Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Huyu jamaa jusa, tena mwarabu na kauli zake..huwaga ananiacha hooiiii..ila i met someone ambae aliniambia kua ..the only problem ya Muungaho wetu ni OMAN, nchii hii ya kiarabu inamapandikizi yake kule zenji na haitaki kuuona muungano ukiendelea..
 
Huwa najiuliza maswali hivi ni kwa nini ROSTAM pamoja na ujambazi wote anaoufanya kwa rasilimali zetu ni kwa nini serikali haimugusi! Nimepata majibu, this man ni DUDE! Sure Watanzania tumeisha! Mashetani wanatuchezea.
 
hii ni hatari ndo maana pinda alisema kuwa kuna kamtandao ka watu wachache wameamua kuziteka rasilimali zetu siku kakiguswa basi serikali yote inatetetereka

Hako kamtandao anakoongelea Pinda anakajua sana kwa sabbabu yeye Pinda ni TIS pia. Kwa maana hiyo vitu vingi vinavyotendeka hapa Tanania anavijua kuanzia wanyama kutoroshwa, siri nzito ya uhusiano mbaya kati ya rais na mkuu wa majeshi aliyepita. Cha ajabu mamabo yanaharibika wakati anayaona.
Kwa kweli usalama wa Taifa la Tanzania ni chombo kilichofeli vibaya sana na kimechangia sana hali kuwa mbaya kiasi hiki
 
Binafsi haikuniingia akilini eti Hilary Clinton amekuja Tanzania just kuwapongeza Symbion kwa uwekezaji kiduuuuuuuuuchu kwenye nishati. Na Symbion hao hao wanenunua miambo ya Dowans, mhhhhh! Sasa nimeelewa. Kumbe alikuja kuangalia kazi yao inayofanywa na RA hapa Tanzania. Oooooh LORD have mercy on us, tuokoe na miokono ya hawa wazungu wasiopenda maendeleo yetu. Binafsi moyoni mwangu natamani tuwe na urafiki na Wachina zaidi kuliko Wamarekani na Waingereza. Nasikia kuna azimio la siri kati ya Wamarekani na washirika wake wa ulaya kuwa hitatokea Afrika iendelee, kwahiyo ni bora tukawa na urafiki na Wachina. Mwandishi Ndambisa Moyo kwenye kitabu chake cha "Winner Take All" anasema Wachina wana nafuu kwani wanakujakuwekeza, wanachukua kiasi na nchi husika inanufaika. Kitu hiki kinawaudhi sana Wamarekani na wanawapiga vita sana Wachina kwani wanaona kuwa wanaweza kuwakomboa Waafrika.
 
Samahani kwa kuingilia kati,unataka watu washindane kutunga hadithi au kutoa hoja?naona kama kuna kitu unachanganya,sorry for interruption lakini,endeleeni kulumbana na jamaa yako..

Hawana ujamaa hawa mkuu!
 
Sasa kama chadema watachukua nchi 2015 hali itakuwaje? Hawa jamaa wataenda wapi?

Kuna machache yaliyoandikwa Rostam yanaukweli ndani yake lakini kuhusu kuwa yeye ni wakala wa CIA hizo ni hadith za Elfu Lela Ulela au mambo ya cindellera Marekani hawana muda wa kutrain mtu asiye smart kama Rostam mwenye kuiba mchana kweupe. Nimeishi na kusoma Marekani najua CIA angalau kidogo wanatafuta watu wa namna gani ukizingatia ilibidi nisome masomo kwa kulipiwa na serikali ya Marekani baada ya kujiunga na jeshi la maji la Marekani sikutaka mkopo nilitaka kusoma bure na kutuma pesa nyumbani za mkupuo kusaidia ndugu baada ya kujiunga na Navy.

Kama mtanzania niongeaye kiswahili na kiingereza CIA waliniapproach hapo Michigan na Baadaye San Diego California kwenye mafunzo ya navy wakitaka kutrain waafrika kwenda afrika masharik makao makuu yakiwa Nairobi kusaidia vita dhidi ya ugaidi ile mitihani yao ya usaili, background check na government clearance yao ni ya hali ya juu Rostam hawezi kupita kwa vile ninavyomfahamu CIA hawaendi kutafuta vichwa maji ukisikia mtu ni undercover wa CIA ni kichwa sio mtu hohe hahe na mwenye mazingaombwe mengi kama Rostam

Kwa bahati mbaya au nzuri mie sikufanikiwa maana nilikataa kwa kuogopa kuweza kutumika kuhujumu nchi yangu mkenya mmoja alibahatika kuchukuliwa na CIA ni kijana wa Mombassa anaongea lugha nne yaani Kiingereza, kiswahili, kiarabu na kifarsi kugha ya wairani yule mkenya ni kichwa naamini atafanya kazi vizuri ya CIA na sio kichwa maji Rostam mwenye usmart wa kuibia watanzania kupitia CCM.

