Kwa hiyo bwana mkubwa ukweli ni kwamba Amir Jamal alizikwa kwa taratibu zote za kiislam...japo hatukuona akizikwa kama tulivyoona kwa marehemu Julius Nyerere ama Edward Sokoine, kwanini kwa Amiri Jamali tunaamini kwa Daudi Balali tunagoma kuamini?
Mkuu Kim Kardash,
Kulinganisha mfano wa Mzee Amir Jamal na Daudi Ballali, ni case mbili tofauti sana ambazo hazifanani kabisa. Kuna utata mkubwa sana au wingu zito kwenye kifo cha Ballali.
Kwanza Amir Jamal alipokuwa anafariki alishaondoka serikalini na alikuwa anaishi maisha ya kawaida, so, whether alitaka kuzikwa Canada au popote pale hilo haliwahusu wa-Tanzania. Ballali wakati anafariki kulikuwa na sakata la EPA, Twin Tower pamoja na Meremeta na madudu mengine ya ufisadi.
Mpaka leo hii ukienda BOT kuwauliza Ballali alikuwa amelazwa Hosp gani, hawakupi jibu, kwamba ni nani alikuwa analipa gharama za matibabu hupewi jibu. Lakini mpaka wakati akiwa mgonjwa alikuwa bado ni Gavana na hata barua ya kujiuzulu aliandika akiwa Hosp, so BOT walikuwa bado wanamlipa mshahara wake na pia kumlipia matibabu. Kuna kipindi BOT iliulizwa ikarusha mpira serikalini [Wizara ya Fedha], ambao nao pia walikana kujibu lolote kwamba iulizwe BOT.
Utata uliongezeka pale waliposema mwili haurudi, na pia mazishi ni ya faragha na hakuna ambaye ataruhusiwa kuuona mwili wa marehemu. Ukijumlisha hayo yote na sintojua ya kwamba Ballali alikuwa anatibiwa wapi, nani alilipa bills zake hosp na hata alikofia nako ni utata tupu. Wapo wanaosema alifia Boston, wengine wanasema alifia nyumbani baada ya kuwa discharged toka hospitalini ingawa hawasemi ni nyumbani kwake ya wapi [Maryland?], wengine wanasema alifia DC [Georgetown University Hosp]. Ndio maana watu wanakuwa na imani haba.
Tomasso alimwambia Yesu kwamba hawezi kuamini mpaka amshike mkono na ku-feel yale matobo ambayo misumari ilipita. Hiyo ndio njia pekee ya kuondoa wasiwasi. So, kama kuna mtu ana mashaka kwamba Ballali yuko hai, ana haki kwa sababu ya huo ukungu na kama kuna mtu anaamini kwamba Ballali alikufa naye ana haki, maana hakuna ambaye ana uhakika 100% kwamba ni kweli Ballali alikufa kwa kuwa hawakuona mwili wake.
Ni hali ya kawaida kwa "person of interest" anapokufa, watu kutaka kuwa na uhakika beyond reasonable doubt kwamba ni kweli huyu shahidi namba moja wa kesi kubwa za kifisadi zilizotikisa nchi na chama tawala amekufa au ndo tunadanganywa. Ballali was a person of interest wakati mauti yanamkuta wakati Amir Jamal was not. Ndio maana Ballali alipoondoka Tanzania kulikuwa na speculation kwamba kalishwa sumu, mara hatarudi tena Bongo na mengineyo mengi sana.