MAONI KWA MKUU WA NCHI
Nasema maoni wa makusudi kwa kuwa huu si ushauri. Ushauri ni rasmi na kutofuatwa kwake kunaweza kuleta madhara baadaye. Lakini yangu ni maoni tu.
Yako mambo duniani ambayo kufanikiwa kwake hakuhitaji demokrasia, na katika hayo mojawapo ni suala la umoja. Nchi nyingi zenye umoja madhubuti kwa mfano Marekani, hazikusubiri wananchi wapige kura au waridhie kwa maoni yao ili umoja wa USA uweze kufanikiwa. Ilipobidi kutembeza bakora, basi zilitembea.
Kati ya mambo yaliyofanikisha utulivu Iraq kabla ya kuvamiwa na marekani ilikuwa ni bakora na mijeledi ya ....Sadam Hussein.
Nguvu ya Iran mpaka sasa inatokana na uongozi wa Sharia. Leo hii wangekuwa wamemeguka kabisa. Mijeledi ya Sharia na siyo demokrasia ya kimagharibi ndiyo inayosababisha Iran Inaitisha Dunia.
China wazee wa HIPHOP Ngumu versus mabishoo wa TAIWAN, Uspinachi wa Dalai Dama, Ukauzu wa Tibet na mengineyo, hapa sipingani na mambo yasiyonihusu wala siwaungi mkono China wala TAIWAN wala yeyote hapa....., ninachokionyesha ni Staili ya China kwenye kudeal na masuala ya KITAIFA. Angalia wanavyo deal na mafisadi. WANANYONGA MAFISADI ATI!!!!!! CHINA HAWANYWI KAHAWA NA MAFISADI...NDIYO MAANA WENGINE WALIJINYONGA WENYEWE HATA KABLA YA KESI MAHAKAMANI!!!!!!!!
Leo hii China wanaitikisa Dunia. Huenda wakaing'oa JAPAN kwenye kilele cha Ugwiji wa Kiuchumi punde tu.
SUALA LA MUUNGANO LISIWE SUALA LA MJADALA, NI AIBU KUBWA KUZUNGUMZIA KUTENGANA. Serikali ikunje ngumi na kuponda kabisa mjadala wowote wa kuuvunja muungano. Suala ni je tutafaidikaje watanzania wote kwa ujumla bara na visiwani kwa muungano tulionao na namna ya kuuboresha na kuondoa kero zilizoko.
AU KAMA TUMECHOKA KUUNGANA BASI TUFANYE YAFUATAYO.
1. Kanda ya ziwa iwe nchi peke yake, Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora ziwe Jamhuri ya kanda ya Ziwa. Mambo ya madini, samaki, maji, mifugo, Kilimo kidogo au vipi?
2. Mikoa ya Msosi, Kusini iungane, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Rukwa iwe Jamhuri ya Watu wa Kilimo Kwanza.
3. Dar es Salaam iungane na Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara na kuunda Jamhuri ya East Coast. Bandari yooote yao mtajiju.
4. Kigoma wajitenge na kuungana na Burundi, wazee wa juhudi binafsi.
5. Arusha, Manyara na Kilimanjaro Ziungane na Kenya, wazee wa pesa kwanza. Utalii kwa sana, madini kiasi fulani, biashara au sio.
6. Dodoma, Morogoro na Singida Ziungane na kuwa Tanganyika. Hawa si ndio wazawa au ikoje?
Dhambi ingekuwa si tamu hakuna ambaye angeifanya. Utengano ni dhambi kwa mujibu wa Mwl Nyerere RIP. Hata vitabu vya kiimani vinaonyesha kuwa mwenyezi mungu hupenda umoja kuliko utengano, ndoa kuliko talaka, mapatano kuliko magomvi.
Mheshimiwa mkuu wa nchi, Jamhuri hizo sita hapo juu za kinadharia ni kukuonyesha kuwa hayo yapo mioyoni mwa watu. Utengano huanzia kwenye kufikiri kuwa maslahi yataongezeka nje ya umoja. Angalia Jamhuri nadharia hapo juu je ni nani asiyedhani kuwa Jamhuri yake itafaidika tukitengana????????????
KUNA MAENEO KAMA MKUU WA NCHI INABIDI UENDE KIDIKTETA, HUWEZI KUJADILIANA NA MTOTO WAKO WA MIAKA SITA KAMA AENDE SHULENI AU LA..KWAMBA UNAMUACHA ACHAGUE KUSOMA AU KUBAKI NYUMBANI NA KUCHEZA......MUUNGANO, UFISADI, USALAMA NA ULINZI WA NCHI, MASLAHI YA KIUCHUMI YA TAIFA NA SIRI ZA NCHI INABIDI UUVAE UBABA HASA, UNGUNGURI..KUNJA SURA HIYO...EBO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!PIGA NGUMI MTU ATI!!!!
UMEWAHI KUONA MTU KASHIKIWA BUNDUKI HALAFU ANAPIGA MWAYO?????????