Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Naungana na wana JF wengi kwamba hata mimi nikiwa kama mgeni (sio mwanachama) humu JF mwaka 2007, niliwahi kumsoma Mwanakijiji sehemu moja akiapa kwamba hatanyamaza mpaka Lowassa anafutika natika anga ya uongozi wa Tanzania na alitoa vigezo vya msingi kabisa ambavyo ndivyo vitatutafunakama taifa.

Sielewi nini kimemsibu ndugu yetu Mwanakijiji katika hilo. Vinginevyo, ni rahisi sana Mwanakiji akaanza kupoteza credibility yake kwenye jamii kutokana na his lack of consistency. Na ni hilo pia linalo na linalo/litakalo mwangusha mtu kama Mitt Romney dhidi ya Obama uchaguzi wa mwaka huu, Marekani. Iwapo hata Mwanakijiji amemwaga manyanga aidha kwa kununuliwa au kukata tama, basi kazi ipo.
Mkuu Mtoa habari,taifa limetikiswa na limetikisika,wengi hawajui lakini wapiganaji wengi wamenunuliwa na imefika mahala hakuna kuaminiana tena! Vita imekuwa ngumu kwasababu waliokuwa mbele kwa muda mrefu wametusaliti wakiwemo wanasiasa na waandishi maarufu! Tunaelekea kushindwa sababu hakuna kiongozi wa dhati wa mapambano haya anaeweza kumobilize wafuasi watiifu na wazalendo. Unajua wakati mgumu alionao Dr Slaa mtu pekee ambae angeweza kusimamia mageuzi haya independently!

Mzee Mwanakijiji sijawahi kuona akibadili msimamo juu ya Lowasa lakini ukimya wake kwenye thread hii unatoa ujumbe fulani! Anaonekana on line lakini amekuwa msomaji tu! binafsi ilipofikia hizi siasa zetu hakuna wa kumwamini ni kama wengine tumeamua kusubiri kuona nini kitatokea! Umejiuliza Ben Saanane kwanini hajachangia lolote? Take it simple (but it's complicated).
 
Woote hawa uliowataja, Kikwete, Rostam ,Mkapa, Shein, Apson Mwang'onda n.k ni Genge la majambazi wanajipanga kwa kila namna ili kuiibia nchi wala si kuwaletea maendeleo wananchi...
Tunawajua ...na sasa hivi baadhi yao wapo katika tuhuma kuwa walihusika kum-ingizia Nyerere viini vya kandsa ya damu ile waje wapate madaraka , kwani walijua wasingekuja kuwa maraisi wa nchi hii Mwalimu akiwa hai.
Kwa vyovyote vile, mimi hiyo naiona ni vita ya mashetani, linapoumizwa moja huwezi kuilionea huruma.....maana yoote ni maovu.
 
Naona watu wanaogopa kuvamiwa na G8!
 
aisee kazi kweli inamaana kama asingewekewa viini vya kansa angeishi milele?je alikuwa ana mkataba na mungu
 
The Boss,
Unakumbuka hili swali lako?

huwa natamani mtu mwenye kujua historia sahihi ya EL ailete hapa
hasa historia ya kabla ya kufika chuo

Je, unaonaje kwa uzi huu, unapata majibu?

mengi yanaongewa kuhusu Lowassa lakni niseme mimi siku niliyomdharau Lowassa ni siku ile ya
bajeti ya kwanza ya serikli ya Kikwete bungeni
alipokuwa anasoma bajeti ya ofisi ya waziri mkuu nafikiri na aka introduce 'mabilioni ya Kikwete'

alikuwa anazungumza kwa kujisifu na kusema kuna wafanyabiashara maarufu wa hapa TZ
wamempigia simu kumsifia juu ya hiyo idea ya kukopesha wajasiriamali utasema ndo 'blue print'
ya kumalza umasikini wa Watanzania......it was very sad.......nilimuona mweupe mno kwenye
suala zima la kupambana na umasikini.......
 
