Story za huyu jamaa ni za kwenda kupigia soga kwenye vijiwe vya kahawa labda, zimejaa uzushi na exaggeration za hali ya juu lakini bahati mbaya sana ndio style ya maisha yetu wabongo toka huu mtandao wa kina kikwete uingie madarakani, Rostam na wenzake waliposhika hatamu za uongozi walinunua vyombo vyote vya habari na kuanzisha style ya kuongoza nchi kwa makala za dizaini hii kwenye magazeti, wakafanikiwa kutulemaza na sasa tumelemaa ndio mana watu kama hawa wanaoutumia mwanya huo kutuingizia mabo vichwani mwetu huku wakielewa mtanzania ukimuingizia jambo kichwani na akaliamini kulitoa ni kazi ngumu sana,jamaa anaonekana kufanikiwa kuwapata baadhi yetu humu lakini naamini hatawapata wote kwa wakati wote bali wachache kwa wakati wote au wote (kasoro mimi) kwa wakati fulani!Naelewa CIA wanavyoendesha operation zao,siwezi kuingizwa choo cha stendi kirahisi namna hii aisee!
mi sitaki na nimeamua kuuacha uongo na uzushi huu ulioandaliwa kwa utaalamu wa hali ya juu na mtu anaeijua kazi yake!tumsubiri yule jamaa yake "mtoa tetesi" nae aje na makala yake!