Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

nasikia anajiita H1NI siku hizi da nilivyoiona thread nikajua jamaa kaludi ha ha ha ha ha jamaa ni legend kwa huku jamii forum yeye pamoja na LALA 1 wa kule MMU
 
Huyu jamaa kakimbilia wapi jamani mbona tunamuhitaji kwa kipindi hiki
 
Rostam aweza kuwa mtu hatari, mwenye kuzichezea siasa za Tanzania. Huyu akiwa pale LSE UK, alijenga urafiki mkubwa sana na binti wa mkubwa mmoja na muhimu katika Tehran (siasa za Iran). Haikufahamika kwa haraka ni nini alichokuwa akikitafuta kwa huyo binti na nani alimtuma ajenge huo urafiki ghafla kiasi hicho. Hili ninalolisema kwa sasa hata Lowassa hawezi kulifahamu.

Ni vigumu kuamini kuwa, Serikali ya Marekani imegharamia masomo ya Rostam LSE (baada ya hii task) na hii serikali kupitia Prof mmoja anayefundisha chuo kikuu kimoja UK huku akiwa ni mfanyakazi wa CIA iliweza kufanikisha urafiki mkubwa wa Rostam na huyu binti huku yeye (Prof) akiwaachia maelekezo vijana wa CIA baadhi kum-monitor Rostam na hatimaye urafiki ukawa mkubwa sana kiasi kwamba ukaweza kumfanya Rostam akubalike na Tehran.

Kwa udhamini na wito kutoka serikali ya US, Rostam akawa anakwenda mafunzo mahsusi ya ki-usalama marekani na huko alikutana na watu wengi sana muhimu wakiwemo wamiliki wa Symbion. Oesa za Kagoda ni msamaha wa deni lililofanikishwa na ushawishi wake pale Tehran.


Kwa bahati mbaya sana hata Mariam (mke wa Rostam) hakuufahamu uhusiano ule akifikiri ni mapenzi mpaka pale alipojua vinginevyo (ingawa hawezi kujua behind the scene kuna nini). Malengo ya Marekani na huu urafiki (Rostam-Tehran) bado yako palepale na nilipokutana na rafiki yangu (huyu aliweza kufanya kazi nzuri sana na Shah Riza kule Middle East) wa siku nyingi sana pale Boston, akanihakikishia kuwa lengo lilipangwa kutimia 2018 au 2022 hivi!. Kule Saudi Arabia na sehemu nyinginezo ameweza kutumiwa sana na hawa '‘mabosi'' wake kwenye masuala ya biashara.

Rostam anafanya kazi kubwa na nyingi za kibiashara na kisiasa na CIA kama agent wao muhimu sana Afrika huku yeye akisaidiana na mtandao wa CIA kule South Africa na ku-control sehemu kubwa Afrika Mashariki na Kati na sehemu nyingine za afrika ambazo US itakuwa na maslahi nazo.

Mambo machache aliyoweza kufanikisha ni pamoja na kumfikisha Raila hapo alipo, mikataba ya kimaslahi na Salva Kiir achilia mikono ya Rwanda na Uganda kule Congo, na Madagascar

Wakati Bush amekuja Tanzania. Kule Arusha, viongozi wa makampuni makubwa yanayomiliki migodi mikubwa ambayo Bush, US na CIA ina maslahi nayo kutoka karibu kila kona ya dunia walikusanyika na walielezea ni kwanini biashara haiendi vizuri.


Hakuna mtanzania yeyote Yule aliyehudhuria except Rostam. Nani alimwalika na alihudhuria akitokea wapi?! Pale waliazimia mambo makubwa na ya hatari sana. Rostam anajua vizuri what happened na maazimio yale yalilenga nini.

Lowassa kaingia kichwa kichwa na huenda pupa yake ya kwenda Ikulu ndiyo iliyotoa mwanya kwa Rostam Aziz kujitokeza tena kwenye siasa za Tanzania. Ni ukweli usiopingika kwamba kama Lowasa atakiwa Rais wa nchi hii ( Mungu atuepushie mbali) atakuwa cover tu bali hatma ya nchi hii itakuwa mikononi mwa Rostam ambaye naye anatumika na CIA.


Ni wakati sasa Watanzania na hasa wana CCM kuliona hili ili nchi yetu isiingie kwenye midomo ya Walafi hasa ikizingatiwa kuwa tunaingia kwenye uchumi wa gesi.

 
Alafu mi nilidhani aliishakufaga zamani kwa laana za watz. INASEMEKANA NI EITHER MSUKUMA AU MNYAMWEZI!!!!.....Wasukuma na wanyamwezi ndo wanajua rostam amewahi kuwatetea vipi akiwa ndani ya bunge.
"Hatutamkataa mtu kwa sababu ya rangi au dini au kabila lake, SA hatukuwapinga na kuwakataa makaburu kwa sababu ya rangi yao ila ni kwa sababu ya ubaguzi wao.....MWL. NYERERE
Lkn pia hatutamkubali mtu kwa sababu ya rangi yake, kabila lake, dini yake ama fedha yake km lowasa na rostamu
Hatutamkataa rstamu kwa sababu ya rangi yake ila tunamkataa kwa sababu ya UFISADI WAKE!
 
Back
Top Bottom