Nadhani tumemkaba Lowasa kiasi cha kutosha. Jamaa ni mjanja sana. Akiona amekabwa hivi atatoa pasi kwa mfungaji mwingine kama alivyofanya mwaka 2005. Goli likishafungwa yeye atajua namna ya kujitokeza! Lowasa anautaka URAIS sio kwa kuwa anajua kuongoza tu. La hasha. Anataka kulinda utajiri wake haramu na wa kundi lake ambalo sasa ni kubwa sana.

Endapo Lowasa atashindwa kutoa pasi kama ile ya mwaka 2005 atatoa krosi ambayo inaweza kusababisha tukajifunga wenyewe kama lile goli la ManU juzi. Baadhi ya mabeki wa upande huu siwaoni. Wako kimya.
 
Nasikia anataka kumpa pasi ya kisigino Amani hasa mkimng'ang'ania kwa kigezo cha "zamu ya zanzibar" ila hataki kuwa mgombea mweza kama itakua hivyo,anataka kurudi kumalizia pale alipopatia ile "ajali yake" mashuhuri!
 
Naungana na wana JF wengi kwamba hata mimi nikiwa kama mgeni (sio mwanachama) humu JF mwaka 2007, niliwahi kumsoma Mwanakijiji sehemu moja akiapa kwamba hatanyamaza mpaka Lowassa anafutika natika anga ya uongozi wa Tanzania na alitoa vigezo vya msingi kabisa ambavyo ndivyo vitatutafunakama taifa.

Sielewi nini kimemsibu ndugu yetu Mwanakijiji katika hilo. Vinginevyo, ni rahisi sana Mwanakiji akaanza kupoteza credibility yake kwenye jamii kutokana na his lack of consistency. Na ni hilo pia linalo na linalo/litakalo mwangusha mtu kama Mitt Romney dhidi ya Obama uchaguzi wa mwaka huu, Marekani. Iwapo hata Mwanakijiji amemwaga manyanga aidha kwa kununuliwa au kukata tama, basi kazi ipo.
Mkuu mtoa habari, japo mimi sio msemaji wa Mzee Mwanakijiji, lakini ufahamu wangu kupitia maandiko yake, ukimya wa Mwanakijiji kwenye mada hii, sio kupoteza credibility, kununuliwa au kukata tamaa, bali baada ya kuelewa the motives behind usafishaji wa Lowassa unaofanyika humu na mimi nikiwa ni mmoja wa waumini wakuu wa usafi wa Lowassa na mmoja wa wapiga debe wake wa kujitolea, Mzee Mwanakijiji ametuelewa na kujinyamazia asiendelee kumbomoa, ili kazi yetu ya kumsafisha ifanikiwe na lengo la usafishaji huo litimie!.

Hata wewe Mkuu Mwanahabari, nakuaminia kama ni mtu unayetaka mabadiliko ya kweli, na unazijua fika polical dynamics za siasa za Tanzania, kama ni kweli unataka mabadiliko, utakuwa upande wetu, tumpigie debe, Lowassa asimamishwe kuwa mgombea wa CCM!.
 
Mkuu Mtoa habari,taifa limetikiswa na limetikisika,wengi hawajui lakini wapiganaji wengi wamenunuliwa na imefika mahala hakuna kuaminiana tena! Vita imekuwa ngumu kwasababu waliokuwa mbele kwa muda mrefu wametusaliti wakiwemo wanasiasa na waandishi maarufu! Tunaelekea kushindwa sababu hakuna kiongozi wa dhati wa mapambano haya anaeweza kumobilize wafuasi watiifu na wazalendo.unajua wakati mgumu alionao Dr Slaa mtu pekee ambae angeweza kusimamia mageuzi haya independently! Mzee Mwanakijiji sijawahi kuona akibadili msimamo juu ya Lowasa lakini ukimya wake kwenye thread hii unatoa ujumbe fulani! Anaonekana on line lakini amekuwa msomaji tu! binafsi ilipofikia hizi siasa zetu hakuna wa kumwamini ni kama wengine tumeamua kusubiri kuona nini kitatokea! Umejiuliza Ben Saanane kwanini hajachangia lolote? Take it simple (but it's complicated).
Mkuu Mtazamo, kiukweli humu ndani sio tuu wengi tunatofautiana mtazamo, uelewa na ufahamu, bali hata imani ya kutokuaminiana!. Kwa watu wanaomfahamu Mzee Mwanakijiji wa ukweli, bado tunamwaminia na ukimuona kimya kwenye issue fulani, ujue ukimya wake una mshindo mkuu, kwa vile Mwanakijiji ni very vocal, akibadili msimamo atasema na sababu zake, ukimya huu ni kutuachia sisi tunaomsafisha Lowassa tuendeleze kazi hii nzuri tuliyoianza ili malengo ya safisha safisha hii yatimie!

