Nadhani ni muhimu sasa tuanze kumjadili Lowassa kwa hoja na vigezo vya sifa za kiongozi, badala ya ushabiki. Zoezi hili ni muhimu sana lianze sasa ili kuwe na muda wa kutosha kabla ya mwaka 2015. Ni zoezi muhimu sana kwa pande zote mbili ule unaotaka kumjenga na ule unaotaka kumboboa. Ikumbukwe kwamba vizazi vya baadae vitarudia mijadala hii na kubaini wazazi wepi walifanya chaguo sahihi, na wepi walifanya chaguo lisilo sahihi. Na Jamiiforum ni mahala pazuri kwa hilo kwani, tofauti na kina Absolom Kibanda na wenzake ambao walishanunuliwa na Lowassa mwaka 2009 na ndio wanayoyalipa sasa mahakamani, wanachama wa JF hawawezi nunulika kirahisi, vinginevyo Lowassa awanunue MODs. Mimi, binafsi ningependa historia ininukuu kwamba, Sikumkubali Lowassa kwa sababu hana sifa wala vigezo vya kuliongoza taifa hili maskini. Sasa kama historia itanihukumu, au kama Lowassa atagundua mimi ni nani, hivyo kunimaliza kwa sumu, hilo ni suala jingine. Sasa ebu tutazame sifa Lowassa na ningependa kina Pasco na wafuasi wengine wa kiongozi Lowassa tusaidiane katika hili.
Moja - Uzoefu wa uongozi ndani ya Chama Hili halina ubishi, kwani Lowassa ana uzoefu mkubwa kichama, pengine kuliko wengine wote wanaotajawa kuwania Urais 2015. Key issue hapa ni miongoni tu mwa wale wanaotajwa tajwa hadi sasa.
Mbili - Uzoefu wa kutosha katika serikali Hii sifa anayo kutokana na Uwaziri wa miaka 12 (1990 1995 PLUS 1998 2005, na Uwaziri Mkuu wa miaka miwili 2006 2008. Lakini ifahamike kwamba pia wapo wengine wengi wenye sifa serikalini kama Lowassa, na pengine kumpita both, uongozi wa muda mrefu kama waziri na utendaji mzuri mawizarani, ni kwamba tu hawajajitokeza bado kutanganza nia ya 2015.
Tatu - Umri Lowassa an umri mzuri kugombea Urais mwaka 2015, kama ilivyo wengine kadhaa.
Nne - Mvuto Lowassa ana sura nzuri, ni mweupe, mrefu, jasiri (ingawa ujasiri wake zaidi unatokanana zaidi na asili yake ya jamii ya wafugaji, ujasiri ambao tunauona pia kwa kina Dr. Slaa, Patrick Koro, Edward Sokoine, Mateo Qaresi, Daniel Ole Njoolay, Tundu Lissu, n.k). Mama mzazi wa Lowassa ni mmasai wa Monduli, kijiji cha Ngarash, Baba yake mzazi ni Mmeru karibia na Tengeru, lakini kule Milimani, anatokea ukoo wa Ndossi, ingawa leo hii Lowassa, hapendi hilo lijulikane sana. Ukifanya utafiti leo hii, utagundua haraka tu kwamba UMASAINI HAKUNA UKOO UNAOITWA LOWASSA, ZAIDI YA ULE AMBAO UTATOKANA NA LOWASSA WA SASA NA WANAE WATATU WA KIUME. Baba yake Lowassa (yani mzee Ndossi) alikuwa mtumishi serikali ya kikoloni, alihamishiwa monduli kikazi akitokea maeneo ya Arumeru. Ukizitazama picha za Mzee Ndossi, mzee huyu alikuwa mtanashati na msafi sana wa kimwili na mavazi. Katika ujana wake, kwa sasa angeitwa Sharobaro, alikuwa anavaa kaptura zake safi, mashati masafi, viatu vinavyowaka, na soksi nyeupe hadi magotini. Mzee Ndossi alikuwa ni mtu wa madaha sana, kwa mwendo na vitendo. Umasaini, mtu wa namna hiyo huitwa LAWASA, na hivyo ndivyo mzee yule alivyopata jina lake la utani wakati ule wa ukoloni kutoka kwa wamasai. Mzee yule baadae akaoa mama wa kimasai, akazaa nae watoto, na baadae akaamua kuwaandikisha shuleni watoto wao kwa majina ya Edward Lowassa badala ya Edward Ndossi n.k, nia ikiwa kuwageuza wawe wamasai. Tuendelee na sifa ya tano ya uongozi.
