Kikwete kainua uchumi wa Tanzania

Kikwete kainua uchumi wa Tanzania

Inshallah! Kwa nguvu za Allah uchumi utapaa kaa ungo wa gagulo la JK. Watoto wooote ombaomba wadogo hadi miaka minne waliojazana barabarani kila kukicha njia panda zote za Dar watafarijika kwa kupewa lawalawa na tende na JK mwenyewe huku akivinjari kwenye mchuma wake mweusi akitabasamu tabasamu lake ngekewa. Mashaalah!

Hata wakati wa Nyerere walikuwepo, tena bora sasa, wanavaa vizuri, wakati wa Nyere, mama yangu, hata viwalo vilikuwa hamna.
 
Huo ukurusedi wako utaishia huko huko Somalia na Afghanistan na wala hautagusa Tanzania unless kama unataka vijana wa kikurya kure kwenye chesi la wananji wakuangusiege abughirebu yako hadi ushangae

Huna hoja wewe, bora utulie tu!
 
  • GDP per capita ndio mdudu gani?
  • Yaani wanauchumi wetu bado wanatumia kigezo cha nchi ambazo ni industrial?
  • Vya wakulima, wafugaji (wanyama na kuku), wavuvi, waokotaji na wachumaji msituni (wa-Barbaig, kwa mfano) vya kwao havipiti through the "market" ili kubaini kuwa vina thamni gani.
  • Kusema kweli, GDPs za nchi maskini ziko juu!
  • Anayesema kuwa takwimu za CIA huwa zinaaminika duniani, ni mwongo! fanyeni utafiti mjue ukweli zaidi kulikao kutundika "over-loaded statements"!
Kuna ushahidi kemkem, kwa mifano:
  1. CIA walikosea katika kutathimini kunaguka kwa the Soviet Union!
  2. CIA walidanganya ulimwengu kuwa saddam Hussein alikuwa na WMD!
  3. Kwa muda mrefu dunia ilikuwa ikiwaambia kuwa joto linazidi (global warming). lakini wenyewe walikuwa wanakataa!
Hawa wenzetu (USA) wakimpenda kiongozi/nchi watampamba tu kwa ajili ya




  • Anayesema kuwa
Nimezisoma hoja nyingi za watoa hoja na kugundua kitu kimoja kwa wote. Watoa hoja wamekuwa waoga au wamefanya kwa makusudi kutotoa takwimu kwa kile wanachokitetea. Kwa mfano kama kweli unaamini kuwa uchummi umeshuka, basi tupe takwimu.

Kwa ujumla hakuna aliyethubutu kutoa takwimu, na badala yake zikatumika lugha kama, uchumi umeshuka, nenda Barbaige uajionee, usiiamini CIA, hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye maendeleo ni kumfukuza JK, wanauchumi wetu bado wanatumia vigezo vya Industrial countries. n.k. Hata ulinganisho hata wa nchi mbili, tatu za Afrika hakuna aliyefanya. Sasa kama wananchi wako unatarajia tutachagua viongozi wa aina gani? Ngoja nifafanue kidogo h apa chini.

Amini usiami, Tanzania ni moja kati ya nchi zisizoendelea ambayo imepata uaminifu mkubwa sana toka nchi zilizoendelea. Nchi zote zinazoendelea zina matatizo yake. Na nchi inapata umaarufu au maksi za juu jnsi ilvyojipanga kutatua matatizo hayo kwa muda mrefu (long term). Kwa muujibu wa nchi zilizoendelea, Tanzania inafanya vizuri sana katika hilo na ndio maana imepata uaminifu huo.

Kikwete ni kiongozi pekee katika awamu zote, aliyesifiwa na kupongezwa kila aendako nchi za nje. Na kila balozi aondokaye Tanzania, haishi kumwagia sifa Kikwete. Toka katika ukuzaji wa Demokrasia , uchumi, uhuru wa vyombo vya habari na hata uhusiano wa Tanzania na nchi za nje. Na hayo ni maeneo muhimu katika kukuza uchumi. Hata hili la ufisadi wameridhishwa jinsi alivyolishughulikia. Lawama pekee aliyepata kubwa sana ni ile ya mauaji ya ALBINO. Kama kwaida muungwana akikosea, hukubal na kuomba kusahihishwa na msaada ikibidi. Alifanya hivyo.

