Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Japo sikubali wala kukataa maoni yako, natoa tahadhari.
Mambo ya baba mara nyingi mama na hata watoto wakubwa huweza kuyajua.
Haitakuwa ajabu kwa Tom kujua mambo ya Mzee wake -Apson.

kwa maneno mengine tunakiri kwamba mzee Apson hakuwa jasusi aliyekomaa hadi alikuwa anakaa kitako na mtoto wake Tom Apson kumpa siri za kazi yake. Hii inafaa tuwe na thread yake kwa wenye ushaidi. kwa wanaomjua mzee Apson jambo hili wanasema ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Huyu mzee ni mmoja wa majasusi wa kuogopwa sana hata CIA na MOSARD ya Israel wanadaiwa walimwogopa sana kipindi chake. kama hii ni kweli huu utakuwa uongo wa kumpaka matope
 
kama kweli ni pumba basi sisi tunachukua nafasi ya Nguruwe, ni chakula kizuri tu kwetu. Hivi unafikiri anapomtaja Mwamunyange kumdharau Jakaya anataka sifa?

we unafikiri hizi tamthilia za HUTAKI UNAACHA ZIMEANZA leo?Alianza na hii hapo chini kwanza,alipoona haikupata mapokezi yaliyostahili akaihariri upya ndio akaibuka na huu mtiririko!msome alivyoanza halafu kaa chini uunganishe dots uone contradictions zake,yalekea anasahu upesi sana...


Hutaki Unaacha

Membe be careful AU



Mh waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hajamfahamu adui yake no 1. Hii inatokana na ukweli kuwa vita anayopigana inamhusisha yeye na adui asiowajua. Membe anaamini adui zake wakubwa ni Rostam na Edward.Amepotoka.

Membe napenda nikufahamishe ya kuwa, usipoangalia, yatakupata makubwa zaidi ya yale yaliyompata Harrison. Unapigana na watu hatari na wanaotumia akili nyingi sana kwenye game hili la siasa.

Katika baraza la kwanza la JK uliteuliwa kuwa deputy wa home affairs. Ulilalamika sana kwa JK. SMS ya kulalamika kwako uliyomtumia JK, iliwafikia Rostam na Edward at the same time bila wewe kufahamu. Tafakari kwanza!

Richmond haijaletwa na Rostam wala Edward nchini. Wewe unafahamu vyema jinsi JK alivyocheza dili la Richmond kishamba akishirikiana na Gire baada ya mazungumzo yao huko U.S. Baada ya mambo kuharibika ndipo rostam na edward wakashirikishwa. Unafahamu vizuri role aliyoicheza rostam kuhakikisha angalau dowans inazaliwa ili kumwokoa JK.Ya lowassa kujiuzulu unayafahamu vizuri sana sitaki kuyazungumzia kwa sasa.

Sitta hakuwahi kuwa rafiki wa Harrison hata siku moja. Alimtumia tu ili kutimiza malengo yake ya kumwondoa Lowassa kwenye nafasi yake. Wewe ndiye uliyekuwa ukiwachonganisha mara kwa mara JK na PM wake Lowassa. Hata nafasi ya nje uliipata kwa jungu kubwa na la ustadi wa hali ya juu ulilochezewa na vijana wawili wa usalama wa taifa kwa kumchafua Lowassa. JK akaanza kukuamini.Ulicheza vizuri karata kwani ulijua fika jinsi gani sitta alivyomchukia rostam na Lowassa kwa yale waliyomtendea ili asiwe PM na kwa ustadi wa hali ya juu ukamshawishi sitta alitumie bunge ili kumwadhibu lowassa.

Mwakyembe ana ugomvi wa siku nyingi na rostam hata kabla ya JK kuwa rais. Alitumia nafasi hiyo kumnyonga Lowassa na rafiki yake Rostam na kwa bahati mbaya akakiri ndani ya bunge kuwa kuna machafu mengi yameachwa ili kunusuru heshima ya serikali. Kosa kubwa sana kuwahi kufanywa na mtu aliyepitia idara ya usalama wa taifa. Unafahamu vyema kuwa hili kosa ndilo linalomgharimu Harrison huko Appollo. Baada ya Lowassa kuangushwa, ulikumbatiana na Mwakyembe, Rais akawapongeza, mkafurahi, mkabweteka na kumwamini JK. Kosa la pili kubwa.

Kwa bahati mbaya sana ukaungana na Mwakyembe, Mengi, Sitta, na wafuasi wake kwa ajili ya kuutafuta urais tena kwa kumtumia mwanaye Ridhiwani. Hili ni kosa la tatu kubwa kwani ulichanganya kwenye kundi lako watu wasio marafiki wa JK ambao kwa hakika wata-demand umburuze JK mahakamani pindi utakapokuwa rais.