Kama ni kweli unaamini Dr. Slaa ndie pekee anayeweza kuleta mageuzi ya kweli hapa nchini, na unampenda kwa dhati, then utamlinda kwa njia zote ili asipotee kabla ya hiyo 2015!. Kuna aina nyingi za upendo moja wapo ni hii " Anayeipenda sana nafsi yake, ataiangamiza, na atakayekubali kuiangamiza nafsi yake ndiye atakayeiokoa"!.

Determinant ya nani atakuwa ndie rais ajaye, lies with CCM candidate!. Kama mgombea wako ni Dr. Slaa, ni washabiki wajinga tuu ndio wataamini Dr. Slaa atapitia njia nyeupe kuingia Ikulu ya Magogoni!. Watu serious wanajua jinsi njia ilivyo ngumu na ilivyojaa miiba!. Hebu imagine chances za Dr. Slaa akisimama na mtu kama Dr. Shein, Dr. Shein atazoa kura zote za compasssion kwa vile Mzee wa watu huyu hawezi hata ku shout!. Just imagine Dr. Slaa anasimamisha na Magufuli unajua nini kitafuatia!. Hivyo determinant ya ushindi lies with mgombea wa CCM na mgombea kipenzi cha watu, kipenzi cha wote, mwenye mvuto wa ajabu, mwenye sura ya kupendeza, mwenye usafi usiokuwa na mashaka, mwenye utakatifu wa kukaribiana na Bwana wetu Yesu Kristo ni Edward Lowassa pekee!. Huyu ndie mkombozi wa taifa letu aliyebakia kwenye safu ya CCM!, tumpiganie yeye asimamishwe, tupate ukombozi wa kweli!

Pasco (wajf)
 
Hivyo determinant ya ushindi lies with mgombea wa CCM na mgombea kipenzi cha watu, kipenzi cha wote, mwenye mvuto wa ajabu, mwenye sura ya kupendeza, mwenye usafi usiokuwa na mashaka, mwenye utakatifu wa kukaribiana na Bwana wetu Yesu Kristo ni Edward Lowassa pekee!. Huyu ndie mkombozi wa taifa letu aliyebakia kwenye safu ya CCM!, tumpiganie yeye asimamishwe, tupate ukombozi wa kweli!

Pasco (wajf)

Orait sasa nimekupata bara bara.😛oa
 
Are you the monster? Acha uongo mkuu usiandike kwa kutumia masaburi.
Tongindi, I might be a monster, wewe ambaye ni human being umeandika nini?. Kama ni uongo, unaonaje kama ukiuonyesha huo uongo halafu ukauweka na ukweli unaouana wewe?. Hili la kuandika kwa kutumia masaburi nalo neno na maandamu ni wewe umelisema, inamaani unafikiri kwa kutumia masaburi, mimi mwenzako naandika kwa kutumia kidole tena naandikia kidole kimoja tuu, ukiona vipi, naweza ...
 
Mkuu mtoa habari, japo mimi sio msemaji wa Mzee Mwanakijiji, lakini ufahamu wangu kupitia maandiko yake, ukimya wa Mwanakijiji kwenye mada hii, sio kupoteza credibility, kununuliwa au kukata tamaa, bali baada ya kuelewa the motives behind usafishaji wa Lowassa unaofanyika humu na mimi nikiwa ni mmoja wa waumini wakuu wa usafi wa Lowassa na mmoja wa wapiga debe wake wa kujitolea, Mzee Mwanakijiji ametuelewa na kujinyamazia asiendelee kumbomoa, ili kazi yetu ya kumsafisha ifanikiwe na lengo la usafishaji huo litimie!.

