hiyo ya utetezi wala haikuwa ina-make sense.

Kama kweli uchumi wa Tanzania ulikuwa unapaa, basi leo hii tusingekuwa tunalia lia kwamba hali ya uchumi ni mbaya huku watu wako gizani. Ni takribani miaka 4 tu iliyopita Lowassa alipotamka maneno hayo, lakini hali tuliyonayo leo wapo wanaoweza kusema heri ya zama za Ukapa wa Mkapa.
Naungana na wana JF wengi kwamba hata mimi nikiwa kama mgeni (sio mwanachama) humu JF mwaka 2007, niliwahi kumsoma Mwanakijiji sehemu moja akiapa kwamba hatanyamaza mpaka Lowassa anafutika natika anga ya uongozi wa Tanzania na alitoa vigezo vya msingi kabisa ambavyo ndivyo vitatutafunakama taifa.

Sielewi nini kimemsibu ndugu yetu Mwanakijiji katika hilo. Vinginevyo, ni rahisi sana Mwanakiji akaanza kupoteza credibility yake kwenye jamii kutokana na his lack of consistency. Na ni hilo pia linalo na linalo/litakalo mwangusha mtu kama Mitt Romney dhidi ya Obama uchaguzi wa mwaka huu, Marekani. Iwapo hata Mwanakijiji amemwaga manyanga aidha kwa kununuliwa au kukata tama, basi kazi ipo.
 
Back
Top Bottom