Tano uadilifu na uaminifu Lowassa sifa hii hana, na hata wafuasi wake wengi wanakubali ukweli huo. Hoja yao ni kwamba, hakuna msafi CCM, bila ya kujua kwamba hoja hiyo ni mbovu kuliko zote, kumtetea Lowassa kama kiongozi mahiri au bora. Uadilifu na Uaminifu ni sifa ni moja ya sifa muhimu sana kwa kiongozi, mbali na ile ya vision/dira/upeo au mwono wa mbali. Ni dhahiri kwamba, wafuasi wa Lowassa kaam vile Pasco na wengineo, hawajui Vision ya Lowassa kwa taifa hili ni nini. Ebu watueleze, je: Ni ile ya kutoa tahadhari kwa taifa kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana Tanzania ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote? Kama ni hiyo, kwanini leo? Kwanini katika ziara yake akiwa waziri mkuu kule kanda ya ziwa, mwaka 2007, mtoto mmoja wa shule ya msingi alipomuuliza Mheshimwa Waziri Mkuu, kwanini vijana hawana ajira, huku unakuta wanasiasa wana vyeo zaidi ya kimoja kama vile ubunge na ukuu wa Mkoa, kwanini Lowassa hakuwa na jibu, na badala yake akawaacha wana TISS wamshughulikie mtoto wa watu na kusema ametumwa? Nani kamtuma Lowassa aje na kauli inayofanana na mtoto yule, miaka minne baadae?
Wafuasi wa Lowassa, jengeni hoja kumwokoa kiongozi wenu kwamba yeye ndiye chaguo pekee lililobakia, msisukumwe na ushabiki. Pia tuelezeeni mna maana gani mnaposema Lowassa ni Chaguo la Mungu. Mungu yupi? Wakati tunasubiri jibu hilo kutoka kwa wafuasi wa kiongozi Lowassa, ebu tuone kwa juu juu watalamu katika masuala ya uongozi wanasemanini juu ya sifa za mtu kuwa kiongozi. Ni muhimu tukaacha tabia ya ku copy and paste sifa za uongozi kutoka kwenye google bila ya kutambua kwamba, yote hayo, asili yake ni pamoja na maandiko ya mwanafalsafa aliyeitwa PLATO ambae alitamka kwamba Being a leader isnt about a persons self interest. Je Lowassa anatosha vipi katika hili?
PLATO anazidi kutamka kwamba: Leadership requires a person to sacrifice his/her immediate self interest
In a city of good men, if it came into being, the citizens would fight in order not to rule . . . There it would be clear that anyone who is really a true ruler doesnt by nature seek his own advantage but that of his subjects. And everyone, knowing this, would rather be benefited by others than take the trouble to benefit them. Ni mtazamo huu wa PLATO ambao unafanya jamii nyingi duniani kubaini kwamba, kiongozi mzuri sio yule anaetafuta madaraka na uongozi kwa udi na uvumba, bali yule anayeo yaogopa madaraka kama ukoma. Katika jamii zilizoendelea, watu huwaogopa sana wale wote wanaoyatafuta madaraka kwa nguvu, hila na vitisho. Kuna mtaalam mmoja wa siasa aliwahi kusema (kutokana na tafsiri yake ya PLATO) kwamba: If you see a person who is too eager to lead, its either, he/she wants the power or position for self interes, or he/she doesnt fully understand the enormous responsibility and burden of leadership.
Inawezekana Lowassa ana sifa kadhaa za kuwa kiongozi wan chi, lakini anakosa vigezo muhimu vya uongozi ambavyo ni Vision, honesty, na integrity. Kwa wale wanaosema Lowassa ni chaguo la Mungu, hakuna sehemu kwenye biblia ambayo inatoa mfano wa mtu anayefanana na Lowassa katika hayo matatu, na kama yupo, tuelezeni ili tuyajadili.