Rostam-JK-lowassa

1. Hawa ni marafiki wakubwa ambao licha ya wawili kuwa nje ya serikali lakini wote watatu wanaendesha serikali na hawasiti 'kuwanyamazisha'' wabaya wao wanaogusa interest zao.Individually wanatofautiana ila wakiwa watatu ni wamoja.Membe naomba ufahamu hili.
2. Wewe ulimtaka sitta awe spika kwa mara nyingine tena. JK alimtaka sitta pia lakini katika kikao cha watatu akakubaliana na pendekezo ingawa kwa shingo upande la Anne kuwa spika.
3. JK atakuwa safe kama lowassa akiwa rais.Hatakuwa safe endapo mmoja wenu atakuwa rais.Anafahamu hili fika.
4. Richmond itarudi bungeni kabla ya 2015.Wakati wa kujadili, wewe na mwakyembe mko tayari kusema ukweli.Ili kuwazima, mwakyembe 'ataondoka' then wewe waweza kufuata!.Haya yatafanywa na umoja wa hawa watatu na si individually
5. Ndani ya CC iliyopita zilipigwa kura za siri ili kumfukuza Lowassa uanachama.Kati ya wajumbe 32, 19 walimsupport lowassa na 13 kwa JK!.Hapa wanaonekana ni wapinzani ingawa wakiwa watatu ni wamoja.
6. JK anaweza kukusikiliza na kujifanya mko pamoja naye. Lengo ni kutaka kujua what's going on in your group ili wawamalize vizuri.
7. JK hakumtaka Bilal, lakini umoja ukalazimisha ndiye awe makamu wa rais. Mkapa alitumwa bila kuelewa.
8. Hawa watatu kwa pamoja walimteua Mkama. Wewe hujui hilo ingawa mwenzako chiligati alishastukia!
9. Membe unafahamu ya kwamba kujivua gamba ni hoja iliyoletwa na rostam kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha watatu hao ili game iishie bungeni kwenye kujadili Richmond upya? Symbion iko nchini Membe. Unajua kaileta nani?. Je, nani kamleta Mama Clinton nchini?
10. Membe muulize Mwandosya akwambie jinsi watatu hawa wanavyomtesa. Umesahau tulipokuwa Marekani jinsi Balali alivyosema kuhusiana na chanzo cha afya yake kuzorota?.
etc, etc, etc, etc

Ushauri wangu kwa Membe:

Be careful sana katika game hili Membe. Kama kweli unautaka urais lazima kwanza uufahamu mchezo unavyokwenda. Wenzako wanacheza game nzito na kisayansi zaidi. Know your enemy first. Na kwa kukusaidia, adui yako namba moja ni huo utatu and not an individual person


​
 
Hapa Jf tuliwahi kuona thread iliyochambua kwa kirefu kwamba Mzee Apson alikuwa hamkubali JK na wachangia walikuwa wengi ajabu leo hii mara kamteua mwanaye Tom Apson mbona taarifa inakatikakatika wengine wakasema RO halikuwa chaguo la mzee Apson lakini leo tena tunaambiwa RO na mzee Apson wako mtandao mmoja. bull shit mnachezea akili zetu
 
kwa maneno mengine tunakiri kwamba mzee Apson hakuwa jasusi aliyekomaa hadi alikuwa anakaa kitako na mtoto wake Tom Apson kumpa siri za kazi yake. Hii inafaa tuwe na thread yake kwa wenye ushaidi. kwa wanaomjua mzee Apson jambo hili wanasema ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Huyu mzee ni mmoja wa majasusi wa kuogopwa sana hata CIA na MOSARD ya Israel wanadaiwa walimwogopa sana kipindi chake. kama hii ni kweli huu utakuwa uongo wa kumpaka matope
Jamani sisi wengine tunachambua vitu tunavyoona vinatufaa na vile tunavyoona tunavitilia mashaka tunandela kuvifanyia uchunguzi. Hii habari ilishatoka na kwa ninavyoijua serikali yetu ni lazima tungeona wametoka kukanusha. kwa mfano hili la Mwamunyange kumdharau Jakaya mimi nalijua Personally. Jamaa huwa akisikia habari za Jakaya anatabasamu kwa dharau!
 
we unafikiri hizi tamthilia za HUTAKI UNAACHA ZIMEANZA leo?Alianza na hii kwanza,alipoona haikupata mapokezi yaliyostahili akaihariri upya ndio akaibuka na huu mtiririko!msome alivyoanza halafu kaa chini uunganishe dots uone contradictions zake,yalekea anasahu upesi sana...
Romantic hakuna mtu anayesema huu ni ukweli wote bali wengi wetu tunaamini kwamba kwenye hii habari kuna UKWELI fulani. Kwa mfano hili la RA kuwa agent wa CIA ndilo lililowafanya watu kama Thomas Nyimbo kuhamia kambi ya Malecela kutoka kambi ya Jakaya. Nyimbo aligombana sana na Jakaya kuhusu RA hadi wakafikia kutupiana maneno mabaya sana. Kwa hiyo kwenye habari hii hili la RA kuwa Agent wa CIA ni la kweli lakini anafanya nini kwa niaba ya CIA hilo ndilo wengine tunalitafakari!