Hata wewe Mkuu Mwanahabari, nakuaminia kama ni mtu unayetaka mabadiliko ya kweli, na unazijua fika polical dynamics za siasa za Tanzania, kama ni kweli unataka mabadiliko, utakuwa upande wetu, tumpigie debe, Lowassa asimamishwe kuwa mgombea wa CCM!.
mkuu lengo kumbe ni kumpigia debe EL asimamishwe kuwa mgombea wa CCM na sio kuwa rais wa TZ?
 
Nadhani ni muhimu sasa tuanze kumjadili Lowassa kwa hoja na vigezo vya sifa za kiongozi, badala ya ushabiki. Zoezi hili ni muhimu sana lianze sasa ili kuwe na muda wa kutosha kabla ya mwaka 2015. Ni zoezi muhimu sana kwa pande zote mbili – ule unaotaka kumjenga na ule unaotaka kumboboa. Ikumbukwe kwamba vizazi vya baadae vitarudia mijadala hii na kubaini wazazi wepi walifanya chaguo sahihi, na wepi walifanya chaguo lisilo sahihi. Na Jamiiforum ni mahala pazuri kwa hilo kwani, tofauti na kina Absolom Kibanda na wenzake ambao walishanunuliwa na Lowassa mwaka 2009 na ndio wanayoyalipa sasa mahakamani, wanachama wa JF hawawezi nunulika kirahisi, vinginevyo Lowassa awanunue MODs. Mimi, binafsi ningependa historia ininukuu kwamba, “Sikumkubali Lowassa kwa sababu hana sifa wala vigezo vya kuliongoza taifa hili maskini. Sasa kama historia itanihukumu, au kama Lowassa atagundua mimi ni nani, hivyo kunimaliza kwa sumu, hilo ni suala jingine. Sasa ebu tutazame sifa Lowassa na ningependa kina Pasco na wafuasi wengine wa kiongozi Lowassa tusaidiane katika hili.

Moja - Uzoefu wa uongozi ndani ya Chama – Hili halina ubishi, kwani Lowassa ana uzoefu mkubwa kichama, pengine kuliko wengine wote wanaotajawa kuwania Urais 2015. Key issue hapa ni “miongoni tu mwa wale wanaotajwa tajwa hadi sasa”.

Mbili - Uzoefu wa kutosha katika serikali – Hii sifa anayo kutokana na Uwaziri wa miaka 12 (1990 – 1995 PLUS 1998 – 2005, na Uwaziri Mkuu wa miaka miwili – 2006 – 2008. Lakini ifahamike kwamba pia wapo wengine wengi wenye sifa serikalini kama Lowassa, na pengine kumpita both, uongozi wa muda mrefu kama waziri na utendaji mzuri mawizarani, ni kwamba tu hawajajitokeza bado kutanganza nia ya 2015.

Tatu - Umri – Lowassa an umri mzuri kugombea Urais mwaka 2015, kama ilivyo wengine kadhaa.

