Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

Kuna watu wanadhani UN ni ccm .........
UN kitu INGINE. Siy CCCM. Amalizie kwanza NGWE yake CCM akapumzike Msoga. Asiote kuwa VASCO da GAMA wa Dunia. Kama alimaliza NUSU ya muda wake wa Urais wa TZ hewani, AKIWA "Rais wa Dunia" si atashinda HEWANI 100% ya maisha yake. Huenda akapendekeza kwenda Mars ama Mwezini kila wiki!
Namtakia safari njema!
Atangulie. JMPJ akimaliza zamu yake atampokea tena kijiti!
 
UN kitu INGINE. Siy CCCM. Amalizie kwanza NGWE yake CCM akapumzike Msoga. Asiote kuwa VASCO da GAMA wa Dunia. Kama alimaliza NUSU ya muda wake wa Urais wa TZ hewani, AKIWA "Rais wa Dunia" si atashinda HEWANI 100% ya maisha yake. Huenda akapendekeza kwenda Mars ama Mwezini kila wiki!
Namtakia safari njema!
Ushauri mzuri nadhani atapita huku na kusoma....
 
mmeshalipwa pesa zenu nini? maana naona mmerudi kujaribu kumjengea tena jina mytu wenu. ni ngumue watanzania walishamaliza heshima zao kwake. abaki huko aliko salama. aliwatumia sana watu kama ninyi anyway mlifaidika lakini kwa propaganda za kijinga na zisizo za kisomi. maana ndege wa rangi moja huruka pamoja. sasa mnashindwa kuelewa kumchagua mtu wa kushika nafasi ya Ban Ki Moon hakuhitaji kampeni za ndani ya nchi maana hachaguliw na watanzania na hata angekuwa anachaguliwa na watanzania hawa ni wa watanzania makini wenye kujielewa si wa miaka ile ya giza.

huwa najiuliza mtu anayeweza kuja hapa kutuletea habari za namna hii ubongo wake unafanya kazi kweli? au ni tumbo na ashki? huwezi kuwa serious ukawataja watu waliofilisi taifa hili kana kwamba ni watu wa maana. nchi imeuzwa hii na walionunua wanaweza kweli wakaamua kumpa mtu shukrani kwa aliyoyafanya na huwez jua pengine kama inatokea basi ndo ulikuwa mpango wa kuifisadi nchi ili mtu aje apewe nafasi kama hizo lakini na uhakika mataifa ya huko nje wana akili si wapumbavu kama wale watanzania waliotuzorotesha kwa miaka 10 nchi hii kila mtu aliyeweza kujichumia akajichumia, kwa madawa ya kulevya na ujangiri.

ninyi ina maana si watanzania? ninyi mnaoleta uozo kama huu hapa jukwaani? ina maana hamna uchungu kabisa na mama, bibi,shangazi na dada zenu walivyokuwa wanalala chini huko muhimbili,amana n.k baada ya kujifungua? ninyi hamjisikii uchungu kabisa? ni nani kawaroga enyi kizazi cha nyoka?mfananishwe na nini?














HUYU NDIYE MRITHI WA BAN KI-MOON
_________________________________________________
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania kwa awamu ya nne (2005 – 2015) ni miongoni mwa wanadiplomasia wakubwa duniani wenye ushawishi na uwezo wa utatuzi wa matatizo mbalimbali duniani, sio tu kwa sababu viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanamkubali bali kwa uwezo wake katika masuala ya kidiplomasia.

Alizaliwa mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete.


Alipata elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam, ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi.

Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida 1977 na baadae kuhamishiwa Zanzibar kwa kazi maalum baada ya muungano wa TANU na ASP mpaka kufikia mwaka 1980 aliporudishwa makao makuu ya chama (CCM).

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mbunge na pia NaibuWaziri wa Nishati na Madini chini ya uongozi wa MH. Al Ahsan Mwinyi mpaka kufikia mwaka 1990 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa maji nishati na madini.

Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi akiwa na umri wa miaka 44 ambapo alikuwa ni waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa. Kufika mwaka 1995 alitueliwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya uongozi wa Rais Benjamin W. Mkapa na kuongoza wizara hiyo kwa miaka 10 mpaka kufikia mwaka 2005 ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Katika Nyanja za kimataifa Mh. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia ambae amefanya mambo mengi katika bara la Afrika na Dunia, kama vile kutatua migogoro katika nchi za maziwa makuu, jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa kama Mwenyekiti wake (EAC) baadhi ya mambo ambayo dunia inampongeza ni pamoja na Mwaka 2005 akiwa kama Mwenyekiti mwenza wa mikutano wa Helsinki (Helisinki process on Globalization and Democracy) aliweza kuongoza mikutano huo kwa mafanikio makubwa.

2013 akiwa ndiye kiongozi pekee kutoka Afrika aliyeshiriki katika mkutano nchi za umoja wa Ulaya EU wa Alpbach Austria aliliwakilisha bara la Afrika vyema katika kutafuta fursa za maendeleo na ushirikiano kimataifa.

Dr. Jakaya Kikwete pia amekuwa Mjumbe tume ya Elimu Duniani ikiongozwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika kutafuta namna ya kugharamia Elimu duniani (TICFGEO) kwa mwaka 2015.