Mnakumbuka jinsi Mkapa asivyokuwa maarufu nchi za nje. Nakumbuka baada ya yale mauaji ya Pemba alikutana na Tim Sebastian katika HARD TALKS. Ukweli nilimuonea huruma, maana alipaniki mpaka akavyonya. Sebastian alitulia na kumuuliza, naona Rais Umekasirika sana? Kweli alijihisi kuwa mkosefu au kuchukua hatua mbaya dhidi ya wananchi wake, na ndio maana alikuwa na hasira kama Shimon Perez alivyojibiwa na Rais Turkey Bwana Erdogan. Mbaya zaidi kwa vile si muungwana hakukubali kosa.

Mkulo alipotamka kuwa uchumi wa Tanzania utapaa kama ndege wengi waliona Hadithi. Sasa wale waziitazo hizo kuwa ni ndoto za mchana, zimekuwa kweli. Angalia Tanzania iliyekuwa JUMBO inavyojitahidi kuzishika nchi za Afrika zilizokuwa mfano:

Tanzan Nigeria Uganda Kenya


2008 2005 2008 2008 2008
Pop 40mil 37mil 146mil 31mil 37mil

Life.E 52y 46years 46 52 56

hum
dev
index 0.503 0.45 0.499 0.493 0.532

GDP $1400 600 2200 1100 1800

literacy
rate 69.4% 61% 68% 66.8% 85.1%

Curru
ption
index 3 7 2.7 2.6 2.1

%women
in perliam 30.4 25 7.3 30.7 9.8

religion Bara musl 50 chr83 78
% chris30, chris 40 musl 12 10
musl 35, indige ind 10
neous 35
Znz, musl 99

deni $5311000000 9132000000 1705000000

Kenya 6749000000


Haya sasa jioneeni wenyewe tonavyowafukuza hao akina MFANO WENU Kenya na Nigeri. Baadhi ya maeneo tumeshawakanyaga.

Ukisema Kikwete hafai, basi thibitisha katka takwimu.
 
.

Ukisema Kikwete hafai, basi thibitisha katka takwimu.

Hio takwimu hazipo. Lakini hata takwimu ulizonukuu wewe haziwezi kuwa sahihi sababu zimetolewa na CIA, Wazungu, Wakristo, Makruseda, na Makafiri adui wa Islamu. Takwimu halali ni zile za Waarabu, Waislamu (haswa Shura ya Maimamu), na Magagula ya Bagamayo. Sasa takwimu kama hizi tuzipate wapi?
 
Hio takwimu hazipo. Lakini hata takwimu ulizinukuu haziwezi kuwa sahihi sababu zimetolewa na CIA, Wazungu, Wakristo, Makruseda, na Makafiri adui wa Islamu. Takwimu halali ni zile za Waarabu, Waislamu (haswa Shura ya Maimamu), na Magagula la Bagamayo. Sasa takwimu kama hizi tuzipate wapi?

Ekzaktile.

Hizo hapo ndizo natafuta maana hizi za makafiri wa kisiaiei haziaminiki kabisa.
 
Una maana kwamba mama yako alikuwa mtoto ombaomba enzi za Nyerere, au? 😀

Wote, hata mama yako, kama alikuwepo wakati huo alikuwa ni omba-omba, unless labda alikuwa katika circle za Nyerere na Mawaziri wake (of which I doubt) ndio walikuwa hawaendi kukaa foleni ya kuomba omba, Muulize akueleze.
 
Wote, hata mama yako, kama alikuwepo wakati huo alikuwa ni omba-omba, unless labda alikuwa katika circle za Nyerere na Mawaziri wake (of which I doubt) ndio walikuwa hawaendi kukaa foleni ya kuomba omba, Muulize akueleze.

