Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Rostam anajua anachofanya Tanzania na East Africa kwa ujumla ndio maana pia yule mtaalamu wa kuchakachua kura wa IT kutoka Usalama wa Taifa walimpeleka Nairobi kumsaidia Kibaki na sasa wanata Raila naye ale bata kwa kipindi kijacho!

Lowassa anajua bila kuwa na Rostam bega kwa bega hawezi kuukwaa Urais maana anachotaka Rostam na Lowassa kwa sasa ni biashara ya Mafuta na Uranium tu pale Tanganyika! Tumekwiishaaaa.....................!! Rostam ana watu mpaka kwenye mtandao wa Usalama utamwambia nini.........??
 
namngojea zaidi UCHAMBUZI WA EDWARD. NAAMINI MCHAMBUZI SWALA LA MKATABA WA MOU UTAFAFANULIWA. UMEASISIWA NA CIA,KUTUNGWA NA NATO NA KUTUMIWA MZEE UFISADI YAANI EL NA HATIMAE MAKANISA YANALINYONYA TAIFA KWA MKTABA HATARI NA WA KINYONYAJI KWA TAIFA LETU CHANGA.
Wewe nawe! Ushaibuka na udini! Yaani unampangia hadi sentensi za kuandika!
 
Pamoja na kushtushwa na taarifa hizi lakini bandugu na Adm nzima ya JF,hapa tunaanza kugusa na maslahi ya Marekani na for sure lazima watafuatilia effect ya taarifa hizi! Ninavyofahamu wanaweza kujaribu hata kuingilia mtandao huu kwa maslahi yao! Naamini JF imekomaa sasa wataweza kudetect any threat! Umakini uongezeke kidogo maana haya ni kwa maslahi ya taifa hili na kumsaidia Rais wetu ajue hali ilivyo kwa mapana yake.
hapo kwenye red umeinajisi comment yako yote!!rudia kusoma utaona sehemu ambapo jk alipokea briefcase zilizojaa dola na hutaji unaacha anauliza mr.president alizipeleka wapi hizo fedha?!
 
ukiunganisha dots katika thread hii unaona kuna watu wanaunganishwa kwamba wanaweza kuunda mtandao mmoja lakini kiukweli hawa watu hawawezi kukaa meza moja na kuaminiana kwa asilimia 100 ili kuweka mpango mkakati mkubwa kama huu kutokana na historia ya siasa za nchi yetu hasa tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza 1992, bila kujali watu hao wako chama kimoja au la. kuuaminisha uuma kwamba sasa kambi hizo zinaaminiana si kweli
Kwa masual yanayohusu intelijensia, futa hiyo kauli yako kabisa!, nasikitika huenda hujui vyema kuwa watu wana kazi mbilimbili au zaidi!.
Usiwatazame watu kwa nje tu, jaribu kutumia jicho la 3!

Mimi nasema tuombe Mungu walau nchi iwe salama(bila vita), lakini vinginevyo, kwa habari ya rasilimali, we are doomed!...huh!

 
Aiseee!.... Umerejea tena na pumba zako, Unachonishangaza ni kwamba huna point wala mpangilio katika uandishi wako. Hata hivyo unatimiza wajibu kama unavyotumwa.
 
kwa nini tunakubaliana na uongo huu mkubwa basi weredi wetu hauna maarifa ya uchambuzi wa kina katika masuala ya kisiasa.
 
wengi tumetekwa nyara na hii mada ambayo kwa undani wake haina jipya bali utunzi mahili wa hadithi njoo utamu kolea. maeneo mengi hujanishawishi kwamba unachoandika kina ukweli
 
Aiseee!.... Umerejea tena na pumba zako, Unachonishangaza ni kwamba huna point wala mpangilio katika uandishi wako. Hata hivyo unatimiza wajibu kama unavyotumwa.
kama kweli ni pumba basi sisi tunachukua nafasi ya Nguruwe, ni chakula kizuri tu kwetu. Hivi unafikiri anapomtaja Mwamunyange kumdharau Jakaya anataka sifa?
 
kwa nini tunakubaliana na uongo huu mkubwa basi weredi wetu hauna maarifa ya uchambuzi wa kina katika masuala ya kisiasa.
Hakuna mtu ANAYEUAMINI bali watu wote humu ndani wanajaribu kuunganisha vifundo ili kama kweli kuna ukweli ndani yake mnyororo unaoangamiza nchi yetu ujulikane umeanzia wapi na kuishia wapi. Duniani hakuna uzushi mtupu lazima ndani yake kuwe na ukweli fulani.
 
kama ingekuwa movie ungepata mapato kidogo kazi yako haina mtiririko tangu part I. kuna kipindi umewahusisha baadhi ya wachezaji wa movie yako lakini hatujawaona wakiwa sehemu ya wachezaji kwenye DVD uliotuwekea kutazama mwishowe ukarukia wachezaji wapya ambao mwanzo hukuwataja na ndio umewapa maelezo marefu. shit
 
Ukiona part II haina kile ambacho nilitarajia kwamba ingeziba mianya ya mapungufu ya part I ulitakiwa kumpelekea mtaalam wa uchambuzi kufanya editing na kukushauri.
 
Umeandika kama mhandisi anayesimamia matengenezo ya barabara yenye kona nyingi ambayo inamsumbua kurekebisha kwa sababu ya ukosefu wa vifaa. katafute vifaa ndio urejee tena na habari ya kweli.
 
Tom Apson si mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa haingii akilini kwamba angejua mambo ya msingi kupitia kwa baba yake eti tu kwa sababu ni mtoto wa aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Idara hiyo ndugu Apson. Tuwe makini na maneno ya mitaani

Japo sikubali wala kukataa maoni yako, natoa tahadhari.
Mambo ya baba mara nyingi mama na hata watoto wakubwa huweza kuyajua.
Haitakuwa ajabu kwa Tom kujua mambo ya Mzee wake -Apson.
 
Tom apson mwenyewe alikuwa mwanamtandao hakuteuliwa kwa sababu ya nguvu ya baba yake hapo pia umekosea. Taarifa kama hizi uwe unaandika kwa makini kwa sababu tupo humu pia tunaofahamu ukweli kwa upande mwingine.

asante kwa kutujuza lakini epuka kuweka uwongo kwenye taarifa muhimu kama hii.
 
Back
Top Bottom