Kwa mwaka huu 2016 Dr. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya Amani nchini Libya katika kusaidia kurudisha amani nchini Libya
Pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza kwa tume ya kusaidia afya ya Mama na motto duniani kwa mwaka huu 2016 ikiwa ni katika jitihada zake kuhakikisha Afya na mama na motto duniani kote zinalindwa.

Kwa mtazamo huo nina imani kubwa kwa kipindi ambacho Mh. Ban Ki-Moon ataachia ofisi, Mwanadiplomasia huyu ndiye atakayechukua viatu vyake .

Hizi ni baadhi ya tuzo za heshima alizowahi kupata toka nchi mbalimbali...

2007: Sullivan Honor
2007: The AAI African National Achievement Award (on behalf of Tanzania).
2009: US Doctors for Africa Award.
2011: Social Good Award from the United Nations Foundation
2011: South-South Award for Global Health, Technology and Development
2012: FANRPAN Policy Leadership Award from the Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network.
2013: Africa's Most Impactful Leader of the Year by the Africa Leadership Magazine
2013: ICCF Mengha Award by the International Conservation Caucus Foundation
2014: Icon of Democracy Award, from The Voice Magazine (Netherlands)
2015: Leadership Excellence Award by the Pan-African Youth Union.
2015: African Achievers Award by the Institute for Good Governance in Africa.
2015: African Statesman of the Year by the The African Sun Times.

View attachment 325689 View attachment 325692 View attachment 325693 View attachment 325694 View attachment 325695 View attachment 325696 View attachment 325697 View attachment 325698
 
Krap! hao UN wakimchukua huyo msanii nao watakua jipu linalohitaji kutumbuliwa, hafai hata ujumbe wa nyumba kumi huyo... what a waste!
 
Watu wengine mmekaririshwa mpaka vichwa vyenu havifanyi kazi kwa kujitegemea,Mwanza sio Dar na haitoweza kuwa Dar! Kuna formula inayofuatwa kwa Secretary General kupatikana sio kwa kutembeza cv ya mtu mitandaoni,haidhuru degree za kununua zinapofanya kazi,inadhuru pale inapodhuru ukweli
 
Kutokana na uongozi wake wa miaka kumi binafsi sidhani kama anaweza kurithi kijiti kutoka kwa Banki-Moon. Ni mtu aliyeshindwa kila nyanja.
 
Tatizo la siasa za Afrika...... kikwete kichwani
anajua kabisa maana ya demokrasia na uwazi kwenye uchaguzi..... anaweza akaandika kitabu kwa siku moja juu ya mambo hayo na kuuza dunia nzima tu... lakini hapa kwetu kajionyesha ni
jinsi gani viongozi hawa ni fisi as per Trump.... sijui ni kwa nini... ni kwamba wanaogopa wapinzani wakichukua kutakuwa na machafuko au.... hata sielewi kwa kweli... JK is smart upstairs na hicho kiti kinamfaa kama ingekuwa zamu ya Afrika lakini anayo tenda do..... (ZENJ, ZEC, NEC, MITA 200, BUNGE....Kweli simwelewi)
 
In fact ukweli unabakia kua JK ni mwanadiplomasia mahiri na mwenye uwezo wa usuluhisha na sifa tajwa hapo juu anazo,regardless what he did with domestic affairs during his term as the head of state.bahati mbaya haitakua kulingana na hiyo rotational style
 
kama unafikiri UN wanachagua tu ili mradi anaweza kupata na labda Trump asiwe rais wa Marekani maana atamtimua mara moja mtu anaenda kufanyiwa operation ya tezi dume nje ya nchi wakati wananchi wake wanakufa kwa kukosa madawa hospital hata bururndi hawawezi kumpa urais
 
Kikwete anapendwa sana na wazungu zaidi ya waswahili!! mnyonge mnyongeni Ila haki yake mpeni!! Jk tunakuombea uzidi kujitangaza Tanzania
Haki gani ya kumpa? Ndiye aliyetufikisha hapa tulipo na CCM yake, kila kitu kiko shagara.... Dr. JPM yupo bize kunyoosha na kutoa makorongo.
 
Jamani naomba tuheshimiane na tusitafutiane ban za makusudi. JK hata akipewa hiyo nafasi ni haki yake maana nchi aliwakabidhi mabepari. Hivi mnasahau namna Maraisi wawili wa Marekani kukutana katika nchi yetu pamoja? Mnaona ni jambo la kitoto? Yaani sitaki hata kumsikia huyu tzdm.
 
Kama kwenye uraisi alipwaya vile je ukatibu mkuu ataweza.
 
Akichaguliwa atahamishia ofice yake kwenye ndege na pale UN ataonekana mara moja moja tu
 
Yan Vijana wa Lumumba kazi mnayooo... Mgogoro wa Zanzibar tu umemshindaaaaa....ataweza Africa na Dunia?
 
Pamoja na tetesi zote hyo nafasi uwa Ni rotation na Afrika ndio tuu tulimaliza alipokuwa Annan, next itakuwa nafasi ya Ulaya au Amerika kwa hyo Kikwete labda apewe nafasi kama ya Migiro
 
....post to u.n .......
if you think he qualify....
hapa ni helpless.....
n.b
****
as chair of ccm he should finalise a [HASHTAG]#znz[/HASHTAG] saga 1st.
**Total disqualifications.
that post means "usuluhishi kwa mataifa mbalimbali hapa kwako znz ni shida tafrani haki inapokwa.
Haya pia ni mawazo yako, wala si vibaya mtu kusema cha moyoni mwake
 
Back
Top Bottom