Nne - Mvuto – Lowassa ana sura nzuri, ni mweupe, mrefu, jasiri (ingawa ujasiri wake zaidi unatokanana zaidi na asili yake ya jamii ya wafugaji, ujasiri ambao tunauona pia kwa kina Dr. Slaa, Patrick Koro, Edward Sokoine, Mateo Qaresi, Daniel Ole Njoolay, Tundu Lissu, n.k). Mama mzazi wa Lowassa ni mmasai wa Monduli, kijiji cha Ngarash, Baba yake mzazi ni Mmeru karibia na Tengeru, lakini kule Milimani, anatokea ukoo wa Ndossi, ingawa leo hii Lowassa, hapendi hilo lijulikane sana. Ukifanya utafiti leo hii, utagundua haraka tu kwamba UMASAINI HAKUNA UKOO UNAOITWA LOWASSA, ZAIDI YA ULE AMBAO UTATOKANA NA LOWASSA WA SASA NA WANAE WATATU WA KIUME. Baba yake Lowassa (yani mzee Ndossi) alikuwa mtumishi serikali ya kikoloni, alihamishiwa monduli kikazi akitokea maeneo ya Arumeru. Ukizitazama picha za Mzee Ndossi, mzee huyu alikuwa mtanashati na msafi sana wa kimwili na mavazi. Katika ujana wake, kwa sasa angeitwa “Sharobaro”, alikuwa anavaa kaptura zake safi, mashati masafi, viatu vinavyowaka, na soksi nyeupe hadi magotini. Mzee Ndossi alikuwa ni mtu wa madaha sana, kwa mwendo na vitendo. Umasaini, mtu wa namna hiyo huitwa “LAWASA”, na hivyo ndivyo mzee yule alivyopata jina lake la utani wakati ule wa ukoloni kutoka kwa wamasai. Mzee yule baadae akaoa mama wa kimasai, akazaa nae watoto, na baadae akaamua kuwaandikisha shuleni watoto wao kwa majina ya Edward Lowassa badala ya Edward Ndossi n.k, nia ikiwa kuwageuza wawe wamasai. Tuendelee na sifa ya tano ya uongozi.

Tano – uadilifu na uaminifu – Lowassa sifa hii hana, na hata wafuasi wake wengi wanakubali ukweli huo. Hoja yao ni kwamba, hakuna msafi CCM, bila ya kujua kwamba hoja hiyo ni mbovu kuliko zote, kumtetea Lowassa kama kiongozi mahiri au bora. Uadilifu na Uaminifu ni sifa ni moja ya sifa muhimu sana kwa kiongozi, mbali na ile ya vision/dira/upeo au mwono wa mbali. Ni dhahiri kwamba, wafuasi wa Lowassa kaam vile Pasco na wengineo, hawajui Vision ya Lowassa kwa taifa hili ni nini. Ebu watueleze, je: Ni ile ya kutoa tahadhari kwa taifa kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana Tanzania ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote? Kama ni hiyo, kwanini leo? Kwanini katika ziara yake akiwa waziri mkuu kule kanda ya ziwa, mwaka 2007, mtoto mmoja wa shule ya msingi alipomuuliza “Mheshimwa Waziri Mkuu, kwanini vijana hawana ajira, huku unakuta wanasiasa wana vyeo zaidi ya kimoja kama vile ubunge na ukuu wa Mkoa”, kwanini Lowassa hakuwa na jibu, na badala yake akawaacha wana TISS wamshughulikie mtoto wa watu na kusema ametumwa? Nani kamtuma Lowassa aje na kauli inayofanana na mtoto yule, miaka minne baadae?

Wafuasi wa Lowassa, jengeni hoja kumwokoa kiongozi wenu kwamba yeye ndiye chaguo pekee lililobakia, msisukumwe na ushabiki. Pia tuelezeeni mna maana gani mnaposema Lowassa ni Chaguo la Mungu. Mungu yupi? Wakati tunasubiri jibu hilo kutoka kwa wafuasi wa kiongozi Lowassa, ebu tuone kwa juu juu watalamu katika masuala ya uongozi wanasemanini juu ya sifa za mtu kuwa kiongozi. Ni muhimu tukaacha tabia ya ku copy and paste sifa za uongozi kutoka kwenye google bila ya kutambua kwamba, yote hayo, asili yake ni pamoja na maandiko ya mwanafalsafa aliyeitwa PLATO ambae alitamka kwamba ‘Being a leader isn’t about a person’s self interest”. Je Lowassa anatosha vipi katika hili?