Acha uongo wewe,

Wamama waliokuwa wanafanya kazi mashambani na kwingineko walikuwa na kipato na walikuwa na uwezo wa kununua nguo.

Wakinamama waliokuwa wakikalia kucheza midundiko na kupiga umbeya tu ndiyo waliolost - kama hao unaowafahamu wewe.
 
....

Haya sasa jioneeni wenyewe tonavyowafukuza hao akina MFANO WENU Kenya na Nigeri. Baadhi ya maeneo tumeshawakanyaga.

Ukisema Kikwete hafai, basi thibitisha katka takwimu.

Badala ya kuweka data za kuonesha uchumi "kukua", wewe unaweka data za kulinganisha na nchi zingine (bila hata kuweka source). Nilikushauri huo muda wako unaoutumia kuona al arabiya ungefaa zaidi kwenye mambo mengine.
 
Acha uongo wewe,

Wamama waliokuwa wanafanya kazi mashambani na kwingineko walikuwa na kipato na walikuwa na uwezo wa kununua nguo.

Wakinamama waliokuwa wakikalia kucheza midundiko na kupiga umbeya tu ndiyo waliolost - kama hao unaowafahamu wewe.

Huko mashambani ndio usiseme, walikuwa wakihamishwa na kupelekwa maporini kuliwa na Simba.
 
Badala ya kuweka data za kuonesha uchumi "kukua", wewe unaweka data za kulinganisha na nchi zingine (bila hata kuweka source). Nilikushauri huo muda wako unaoutumia kuona al arabiya ungefaa zaidi kwenye mambo mengine.
Asante. Chanzo ni kile kile www.aneki.com. Tembelea huko utafaidika.
 
Hakuna doubt kuwa, JK bado hajaja na jipya. Sanasana naona kuwa kwenye kipindi chake uchumi umetetereka na utekelezaji wa sera madhubiti za Mkapa kuhusu kudestabilize uchumi zimelegalega, tunaona inflation tunaona increase in gvt spending. Uchumi wetu unashuka, hatuwezi kujifananisha na Zimbabwe ambayo inaporomoka au Somalia. Tujaribu kujifananisha na Kenya au Rwanda.GDP per capita sio kigezo kizuri cha kuonesha maendeleo uchumi au kuonesha maisha bora ya wananchi. Kama tajiri mmoja ameingiza mabilioni ya pesa nchini basi per capita inaweza kupanda hata kufikia dola 2000 lakini inawezekana mtanzania wa kawaida akawa na per capita ya dola 50 tu.

Wenzio wanatoa data wewe unaleta siasa.Soma vizuri maelezo yaliyotolewa na acha jazba za kisiasa.
 
Kwa ukweli mtu anayehitaji hongera ni Mkapa. Mkapa kafanya kazi kubwa sana kwenye uchumi lakini anamapungufu yake ya kuwaachia mafisadi na kusaini mikataba mibaya. Mkapa pamoja na kuchukiwa alikuwa na mipango mizuri zaidi kwa wawekezaji hata kwenye sera ya afya kuliko Kikwete. Kikwete amekuwa raisi kwa muda mfupi sana na ni wawekezaji wachache wapya wamekuja wakati wa kikwete. Kikwete lakini atasaidiwa na Pinda wawekezaji wameshajua Pinga ni mtu anayejua mambo na mfuatiliaji kuliko Kikwete sana wanamtumia pinda, Kenya wamemtumia pinda na alikuwa huko majuzi na sasa hawalalamiki tena, South Korea wametumia Pinda. Pinda ndiye mtu atakaye msaidia kikwete kwani anaonekani ni mtu serious na muda unavyoenda watu wanamuona pinda atakuwa kama Putin wa Russia.

tuko ukurasa mmoja kiongozi ...mkapa ndo wa kupewa sifa
 
Kusema "Kikwete kainua uchumi wa Tanzania" ni kuwahadaa Watanzania. Yaani ni Kikwete peke yake anayefanya kazi nchi hii? Ni Kikwete pekee anayefikiri? La hasha.