Kumbuka Thomas Nyimbo alikuwa ni mtu wa mawasiliano ndani ya TISS kwa hiyo naye anajua mengi!!
 
Jamani sisi wengine tunachambua vitu tunavyoona vinatufaa na vile tunavyoona tunavitilia mashaka tunandela kuvifanyia uchunguzi. Hii habari ilishatoka na kwa ninavyoijua serikali yetu ni lazima tungeona wametoka kukanusha. kwa mfano hili la Mwamunyange kumdharau Jakaya mimi nalijua Personally. Jamaa huwa akisikia habari za Jakaya anatabasamu kwa dharau!

Ni kutaka kumgombani Davis mwamunyange na Jk na wewe utakuwa uko lile kundi la Omar Shimbo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi mnaosigana jeshini ili kupata mkate wa leo. kwa taarifa yake Davis ana heshima ya kutosha kwa JK na hili mnalifanya kwa malengo yenu. Davis ni mtu wa JK muda mrefu na asifika kuwa Mkuu wa Mjeshi kutoka JKT bila JK na hiyo haijawahi kutokea tangu uhuru ambapo baadhi ya wanajeshi hawakupenda mtu kutoka JKT ndio wanaleta uchonganishi.
 
kama Rostam unamtaja kuwa ni mtu mwenye akili nyingi kiasi hicho basi awe Rais wetu wa Tanzania 2015 bila shaka unachanganya akili nyingi na ujanjaujanja unaopata kinga ya fedha alizonazo mtu kutekeleza malengo yake.
Hivi kwa nini serikali inashindwa kuuzuia ujanja janja wa RA na hizo fedha alizonazo amezitoa wapi kwa biashara ipi, je ni fedha nyingi kiasi gani gani?
 
Romantic hakuna mtu anayesema huu ni ukweli wote bali wengi wetu tunaamini kwamba kwenye hii habari kuna UKWELI fulani. Kwa mfano hili la RA kuwa agent wa CIA ndilo lililowafanya watu kama Thomas Nyimbo kuhamia kambi ya Malecela kutoka kambi ya Jakaya. Nyimbo aligombana sana na Jakaya kuhusu RA hadi wakafikia kutupiana maneno mabaya sana. Kwa hiyo kwenye habari hii hili la RA kuwa Agent wa CIA ni la kweli lakini anafanya nini kwa niaba ya CIA hilo ndilo wengine tunalitafakari!

Kumbuka Thomas Nyimbo alikuwa ni mtu wa mawasiliano ndani ya TISS kwa hiyo naye anajua mengi!!


basi CIA hawana maana basi kwa kumpa RA kuwa agent wao na kashfa zake zote hizo. sitakubaliana hata kidogo na upuuzi huu hata mkisema Thomas Nyimbo alikuwa TISS. Tungesema CIA inamtafuta RA ningekubali. Nani kasema Nyimbo ni msemaji wa TISS tukubali tu hata kwenye mashaka
 
Leo mnatuambia eti fisadi Rostam Azizi ni CIA kwa maana ya agent kwa hiyo siku hizi CIA wanakumbatia mafisadi?
 
Romantic hakuna mtu anayesema huu ni ukweli wote bali wengi wetu tunaamini kwamba kwenye hii habari kuna UKWELI fulani. Kwa mfano hili la RA kuwa agent wa CIA ndilo lililowafanya watu kama Thomas Nyimbo kuhamia kambi ya Malecela kutoka kambi ya Jakaya. Nyimbo aligombana sana na Jakaya kuhusu RA hadi wakafikia kutupiana maneno mabaya sana. Kwa hiyo kwenye habari hii hili la RA kuwa Agent wa CIA ni la kweli lakini anafanya nini kwa niaba ya CIA hilo ndilo wengine tunalitafakari!