PLATO anazidi kutamka kwamba: Leadership requires a person to sacrifice his/her immediate self interest…In a city of good men, if it came into being, the citizens would fight in order not to rule . . . There it would be clear that anyone who is really a true ruler doesn’t by nature seek his own advantage but that of his subjects. And everyone, knowing this, would rather be benefited by others than take the trouble to benefit them. Ni mtazamo huu wa PLATO ambao unafanya jamii nyingi duniani kubaini kwamba, kiongozi mzuri sio yule anaetafuta madaraka na uongozi kwa udi na uvumba, bali yule anayeo yaogopa madaraka kama ukoma. Katika jamii zilizoendelea, watu huwaogopa sana wale wote wanaoyatafuta madaraka kwa nguvu, hila na vitisho. Kuna mtaalam mmoja wa siasa aliwahi kusema (kutokana na tafsiri yake ya PLATO) kwamba: If you see a person who is too eager to lead, its either, he/she wants the power or position for self interes, or he/she doesn’t fully understand the enormous responsibility and burden of leadership.

Inawezekana Lowassa ana sifa kadhaa za kuwa kiongozi wan chi, lakini anakosa vigezo muhimu vya uongozi ambavyo ni Vision, honesty, na integrity. Kwa wale wanaosema Lowassa ni chaguo la Mungu, hakuna sehemu kwenye biblia ambayo inatoa mfano wa mtu anayefanana na Lowassa katika hayo matatu, na kama yupo, tuelezeni ili tuyajadili.

Mtoahabari, hapa umemaliza kila kitu!. Taarifa kuwa Lowassa sio Mmasai nilikuwa nazo ila hazikuwa deep kihivi. Thanks.
Jee wewe mtoa habari unataka mabadiliko ya kweli 2015?. Kama jibu ni ndiyo, then please join the team Lowassa asimamishwe CCM tuende kwenye mabadiliko, hata kama humkubali Lowassa, nakuomba ujinyamazie kama Mzee Mwanakijiji, mtuachie sisi tuendeleze kazi ya kumsafisha mpaka atakate na kumpaka mafuta ang'are na kumeremeta!. Please!.
 
Lowasa ni MMASAI bwana, nasema yeye ni Mmasai. Wanawake wa Kimasai wana tabia kama ya wale wa Kitutsi ya kurudi kutafuta mimba nyumbani halafu huyo Ndosi anaambiwa mimba ni yake! Juzi nilimwona akitajwa kwa cheo kizito tu cha Kimasai.
 
Nasikia anataka kumpa pasi ya kisigino Amani hasa mkimng'ang'ania kwa kigezo cha "zamu ya zanzibar" ila hataki kuwa mgombea mweza kama itakua hivyo,anataka kurudi kumalizia pale alipopatia ile "ajali yake" mashuhuri!
Sasa nimeielewa ile kauli ya Maalim Seif. Kumbe anataka kurudisha fadhila pia. Karume ndie amemfikisha hapo alipo sasa.
 
Mkuu Mtazamo, kiukweli humu ndani sio tuu wengi tunatofautiana mtazamo, uelewa na ufahamu, bali hata imani ya kutokuaminiana!. Kwa watu wanaomfahamu Mzee Mwanakijiji wa ukweli, bado tunamwaminia na ukimuona kimya kwenye issue fulani, ujue ukimya wake una mshindo mkuu, kwa vile Mwanakijiji ni very vocal, akibadili msimamo atasema na sababu zake, ukimya huu ni kutuachia sisi tunaomsafisha Lowassa tuendeleze kazi hii nzuri tuliyoianza ili malengo ya safisha safisha hii yatimie!

Kama ni kweli unaamini Dr. Slaa ndie pekee anayeweza kuleta mageuzi ya kweli hapa nchini, na unampenda kwa dhati, then utamlinda kwa njia zote ili asipotee kabla ya hiyo 2015!. Kuna aina nyingi za upendo moja wapo ni hii " Anayeipenda sana nafsi yake, ataiangamiza, na atakayekubali kuiangamiza nafsi yake ndiye atakayeiokoa"!.

