Dr. Slaa amemaliza kuhutubia Dar es Salaam. Tulikuwa Kawe tunamsikiliza. Ahadi zake kwa wananchi zinazidi kuongezeka. Sasa ameahidi akichaguliwa,wananchi wataruhusiwa kupika na kunywa pombe ya gongo,pia watasaidiwa kuitengeneza vizuri.
Inaelekea sasa kwamba kama mtu yoyote atamshinda Kikwete,ni huyu Dr. Slaa. Nimemsikiliza jana katika mdahalo wa ITV na leo Kawe,na,ninacho kila ninachohitaji ili kufunya uamuzi wa kumpigia au kutompigia kura Dr, Slaa. Natumani wengine,kama Lipumba na Kikwete watafanya mdahalo kama alivyofanya Dr, Slaa.
Wasipofanya hivyyo,wanaweza kuhesabika kama washindani ambao hawataki kufika kwenye mashindano,kwa hiyo watampa ushindi Dr. Slaa.
Ili mtu achaguliwe kuwa Rais,lazima ajulikane ametoka wapi. Dr. Slaa alikuwa anasema jana kwamba'' kila Mtanzania anafahamu kwamba mimi nilikuwa padre wa Kanisa Katoliki'' Mimi nilikuwa sifahamu kwamba Dr. Slaa alikuwa padre wa Kanisa Katoliki. Kwa hiyo hawa wagombea wafanye mdahalo kama alivyofanya Dr. Slaa,na wasiwalazimishe wananchi kununua mbuzi ndani ya gunia.
Kiongozi lazima ajulikane rafiki zake ni nani,na wanahusiana vipi. Kuhusu Dr, Slaa,tunafahamu kiasi fulani kuhusu rafiki zake,kwa vile tumeelezwa kuhusu Josephine. Lakini kuhusu wagombea wengine wa Urais there is too much opaqueness kuhusu mahusiano yao na rafiki zao. Yaani,bila kuingila mambo ya binafsi ya mtu,ni lazima generally ufahamu anahusiana vipi na swahiba zake.
Dr. Slaa alikuwa anasema kwamba akichaguliwa yeye,angependa Halima Mdee pia achaguliwe,ili aweze kupata wabunge kupitisha sera zake. Hilo ni wazo zuri. Lakini itakuwa ni bora hizi category zote za kura,Urais,Ubunge na Udiwani,zijitegemee,hapo ndipo wapinzani watapata nafasi ya kumuondoa Kikwete. Lakini ikibidi na Mbunge pia itabidi achaguliwe,labda wapiga kura wengine watashindwa.
Huu ni wakati wa kuanza ukurasa mpya. Wachaguliwe wabunge ambao wataiwezesha Tanzania kufungua ukurasa mpya.
Againmwe say,Rais yoyote akichaguliwa,Tanzania haitapata matatizo yoyote. Wanachi wamchague yoyote wanayetaka awe Rais.