Sikatai Kikwete kama rais anafanya kazi nzuri. Lakini katika kumsifia Kikwete, tusidhalilishane namna hii. Tusionyeshe kutokujiamini kwa kiasi hiki. Uchumi wa nchi kamwe hauinuliwi kwa juhudi za mtu mmoja tu, hata awe nani.

Mawazo kama haya yanafanya tuchekwe na wenzetu wa nchi jirani.
 
Mkisema JK ndo kaudidimiza uchumi wa TZ nitawaelewa lakini mnaposema kainua uchumi wa TZ nashindwa kuwaelewa ndo tuseme mnajikomba kwake ili angalau mpate kaupendeleo flani au? Maana ukiangalia bei za vitu zipo juu kulinganisha na kipato cha mtu wa kawaida Tanzania vile vile JK ameongeza gap baina ya walio nacho na ambao hawana kitu yaani maskini matajiri kipindi hiki cha miaka 4 ndo wamepaa maradufu na maskini wameshuka balaa ngoja tuone miaka mingine hiyo mtakayo mchagua.
Huyu kashindwa kabisa kudhibiti mfumuko wa bei atajitetea ooh mdororo wa uchumi ndo umesababisha acheni kututania jamani mdororo wa uchumi nyi watanzania mnauza nini nje mpaka mkakubwa na mdororo? Zaidi ya Pamba napo inauzwa kwa kusua sua ni nn kingine mnauza nje? Ambacho TZ mnajivunia kuwa kinatuingizia kipato na fedha za kigeni. Nafikiri mnasifika kwa kutembeza bakuri kwa hisani badala ya kukomalia KILIMO ambacho ndo uti wa mgongo.

Kwa kweli Mkwere amenivunja nguvu mpaka najutia kura yangu niliyompa. Kila mwezi yeye yuko majuu na watu kibao kutafuna akiba yetu ya fedha za kigeni. Mfumuko wa bei (inflation) umepaa kutoka 4% mwaka 2005 Mmakua alipomwachia madaraka mpaka 20% leo hii. Mmakua ni journalist by profession lakini alifanya shilingi ikaeshimika. Mkwere uchumi alio soma DSM Chuo Kikuu sijui unamsaidiaje. Ebu fikiria alipeleka watendaji Ngurdoto kwenye semina elekezi wakala kuku kwasana lakini leo hii hakuna la maana hao maofisa wake wamefanya. Hii gear ya Kilimo Kwanza nayo haina mashiko. Maazimio kama haya tulishasikia sana hapa Tanzania bara kwa mfano Siasa ni Kilimo; Kilimo ni uti wa mgongo n.k. Je tuko wapi hadi leo hii. We need to think twice in 2010.
 
Zawadi nadhani unapiga propaganda za siasa hapa, mimi nimetoka huko vijijini watu ni maskini wakutupwa, Wazee wale hawana hata kiberiti!

Mazao sasa hivi ebu niambie ni zao gani linaingiza pesa serikalini na kumkomboa mkulima? (Pamba, Kahawa, katani) yote hiyo sasa hivi ni historia! Enzi za Nyerere hayo mazao ndo yalikuwa mkombozi kwa mkulima kwa kusomesha watoto,kujenga nyumba bora n.k.

Hapa Dsm ebu angalia mfumuko wa bei na maisha yalivyopanda kwa kasi ya ajabu (bei za vyakula, Petrol, umeme n.k.)

Angalia mishahara ya Wafanyakazi, madai ya walimu n.k.

Sasa huo uchumi alioinua ni upi? mimi sitatumia percent danganya toto natoa mifano ninayokumbana nayo kwenye maisha kwa kulinganisha Nyerere/Mwinyi/Mkapa/JK.
 
Wenzio wanatoa data wewe unaleta siasa.Soma vizuri maelezo yaliyotolewa na acha jazba za kisiasa.

Data hazisaidii ndo maana viongozi wetu wakienda huko vijijini kuelezea bajeti wanazomewa na kupigwa mawe! mtu ni maskini we unamsomea data!
 
Back
Top Bottom