Chadema wakichukua nchi hali itakuwa shwari na hakuna tatizo kwani huko Kenya, Malawi, Zambia, na Burundi wapinzani walipochukua nchi mambo yalienda kawaida ingawa kuna mafia wengi tu kama Rostam, Karume na wengine
 
Ndugu yetu Hutaki Unaacha, kwanza asante kwa muendelezo huu, pili naweza kukubalia yote uliyoyasema kwa sababu mengi siyajui japo baadhi niliwahi kuyasoma katika zile dossier za Mzee Mwanakijiji ambazo alizitoa kwa subscription.

Ila hili la ubunge wa Tom hoja zako si za kweli. Ukweli kuhusu ubunge wa Tom ni juhudi binafsi za baba mtu kujaribu kuestablish his legacy baada ya yeye kuondoka ili angalau angalau jina lake lisi persish jumla kwenye power corridors kama Mwinyi, Karume, Kawawa etc.

Hivyo kabla ya uchaguzi alitumia fedha nyingi kuwekeza kwenye kilimo Mbeya huku akimgroom mwanaye kwenye politics huku akisaidiwa sana na vijana wa idara!.

Kusema ukweli lobbying ya hali ya juu ilifanyika ili kijana abebwe na vikao vya juu ila kwa vile Mpesya alisha cry foul ndipo aibu ikawashika na kuamua kumtosa mtoto wa Mzee jambo ambalo lilimsononesha sana baba.

Ndipo kwa kutumia utaratibu wa scrach my back and I'll scrach yours kwa huko walikotoka, then It was time to pay off kwa Mzee kumuomba muungwana ambebe kijana wake hata kwa mbeleko tuu ili kumsetiri aibu ya kushindwa!. Ndipo akamteua!.

Si kweli uteuzi ule ulikuwa ni asante kwa kuiba siri za kambi kwa sababu its obviously Waarabu wa Pemba hujuana kwa Vilemba with reference ya siasa za Mbeya, Baba na mwana walikuwa lazima wawe kambi moja ya mwenzao Prof. lakini ili kuua so, ilimbidi baba amtume mwana kule na yeye abaki kambi ya Jk hivyo hakuna cha wizi wa siri wala nini!.

Nasisitiza ubunge wa kijana yule sio ubunge wa shukrani kwa kazi yoyote nzuri bali ni ubunge wa hisani tuu!. Ungekuwa wa shukrani ungeandamana na uteuzi wa ujumbe wa bodi kwenye bodi zozote nono nono ili kijana ajilie vinono!.

Wanasema ukishikwa, shikamana na ukibebwa, bebeka!. Kijana mpaka kabebwa habebeki aingekuwa ni shukranisi angeendelea kuning'inizwa huko huko juu alikopandishwa?. Mbona sasa ameachwa akaporomoka?!. Sio shukrani ni hisani tuu!.


....Tom??? who is he?
 
SASA MTAONA HUO UKANDA MNAOPIGIA KELELE MWISHO WENU NI MBAYA KWA CCM.LOWASA,MBOWE,SLAA WOTE NI WA KASKAZINI SASA CCM MNA LENU?ANNA MAKINDA MAZAO YA LOWASA NA CHENGE NA ROSTAM,USALAMA WA TAIFA 95% UKIWAONDOA AKINA OTHMAN NI MATUNDA YA ROSTAM SASA MTAELEWA KUWA KASKAZINI THIS TIME NI YAO POLENI MNOCHEZA NGOMA MSIOIJUWA HASWA CCM MBUZI KAMA WEWE LITZ NGOMA INOGILEUOTE=Ritz;3105673]Chadema kuchukuwa nchi matope yatageuka blue band![/QUOTE]
 
Bado kuna watu mnahangaika na hii story ambayo wakati wake umepita kwa kuwa ililetwa hapa purposely kipindi kile lowassa akitaka kujitutumua kupambana na mwenyekiti kwenye kikao cha nec kilichomchinja mbaya kwa kuamua kwamba wana ccm watatakiwa kuchagua ama kugombea ubunge au ujumbe wa vikao vya chama kama U NEC n.k. ya kwamba ukigombea ubunge huruhusiwi kuwa mjumbe wa nec and vice versa
 
aisee safi sana imependeza tunashukuru kwa ukweli wako.. Umeiweka serikali NAKED
 
Back
Top Bottom