Kumbuka Thomas Nyimbo alikuwa ni mtu wa mawasiliano ndani ya TISS kwa hiyo naye anajua mengi!!

jamani watz wenzangu achaneni na hadithi za mitaani zenye lengo la create fear isiyokuwepo,Rostam is a dead person politically,hivi huyu mtu angekuwa nayo kweli hiyo miguvu ccm ingeshinda kweli jimbo la igunga??maana ni wazi kina Bashe walisikika wakitamba mpaka mbele ya mukama kwamba "wameamua" ccm ipoteze jimbo ili kurejesha heshima yao na ya bosi wao,unadhani mtu mwenye nguvu kama hizi tunazoaminishwa hapa angeshindwa kulipata jimbo la pahala alipozaliwa an kukulia na zaidi amekua mbunge na mfadhili mkubwa wa jimbo hilo for years????kuna maswali mengi kuliko majibu hapa,na je mtu kama zakia ambae alipata kuwa bibi yake alikua hazijui nguvu za "CIA" agent huyu mpaka amshambulie hadharani siku ile ndani ya cc,hapa nchini panakuwaga na uzushi mwigi sana hata mzee mengi labda wengine mlikua wadogo imeshawahi kudaiwa nae ni agent wa CIA anatumiwa na marekani kuua ujamaa!
 
Rostam Aziz ana asili ya Teheran - Iran na ndugu zake wengi wako huko Iran akiwa anatoka kwenye falimia ya ma-sheriff asili yao huko Iran kuna mji ambao watu hufika kwa swala maalum kwani kuna imam mmoja maarufu aliyetokea kwenye ukoo wao hufanyika mji huo. kusema anajenga urafiki na binti wa mkubwa wa huko it's obvious. Rostam anajulikana kwa mabaya yake na mazuri yake kutegemeana na dhamira yake.
 
Hivi kwa nini serikali inashindwa kuuzuia ujanja janja wa RA na hizo fedha alizonazo amezitoa wapi kwa biashara ipi, je ni fedha nyingi kiasi gani gani?

serikali imeshamdhibiti ndio mana unaona ana tapa tapa kutuma watu humu kuja create fear,hizo zote ni strategy kwani unadhani haingii humu na kuijua nguvu ya jf?anajaribu kuitumia nguvu hiyo kwa maslahi yake!na yeye kama mfanyabiashara yeyote yule unadhani anapata usingizi saa hizi?anaumiza kichwa kwa sababu hajui mtawala gani ataingia ikulu baada ya jk na biashara zake zitakuaje ndio maana anahangaika kila kona,mara cuf kupandikiza watu wa kumlinda na biashara zake mara cdm n.k.
 
Hutaki Unaacha.
You are more than a normal GreatThinker, You are beyond tommorow GreatThinker.
 
Acheni wasiwasi, hakuna ambacho kinasemwa hapa ambacho hakijulikani in the corridors of power za Tanzania. Na kwa wale wasomaji wa muda mrefu wa JF wanaweza kukumbuka mengi humu yameshasemwa hadi yamechosha. "Hutaki Unaacha" ameyaweka kwa mtiririko wake wa asili na kuunganisha. Mada hii itakuwepo na itaendelea kusoma JF is where "where we dare to talk openly"... just returning to our roots!

Jukumu la mwenye akili ni kujua hesabu za MAGAZIJUTO!

nakubaliana na wewe, ila nchi hii inahitaji mapinduzi ya kifikra zaidi kuliko mengineyo
 
Rostam Aziz ana asili ya Teheran - Iran na ndugu zake wengi wako huko Iran akiwa anatoka kwenye falimia ya ma-sheriff asili yao huko Iran kuna mji ambao watu hufika kwa swala maalum kwani kuna imam mmoja maarufu aliyetokea kwenye ukoo wao hufanyika mji huo. kusema anajenga urafiki na binti wa mkubwa wa huko it's obvious. Rostam anajulikana kwa mabaya yake na mazuri yake kutegemeana na dhamira yake.

waeleze hii watu wengi hawaijui,wengi wanadhani jamaa ni muarabu wa yemen labda kama kina bakhresa,rostam ni mburushi,na waburushi ni watu wa iran,wanapatikana kwa hapa africa mashariki usangu(mbeya)ambako wako wajomba zake rostam kina Mehrab na kina mulla (yule m/kiti wa ccm mbeya)na Igunga(Tabora)na wengine wapo sehemu moja huko uganda jina nimelisahau!
 
Si kwamba CIA wanakumbatia mafisadi au nini. Kuna wakati CIA wanatumia watu fulani ambao either watakua wamewaandaa wao au ni wafanyabiashara wakubwa kuwa "Contractor" wao kwenye various operations. Hawa watu wanakuwa si waajiliwa wa moja kwa moja wa CIA, ila wanakuwa for special au specific tasks. Ukipata muda, soma confession of an economic hitman utaelewa, au soma historia ya vita ya Balkan. Mimi sishangai kwa RA kuwa agent.

Pia, kwa nchi kama Tz ambayo ina various invaluable resources, lazima CIA watakuwa macho na nchi yetu na ndio maana wakawa wanataka mfumo wa ulinzi ubadilike.
 
unadhani ukitaja majina ya viongozi wakubwa ndo utatutsha sana tuseme unajua sana mambo ee!huna lolote wewe,story yako feki tu hii.uguza majeraha yako taratibu utapona.
 
Back
Top Bottom