Determinant ya nani atakuwa ndie rais ajaye, lies with CCM candidate!. Kama mgombea wako ni Dr. Slaa, ni washabiki wajinga tuu ndio wataamini Dr. Slaa atapitia njia nyeupe kuingia Ikulu ya Magogoni!. Watu serious wanajua jinsi njia ilivyo ngumu na ilivyojaa miiba!. Hebu imagine chances za Dr. Slaa akisimama na mtu kama Dr. Shein, Dr. Shein atazoa kura zote za compasssion kwa vile Mzee wa watu huyu hawezi hata ku shout!. Just imagine Dr. Slaa anasimamisha na Magufuli unajua nini kitafuatia!. Hivyo determinant ya ushindi lies with mgombea wa CCM na mgombea kipenzi cha watu, kipenzi cha wote, mwenye mvuto wa ajabu, mwenye sura ya kupendeza, mwenye usafi usiokuwa na mashaka, mwenye utakatifu wa kukaribiana na Bwana wetu Yesu Kristo ni Edward Lowassa pekee!. Huyu ndie mkombozi wa taifa letu aliyebakia kwenye safu ya CCM!, tumpiganie yeye asimamishwe, tupate ukombozi wa kweli!

Pasco (wajf)

pasco, hapo kwenye nyekundu nimecheka kama chizi.

infact wadadavuaji kama mwanakijiji inawezekana wako kimya kwa vile they have found out what you are up to......
good luck with your hitherto successful research work.
 
Lowasa ni MMASAI bwana, nasema yeye ni Mmasai. Wanawake wa Kimasai wana tabia kama ya wale wa Kitutsi ya kurudi kutafuta mimba nyumbani halafu huyo Ndosi anaambiwa mimba ni yake! Juzi nilimwona akitajwa kwa cheo kizito tu cha Kimasai.
WildCard, kiukweli Wamasai ndilo kabila linaloongoza kwa birth controll, ile tabia ya watu wa rika moja kujivinjari na wake wa wenzao kwa kuchomeka mkuki mlangoni ni ya kweli, ila mimba itakayoingia ni ile tuu ya mwenye mke!.

Kwa vile Baba Mzazi wa Lowassa, Mzee Ndossi alioa mwanamke wa Kimasai, then wanawake wa Kimasai sio wahuni, sio mala.. wa kuwalangua waume zao ukiondoa ile mila ya kujivinjari, hivyo naamini watoto wote waliozaliwa kwenye familia hiyo ni damu ya Ndossi!. Wanawake wenye tabia ya kuchepuka na kutengeneza katoto ka nje ni Wachagga!.
 
Pasco,

Pamoja. Nimekupata. Tulitulize kisha tuanze tena karibu na uchaguzi wa chama, pending na matokeo....yakiwa kama tulivopanga basi tuendelee kumpigia debe 2014 Mungu akipenda.

Inshallah!

Ngoja niadjust kiti nilala ELairline. (Edson najua utasema tu!)

nyie watu wawili nyie sijui vipi? yaani na uelewa wenu wote huo mmetekwa na lowassa?? ...anayway nyie endeleeni lakini nawambia huyu hashiki urais wa nchi hii.....hili nawambia kabisa...we psco nani alikwambia lowasa ni chaguo la Mungu? Mungu yupi wewe unayemzungumzia....hivi lowasa ana tofauti gani na hili juha muliloinstall hapo magogoni?

narudia tena lowasa hatakuwa rais wa nchi hii subirini kwani june mbali?? nyie endeleeni kukunjua viti mlale huko Elairline siku ikifika mtashindwa hata kwenda kutoa heshima za mwisho...
 
Edison, japo ni kweli JK alikuwa ni chaguo la mungu, Lowassa ndio cha Mungu!. Tofautisha!.

wewe itabidi nikutafutie mda tuonane nikifika huko..sitakualika pale club itabidi tuonanie eneo jingine....halafu ile tabia yako ya kualikwa mahali halafu unajilipia gharama ilumuudhi yule jamaa sana siku ile pale kanda ya kati...ulimuona alivyoshangaa...

uliweza kujilipia bill japo ulialikwa lakini leo ile dhamira huna tena unanunulika kirahisi sana....hivi umetwa na nini? huyu ENL amekuahidi ee!!
 
Back
Top Bottom